Usiogope wanavyomshangilia

Usiogope wanavyomshangilia

UNAUMIA JINSI WANAVYOMSHANGILIA? NISIKILIZE MIMI.

Baada ya Idd Amin kumpindua aliyekuwa Rais wa Uganda (Milton Obote) kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kueneza propaganda kwa wananchi wa Uganda ili wampende.

Inaaminika kuwa kati ya Madikteta wataalamu katika ushawishi ni pamoja na Idd Amin Dadaa,
Alikuwa ana uwezo wa ajabu sana katika kupepeta mdomo huku akijiamini sana.

Ghafla wananchi wa Uganda walianza kumpenda na kumuona mkombozi wao, kila aliyeinuka kumpinga alitengenezewa propaganda za uongo na hatimaye kuonekana sio mzalendo.

Yeyote aliyesimama kumkanusha wananchi walikuwa tayari kumpiga hata mawe.

Kwakuwa alitengeneza mazingira ya kusikilizwa yeye peke yake ilikuwa rahisi kwake kusema uongo.

Alitunga uongo mwingi na kuumwaga kwa wananchi ili wampende huku akimzuia yeyote kuinuka kwa lengo la kumkanusha.

Hata pale wasomi walipoonya kuhusu masuala kadhaa hususani ya kiuchumi waligeuka kuwa maadui zake.

Mfano ni pale alipomuua gavana wa Benki kuu kwa kosa la kumwambia kuwa fedha hamna na hali ya uchumi ni mbaya.

Katika kutafuta uungwaji mkono na wananchi alidiriki hata kutengeneza matatizo na kuyatatua ili aonekane ni Rais anayejali.

Kwa mfano anapokuwa kwenye ziara zake humuandaa mtu atakayedanganya kuwa ni mgonjwa alafu anamlilia akiomba msaada kwa Rais na hapo utamuona Idd Amin anaandika cheki hapo hapo na kumpatia akatibiwe kumbe yote ni maigizo.

Katika matukio kama hayo wananchi hujikuta wanamshangilia huku wakimuona ni mwenye huruma.

Wakati mwingine alikuwa anawaua baadhi ya wapinzani wake hata wale waliokuwa waandamizi kwenye serikali yake huku akiwa wa kwanza kumwaga machozi wakati wa misiba ya aliowaua.

Mfano ni Pale alipomuua waziri wake wa Afya na kisha kulia machozi huku akitangaza kiama kwa waliofanya tukio lakini baadae ilibainika kuwa kichwa cha waziri huyo kilikuwa kwenye Jokofu la Amin huko kwake. Yaani amemla nyama.

Pamoja na propaganda zote na maigizo kibao bado wapo watu waliokuwa ni waaminifu kwa Milton Obote wakiwemo maaskari na wanajeshi pia...

THE LAST KING OF SCOTLAND...

Hii ni Movie iliyoigiza maisha ya Idd Amin na kupata tuzo nyingi kuliko movie zote zilizomuigiza Amin kwani ilikuwa ni kama uhalisia kwa wale waliowahi kumfahamu Idd Amin Dadaa.

Movie hii ina kijana aliyeitwa Nicholas Gharigan ambaye anakuja Uganda kujitolea kufanya huduma ya kidaktari katika nchi maskini za Afrika.

Alipotua Uganda anapokelewa na Daktari mwingine ambaye anakuwa kama mwenyeji wake kwani japokuwa naye pia ni mzungu lakini yeye ameshalowea kwa muda kiasi ndani ya Uganda naye akitoa huduma za tiba.

Wakiwa kwenye pitapita zao wakakutana na watu wakiwa wanajiandaa kwa kuimba nyimbo na shamrashamra kibao.

Dr Nicholaus Gariggan akamuuliza mwenyeji wake. Kulikoni?

Alijibiwa kuwa wanajiandaa kumpokea Rais Amin kwani anakuja hapo kijijini siku hiyo.

Dr Garigan aliomba wabaki kidogo ili nao wamuone huyo Amin.

Baada ya muda kidogo Gari nyingi zilianza kuingia pale huku watu wakimwagika kwa nderemo na vifijo huku vumbi likitimka kwa nyimbo na kucheza.
Ngoma zilisikika huku msafara wa magari ukiendelea kumiminika.

Baadae Jitu kubwa, Refu,Jeusi lililovalia mavazi ya Kijenerali wa Jeshi lilipanda jukwaani huku likishangiliwa kwa nguvu mnooo....

