Usiri ajira TISS

Usiri ajira TISS

Uko sahihi, akili kubwa sana
Kuna vitu vinafanywa usiri wakati hajikutakiwa kuwa vya siri, na usiri huu unaofanywa unakuta ni terget tu ya kuweka watu wao wanaowataka, na ndo maana tunapata watu wasio na weledi na wenye IQ ndogo sana kiutendaji yawezekana ni mkakati tu wa mtu. Kinachotakiwa watangaze nafasi za kazi watu waombe lakini mchakato wa kuwachukua waliokidhi vigezo ndo ufanyike kwa siri.
 
Rafiki angu mmoja alianza kama Uvccm mpaka leo nae yupo huko. Hua nampima vitu vidogovidogo tu vya uelewa ila ni mweupe. Uchawa na Ccm ni janga la taifa.

UVCCM imegeuka kadi ya TANU kwa kipindi hiki, vijana wengi tu unakuta haamini wala haipendi CCM ila anaingia huko ili kupata fursa nyeti kama hizo au akianzisha biashara zake awe na network ya kumlinda asisumbuliwe

Ila TISS wangeliangalia hili, wao ndio usalama wa nchi hivyo, wangeangalia namna bora ya kupata best brains and characters ili iwe future ya TISS, haya, Mambo ya kuwalea makada ambao ni opportunist wasio na chembe ya uzalendo. Ipo siku TISS itabaki uchi
 
Ili Tanzania iendelee yatupasa kuwekeza katika ujasusi wa ndani na nje TISS igawanywe na itambulike kwa address.
Mtu anaweza kuwa na taarifa muhimu anashindwa pa kuipeleka au kuituma.

Huu Usiri usio na maana maana yake kuna vitu hawataki vijulikane, kwani vikijulikana vitasababisha wengine kuondolewa au kustaafishwa maana wengi wao wameingia kimagimashi.
Ni kwamba kila Rais hupenyeza kundi lake ndani ya TISS.

TISS haiko huru kufanya jambo lolote lile kwa manufaa ya nchi bali wanafuata matakwa ya Rais
 
Kwanini panakuwa na Usiri katika ajira ndani ya Usalama wa Taifa?
Km ilivyo kwa Upadre na Usista connection mkuu huna connection hupati hio nafasi kwenye hizo nafasi, connection kuanzia juu mpaka chini hauingii km unaingia kwenye dampo fulani hivi kuna watu wanakusolola tangu ukiwa yanki wanachukua data zako from the very beginning of your life, uonekane kweli kazi utaiweza na kuna familia hua zinalengwa sio kila familia unaweza kutoa hao watu, kibongo bongo Usiri ndio jambo la muhimu km huwezi kutunza Siri huwezi kua Padri huwezi kua Sista huwezi kua Usalama wa Taifa,

Kuna Siri unabebeshwa ambazo unahitaji umakini mkubwa kuishi nazo, nilishtuka nilipoambiwa hadi leo huko Masasi kuna waingereza wamechimbia hazina zao wakija wanajua eneo kwa kutumia compass, Ila wabongo hakuna hata anaejua hadhina za waingereza zilipo hata hao Usalama wa Taifa, usisahau waingereza ndio walitawala kwa kutumia mkono wa Damu
 
Huoni kama kada unakua unamjua kuliko kuokoteza mtu mtaani. Teknolojia yetu ya kuwamonitor watu iko chini compared to hao CIA. Wakiruhusu watu kuomba kazi na kufanyiwa usaili etc huoni kama usalama wa taifa utaweza kuwa compromised na watu wasio na nia njema. Bora shetani unaemjua kuliko malaika usiemjua. Anaweza akapandikizwa mtu huko akaja kuwa na influence ya ajabu akavuruga.

Hadi leo marekani wanapambana na wasaliti ndani ya system. Kama hufatilii historia basi angalia angalia hata movie zao tu. Acha waweke hao makada na uvccm sijui watu wanaowajua kwasababu wanawajua uwezo wao, vetting inakua imefanyika haswa. Wanajua hadi kijiji ulichotoka. Cha msingi si nchi iko salama? Mi na wewe tuendelee kubanana kwenye kujitafuta kimaendeleo mengine tusitafute lawama.
Nyerere aliwatafuta mpaka chooni, ukada ni sawa lakini cream bora ipo ndani ndani huko.Mfano januari ni tiss we unaona ni sawa.Mfano tu.
 
