Usiombee kukosa hela

Usiombee kukosa hela

haya maisha haya, kuna wakati mate yalinidondoka kwa kutamani chakula alichokuwa anakula mtoto wa jirani yangu, baada ya kushinda njaa takribani siku nne,yaani sikuwa na hata mia mbovu.

namwomba Mungu nisirudi nilipotoka.
Usikute ulikuwa na hangover baada ya kunywa pombe bila kula. Jokin
 
Daaah, mzee umegusa mule mule. Mm hapa tangu juzi nimefagia nyumba nimefua nguo ila nimejikuta nimeambulia 250tsh. Hapa naviazi nimechemsha vinasiku tano nakula kimoja kimoja. Daaah, hii hatari. Nakula wali bila mboga nikimaliza nashushia maji ya moto sio chai tena. Unapigika hadi unamwita Mungu alafu unacheka hata kuomba unashindwa. Yani hiki kindoo cha mchele kikiisha kabla ya tarehe 25 nitaumbuka kabisa
 
FB_IMG_1618081445554.jpg
 
Mm siombi hela home. Nakaza hivi hivi hadi nione nitakufa nikila wali na maji. Ila nimepata somo nikipata mtonyo ni mwendo wakujaza misosi na kutunza hela tu marufuku kutoa hela kizembe. Hata bodaboda sipandi tena maishani mwangu, sitakula tena mgahawani sababu sehemu unakula kila siku alafu siku huna hela mwenye hotel anakwambia umekuja mapema sana mm sikopeshagi wateja mapema sababu siku nzima itakua wateja wanakopa tu. Daaah, sitafanya makosa tena.
 
Niliwahi shinda njaa siku mbili Sina hata Mia ,
Afu nilikuwa nafanya special exam so washikaji wengi wameenda kwao,
ghafla watot wa jirani wakanambia uncle mama alinunua vitumbua asubuhi ,

Dah nilivila kwa uzuni kinoma nikashushia na maji ,
Kesho yake asubuhi kwenye paper,
Cha kusikitisha mbaka saizi hali ni hovyo.

Umasikini ni mazafaka
FB_IMG_1617348721601.jpg
 
Haya maisha yana mambo mengi sana.kipindi hichoo nkiwa chuo ilikiwa ikikaribia mwisho wa semester nimeishiwa kabisa yan nina pesa ya kula jioni tu.Nlikuwa naingia kwenye vipindi mwisho saa sita.kuanzia huo muda naenda kulala had saa 11 hv jion naamka nianze maandalizi ya kwenda kula wali njegere pale cafeteria dahh.Hadi sasa hv nikiishiwa huwa nalala tu sitamani kwenda popote.Mungu akutie nguvu maana kuishiwa hata pesa kidogo tu ya kutumia huwa inaumiza sana
 
Kuna kipindi nlitoka mkoani kuja Dsm kwa interview.Nlitakiwa kufikia kwa ndugu yangu mmja hv.Mwanzoni alikuwa anaishi Riverside ila akahamia kwake Goba.nikafika Dsm muda wa saa moja.Mfukoni nina sh elf mbili nkaenda hadi mawasiliano nkapanda daladala.dah nkashuka kituo nlichoambiwa.mwenyeji wangu akaniambia chukua bajaji alaf nipe simu niongee na dereva.Hapo moyo wangu unadunda ntamlipa na nin na hela sina.Nkafanya kama alivyonambia akamwagizia dereva bajaj.Tulipofika mahali napotakiwa kushuka nkamuuliza dereva nauli sh.ngapi,akanijibu ni elf nne.Dah nkamwambia nnayo kwa mpesa nisubiri nitoe.nikaenda kwa wakala nikasongesha nikampa.Niliumia sana hiyo siku.Kukosa pesa ni kubaya sana Mungu akamsaidie kila anayepitia magumu
 
4 days nakula kalanga mbichi zile za maganda,hadi ikafika time nikienda chooni nakunya karanga tu.

kuna kipindi pia niliwahi kuishiwa kabisa week nzima natembea kwa miguu home hadi kazini kilometa 15 nilikua naponea kazin kwasabab chai na andaz ilikua bure.

Kuna kipindi tena niliwahi kuishiwa njaa inauma siku zaid ya 3 nakunywa chai tu asubuh, sikuhio usiku saa 3 nikaamka nikajiambia ngoja nikazurure, njiani nikawa nina sali kama naongea na Mungu ila sauti inanitoka, tena maombi ya kummaindi Mungu kwanini ananipitisha ktk magumu wakat kuna watu wa hovyo wanakula bata.

Kuna eneo lina makaburi mengi sana na ni usiku panatisha hakuna mtu anaepita, kwa hasira nikasema nakatisha katkat ya haya makaburi nikatokee barabara ya rami... Mungu wa ajabu sana ile namalizia kupita makaburi nikajiambia embu ngoja niwashe tochi ya cm yangu... Huwez amini niliona Elfu10 ipo katkat ya njia, niliiokota nikamshukur sana Mungu.

Kuna kipindi kingine pia nimeishiwa sina hata mia nazurura mjini usiku wa saa4 nikaokota Elfu1 tu nikapitiliza moja kwa moja mgahawani nikala nikamshukur Mungu...

Kuna watu hawayajui haya maisha wanaona ni story tu, ila muombe sana Mungu usiyapitie 😭
Namshukur Mungu nimeyasahau hayo maisha, vihela havinipigi chenga tena...
 
Mm siombi hela home. Nakaza hivi hivi hadi nione nitakufa nikila wali na maji. Ila nimepata somo nikipata mtonyo ni mwendo wakujaza misosi na kutunza hela tu marufuku kutoa hela kizembe. Hata bodaboda sipandi tena maishani mwangu, sitakula tena mgahawani sababu sehemu unakula kila siku alafu siku huna hela mwenye hotel anakwambia umekuja mapema sana mm sikopeshagi wateja mapema sababu siku nzima itakua wateja wanakopa tu. Daaah, sitafanya makosa tena.
Ha ha ha
 
Da yaan hapa nimekumbuka wakati nimetoka mkoani kuja dar kufanya biashara baada ya kupewa michongo ya biashara hiyo nlikuja na mtaji wangu wa kutosha kabisa kwa hiyo biashara nikiwa nimeacha familia mkoa ili niweke mazingira sawa kisha wanifuate kweli baada ya kukutana na wadau kadhaa ambao ni madalali wa mzigo ninaotaka kufanyia mchakato nikaagiza mzigo nikamkabidhi dalali sikuamini siku ambayo tulikubaliana na dalali mzigo utakua umeisha ili anikabidhi changu dalali akaumwa akalazwa hapo ndio ngoma ilipoanzia sikua na mia hela ikajikuta imeteketea mkoa nadaiwa ada nadaiwa kodi mwenyewe hapo nna Siku kama tatu nashindia maji nalalia maji phone book haina msaada tena maana ushapiga ukware wa kutosha
 
Back
Top Bottom