Utafiti mpya: Lowassa aongoza tena mbio za urais

Utafiti mpya: Lowassa aongoza tena mbio za urais

Hizi tafiti bado naamini kuwa ni tafiti za kutengeneza hazina mantiki yoyote tutazisahau kabisa wakati ukifika.

Zingekua zimemtaja mpenzi wako ndiye anae ongoza ungekuja kivingine.
 
Hata ya JK mlisema inang'aa lakini matokeo yake mmeyaona ni ufisadi kianzia baba, mama mpaka watoto. Nyie ndio mnaochangia taifa kuangamia kwa kuchagua majina ya watu.

Lakini kaka yangu huwezi mfananisha lowaasa na jk.Lowassa kawaacha mbali sana
 
Hata shetani ana watu wake wanaoongoza kila siku na nahisi wengine ndo wako hapa hapa Tz kwahiyo msishangae
 
mi sio mkewe ila kura yangu anayo.we watu waulizwe waseme watamchagua lowasa we mapovu kama mk fafa.watu wanamtaka lowasa jembe.hana kashfa kama udhanivyo ni fitna ya sita na jk tu.mbona sasa escrow na epa wapo wengi na wanautaka "urahisi"

Aliekuambia Lowasa hana kashfa nani? Hatakama unaingiza siku kupitia yeye, ukweli bado utasimama pale pale. LOWASA NI MIONGONI MWA VIONGOZI WASIO WAADILIFU WA TAIFA HILI. Huyu si alikuwepo BMK? Mbona basi hatukusikia walau akitetea kipengele cha 'uadilifu" kibakie kwenye Tunu za Taifa?
 
Kwa nini Lowasa awe adui mkubwa kwa wana wa CCM wenyewe na siyo Ukawa ? Mbona Kinana anapiga kampeni kwa cheo chake ?!
 
Watanzania tuli lishwa sumu kuwa lowassa ndiye muhusika wa richmond leo watanzia wamejuwa mwenye mzigo wa richmond,lowassa aliwajibika tu kisiasa
 
Aliekuambia Lowasa hana kashfa nani? Hatakama unaingiza siku kupitia yeye, ukweli bado utasimama pale pale. LOWASA NI MIONGONI MWA VIONGOZI WASIO WAADILIFU WA TAIFA HILI. Huyu si alikuwepo BMK? Mbona basi hatukusikia walau akitetea kipengele cha 'uadilifu" kibakie kwenye Tunu za Taifa?

angekuwa na kashfa angekuwa ameshapelekwa mahakamani.Muulizen baba riz huo mzigo wa richmond
 
ImageUploadedByJamiiForums1416458920.102200.jpg
 
Watanzania tuli lishwa sumu kuwa lowassa ndiye muhusika wa richmond leo watanzia wamejuwa mwenye mzigo wa richmond,lowassa aliwajibika tu kisiasa

Na sijui kwanini waaatu wengine hawaelewi hili!! Ni Richmond, richmond kila kukicha wakati ukiwa na akili kama punje ya ulezi tu na ukifwatilia kwa makini ile saga unaona kabisa hapakua na haki iliyotendeka na Lowassa alihukumiwa kwa mob injustice.
Ila inatia moyo sababu wabaya wake hawana kete zaidi ya RICHMOND ikifika mda atakavyoipangua na kueleza ukweli wake ambapo mpaka kina Slaa watakubali ndipo utawaonea huruma hawa watu wanaoendeshwa na mihemeko badala ya akili.

Wameshupalia false accusation ya Richmond, ila kama Lowassa ni fisadi nguli mbona kwenye pembe hatujamsikia, tpdc hamna kitu, escrow hata kwa harufu hayupo ila bado vichaa ndio wanamwona fisadi namba 1.
 
Anaongoza kwa kugawa hela?

hili ndio jibu halisi. huyu mpenda madaraka anaongoza kwa kugawa hela...na tulivyowachumia tumbo tafiti nying tu zitasema anaongoza
 
Ni Mambo MAWILI MAKUU tu yanayomfanya Lowassa kuendelea kubaki katika chati za siasa ya Tanzania


  1. PESA/UTAJIRI WAKE
Suala la pesa/utajiri wake umeupataje, hii iwe topic ya siku nyingine. Lakini kwa sasa tukubaliane kuwa Lowassa ana utajiri usiopimika. Kwakuwa Watanzania wengi ni masikini aidha wa FEDHA au AKILI, basi Lowassa anatumia utajiri wake huo kuwanunua Watanzania hao ili aweze kutimiza ndoto safari yake.

Ametumia utajiri wake huo kuwanunua baadhi ay viongozi wa chama chake, wasomi, wamiliki ya vyombo vya habari, Spin doctors na Watanzania wa kawaida. Hao ndio wanaoendelea kumuweka juu katika siasa za Tanzania pamoja na kashifa za ufisadi zinazomuandama, lakini pia pamoja na kukataliwa na Muasisi wa chama chao CCM JK Nyerere kwamba hafai kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Lowassa kwa kufahamu hayo amefuata maneno ya busara ya wahenga wetu kwamba PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA!