Kuna vitu vinafanywa usiri wakati hajikutakiwa kuwa vya siri, na usiri huu unaofanywa unakuta ni terget tu ya kuweka watu wao wanaowataka, na ndo maana tunapata watu wasio na weledi na wenye IQ ndogo sana kiutendaji yawezekana ni mkakati tu wa mtu. Kinachotakiwa watangaze nafasi za kazi watu waombe lakini mchakato wa kuwachukua waliokidhi vigezo ndo ufanyike kwa siri.
TISS ambao nimebahatika kuwa nao karibu, ni mavi matupu kichwani.. kama kwenye bongo zao kuna mavi badala ya brain.. kwa ufupi vyombo vyetu vya ulinzi vina vichwa maji wengi sana hata Polisi, JWTZ hali ni ilele..
 
Nyerere aliwatafuta mpaka chooni, ukada ni sawa lakini cream bora ipo ndani ndani huko.Mfano januari ni tiss we unaona ni sawa.Mfano tu.
Mi January akiwa Tiss ananihusu nini sasa. Wakati kalelewa humo humo kakulia humo humo. Nyerere aliwatafuta chooni kwa kupitia nani? Aliingia mwenyewe kwenye mashimo si kuna watu wanafanya kazi hiyo. Sasa wewe kila wakija kukufanyia vetting unaongozana na wavuta shisha, mara uko na makundi ya vichaa kidimbwi huko. Nani akuchukue? Mi naona acha waweke watu wanaoona wanafaa au kuwajua kwasababu kuingiza mamluki ni hasara kwa taifa tena vibaya sana.

Acha tu tulalamikie taasisi za ajira kuwekana wao kwa wao ila sio usalama. Kwanza wale wenyewe deep mnajua wanakotoka? Mnalalamikia hao uvccm ni ma informer tu. Kazi inafanywa na watu wenye uweledi hata kujitapa huwaskii.
 
Kila lifanywalo na wakoloni LAZIMA tuliige...

Hili nalo mkalitazame...

Au nasema uongo ndugu zangu?
Visivyotakiwa kuigwa mnaiga ila vyakuiga mnavipiga vita. Tanzania nchi yangu aisee, hata wananchi wake bado hawajitakii mema
 
Mi January akiwa Tiss ananihusu nini sasa. Wakati kalelewa humo humo kakulia humo humo. Nyerere aliwatafuta chooni kwa kupitia nani? Aliingia mwenyewe kwenye mashimo si kuna watu wanafanya kazi hiyo. Sasa wewe kila wakija kukufanyia vetting unaongozana na wavuta shisha, mara uko na makundi ya vichaa kidimbwi huko. Nani akuchukue? Mi naona acha waweke watu wanaoona wanafaa au kuwajua kwasababu kuingiza mamluki ni hasara kwa taifa tena vibaya sana.

Acha tu tulalamikie taasisi za ajira kuwekana wao kwa wao ila sio usalama. Kwanza wale wenyewe deep mnajua wanakotoka? Mnalalamikia hao uvccm ni ma informer tu. Kazi inafanywa na watu wenye uweledi hata kujitapa huwaskii.
Mkuu hao welediupatikanaji wake hautumiki siku hizi.Kwanini usikubali kwamba kuna taratibu zinapindishwa.Kwani tukisema nyerere unakuwa hujaelewa nyerere alikuwa raisi hili nalo tukufafanulie.Unauliza alienda mwenyewe kweli.
 
TISS ambao nimebahatika kuwa nao karibu, ni mavi matupu kichwani.. kama kwenye bongo zao kuna mavi badala ya brain.. kwa ufupi vyombo vyetu vya ulinzi vina vichwa maji wengi sana hata Polisi, JWTZ hali ni ilele..
Ndo maana nasema ni ngumu hii nchi kusonga mbele.
Leo hii Wachina wamekuwa machinga
 
Back
Top Bottom