KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,886
- 40,068
Kakudanganya nani wewe?fweeezaaaa ndio kila kitu na ni sabuni ya rohoKama una pumua.shukuru sana mungu.hakuna utajili mkubwa kama afya.pesa ni matokeo
Wameamua kutumia fursa ipasavyoHile pale opossite na mlimani city sio jengo la NSSF wao wamekodi tu me namjua mmiliki wa lile jengo na ndugu yake ni kigogo NSSF ndio alimsaidia ktk kupata wapangaji
Anzisha thread ya kufunguliwa daraja hapa tunazungumzia ufisadi wa Dau au mfuturishaji wa zamani wa NSSFHivi daraja la Dau linafunguliwa rasmi lini vile?
Kuna daraja la dola bilioni 88 ? Asante nilikua sijui hiliLile la dollar Billion 88? Au lipi? Au lile linaloitwa Xiao Dau Ping?
Inafaa Magufuli ajieleze si ndiye alikuwa waziri wa ujenzi na akilisimamia sana hili daraja, au siyo?
Sasa hii picha ndio inamiliki timu au documents ndio zinaonesha umiliki? Bwashee vipi? Mbona hata mtoto wa Nursery school hawezi kukuelewa.
Mmiliki wa Newcastle United ni mtu mmoja tu 'Mike Ashley' mwenye hisa 100%
Huo sasa ndio uandishi kanjanja inabidi watu wachukuliwe hatua za sheria sujui yapi mengine ya kutunga katika habari nzima kampuni ya kichina iliyojenga daraja la Kigamboni pia ni ya Dr.Dau kama tender zote alijipa mwenyewe?
utajiri wako jeUtajiri wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF, Dr. Ramadhani Dau unafika zaidi ya Tsh 100 Bilioni.
- Ni mmoja wa wamiliki wa timu ya Newcastle ya Uingereza.
- Kampuni zake pekee ndizo zinazopewa tenda ya kufanya kazi NSSF.
Chanzo: Dira ya Mtanzania - 18 Aprili 2016
inabidi ziwe ngapi?Billion 100.utamiliki timu UK? Jamani tuwe wa kweli jamani!
Hehehe!!! Mimi namshauri Dr atoke hadharani aombe uthibitisho wa habari hizi kama hawana awafilisi maana wamezidi sasa
Sosipae kupepa, abamchwewa simmatini kumbaliwane, isikisi 100%? Tobeanti sikiati 80%? 60%? 40%? nadi 20%? Billioni 100 sangasawela palimbwe?
Najua sasa umeelewa!.
Hahahahaha.... umenasa kwenye trapha ha ha.....dau ni fisadi...
MIKE ASHLEY NDIYE MMILIKI PEKEE KIJANA NADHANI UNGEGOOGLE UNGEPATA MAJIBU SAHIHI..
Tunachotakiwa kufahamu ni kuwa UTAJIRI HUNUNUA WAFUASI. Kuwa na wafusi wengi wa kutetea bila ya kujibu hoja za msingi ni dalili ya nguvu ya fedha.
Gazeti la DIRA Jumatatu inaonekana limefanya kazi nzuri ya kiuchunguzi. Dondoo halisi za 'UTAJIRI WA DAU NSSF HATARI kwa kadiri ya gazeti hilo ni kama ifuatavyo:
Mimi ninaamini kama kuna uwongo kwenye taarifa hizi, Dau au NSSF watachukua hatua ya kukanusha kwa vielelezo kama walivyofanya gazeti la Dira, au kuamua kulipeleka gazeti hili mahakamani. Maana taarifa hii ipo ukurasa wa mbele wa gazeti, na wala haijatolewa kwa kujificha kama walivyojificha watetezi wa Dau ndani ya JF.
