Utabiri: 2025 Upinzani utachomoza na kushinda viti vingi kupitia agenda ya Hayati Magufuli

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Marehemu JPM hadi sasa ndiye kitisho kikubwa kwa mrithi wake ambapo Chawa Fc wanapambana bila kupumzika kuchafua kwa makusudi jina lake na legacy aliyoiasisi.

Eneo ambalo kwa haki kabisa marehemu hakulitendea haki ni Haki za Binadamu. Na eneo hilo alikuwa mkali kweli kweli kuanzia kwa watu wake chamani ambapo hilo lilikuwa ni sahihi mno. Lakini kuwabana upinzani wasitimize haki yao ya kikatiba ya kufanya siasa alikiuka sana sana utawala bora

Tuendelee kumuombea makamu Mwenyekiti CHADEMA aendelee kuimarika kiafya. Lisu ambaye ni ushuhuda wa namna awamu ya tano ilivyosimama bampa to bampa dhidi ya upinzani na fikra mbadala.

Alisimamia nidhamu serikalini na hata wakwapuaji mali ya umma walilia na kusaga meno.

Kinachoendelea leo ni namna CCM inavyosimamia mradi wa kumchafua hayati JPM ambapo inaamini kuwa inatengeneza mazingira ya kukubakiwa na wananchi. Kwa wanagenzi wa siasa nchini hawaoni ni shida ama changamoto kwa upinzani kumsema vibaya JPM kwa sababu macho yote yaliona kilichojiri kwenye medani ya siasa katika mhula wake.

Lakini chama cha CCM kuasisi kampeni za kumchafua Mwenyekiti wake Taifa awamu ya tano ni wazi kwamba kimeshika garasa tupu katika karata zake za kisiasa.

Wananchi waitwao WANYONGE walikuwa wanufaika wakubwa kwenye utawala wa JPM ambapo alisimama kuwatetea dhidi ya majambazi ya CCM ambayo bila huruma yanakwapua fedha za umma hata kufikia kuipiku serikali kwa ukwasi ilihali wao ni watumishi wa umma ambao hawana background ya utitiri wa utajiri huo.

Uchaguzi TAMISEMI 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025
Vyama vya upinzani vitaanza kutumia rasmi agenda ya Magufuli (positive na negative) kupambana na chama tawala na hatimaye vitachukua viti vingi vya serikali za mitaa, vijiji na vutongoji.... ambapo kuelekea 2025 ndipo CCM itaanza kunyweshwa dawa iliyoitengeneza yenyewe na itasababisha watu wengi kupigq kura za hasira dhidi yake. Lakini angalizo dogo ambalo halina umuhimu sana naliweka hapa. Intelejensia ya ndani ya CCM inapokea fungu kutokq Hazina. Mwenye akili na afahamu. Hao watasimama kujaribu kuokoa jahazi lakini hawatoweza kukwapua kama ilivyofanyika awamu zilizopita.

Kablq ya uchaguzi nchi itatikisika tena.

Nimeonq niyaseme haya sasa kwani kila kinavyokucha ndivyo CCM inavyosogelea mlango wa kutokea kwa speed isiyo ya kawaida.

Tuendelee kula nyama, mtori upo chini
 
watakao itesa ccm ni haohao ccm wenzao
nakuhakikishia mpaka sahivi humohomo chamani kwao hawaelewani,makundi makubwa mawili yanakinzana mitazamo,
kuna kundi linaona limetengwa na ndio haohao watawasumbua ccm wenzao,we subiria mbilinge za wajumbe zikaribie utaona wakavyo kanyagana,
tujiandae kupata chama kingine kikubwa cha upinzani
 
Neno upinzani lina maana kubwa sana mkuu
 
Wapinzani wa sasa ni projection ya CCM hawawasumbui sana.

Subiri mziki wa 2025
 
wapinzani kimya kabisa baada ya kupokea ruzuku, wapinzani hawako pamoja na wananchi, wapinzani wako kimaslahi ili kujenga vyama vyao pamoja na kuimarisha maisha yao. Walikuja na kasi ya katiba mpywa pamoja na kuanza kuongelea mambo ya kupanda bei, ghafla wamezima. Kuwatetea wapinzani ni sawa, lakini kuwatetea ili uwe na wewe waje kukupa maisha bora huo ni ujinga wa mwisho!
 
Upinzani haujafa namaanisha wapo wapinzani wa kweli wanajipanga kuingiza timu kwenye uchaguzi
 
MAMBURULAZ yenye vyeti feki yana uchungu na mwamba wa Afrika JPM.

