Utaifiti: ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, unahusishwa na matatizo ya utasa miongoni mwa wanawake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
Mwanamke akila burger na vibanzi

Maelezo ya picha,
Mwanamke akila burger na vibanzi

Mwanamke ambaye ana mazoea ya kula vyakula vyenye mafuta mengi na sukari bila ya kutumia matunda kwa wingi, yumo kwenye hatari ya kutopata uja uzito, utafiti unasema.
Utafiti uliofanyiwa wanawake 5,598, uliwapata wale ambao wana mazoea ya kula vyakula vyenye mafuta mengi, mara 4 au zaidi kwa wiki, wanachukua zaidi ya mwezi mmoja kupata uja uzito, kuliko wanawake ambao hawatumii kabisa chakula cha aina hiyo.
Walaji wengi wa chakula cha aina hiyo, pia sio rahisi kupata mimba, katika kipindi cha mwaka mzima, hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya uzazi wa binadamu.
Wataalamu wanasema kwamba, lishe bora huboresha uwezekano wa kushika mimba.
Hata hivyo, kumekuwa na changamoto fulani na utafiti huo, ukiwemo swala la wanawake kujaribu kukumbuka, kile walichokuwa wa kila wakati wana uja uzito.
Wanawake nchini Australia, New Zealand Ireland na Uingereza, waliulizwa kuhusiana na kile walichokuwa wakila mwezi mmoja kabla ya kushika mimba, hasa wakati wa mimba yao ya kwanza

Wakunga waliwatembelea kina mama hao, walipokuwa na mimba ya wiki 14 hadi 16, na wakaulizwa ni mara ngapi walikula matunda, mboga za majani na samaki, mbali na chakula kama burgers, pizza, kuku wa kukaangwa pamoja na vibanzi, kutoka katika migahawa inayouza vyakula vya mafuta mengi na sukari.
Watafiti hao walibaini kuwa, wanawake wanaotumia matunda mara tatu kwa mwezi, wanachukua kiwango cha nusu mwezi kwa wastani kushika mimba, kuliko wale ambao wamekula matunda mara tatu au zaidi kwa siku.
Pia walipiga hesabu kuwa, wanawake walio na kiwango kidogo mno cha ulaji wa matunda mwilini, wako kwenye hatari ya 12% ya kutokuwa na uwezo wa kushika mimba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja, huku hali kama hiyo ni asilimia 16% ya wale ambao wamekula chakula kilicho na mafuta mengi, mara nne au zaidi kwa wiki.
Hii kwa ujumla ni hatari kwa asilimia 8% katika kundi sawa na hilo.
Mwanamke mja mzito akinunua mboga katika duka la jumla

Maelezo ya picha,
Mwanamke mja mzito akinunua mboga katika duka la jumla

Watu waliooana hawakutumika katika utafiti huu, hasa ikiwa mpenzi wa kiume alikuwa akipokea matibabu ya uzazi.
Mhadhiri Claire Roberts, kutoka Chuo kikuu cha Adelaide, Australia, ambaye aliongoza jopo la watafiti hao, anasema: "Matokeo hayo, yanaonyesha kuwa, ulaji chakula bora, kinachojumuisha matunda na upungazaji wa chakula chenye mafuta mengi na sukari, yatapunguza pakubwa muda wa kushika mimba kwa wanawake."
Hata hivyo, huku watafiti hao wakipata uhusiano uliopo kati ya utumiaji wa matunda na chakula chenye mafuta mengi, kwa uwiano wa muda unaochukua mwanamke kutunga mimba, lakini cha ajabu utafiti wao haukupata chochote dhidi ya uhusiano wa ulaji maboga na samaki.
Daktari Gino Pecoraro, mhadhiri mkuu wa Chuo Kikuu cha Queensland, ambaye hakujumuishwa katika utafiti huo, anasema kuwa, "Kwa ujumla, utafiti huo, hauungi mkono, jinsi wataalamu wa vyakula, wanavyoamini - wanaosema kuwa vyakula vyenye lishe bora, ni vizuri kwa wanandoa kuwasaidia kupata mimba." chanzo.BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom