Nakumbuka enzi hizo ukipikwa wali nyama au maharage ama pilau watu tulikua tunaoga mapema na kutulia home nyakat za jioni
Wakati mwingine ilikua ukimaliza kula unaweka kipunje cha ubwabwa juu ya mdomo na kuanza kukiringisha....😀😀😀
acha tu, maisha haya tunayoishi nje ya mji hata siku munyu ukikuishia usiku huna pakuomba huwezi kamwe kushare na mikono yote hiyo.... Nyani kwenye mikono hiyo kuna wale wanawatia wenzao kinyaa anachota ubwa mkono umejaa akitia mdomoni mkono mzima kisha anarudisha kwenye sinia anakung'ung'utia, wote mna muacha....!Hahaaaa sinia moja mikono ishirini!
Watu wanafinyanga matonge, wanalamba mikono, wanarudi tena kufinyanga.
Ni uchafu lakini kuna raha yake. Leo hii siwezi hata kula ugali na watu halafu wote tuwe tunachovya kwenye bakuli moja.
Halafu nani humu keshawahi kunya pombe chafu? Basi bana, mi nshawahi. Kuna mshikaji wangu mmoja anaitwa Eriki, mama yake alikuwa anazipika na kuziuza hizo pombe chafu.
Sisi tulikuwa haturuhusiwi kula na madogo kabisa maana lazima washinde au kulala njaa!!!!!!!
Halafu kulikuwa na dogo mmoja, akiona anazidiwa basi anamwaga pili nyingi sana kiasi kwamba ukila hicho chakula lazima uchubuke midomo...
Wakati mwingine anatemea mate msosi wake wote ili kuwafukuzia mbali walafi...lol!
Lazima hata leo umekula nyama mwishoni
Bisha........
mwaka mmoja mkubwa hivyo?? mi nimeanza nkiwa na siku moja tu...hahahahaha heri yako wewe mimi nimeanza kula mwenyewe na mwaka mmoja tu
ila mwanangu nahisi nitamlea kiyai yai
Halafu utakuwa unamalizia na nyama..........
Mkuu hiyo kwenye sufuria mbona kama ni ngararimu?
CC: Mkirua miss chagga !!!!!![/Q
special ya wameru hiyo, bila makande kwenye sikukuu hainogi
Wee nawe ufuatilie mbebz kwani ulishapevukaHalafu nani mwingine humu keshawahi kupotea kwa kufuata mdundiko? Basi mi nashawahi bana. Kisa nilikuwa namfuata mbebz mmoja anaitwa Kuluthumu. Mdundiko ulianzia Mlalakuwa mie nikajikuta niko Sinza Abajaro! Kupotea nikapotea na mbebz sikumpata.