Usiogope wanavyomshangilia

Usiogope wanavyomshangilia

UNAUMIA JINSI WANAVYOMSHANGILIA? NISIKILIZE MIMI.

Baada ya Idd Amin kumpindua aliyekuwa Rais wa Uganda (Milton Obote) kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kueneza propaganda kwa wananchi wa Uganda ili wampende.

Inaaminika kuwa kati ya Madikteta wataalamu katika ushawishi ni pamoja na Idd Amin Dadaa,
Alikuwa ana uwezo wa ajabu sana katika kupepeta mdomo huku akijiamini sana.

Ghafla wananchi wa Uganda walianza kumpenda na kumuona mkombozi wao, kila aliyeinuka kumpinga alitengenezewa propaganda za uongo na hatimaye kuonekana sio mzalendo.

Yeyote aliyesimama kumkanusha wananchi walikuwa tayari kumpiga hata mawe.

Kwakuwa alitengeneza mazingira ya kusikilizwa yeye peke yake ilikuwa rahisi kwake kusema uongo.

Alitunga uongo mwingi na kuumwaga kwa wananchi ili wampende huku akimzuia yeyote kuinuka kwa lengo la kumkanusha.

Hata pale wasomi walipoonya kuhusu masuala kadhaa hususani ya kiuchumi waligeuka kuwa maadui zake.

Mfano ni pale alipomuua gavana wa Benki kuu kwa kosa la kumwambia kuwa fedha hamna na hali ya uchumi ni mbaya.

Katika kutafuta uungwaji mkono na wananchi alidiriki hata kutengeneza matatizo na kuyatatua ili aonekane ni Rais anayejali.

Kwa mfano anapokuwa kwenye ziara zake humuandaa mtu atakayedanganya kuwa ni mgonjwa alafu anamlilia akiomba msaada kwa Rais na hapo utamuona Idd Amin anaandika cheki hapo hapo na kumpatia akatibiwe kumbe yote ni maigizo.

Katika matukio kama hayo wananchi hujikuta wanamshangilia huku wakimuona ni mwenye huruma.

Wakati mwingine alikuwa anawaua baadhi ya wapinzani wake hata wale waliokuwa waandamizi kwenye serikali yake huku akiwa wa kwanza kumwaga machozi wakati wa misiba ya aliowaua.

Mfano ni Pale alipomuua waziri wake wa Afya na kisha kulia machozi huku akitangaza kiama kwa waliofanya tukio lakini baadae ilibainika kuwa kichwa cha waziri huyo kilikuwa kwenye Jokofu la Amin huko kwake. Yaani amemla nyama.

Pamoja na propaganda zote na maigizo kibao bado wapo watu waliokuwa ni waaminifu kwa Milton Obote wakiwemo maaskari na wanajeshi pia...

THE LAST KING OF SCOTLAND...

Hii ni Movie iliyoigiza maisha ya Idd Amin na kupata tuzo nyingi kuliko movie zote zilizomuigiza Amin kwani ilikuwa ni kama uhalisia kwa wale waliowahi kumfahamu Idd Amin Dadaa.

Movie hii ina kijana aliyeitwa Nicholas Gharigan ambaye anakuja Uganda kujitolea kufanya huduma ya kidaktari katika nchi maskini za Afrika.

Alipotua Uganda anapokelewa na Daktari mwingine ambaye anakuwa kama mwenyeji wake kwani japokuwa naye pia ni mzungu lakini yeye ameshalowea kwa muda kiasi ndani ya Uganda naye akitoa huduma za tiba.

Wakiwa kwenye pitapita zao wakakutana na watu wakiwa wanajiandaa kwa kuimba nyimbo na shamrashamra kibao.

Dr Nicholaus Gariggan akamuuliza mwenyeji wake. Kulikoni?

Alijibiwa kuwa wanajiandaa kumpokea Rais Amin kwani anakuja hapo kijijini siku hiyo.