Uganda hoyeeeeeeee
Hoyeeeeeeee...

Ni sauti ya Amin akiwasalimu watu wa kijiji kile.

Butwaa lilimshika Dr Garigan ambaye ilibidi amuulize mwenyeji wake...

"Hivi wanampenda sana huyu Raisi eeenh"

Jibu alilojibiwa ni kwamba...

"Hata Obote akija wanamshangilia hivi hivi"

Hivyo basi...


USISHTUSHWE NA JINSI WANAVYOMSHANGILIA!

Hawa watu watakua na undugu, sema mmoja mfupi mwingine mrefu.
 
No worry, I will do that
Ni No worries Mkuu just saying...... what will you do? Kuweka kwenye mifuko ukatupe baharini au? Tusaidie kwa hili Mkuu!
Your first reply umesema Rubbish kwani hakuwa Iddi Amini au ulitaka Mtoa mada abadilishe jina aweke la nani anayefanana na ukweli huu? Tusaidie turekebishe
 
Ni No worries Mkuu just saying...... what will you do? Kuweka kwenye mifuko ukatupe baharini au? Tusaidie kwa hili Mkuu!
Your first reply umesema Rubbish kwani hakuwa Iddi Amini au ulitaka Mtoa mada abadilishe jina aweke la nani anayefanana na ukweli huu? Tusaidie turekebishe
Kipi unahitaji kuhusu rubbish yenu?
 
IDD Amini alikua na mabaya yake mengi lakini pia mengi dhidi yake yalikua ni propaganda chafu na uwongo dhidi yake kama hilo la kula nyama za watu. Hiyo movie The Last King Of Scotland ina exaggerations nyiingi tu zingine kweli zingine uongo. Kama ni kupata tuzo nyingi inaeleweka nchi za magharibi hazikumpenda kabisa mtu huyu na wazungu wakikuchukia mambo yako yote huwa mabaya na atakaekuchafua watampa tuzo lukuki. Wapo watu Uganda tena kwa mamilioni wanamkumbuka kwa mazuri Idd Amini Dadda
Waulize wakutajie Mazuri yapi aliyofanya kafiri huyu.Hata moja tu.Hazikuwa propaganda ndo alivokuwa akitegemea nguvu za giza. Kaacha makovu mengi sana hata hawakutaka mzoga wake uje kuzikwa kule ungeleta laana ya udhalili alowatendea waja,kamwaga damu nyingi sana zisizo na hatia,utadhani angeishi milele,kumpa masikini dhima kubwa ya kuamua hatma maisha ya watu hakujawahi iacha jamii hio salama, mtu masikini huwa na mawazo ya kimasikini ya kujikweza Kwa maisha yapitayo km alivo amini.
 
Ukiwa mshirikina lazima ule nyama za watu,km moja ya kanuni zao
 
Hakuna kitu kama hicho ndugu, Major General Mayunga au Kamanda Mti Mkavu ambaye alikua jemedari hasa wa vita na ninamuheshimu sana aliwahi kumuelezea huyu mtu sababu walisoma wote kwenye chuo cha jeshi Kenya. Kubwa alilosema ni kwamba Amin alikua mtu matata na akipenda sana presence yake iwe noticed popote atakapokua, na atafanya hivo kwa kufanya vitu vya kibabe(aliwahi kua bondia). Mambo mengine kama ukatili na kuua sikatai kua alifanya kama ambavyo viongozi/watawala wengi tu wa Afrika walifanya kwa maadui zao kisiasa kwa wazi au kimyakimya.
Kama ambavyo na wewe huwezi kunithibitishia kama alikua anakula nyama za watu na mimi siwezi kukuthibitishia kinyume chake. Kwamba General Mayunga RIP aliwahi kusema hivo ni propaganda tu za vita, vinginevyo tuamini pia eti wakati flani alikua akibadilika na kua joka kubwa, maana na hilo nalo tuliambiwa!
Idd Amin alikua ni dictator, mtawala katili na mwenye vituko lakini kuna mengine meengi alizushiwa kama mbinu na hamasa za kivita. Uliza kwa Waganda walio iishi historia yake na wasio biased wakueleze

Kwangu mimi siwezi kukataa kuwa Idd Amin hakuwa Lucifer incarnate, na kama ni hivyo kula nyama za watu ni inevitable. Na kula nyama za watu kwako wewe ni jambo baya ila kwake ni nguvu ya ushetani ya kuimarisha utawala wake.

