Kaka acha tu. Kwenye maisha kila mtu ana yake Moyoni aliyopitia. Nimepitia Magumu. Nishatokaga Kariakoo mpaka Kinondoni A kwa Miguu. Kariakoo nilifuata Mchongo wa kazi lakini sikumkuta alieniahidi. Nikaunga Kinondoni nako nikapewa Kisomo tu.
Nikarudi home Magomeni nipo hoi.
Niliacha Vitumbua Geto nikachemsha Chai na Vitumbua nikanywa nikalala.
Kuna muda huwa nikimfikiria Mungu we acha tu. Nipo First World, eti na mimi sasa hivi nikija Africa Nadinya wanawake wenye hadhi zao, wenye kazi nzuri, wenye kipato, Dah!! Maisha yana siri nyingi sana Kwa sisi Maskini.
Yote Kwa yote kwenye maisha ni marufuku kukata tamaa.