Nendeni shule acheni janja janja.

Hakuna ugali wa bure wa kudoea vyeti vya wizi.

Lazima ukae darasani usote upate degree ili uwe SMART na sio MBURULAZZ
 
Wapo na wataendelea kuwepo, mtaji wao mkubwa ni wananchi. Wapinzani wa Tanzania wana roho mbaya na hawako tayari kusaidia yoyote zaidi ya maisha yao. CCM ni bora kuliko wapinzani, siku wakija chukua nchi ndio mutaona makucha yao. Au tunadhania kukaa jela ni kwa ajili yetu sisi? Mbona sasa hivi hakuna hata anayetoka kuongelea mambo yanayotokea, wakati nyuma walikuwa hawalali asubuhi na usiku wanalalamika wakati nyuma maisha yanajulikana yalivyokuwa tofauti na sasa.
Upinzani upo isipokuwa lazima tuamini hakuna mpinzani mwenye nia njema na nchi hasa wananchi wenye kipato kidogo ambao hata wanyang'anywe hawawezi kuleta madhara yoyote.
Kugombea nchi si kwa ajili ya kuijenga, badala yake ni kwa ajili ya kujenga miradi na maisha yao binafsi. Kama mtu ni wa kwanza kupinga miundombinu kujengwa akidanganya wananchi kwamba hautokula barabara, wakati anajua fika barabara ni moja ya kuendeleza uchumi, basi huyo hafai hata kuwa diwani.
 
Hata ww ni mmoja wa wale walioko kwenye huo unaoitwa mpango wa kumchafua magufuri... yaani ukileta Uzi kuhusu huyo mtu ni lazima atashambuliwa tu, wala hakuna mpango wwte wa kumchafua magufuri, bali anachafuliwa kwa matendo yake mwenyewe.. yaani yule mtu hapa jamvini hakubaliki kwa 80% na wananzengo ...msimsingizie mama wa watu kuwa ameandaa watu wa kufanya kz hiyo...ila tupo aliotutesa na hatutakubali utuletee sifa za kubumba tusimpinge ...kama hutaki mtu wenu asichambwe basi acheni kuleta story zake hapa jamvini...
 
hoja zinakuwa ni zilezile mlizo cremishwa

  • watu kupotea
  • watu kuporwa hela zao
  • matajiri kufilisiwa
  • tundu kupigwa risasi
  • ben saa nane kupotea
hakuna mwenye evidence kuhusu haya matukio...
 
Neno upinzani lina maana kubwa sana mkuu
safi kwa kulitambua hilo mapema,
kuna upepo unaonekana siasa zinaenda kubadilika kwa kiasi kikubwa,sio tena zile upinzani wa Mbowe na Lissu,
raia wanamitazamo yao tofauti,, ukiachana na hizi baadhi ya kelele za Jf na twitter,
 chaguzi zijazo zitakuwa ngumu na za tofauti sana
 
Hata ww ni mmoja wa wale walioko kwenye huo unaoitwa mpango wa kumchafua magufuri... yaani ukileta Uzi kuhusu huyo mtu ni lazima atashambuliwa tu, wala hakuna mpango wwte wa kumchafua magufuri, bali anachafuliwa kwa matendo yake mwenyewe.. yaani yule mtu hapa jamvini hakubaliki kwa 80% na wananzengo ...msimsingizie mama wa watu kuwa ameandaa watu wa kufanya kz hiyo...ila tupo aliotutesa na hatutakubali utuletee sifa za kubumba tusimpinge ...kama hutaki mtu wenu asichambwe basi acheni kuleta story zake hapa jamvini...
Umeteswaje, au maisha yako yalikuwa magumu, pesa hakuna, mpendwa wako TUndu alishambuliwa? subiri niotee kitu : mpaka sasa maisha yako ni magumu?
 
hoja zinakuwa ni zilezile mlizo cremishwa

  • watu kupotea
  • watu kuporwa hela zao
  • matajiri kufilisiwa
  • tundu kupigwa risasi
  • ben saa nane kupotea
hakuna mwenye evidence kuhusu haya matukio...
Tulia askari wa zenj ... mtu wenu alikuwa ibirisi
 
Wapinzani wa sasa ni projection ya CCM hawawasumbui sana.

Subiri mziki wa 2025
atajayeiokoa ccm ni Samia wananchi wameanza kumwamini. watu wanamtazama mtu aliye juu kabisa hawajali kitu kinaitwa ccm
 
Back
Top Bottom