Hapo kuna ile mnaacha firigisi, au paja ale baba au mgeni. Kuna siku tunapiga mpunga kwenye sinia mbele yangu limekaa paja. Kwa kweli ilibidi nirefushe mkono kuchukua nyama ya mbali kwa sababu paja ni la wakubwa, ngoma ikaenda karibia na finali hakuna mtu wa kuichukua. Wananiambia mbona hauli nyama huku nasuasua nikachangamkia fursa japo nilijisikia vibaya lakini wote wanaelewa taratibu zetu. Ina maana nilikula nyama zaidi ya mgawanyo wa 2 kwa kila mtu. Ilinitokea kwa family friend!
Karibu vipapatio vya vitwitwi.
Hahahahahahahah. .tunaita advance eating..just in case.
Kwa maelezo yako ya kupotea kwenye mdundiko kwa ajili ya kufukuzia mbebzKwani we wabebz umeanza kuwafukuzia ukiwa na umri gani?
Hahahahahaaaaaaaaaaaa ....lol!!!!!!!!!!
Dah! Walikuwa wanakera mbaya, umejipanga ule kuku then anakulenga! Na nia yako n kuku sio wali! So ikabidi strategy zibadilike!Kunguru wakawafanya muwe mnakula nyama kwanza
Kwanini msitengeneze manati mkuu?
ukimlea kiyai yai dada atamfundisha tu. wangu anamiaka 4 dada keshanisaidia kumfundisha kunawa akijisaidia yeye dada anamwagia maji ananawa mwenyewe tena na sabuni
Ikilikuwa kama una history mbaya kwenye minuso ya kuwahi kukimbilia nyama basi nyumbani wako radhi wafunge vioo then wanakununulia kilo moja ya utumbo unapikiwa kisha unaambiwa ukombe hadi iishe yani kitakachofata hapo utakuwa mbali na nyama kabisa
Hii inaitwa komesha ...lol!!!!!!!!!
Mkuu hii lazima itakuwa early 90's na midle 90's
Hizo bei nazikumbuka sana!!
Mkuu hii menu ya 2000's, sa hizi huwezi kupata 'Chai cha maziwa' kwa bei hiyo. Ila maandishi yake ni burudani tosha hata kabla haujaagiza!