Uswazi na misosi!

Uswazi na misosi!

Mie enzi zangu basi likiletwa sinia la wali yani kabla halijawekwa mezani naanza kuangalia wapi kuna nyama kubwa yani likifika tu naidaka ile nyama kubwa then ndo naendelea kula

dawa yako ni hii...
1174908_628989643805400_277135028_n.jpg
 
Kuna siku nilijikuta humo ndani kikazi. Wageni walipoondoka kilibaki chakula cha Kumwaga. Nikaona hapa leo wali Utanisamehe. Ilikua ni kuchapa nyama pori,vyuku,samaki,mbuzi,swala,bata yaani mpk unachemsha. Mule ndani jamaa wanafaidi bana.

Mkuu inaonekana baada ya huo mtanange hakuigusa nyama kwa muda....!!!!!!
 
Hahahaaaaa Eiyer hiyo tabia hadi sasa ninayo hasa kuku huwa namla wa mwisho kabisa, sjui ndo imeniathiri tangu mdogo, nikipakua chakula kwenye bufee hata nikiwa kwenye sherehe ntaanza kula wali salad viazi ndizi nyama na kuku na samaki kama zipo zinakuwa za mwisho kula daaah itabidi nibadilishe style ya kula.
Ila nile kwenye sahani yangu peke yangu, uke ya kula sinia moja siku hizi siiwezi tena
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaa Eiyer hiyo tabia hadi sasa ninayo hasa kuku huwa namla wa mwisho kabisa, sjui ndo imeniathiri tangu mdogo, nikipakua chakula kwenye bufee hata nikiwa kwenye sherehe ntaanza kula wali salad viazi ndizi nyama na kuku na samaki kama zipo zinakuwa za mwisho kula daaah itabidi nibadilishe style ya kula.
Ila nile kwenye sahani yangu peke yangu, uke ya kula sinia moja siku hizi siiwezi tena

Misibani huwa unapewa sahani yako peke yako?
 
Mie nikishashiba siwezi kula tena nikafurahia ninachokila kwahiyo hapo ningeanza na kitu adimu kwanza ili hata nikishiba kwenye sinia ukabaki wali poa tu huo unaliwa daily!!!

Inaonekana wanawake mnapenda sana kuanza na nyama ......!!!!!!!
 
Nyama yaliwa mwisho coz we always spare the best for last...lkn mi naenda viceversa nyama kwanza niishibe kisha ndo naendelea na msosi ha ha haa

Wewe ni kama mimi, nakula nyama, kuku au fish kwanza, hata waifu ameshanijulia. Anaweka ugali kidogo nyama kibao.

Nyie mnaojifanya mnakula nyama ya mwisho inatakiwa nikutane na nyie kwenye kolabo la msosi, mtajuta......
 
Hahahahahaaaaaaaaaa!!!!

Na sisi tulikua na dogo ambae tulikua hawawezi kuruhusu tule nae maana lazima alikua analala au kushinda njaa maana tulikua tunakwenda speed ya jet kwenye kurusha matonge mdomoni ....lol!!!!!!!!!!!

Halif hapa umenivunja mbavu..... Speed ya jet
 
acha tu, maisha haya tunayoishi nje ya mji hata siku munyu ukikuishia usiku huna pakuomba huwezi kamwe kushare na mikono yote hiyo.... Nyani kwenye mikono hiyo kuna wale wanawatia wenzao kinyaa anachota ubwa mkono umejaa akitia mdomoni mkono mzima kisha anarudisha kwenye sinia anakung'ung'utia, wote mna muacha....!

Sio kwa madenti wa boardind school, haachiwi mtu hapo: enzi tunasoma shuleni kwetu viranja wanaohusika na misosi walikuwa wanajidelea sana siku ya nyama na punje.
Walikuwa wakitenga nyama kwenye kindoo ili baadae wale; siku moja jamma mmoja akasema leo sikubali lazima nitoke pasu na hawa viranja, alipofik kwenye eneo la mgao wakamzuia; alichikifanya alitemma kihozi kwenye ndoo alafu akawambia wajamaa mtaiacha na nitaila yote mwenyewe.

We thubutu hakuna mtu aliyekubali denti alikuwa anaingiza mkono kwenye bdio huku anaangalia pembembeni anashuka finyango anaikung'utakung'uta kwenye ndoo
Anatia mdomoni na kusepa mpaka zikaisha. Chezea boarding school weye
 
Last edited by a moderator:
Misibani huwa unapewa sahani yako peke yako?

Msema ukweli mpenz wa mungu kwa hapa dar misiba niliyohudhuria kunakuwa na bufee kila mtu na sahani yake hata kama ni wali harage, ila hata ile ya hali ya chini nilishahudhuria ma kwenye sinia likija nahakikisha nakula tonge tatu tu za mwanzo baada ya hapo nashika simu na kujifanya nimepigiwa basi napotelea huko na happ watu wataona nimeshiriki chakula ila simu imeingilia kati so hawataona naringa ila kula kwenye simia mmmhh mikono ya watu bana uchafuu mwengine kapenga kamasi mwengine katoka kujikuna sehemi nyeti halafu anapeleka mkono kwenye sinia mmmhh mie huwa nawaza hadi nashindwa kukimeza chakula.
 
Yote tisa nawapenda sana kabila la kisukuma kwa ukarimu wao kwa wageni.

Mkienda kuwatembelewa mkabahatika kuchingiwa kuku, yaani mnaletewa kila kitu kasiro kichwa na miguu.

Sasa usiombe tu visit na ninyi wala nyama mwisho mtaisona namba, wakati una tonge 1 nina finyango 2 hahahaha c
 
Wewe ni kama mimi, nakula nyama, kuku au fish kwanza, hata waifu ameshanijulia. Anaweka ugali kidogo nyama kibao.

Nyie mnaojifanya mnakula nyama ya mwisho inatakiwa nikutane na nyie kwenye kolabo la msosi, mtajuta......

Hahahaha hao wala nyama mwisho tajiju zao maana akitokezea mgeni yabidi umkaribishe kwahiyo nyama zote atafaidi mgeni

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
mbavu zangu mieeeeee......... mbona hamjaongelea soda? na zenyewe zilikuwa na vituko vyake!
 
Back
Top Bottom