Uswazi na misosi!

Uswazi na misosi!

Nakumbuka enzi hizo ukipikwa wali nyama au maharage ama pilau watu tulikua tunaoga mapema na kutulia home nyakat za jioni
Wakati mwingine ilikua ukimaliza kula unaweka kipunje cha ubwabwa juu ya mdomo na kuanza kukiringisha....😀😀😀

Mkuu umecheza mule mule

Tena kwa wale waliokuwa mikoa ya kaskazini ambako mchele ulikua adimu hii makitu ndo ilikuwa noma

Ukitumwa unarudi fasta ili usiambiwe hakuna kula ...lol!!!!!!!!!!
 
Hahaaaa sinia moja mikono ishirini!

Watu wanafinyanga matonge, wanalamba mikono, wanarudi tena kufinyanga.

Ni uchafu lakini kuna raha yake. Leo hii siwezi hata kula ugali na watu halafu wote tuwe tunachovya kwenye bakuli moja.
acha tu, maisha haya tunayoishi nje ya mji hata siku munyu ukikuishia usiku huna pakuomba huwezi kamwe kushare na mikono yote hiyo.... Nyani kwenye mikono hiyo kuna wale wanawatia wenzao kinyaa anachota ubwa mkono umejaa akitia mdomoni mkono mzima kisha anarudisha kwenye sinia anakung'ung'utia, wote mna muacha....!
 
Last edited by a moderator:
Halafu nani humu keshawahi kunya pombe chafu? Basi bana, mi nshawahi. Kuna mshikaji wangu mmoja anaitwa Eriki, mama yake alikuwa anazipika na kuziuza hizo pombe chafu.
1521866_666018816769149_1078987164_n.jpg
 
Sisi tulikuwa haturuhusiwi kula na madogo kabisa maana lazima washinde au kulala njaa!!!!!!!

hahahaah mimi kwetu dogo nilikuwa peke yangu lakini sikubali kuwekwa pembeni ya mtanange wote humo humo
 
Halafu kulikuwa na dogo mmoja, akiona anazidiwa basi anamwaga pili nyingi sana kiasi kwamba ukila hicho chakula lazima uchubuke midomo...

Wakati mwingine anatemea mate msosi wake wote ili kuwafukuzia mbali walafi...lol!

Yaani mkuu tulikua tukila wali hanawi mtu mikono ili marafiki zetu wakaipate

Lazima wanukishiwe mikono .....lol!!!!!!!!
 
hahahahaha heri yako wewe mimi nimeanza kula mwenyewe na mwaka mmoja tu
ila mwanangu nahisi nitamlea kiyai yai
mwaka mmoja mkubwa hivyo?? mi nimeanza nkiwa na siku moja tu...
 
huo uvumilivu wa kula nyama mwisho sina..yani tonge nyama,tonge nyama..na nikiona ni ndogo nakata vipande vidogo vidogo twende sawa
Halafu utakuwa unamalizia na nyama..........
 
Mkuu naongezea

Mkiachwa watoto peke yenu chakula mnakula vizuri mwishoni mnaanza kugombania

Cha ajabu chakula bado kipo msiposhiba mnaongezwa

Utoto raha sana

Yaani mkuu we acha tu!!!!!!!!!!!!!
 
Halafu nani mwingine humu keshawahi kupotea kwa kufuata mdundiko? Basi mi nashawahi bana. Kisa nilikuwa namfuata mbebz mmoja anaitwa Kuluthumu. Mdundiko ulianzia Mlalakuwa mie nikajikuta niko Sinza Abajaro! Kupotea nikapotea na mbebz sikumpata.
Wee nawe ufuatilie mbebz kwani ulishapevuka

Sema ulikuwa unabahashia tuu
 
huo uvumilivu wa kula nyama mwisho sina..yani tonge nyama,tonge nyama..na nikiona ni ndogo nakata vipande vidogo vidogo twende sawa

Hahahahahaaaaaaaaaaaa ....lol!!!!!!!!!!
 
special ya wameru hiyo, bila makande kwenye sikukuu hainogi

Mkuu hiyo nim ngararimu na sio makande

Makande kwa wapare ni maarufu sana kwasababu ya ijumaa kuamkia sabato!
 
Back
Top Bottom