Usipuuzie ulaji wa matunda. Ina faida kubwa sana kiafya

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Shukrani ziwaendee wote waliotoa mada zinazohusiana na ulaji matunda humu jukwaani. Natumaini kuna walionufaishwa na hiyo Elimu kama nami nilivyonufaika.

Nilikuwa ninafahamu kuwa ni muhimu kula matunda kila siku, lakini JF kumeniongezea maarifa na kunihamsisha kuchukua hatua stahiki.

Imeshakuwa ni kawaida yangu kula matunda kila siku. Ni nadra sana siku kupita bila kula matunda.

Kuna kipindi niliamua kutokula chakula kingine chochote, isipokuwa matunda tu, kwa wiki kama moja hivi. Ilikuwa niendelee kufanya hivyo kwa muda mrefu zaidi, lakini nilibadilisha msimamo baada ya kusoma mtandaoni kuwa kula matunda pekee kunaweza kusababisha upungufu wa baadhi ya virutibisho mwilini.

Kwa siku hizi, ratiba yangu ni kama ifuatavyo:
Ninapoamka Asubuhi, kabla ya kupiga mswaki, napata kijiko kimoja cha asali mbichi.

Baadaye, nikishapiga mswaki, napata "breakfast" ya matunda na kisha kuelekea kazini. Chai nainywa saa nne kazini.

Mchana napata lunch ya kawaida, lakini ikishafika saa kumi na mbili Jioni, nimekuwa nikikwepa kula chakula cha kawaida. Imekuwa ni nadra sana Mimi kula chakula cha kawaida kama wali, ugali, n.k. baada ya saa kumi na mbili Jioni. Nakula matunda peke yake. Na Usiku kabla ya kulala, ninapata tena kijiko kimoja cha asali.

Matunda ambayo nimekuwa nikiyala kila siku ni ndizi mbivu na machungwa. Mara nyingi nakula ndizi 2 Asubuhi na mbili Jioni, ingawa wakati mwingine nazidisha kidogo, pamoja na chungwa moja Asubuhi na moja Jioni. Lakini huwa napishanisha kwa muda ulaji wa hayo matunda: ndizi na machungwa. Siyali pamoja.

Aidha, nimekuwa pia nikila karoti mara tatu kwa wiki: Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Vile vile, nimekuwa nikila parachichi mara mbili kwa wiki.

Baada ya kutembea na hiyo ratiba kwa mwezi mmoja hivi, nimeona matokea chanya ya kiafya. Ngozi ya mwili wangu imekuwa na mng'ao mzuri wa kiafya ambao naamini ni matokeo ya ulaji wa matunda.

Si lazima ufanye kama mimi, lakini jitahidi kula matunda, ikiwezekana, kika siku. Ni muhimu sana.

Kula matunda kila siku wewe na wapendwa wako. Naamini huo ni uwekezaji mzuri wa kiafya.
 
20230901_223412.jpg
 
Mbona ni Matunda ya aina moja, Parachichi, tikiti, tango etc.... Vipi au hayapandi
Ni mazoea tu! Ila parachichi nimekuwa nikila alau mara mbili kwa wiki.

Ndizi na machungwa nimeyachagua yawe ya kila siku.

Mengine kama tikiti, nanasi, pera, tango, nimekuwa nikiyala ama wakati wa kawaida au yanapopatikana, ila hayo mawili: machungwa na ndizi ndiyo nimeamua kuyafanya ya kila siku.
 
Shukrani ziwaendee wote waliotoa mada zinazohusiana na ulaji matunda humu jukwaani. Natumaini kuna walionufaishwa na hiyo Elimu kama nami nilivyonufaika.

Nilikuwa ninafahamu kuwa ni muhimu kula matunda kila siku, lakini JF kumeniongezea maarifa na kunihamsisha kuchukua hatua stahiki.

Imeshakuwa ni kawaida yangu kula matunda kila siku. Ni nadra sana siku kupita bila kula matunda.

Kuna kipindi niliamua kutokula chakula kingine chochote, isipokuwa matunda tu, kwa wiki kama moja hivi. Ilikuwa niendelee kufanya hivyo kwa muda mrefu zaidi, lakini nilibadilisha msimamo baada ya kusoma mtandaoni kuwa kula matunda pekee kunaweza kusababisha upungufu wa baadhi ya virutibisho mwilini.

Kwa siku hizi, ratiba yangu ni kama ifuatavyo:
Ninapoamka Asubuhi, kabla ya kupiga mswaki, napata kijiko kimoja cha asali mbichi.

Baadaye, nikishapiga mswaki, napata "breakfast" ya matunda na kisha kuelekea kazini. Chai nainywa saa nne kazini.

Mchana napata lunch ya kawaida, lakini ikishafika saa kumi na mbili Jioni, nimekuwa nikikwepa kula chakula cha kawaida. Imekuwa ni nadra sana Mimi kula chakula cha kawaida kama wali, ugali, n.k. baada ya saa kumi na mbili Jioni. Nakula matunda peke yake. Na Usiku kabla ya kulala, ninapata tena kijiko kimoja cha asali.

