Usiogope mabaki hayana madhara tena

Usiogope mabaki hayana madhara tena

Hili ni aina ya mabomu yale yanayobeba sumu endelevu halina tofauti na kuvunja chungu kisha kuwawekea watu kwenye maji.. Mauaji ya halaiki
Kuna MUMA huu uhusishwa mkungu wa ndizi kwenye mgomba haukatwi hufanywa hasa kwenye mgomba aina ya kipukusa mkungu huachwa tu ila kila ndizi itakayo iva na kudondoka basi huondoka na mtu na unapo dondoka mgomba mzima jawabu utalipata je! umesha fanya tasmini vifo vinavyo husisha familia nzima au ukoo mzima tena mfululizo ni nini kilicho nyuma ya pazia?
 
mshana naomba unijibu ndg yangu ivi kwli wewe ni mchawi? naomba jibu moja kweli au hapana na kama ww ni mchawi huogopi wachawi wenzako kwa kutoa siri zao? na kama sio huu utaalam wa kichawi umeujulia wap??
majibu plz ndg yangu
Mimi sio mchawi na wala sio mganga... Siwaogopi wachawi kwakuwa matendo na kazi zao ni za kishetani na mimi nalindwa na damu ya Kristo aliye hai... Wakitaka kunidhuru wanakutana na moto mkali sana
 
Mshana Jr. Kuna msemo huwa nausikia mara nyingi kutoka kwenye jamii yangu...

Mfano. Kunakuwa na harusi afu unatokea msiba harusi inahairishwa na kusogezwa mbele, basi hapo wanasema target ilikuwa bwana/bibi harusi ila skadi imepindishwa na aidha mzimu wa mhusika...

Unalisemeaje hilo?
Hili jambo lipo na imeshatokea maharusi wengi tu kufariki siku ya harusi karibia na harusi au mara tu baada ya harusi
 
Kuna MUMA huu uhusishwa mkungu wa ndizi kwenye mgomba haukatwi hufanywa hasa kwenye mgomba aina ya kipukusa mkungu huachwa tu ila kila ndizi itakayo iva na kudondoka basi huondoka na mtu na unapo dondoka mgomba mzima jawabu utalipata je! umesha fanya tasmini vifo vinavyo husisha familia nzima au ukoo mzima tena mfululizo ni nini kilicho nyuma ya pazia?
Nakuelewa sana shusha vitu...
 
Nimemuelewa sana Guru wangu Mshana Jr. Nazi ikishavunjwa njia panda, ule mpasuko ndio una uchawi wenyewe. Lakini Yale mabaki ni salama Na hayana madhara. Hali kadhalika mbuzi wa kafara nyama yake iko poa tu kuliwa
Ni kweli Buji. Tulipokuwa tunaroga zile mechi za mchangani,wale njiwa,kuku, mbuzi tukiwachinja nyama yake ililiwa na ubwabwa.
Nazi walipewa watoto kutafuna. Na zile sarafu za kunuiya walipewa watoto wakanunue peremende( pipi jojo buble gum).
 
mshana napatambuaje kilingeni??
kuna sehem hapa mtaani wanasema ni kilinge cha watu wa kazi za usiku!!?? nataka NITHIBITISHE je nafanyaje?
 
mshana napatambuaje kilingeni??
kuna sehem hapa mtaani wanasema ni kilinge cha watu wa kazi za usiku!!?? nataka NITHIBITISHE je nafanyaje?
Ikifika saa sita usiku nenda hapo panaposemwa ukiwa na ndulele mfukoni na ukiwa umegeuza ndala
 
Hahaha sasa hawawachungaji hutolea mapepo kanisani halafu hawayaambii yaende wapi si mabalaa hayo, likimtoka mtu likakuparamia si inakuwa shughuli?! Ukute ni la ngono, unajikuta unaanza kutongoza wapendwa kanisani. Mi ndio maana naenda sabato na katoriki hakuna kutoana mapepo hahaha.
Una vituko Shemeji
 
Mshana Jr. