Usiombee kukosa hela

Mungu akubariki kwa upendo wa kweli
 
Acha kabisa kunikumbusha habari hizo. Nakumbuka 2017 nilitembea kwa mguu kutoka Kongowe hadi Feri na sikuokota hata sh.100. Lakini Mungu ni Mwema sana, disemba mwaka huo huo nilipata shavu kwenye kampuni moja ya kimataifa.
 
Kama sina pesa hata njaa inawahi kunikamata, sijui kwa nini hivi hua ni peke yangu tu maana njaa inauma hadi na kichwa kinauma
 
Ndio mkuu na Sasa nko nakunywa ka bia
Upside down Kama hzi zipo tu au nasema uongo?
Noma sana.. unakuywa bia unajichekesha sanaaa story mingi ukiwa na tumaini jamaa anaenunua atakutoa ata mi5 ya kuanzia kesho
af hola..
 
Yani achatu Mzee nilikua nimebakiwa na buku nikaona Acha niibetie nikapanga na malengo kabisa sasa buku imeliwa nimebaki napiga miyayo tuu nawaza yanini nimebeti
 
Halafu ukiwa hauna hela kichwa kinawasha bila sababu sijui inakua chawa zishaingia maana utajikuta unajikuna nusu ung’oe nywele yaani ilimradi tu usumbuke si unajua maskini lazima apate usumbufu
 
Usiombe kuishiwa..kunasiku nilitoka dar na gari private nakwenda bunda..hela niliokua nayo nikajua itanifikisha tu.. basi kufika igunga ile naitafuta nzega pale kulikua na mashimo mashimo basi tairi moja ika burst ikabidi niweke spear tairi..kufika ziba ile tairi ya spear ikapasuka nayo..hapo ni usiku..nikiangalia mfukon nina kilo tu..nikalala hapo asubuhi nikajangaikia tairi nikapata kwa 80k maana zile tair zilionekana hazifai..hapo mfukon nikawa nina buku 5 tu..jion ndo nimeondoka hapo ziba maana ilikua jpil so kupata tair ilikua mbinde so nilichelewa kuondoka..nafika magu usiku na taa imewaka kwa maana mafuta yanakata na sina hela na safar bado..nikasema ngoja nilale hapa magu..nikaingia kwa mama ntilie nikala..nikalala kweye gari kulipokucha hyo j3 ndo nawaza napata wap hela ya mafuta…?nikakumbuka kuna mshkaj anafanya kaz bank nmb..nikaenda bahat nikamkuta baada ya kumpa stori akasema yeye hana hela ila atanipa mafuta ya ofis kama lita 20 hv nikasema we nipe yatakapo ishia hapo hapo.. ashkuru nilifika bunda ila hakuna issue mbovu kama kuishiwa unaona kama dunia haipo upande wako hv
 
Tuko wengi ila tutafutane siku moja moja nakuwa mungu anasaidia 2000 naweza kukupa
 
Mm nimeshawah saidiwa mtaji na mtu anayeitwa Silicon Valley kifup jf inawatu wema bado wapo humu

Barikiwa mkuu bado napambana na mtaj ulionipa
 
Very risk..yaan unasafiri huna hela? Kwann ulienda sasa na gari? Si ungepanda najimunisa tu
 
Sijui kwanini maranyingi unakuta mtu anakulilia shida wakati ambao wewe mwenyewe hauko poa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…