Kwa haraka utaona kwamba kama vile anafanikiwa, kwani katika Chama chake amewapiku wataka urais wengine wote (rejea utafiti wa TWAWEZA). Lakini Lowassa ana vikwazo VIWILI VIKUU kufikia hiyo safari ya ndoto yake. Kwanza ni KAMATI KUU ya CCM, tetesi zilivyo sasa ni kwamba CC itakata JINA lake na huo ndiyo utakuwa mwisho wa safari ya ndoto yake. Lakini PILI KIKWANZO cha pili kitakuwa wananchi kama kweli Kamati kuu itaogopa KUKATA JINA LAKE, Lowassa is UNELECTABLE, sidhani kama utajiri wake UTAHIMIRI kuwahonga wapiga kura wote wa JMT. Maana nguzo yake kubwa ni utajiri wake. Hata kama utajiri wake utahimiri kuna makundi ya jamii hayahongeki linapokuja suala la kuchagua viongozi kama vile Wapemba.

2. UPINZANI MADHUBUTI

Upinzani madhubuti pia umemusaidia Lowassa kuendelea kuwepo kati chati ya political landscape za Tanzania. Kama tunavyofahamu vigogo wa vigogo wa CCM hawataki kabisa Lowassa awe mgombea wa urais kwa CCM. Wote tunafahamu kampeini inayoneshwa wazi wazi na WAMA dhidi ya Lowassa, ambayo ni Taasisi ina MKONO WA IKULU. Kwasababu vigogo hao hawa uhakika nini atafanya Lowassa akiwa Rais, baada ya kutoswa na kutishwa ZIGO LA RICHMOND. Kama mnavyofahamu CCM ni chama cha MIZENGWE NA FITINA! Mambo yao hayafanyi kwa uwazi au kwa taratibu zinazofahimika. Mabo ya CCM yanaendeshwa kwa MIZENGWE NA FITINA. Rejea kisa cha Sitta alipoambiwa kwamba kama anataka kugombea tena uspika wa bunge la JMT, basi abadilishe jinsia na kuwa mwanamke, kwani zamu hii lazima speaker awe mwanamke.

Wakati CCM wanategemea kutumia MIZENGO NA FITINA kumuengua Lowassa au kumzuia kugombea nafasi Urais wa JMT kupitia CCM, CCM mara hii wanaokana kukwama kutumia mizengwe na fitina kuzima ndoto ya safari ya Lowassa, kwasababu ya upinzani madhubuti na imara.

CCM wanafahamu kwamba kama watatumia mizengwe na fitina kuzima ndoto ya safari ya Lowassa, Lowassa alishawaambia kabisa CCM, kuwa yuko tayari kukipasua chama vipande viwili. CCM wanafahamu kwamba Lowassa anao wanachama na wapenzi wengi sana nje na ndani ya CCM nchi nzima.

Kutokana na uimara ya ya vyama vya upinzani na hasa baada ya Muungano wa UKAWA. CCM wanafahamu fika kabisa kwamba kama Lowassa atatoka CCM na kuelekea huko atakapoamua, CCM asilani haitaweza kushinda UCHAGUZI MKUU. Wakati ambapo opposition parties zilikuwa weak CCM wasingejari kabisa. Kwani CCM wangefahamu fika kwamba hata akienda huko atakapokwenda CCM wana uhakika wa kushinda uchaguzi mkuu, japo wangeaathrika kidogo na percentage ya kura. Lakini nyakati hizi wanafahamu Lowassa akitoka nao CCM wamekwisha, political landscape ya Tanzania imebadilika. Ndiyo maana CCM waliweza kufanya hivyo kwa akina Mrema, Marehemu Prof Malima. Lakini kwa nyakati hizi CCM hawawezi kabisa kufanya hivyo, unless wamejibariki kwamba sasa CCM wanakuwa opposition party.

Kutokana na UIMARA wa opposition party, hivyo CCM wanataka kumu CONTAIN Lowassa. Yaanu KUMUDHIBITI Lowassa akiwa NDANI ya CCM, kwani akitoka NJE ya CCM itakuwa na sawa genie out of the bottle, hawataweza KUMDHIBITI tena Lowassa.

Hii strategy ya CONTAINMENT ya CCM dhidi ya Lowassa ndiyo pia inamuweka juu kwenye political landscape za Tanzania. Kwani Lowassa anaendelea kufanya vitu vyake kufikia ndoto ya safari yake. Ni vipi CONTAINMENT POLICY ya CCM itafanya kazi dhidi ya Lowassa that is remained to be seen, But once thing is CLEAR sio wote watakaoshinda vita hii yaani CCM on other hand and Lowassa on the other hand. LAZIMA mmojawapo kati ta CCM na Lowassa ATASHINDWA hiyo VITA?

Je kati ya CCM na Lowassa nani ATASHINDA hiyo VITA? BE THE JUROR YOURSELF.
 
Gazeti la Rostam Aziz,mkurugenzi wake Hussein Bashe ambaye nd'o mtu wa kati,kati ya Lowassa na Rostam Aziz sasa mnategemea nini hapo? Msitoke povu bure,Lowassa peke yake anaweza kuvinunua hivi vyombo vya maamuzi times and again,na kumbukeni hawa jamaa wamejipanga kivyotevyote tu,shida iliyopo ni kuwa watanzania tumezoea kurubuniwa na ni wachache wanaeeza kuona mbali.Na hata hao wachache wanaoweza kuona mbali wananunulika kuhadaika kirahisi tu,kwa ajili ya matumbo yao wapo tayari hata kushabikia upuuzi kama huu kwa sababu ya kurutubisha tu matumbo yao.
 
Back
Top Bottom