Dr Garigan aliomba wabaki kidogo ili nao wamuone huyo Amin.

Baada ya muda kidogo Gari nyingi zilianza kuingia pale huku watu wakimwagika kwa nderemo na vifijo huku vumbi likitimka kwa nyimbo na kucheza.
Ngoma zilisikika huku msafara wa magari ukiendelea kumiminika.

Baadae Jitu kubwa, Refu,Jeusi lililovalia mavazi ya Kijenerali wa Jeshi lilipanda jukwaani huku likishangiliwa kwa nguvu mnooo....

Uganda hoyeeeeeeee
Hoyeeeeeeee...

Ni sauti ya Amin akiwasalimu watu wa kijiji kile.

Butwaa lilimshika Dr Garigan ambaye ilibidi amuulize mwenyeji wake...

"Hivi wanampenda sana huyu Raisi eeenh"

Jibu alilojibiwa ni kwamba...

"Hata Obote akija wanamshangilia hivi hivi"

Hivyo basi...

USISHTUSHWE NA JINSI WANAVYOMSHANGILIA!
Yaani vilevile... Du!
 
Unataka kutwambia nini sasa. Kufananisha nini
 
Waganda wenyewe wanakwambia museveni ameua watu wengi kuliko idd amin
Hilo watu hawalioni mkuu, watu wakikuchukia watakupa majina yote mabaya. Gaddafi na Sadam Hussein waliitwa madicteta katili waliokua wanachinja watu wao. Leo hii majeshi 'pendwa ya ukombzi' ya nchi za Magharibi uameua maradufu zaidi ya hao 'madikteta' na wezivuruga kabisa nchi hizo
 
bavicha wapika majungu Katika ubora wao.
 
1. Serikali hii ya JK Ni dhaifu, nchi inahitaji Raisi dikteta ili isonge mbele - Mnyika
Dikteta kwenye nini??ninyi watu wagumu sana kuelewa dhana ya upinzani kuhitaji raisi dikteta kifupi hatukuhitaji raisi asiyeshaurika,anaepuuza katiba na sheria ya vyama vingi,anaependa asikike yeye tu wengine hapana,anaependelea ukanda,anaependa vyombo vya habari vimwongelee yeye tu tena kwa kumsifia kinyume chake vinafungiwa,raisi mwenye upendeleo wa wazi wa watu anaowapenda sana(Bashite)ni mfano wa pekee,anaezima bunge live bila sababu za msingi,mwenye vitisho kwa wafanya biashara na wawekezaji(kubadilisha noti na kuishi kishetani)mwenye hasira na ubabe ambao hata hauna sababu,asieheshimu mihimili mingine ya dola,yule ambae watu hupotea na wasionekane tena,yule ambae miili ya watu waliokufa vifo vya mateso na kuokotwa baharini na watawala hawasemi chochote juu ya jambo hilo,Asieheshimu mikataba ya kimataifa ya utawala bora na misingi ya haki za binadamu HUYO HATUMUHITAJI KAA NAE MWENYEWE HUTUKUMAANISHA HIVYO.
 
Hilo watu hawalioni mkuu, watu wakikuchukia watakupa majina yote mabaya. Gaddafi na Sadam Hussein waliitwa madicteta katili waliokua wanachinja watu wao. Leo hii majeshi 'pendwa ya ukombzi' ya nchi za Magharibi uameua maradufu zaidi ya hao 'madikteta' na wezivuruga kabisa nchi hizo
Ila hawakuwa madikteta... au sio
 
Hilo watu hawalioni mkuu, watu wakikuchukia watakupa majina yote mabaya. Gaddafi na Sadam Hussein waliitwa madicteta katili waliokua wanachinja watu wao. Leo hii majeshi 'pendwa ya ukombzi' ya nchi za Magharibi uameua maradufu zaidi ya hao 'madikteta' na wezivuruga kabisa nchi hizo
kwahiyo kuua ni sawa mbwa
 
Back
Top Bottom