Usiogope wanavyomshangilia

Usiogope wanavyomshangilia

Mmh wakati naisoma hii thread kuna vipicha Fulani vya mtu asiefahamika vilikuwa vinapita kichwani, kuna baadhi ya taswira za vitu na matukio yalikuwa yanapita kama filamu hivi!!!! Anyway ntaimalizia baadae kuisoma maana Leo huku kagera kuna ziara za mh.ngoja nikamsikilize kwanza
 
UNAUMIA JINSI WANAVYOMSHANGILIA? NISIKILIZE MIMI.

Baada ya Idd Amin kumpindua aliyekuwa Rais wa Uganda (Milton Obote) kazi kubwa aliyokuwa nayo ni kueneza propaganda kwa wananchi wa Uganda ili wampende.

Inaaminika kuwa kati ya Madikteta wataalamu katika ushawishi ni pamoja na Idd Amin Dadaa,
Alikuwa ana uwezo wa ajabu sana katika kupepeta mdomo huku akijiamini sana.

Ghafla wananchi wa Uganda walianza kumpenda na kumuona mkombozi wao, kila aliyeinuka kumpinga alitengenezewa propaganda za uongo na hatimaye kuonekana sio mzalendo.

Yeyote aliyesimama kumkanusha wananchi walikuwa tayari kumpiga hata mawe.

Kwakuwa alitengeneza mazingira ya kusikilizwa yeye peke yake ilikuwa rahisi kwake kusema uongo.

Alitunga uongo mwingi na kuumwaga kwa wananchi ili wampende huku akimzuia yeyote kuinuka kwa lengo la kumkanusha.

Hata pale wasomi walipoonya kuhusu masuala kadhaa hususani ya kiuchumi waligeuka kuwa maadui zake.

Mfano ni pale alipomuua gavana wa Benki kuu kwa kosa la kumwambia kuwa fedha hamna na hali ya uchumi ni mbaya.

Katika kutafuta uungwaji mkono na wananchi alidiriki hata kutengeneza matatizo na kuyatatua ili aonekane ni Rais anayejali.

Kwa mfano anapokuwa kwenye ziara zake humuandaa mtu atakayedanganya kuwa ni mgonjwa alafu anamlilia akiomba msaada kwa Rais na hapo utamuona Idd Amin anaandika cheki hapo hapo na kumpatia akatibiwe kumbe yote ni maigizo.

Katika matukio kama hayo wananchi hujikuta wanamshangilia huku wakimuona ni mwenye huruma.

Wakati mwingine alikuwa anawaua baadhi ya wapinzani wake hata wale waliokuwa waandamizi kwenye serikali yake huku akiwa wa kwanza kumwaga machozi wakati wa misiba ya aliowaua.

Mfano ni Pale alipomuua waziri wake wa Afya na kisha kulia machozi huku akitangaza kiama kwa waliofanya tukio lakini baadae ilibainika kuwa kichwa cha waziri huyo kilikuwa kwenye Jokofu la Amin huko kwake. Yaani amemla nyama.

Pamoja na propaganda zote na maigizo kibao bado wapo watu waliokuwa ni waaminifu kwa Milton Obote wakiwemo maaskari na wanajeshi pia...

THE LAST KING OF SCOTLAND...

Hii ni Movie iliyoigiza maisha ya Idd Amin na kupata tuzo nyingi kuliko movie zote zilizomuigiza Amin kwani ilikuwa ni kama uhalisia kwa wale waliowahi kumfahamu Idd Amin Dadaa.

Movie hii ina kijana aliyeitwa Nicholas Gharigan ambaye anakuja Uganda kujitolea kufanya huduma ya kidaktari katika nchi maskini za Afrika.

Alipotua Uganda anapokelewa na Daktari mwingine ambaye anakuwa kama mwenyeji wake kwani japokuwa naye pia ni mzungu lakini yeye ameshalowea kwa muda kiasi ndani ya Uganda naye akitoa huduma za tiba.

Wakiwa kwenye pitapita zao wakakutana na watu wakiwa wanajiandaa kwa kuimba nyimbo na shamrashamra kibao.

Dr Nicholaus Gariggan akamuuliza mwenyeji wake. Kulikoni?

Alijibiwa kuwa wanajiandaa kumpokea Rais Amin kwani anakuja hapo kijijini siku hiyo.

Dr Garigan aliomba wabaki kidogo ili nao wamuone huyo Amin.

Baada ya muda kidogo Gari nyingi zilianza kuingia pale huku watu wakimwagika kwa nderemo na vifijo huku vumbi likitimka kwa nyimbo na kucheza.
Ngoma zilisikika huku msafara wa magari ukiendelea kumiminika.

Baadae Jitu kubwa, Refu,Jeusi lililovalia mavazi ya Kijenerali wa Jeshi lilipanda jukwaani huku likishangiliwa kwa nguvu mnooo....

Uganda hoyeeeeeeee
Hoyeeeeeeee...

