Utafiti wa Urais uliochapishwa na gazeti la Rai linalomilikiwa na Rostam Azizi unaoonesha Lowassa anaongoza kwa 52% akifuatiwa na Dr Slaa na January Makamba umetajwa kuwa ni kiini macho na hadaa kwa watanzania, imebainika. Utafiti huu uliokataliwa na wahariri wakuu wa magazeti karibu yote nchini kuandikwa inasemekana inatokana na mapungufu yafuatayo ambayo hayakupata majibu kutoka kwa waandaaji :-
1. Umeandaliwa na vijana wa Edward Lowassa wanaofanya kazi maalum mitandaoni kwa lengo la kumjenga kisiasa, kumsafisha na tuhuma lukuki za kifisadi alizonazo na kumpigia kampeni hii ikiwa sambamba na kudhoofisha umaarufu na heshima za wagombea wengine ndani ya chama.
2. Kura ilikua haina ukomo, unaweza kupiga mara nyingi uwezavyo na wamekuwa wakihamasishana kumpigia kura Edward Lowassa mara nyingi kwa kadri inavyowezekana. Kampeni hii imekuwa ikifanywa na watoto wa Lowassa ambao ni Fred, Nelson na Neema kwa kushirikiana na vibaraka wao akiwemo Hussein Bashe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya New Habari Corporation inayomiliki gazeti la Rai na Mtanzania na aliyekuwa Makamu M/kiti wa UVCCM Taifa Beno Malissa.
3. Vijana wa Lowassa waliandaliwa utaratibu wa kupiga kura usiku na mchana ili tu mgombea wao aongoze kwa mbali sana ambapo kila siku vijana hao walilipwa posho ya shilingi za kitanzania 50,000 kwa kila mmoja.
4. Admin au muendeshaji wa kura hiyo alikua na mamlaka ya kuingia na kutazama na hata kudhibiti nani aendelee kuongoza na nani afuatie.
5.Dr Slaa ametengenezwa aonekane anafuatia nyuma ya Lowassa ili ionekane kuwa CCM isipomsimamisha Lowassa basi wapinzani watachukua nchi. Baada ya waandishi na wahariri wote kukataa katakata kuchapisha Utafiti huo wa hovyo na kipuuzi wakihoji nani kauandaa na ulipimwa kwa vigezo gani vya kisayansi, ni gazeti la Rai pekee linalomilikiwa na Rostam Azizi, rafiki mkubwa wa Lowassa ndilo pekee limechapisha habari hiyo.
6. Itakumbukwa kuwa hata Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa aliwahi kuongea na vyombo vya habari kuwa amenasa mawasiliano ya barua pepe (E-mail) kati ya Lowassa na maofisa wa Twaweza ili kutenegeza matokeo ya tafiti hiyo ambayo yalimbeba ndugu Edward Lowassa kwa tofauti ya asilimia moja (1%) akifuatiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Hatahivyo ushindi huo wa tofauti ya asilimia moja ulionekana kumkwaza sana Ndugu Lowassa na hivyo kupekea kutoa agizo kwa vibaraka wake kuwa kazi kubwa ifanyike ya kutengeneza utafiti mpya utakao mbeba kwa tofauti ya asilimia kubwa dhidi ya wapinzani wake ndani ya chama.
My take:
Ni dhahiri kuwa ndugu Edward Lowassa sasa ameamua kujitekenya na kucheka mwenyewe huku akidhani anawahadaa watanzania kumbe anaidanganya mwenyewe na vibaraka wake ambao wamekuwa wakibuni mikakati mbalimbali ya kumchuna inayotumia pesa nyingi huku wakimcheka pembeni.
Ndugu wadau na Great Thinkers wenzangu naomba tujadili kwa hoja kashfa hii.
Naomba kuwasilisha