Shetani/Joka aliyekuwa anakaa ndani ya mwili wake na ambaye alikuwa anaendesha taifa la Uganda ndiye aliyekuwa anademand damu kama kafara, so its normal, at least for me who knows the spiritual world.

Kuna watawala kwenye biblia ambao walikuwa ni nje mtu ndani devil kabisa. Mfano ni mfalme wa Tiro mashariki ya kati ambaye Mungu alimuonesha nabii Ezekiel kuwa ni Kerubi aliyeasi mbinguni (Lucifer) akatupwa duniani.

Mungu alimwonesha nabii Ezekiel kuwa huyo unayemuona kwa nje kama mfalme wa taifa la Tiro actually ni shetani amevaa sura ya mwanadamu. Kwa home work soma Ezekiel 28:12-19
 
Mkuu kama unataja last king of scotland hautasita kujua misimamo ya forest whitaker anaamini idd amin hakuwa dikteta

hao wamarekani mpaka nyakati ambazo waingereza wanamwita idd amin dikteta wao walikuwa wananunua kahawa kwake

utaumia sana kuona magufuli anashangiliwa kwa sababu hamjataka kujadili kwa uhuru, anayesema kinyume chenu mtamwita lumumba au buku 7 au msaliti au ccm...

hampati muda wa kukaa na kuelewa filosofia ya wakati huu, kuna vitu vizuri magufuli anavifanya na kuna vitu anakosea na ni kawaida sana tu

sasa wewe na wenzako mmejiweka upande wa chuki tena chuki isiyoisha, kuwa magu apatie au akosee nyie ni chuki tu

sasa leo unaona uchungu anaposhangiliwa na watu!! unaumia na utaumia kwa miaka 8 ijayo...imagine....kwa sababu unaumia unajipa faraja kwa kuandika post kama hizi isssshhh, so so sad

angalia hapa msimamo wa forest whitaker Idi Amin was not so bad, says US actor
Sijamtaja magufuli sehemu yeyote. Take care!
 
Wa sasa anamzid id amini. Sijawahi kumwona kiongoz mwongo kama wa kwetu. Tena hana aibu kabisaaa!!
 
Wakati mwingine alikuwa anawaua baadhi ya wapinzani wake hata wale waliokuwa waandamizi kwenye serikali yake huku akiwa wa kwanza kumwaga machozi wakati wa misiba ya aliowaua.

Kwa sababu hujataja jina imekuwa vigumu kujua unamaanisha ni nani. Unajua hata Sokoine alipofariki yalimwaga machozi mengi.
 
Kweli uandishi ni kipaji.Stori ndefu lakini haichoshi kusoma, inabidi uungane na Paschal Mayalla naye pia yuko vizuri kwenye flow ya uandishi.Pongezi Mjema
 
Hii nayo ni propaganda nyingine, hivi Amini ulimjua au hadithi za kusadikika ulizokua unahadithiwa na wabaya wake, endelea kudanganya wasio na akili
 
IDD Amini alikua na mabaya yake mengi lakini pia mengi dhidi yake yalikua ni propaganda chafu na uwongo dhidi yake kama hilo la kula nyama za watu. Hiyo movie The Last King Of Scotland ina exaggerations nyiingi tu zingine kweli zingine uongo. Kama ni kupata tuzo nyingi inaeleweka nchi za magharibi hazikumpenda kabisa mtu huyu na wazungu wakikuchukia mambo yako yote huwa mabaya na atakaekuchafua watampa tuzo lukuki. Wapo watu Uganda tena kwa mamilioni wanamkumbuka kwa mazuri Idd Amini Dadda
Waganda wenyewe wanakwambia museveni ameua watu wengi kuliko idd amin
 
IDD Amini alikua na mabaya yake mengi lakini pia mengi dhidi yake yalikua ni propaganda chafu na uwongo dhidi yake kama hilo la kula nyama za watu. Hiyo movie The Last King Of Scotland ina exaggerations nyiingi tu zingine kweli zingine uongo. Kama ni kupata tuzo nyingi inaeleweka nchi za magharibi hazikumpenda kabisa mtu huyu na wazungu wakikuchukia mambo yako yote huwa mabaya na atakaekuchafua watampa tuzo lukuki. Wapo watu Uganda tena kwa mamilioni wanamkumbuka kwa mazuri Idd Amini Dadda
Hicho ndicho nilichomwambia huyu mpiga tarumbeta, swala la kula nyama za watu ilikua hadithi ya kusadikika tu, huyu mfipa anajaribu nae kutulisha propaganda
 
Back
Top Bottom