Ni sauti ya Amin akiwasalimu watu wa kijiji kile.

Butwaa lilimshika Dr Garigan ambaye ilibidi amuulize mwenyeji wake...

"Hivi wanampenda sana huyu Raisi eeenh"

Jibu alilojibiwa ni kwamba...

"Hata Obote akija wanamshangilia hivi hivi"

Hivyo basi...


USISHTUSHWE NA JINSI WANAVYOMSHANGILIA!

Mkuu kama unataja last king of scotland hautasita kujua misimamo ya forest whitaker anaamini idd amin hakuwa dikteta

hao wamarekani mpaka nyakati ambazo waingereza wanamwita idd amin dikteta wao walikuwa wananunua kahawa kwake

utaumia sana kuona magufuli anashangiliwa kwa sababu hamjataka kujadili kwa uhuru, anayesema kinyume chenu mtamwita lumumba au buku 7 au msaliti au ccm...

hampati muda wa kukaa na kuelewa filosofia ya wakati huu, kuna vitu vizuri magufuli anavifanya na kuna vitu anakosea na ni kawaida sana tu

sasa wewe na wenzako mmejiweka upande wa chuki tena chuki isiyoisha, kuwa magu apatie au akosee nyie ni chuki tu

sasa leo unaona uchungu anaposhangiliwa na watu!! unaumia na utaumia kwa miaka 8 ijayo...imagine....kwa sababu unaumia unajipa faraja kwa kuandika post kama hizi isssshhh, so so sad

angalia hapa msimamo wa forest whitaker Idi Amin was not so bad, says US actor
 
IDD Amini alikua na mabaya yake mengi lakini pia mengi dhidi yake yalikua ni propaganda chafu na uwongo dhidi yake kama hilo la kula nyama za watu. Hiyo movie The Last King Of Scotland ina exaggerations nyiingi tu zingine kweli zingine uongo. Kama ni kupata tuzo nyingi inaeleweka nchi za magharibi hazikumpenda kabisa mtu huyu na wazungu wakikuchukia mambo yako yote huwa mabaya na atakaekuchafua watampa tuzo lukuki. Wapo watu Uganda tena kwa mamilioni wanamkumbuka kwa mazuri Idd Amini Dadda
Unaweza kuyataja mazuri kadhaa ya Idd Amin Dada, naona maelezo yako ni sweeping zaidi hayajawa specific.
 
IDD Amini alikua na mabaya yake mengi lakini pia mengi dhidi yake yalikua ni propaganda chafu na uwongo dhidi yake kama hilo la kula nyama za watu. Hiyo movie The Last King Of Scotland ina exaggerations nyiingi tu zingine kweli zingine uongo. Kama ni kupata tuzo nyingi inaeleweka nchi za magharibi hazikumpenda kabisa mtu huyu na wazungu wakikuchukia mambo yako yote huwa mabaya na atakaekuchafua watampa tuzo lukuki. Wapo watu Uganda tena kwa mamilioni wanamkumbuka kwa mazuri Idd Amini Dadda
Weka mazuri yake basi ,,maana mi nasikiaga mabaya yake mara alikua akimtaka mwanamke kwa lazima anamchukua
 
Pia usisahau kuwa propaganda zingine zilipikwa na nyerere sio kila kitu ni kweli.uganda ukienda leo maduka mengi makubwa yana milikiwa na wazawa na sio wahindi kama ilivyo tz
 
Kunikumbuka maneno ya JK kwamba 75% ya watanzania huwa wanafuata upepo unakovuma.
 
Hata mbowe alitaka kuongoza mazishi ya marehemu Chacha Wangwe ila Wakulya wakagoma wakamtoa mbio, pia anamuuguza Tundu Lisu huku akijikamua machozi, kwa kweli hii ni zaidi ya maigizo ya Mh. Idd Amin
 
Akawatembelee Mashehe wa Uamsho ili hizo kauli zake za kipuuzi azisemee ndani mwake.
 
IDD Amini alikua na mabaya yake mengi lakini pia mengi dhidi yake yalikua ni propaganda chafu na uwongo dhidi yake kama hilo la kula nyama za watu. Hiyo movie The Last King Of Scotland ina exaggerations nyiingi tu zingine kweli zingine uongo. Kama ni kupata tuzo nyingi inaeleweka nchi za magharibi hazikumpenda kabisa mtu huyu na wazungu wakikuchukia mambo yako yote huwa mabaya na atakaekuchafua watampa tuzo lukuki. Wapo watu Uganda tena kwa mamilioni wanamkumbuka kwa mazuri Idd Amini Dadda
Hakika mkuu,

Idd Amini amepakaziwa mengi, japo ni kweli alikuwa kiongozi katili kwa wananchi wake na wapinzani lakini kwa Waganda anabaki kuwa ni Rais pekee aliyeiletea maendeleo makubwa Uganda hadi leo.

Mambo mengine kama kula nyama na yafananayo na hayo ni uzushi wa kisiasa tu.
 
Back
Top Bottom