Binafsi naishukru sana JF, kuna miezi nilikuwa nimeishiwa kabsa mda huo biashara ilikuwa imekwama at the same time nadaiwa pesa ya Pango la frame sh 210,000 afu kule ninapoishi napo nadaiwa hela ya pango ya miezi 4
Sehemu zote hizo wamecharuka hawataki tena excuses, asbh nilipoamka tu nakutana na sms inasema " habari yako John kama itafika jioni hujalipa kodi yangu uje kuhamisha vitu vyako"
Mda huo nilikuwa nimejifungia ndani sioni pa kwenda, ghafla likaja wazo la kuandika uzi humu JF, nikaandika nikiwa na uchungu sanaaa, wakatokea watu watatu wa kunifariji ( DM) kwa kunitia moyo Ila mmoja wao akanitumia pesa sh 420,000 aiseee machozi yalinitoka maana sikuamini kabsa
Hii ilikuwa ni mwaka Jana tu mwezi wa 10, 2020 nilienda kwa wakala na kuitoa baada ya hapo nilakipia kodi na nikaagiza mzigo, to cut the story namshukuru sana yule ndugu japo simjui hata kwa sura mpaka sasa
Nipo naendelea na biashara yangu, na huwa namsalimia Mara kwa Mara sana kupitia DM, afu leo ngoja nimtumie hela ya soda aiseee