Matunda ambayo nimekuwa nikiyala kila siku ni ndizi mbivu na machungwa. Mara nyingi nakula ndizi 2 Asubuhi na mbili Jioni, ingawa wakati mwingine nazidisha kidogo, pamoja na chungwa moja Asubuhi na moja Jioni. Lakini huwa napishanisha kwa muda ulaji wa hayo matunda: ndizi na machungwa. Siyali pamoja.

Aidha, nimekuwa pia nikila karoti mara tatu kwa wiki: Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Vile vile, nimekuwa nikila parachichi mara mbili kwa wiki.

Baada ya kutembea na hiyo ratiba kwa mwezi mmoja hivi, nimeona matokea chanya ya kiafya. Ngozi ya mwili wangu imekuwa na mng'ao mzuri wa kiafya ambao naamini ni matokeo ya ulaji wa matunda.

Si lazima ufanye kama mimi, lakini jitahidi kula matunda, ikiwezekana, kika siku. Ni muhimu sana.

Kula matunda kila siku wewe na wapendwa wako. Naamini huo ni uwekezaji mzuri wa kiafya.
Halafu baadaye unatusumbua kukuuzia vumbi la kongo
 
Mimi ni mdau wa matunda

adriz
 
Nina tatizo la kutoweza kula matunda machache, je, ina athari?!!!
Yaani nikikuta ndizi basi kama sio tano au sita si mimi huyo. Machungwa napiga hadi 10.....hiyo nazungumzia wakati mmoja tu. Kuna shida yoyote ya kiafya?
 
Hakuna yeyote aliyewahi kukatazwa asile matunda mengi wala kunywa maji ya kunywa mengi kiafya isipokuwa nyama nyekundu, chemical foods, wanga, sigara, pombe n.k.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Nina tatizo la kutoweza kula matunda machache, je, ina athari?!!!
Yaani nikikuta ndizi basi kama sio tano au sita si mimi huyo. Machungwa napiga hadi 10.....hiyo nazungumzia wakati mmoja tu. Kuna shida yoyote ya kiafya?
Sidhani kama ni tatizo. Muhimu tu yasikufanye ushindwe kula na vyakula vingine vinavyohitajika mwilini.
 
Shukrani ziwaendee wote waliotoa mada zinazohusiana na ulaji matunda humu jukwaani. Natumaini kuna walionufaishwa na hiyo Elimu kama nami nilivyonufaika.

Nilikuwa ninafahamu kuwa ni muhimu kula matunda kila siku, lakini JF kumeniongezea maarifa na kunihamsisha kuchukua hatua stahiki.

Imeshakuwa ni kawaida yangu kula matunda kila siku. Ni nadra sana siku kupita bila kula matunda.

Kuna kipindi niliamua kutokula chakula kingine chochote, isipokuwa matunda tu, kwa wiki kama moja hivi. Ilikuwa niendelee kufanya hivyo kwa muda mrefu zaidi, lakini nilibadilisha msimamo baada ya kusoma mtandaoni kuwa kula matunda pekee kunaweza kusababisha upungufu wa baadhi ya virutibisho mwilini.

Kwa siku hizi, ratiba yangu ni kama ifuatavyo:
Ninapoamka Asubuhi, kabla ya kupiga mswaki, napata kijiko kimoja cha asali mbichi.

Baadaye, nikishapiga mswaki, napata "breakfast" ya matunda na kisha kuelekea kazini. Chai nainywa saa nne kazini.

Mchana napata lunch ya kawaida, lakini ikishafika saa kumi na mbili Jioni, nimekuwa nikikwepa kula chakula cha kawaida. Imekuwa ni nadra sana Mimi kula chakula cha kawaida kama wali, ugali, n.k. baada ya saa kumi na mbili Jioni. Nakula matunda peke yake. Na Usiku kabla ya kulala, ninapata tena kijiko kimoja cha asali.

Matunda ambayo nimekuwa nikiyala kila siku ni ndizi mbivu na machungwa. Mara nyingi nakula ndizi 2 Asubuhi na mbili Jioni, ingawa wakati mwingine nazidisha kidogo, pamoja na chungwa moja Asubuhi na moja Jioni. Lakini huwa napishanisha kwa muda ulaji wa hayo matunda: ndizi na machungwa. Siyali pamoja.

Aidha, nimekuwa pia nikila karoti mara tatu kwa wiki: Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Vile vile, nimekuwa nikila parachichi mara mbili kwa wiki.

Baada ya kutembea na hiyo ratiba kwa mwezi mmoja hivi, nimeona matokea chanya ya kiafya. Ngozi ya mwili wangu imekuwa na mng'ao mzuri wa kiafya ambao naamini ni matokeo ya ulaji wa matunda.

Si lazima ufanye kama mimi, lakini jitahidi kula matunda, ikiwezekana, kika siku. Ni muhimu sana.

Kula matunda kila siku wewe na wapendwa wako. Naamini huo ni uwekezaji mzuri wa kiafya.
Hasa afya ya via vya uzazi
 
Back
Top Bottom