Utafiti wa Urais uliochapishwa na gazeti la Rai linalomilikiwa na Rostam Azizi unaoonesha Lowassa anaongoza kwa 52% akifuatiwa na Dr Slaa na January Makamba umetajwa kuwa ni kiinimacho na hadaa kwa watanzania, imebainika.
Utafiti huu uliokataliwa na wahariri wa magazeti karibu yote kuandikwa inasemekana inayokana mapungufu yafuatayo ambayo hayakupata majibu kutoka kwa waandaaji :-
1.Umeandaliwa na vijana was Lowassa wanaofanya kazi mtandaoni.
2.Kura ilikua haina ukomo, unaweza kupiga mara nyingi uwezavyo
3.Vijana wa Lowassa waliandaliwa utaratibu wa kupiga kura usiku na mchana ili tu mgombea wao aongoze kwa mbali sana.
4.Admin au muendeshaji wa kura hiyo alikua na mamlaka ya kuingia na kutazama na hata kudhibiti nani aendelee kuongoza na nani afuatie.
5.Dr Slaa ametengenezwa aonekane anafuatia nyuma ya Lowassa ili ionekane kuwa CCM isipomsimamisha Lowassa basi wapinzani watachukua nchi.
Baada ya waandishi na wahariri wote kukataa kuchapisha Utafiti huo wa hovyo wakihoji nani kauandaa na ulipimwa kwa vigezo gani vya kisayansi, ni gazeti la Rai pekee linalomilikiwa na Rostam Azizi, rafiki mkubwa wa Lowassa ndilo pekee limechapisha habari hiyo.
Lowassa ajajitekenya na kucheka mwenyewe.