- Utajiri wake ni zaidi ya shilingi bilioni 100
- Utajiri huo aliupata akiwa boss wa NSSF
- Dau ana hisa nyingi katika timu ya mpira ya Uingerezaya Newcastle
- Menejiment ya NSSF chini ya Dau iliipitisha kampuni ya Dau iitwayo Derm Electrics kwaajili ya tenda za kuweka umeme kwenye majengo yote ya NSSF
- Pesa ambazo kampuni hiyo ya Derm Electrics ililipwa na NSSF - Shilingi 136,596,496 (2011), shilingi 178,691,940 (2012), shilingi 228,049,368 (2013), shilingi 343,280,613 (2014)
- Dau aliidhinisha miradi mbalimbali yenye gharama kubwa kwa maslahi binafsi
- Ripoti ya CAG akishirikiana na kampuni ya ukaguzi ya kimataifa Ernest & Young iliibua upotevu wa mabilioni ya fedha kwa mwaka 2014/2015 ndani ya NSSF
- Mtaalam mshauri wa mradi wa Arumeru alilipwa zaidi ya shilingi bilioni 400
- NSSF iliingia ubia na kampuni ya AHEL yenye mtaji wa shilingi milioni 10 (kwa kadiri ya ripoti ya BRELA)
- AHEL ilipewa mradi wenye thamani ya shilingi trilioni 7.18
- Ripoti ilibaini NSSF ilikiuka katika ununuzi wa ardhi yenye thamani ya bilioni 15.159 katika maeneo ya Madale, Mataya, Bagamoyo, Misugusugu, Ngarambe, Kibaha na Mkuranga
- Ripoti iliibua ufisadi wa shilingi bilioni 16.98 katika ujenzi wa jengo la hoteli ya Kitalii Mwanza
- Ripoti iligundua kuwa kwenye mradi wa hoteli ya Mwanza, kampuni mbili zililipwa kwa kazi za aina moja kwa kadiri ya mkataba
- Ripoti iligundua pia ufisadi katika ununuzi wa sare za wafanyakazi kwa gharama ya shilingi bilioni 1.078 kutoka kampuni ya Pink Diamond
Ukimwa wa NSSF na Dau unadhihirisha kuna uwezekano mkubwa taarifa hizi ni za kweli. Tunachosikia zaidi ni kelele za wapambe ambalo si jambo la ajabu maana pesa hununua watu hata kutetea uovu.
Mungu wa kweli awajalie hekima Watanzania ili wauone wema au ubaya wa mtu kwa mtizamo wa kiimani, ambao ni upofu hatari, upofu ambao hata Baba na Babu zetu hawakuwa nao toka uhuru.
Kwa vyanzo halali si kwa ufisadiKwani haturuhusiwi kuwa matajiri?
Wewe ndio utumie akili, umeleta picha ya bwanyenye la kizungu na unatuambia anamiliki kwa 100% hiyo ni wajibu wako kuthibitisha with vivid evidence.Tumia akili kidogo 'Chekunde' hili sio kama jukwaa la kule chini unapochekesha si uangalie basi kama Newcastle UTD ni public listed company.
Kuna wakati mwingine kuna magazeti yapo kwasababu ya kuchafua wengine. Hivi Una bilioni mia moja unaweza kuwa mmiliki wa Timu Inayoshiriki EPL? Hiyo pesa utaweza kununua wachezaji kama Yohane cabaye au CHEIKH TIOTE ambao wote thamani Zao ni Zaidi Pesa hizo? kwa
nadhani hili swali ungelipeleka kwa mtoa bandikoSasa kama ni mmiliki pekee wa Newcastle Dau anamiliki New castle ipi?
Kazi kubwa sio kuandika uongo bali ni kuutetea!
Dau amekiuka azimio la arusha..linasema,"Ni marufuku kwa kiongozi yeyote kuwa na hisa katika makampuni yeyote,wala kumiliki biashara yeyote ile"
Gazeti halijaandika anamiliki, bali limeandika ana hisa nyingi kwenye Timu ya Newcastle.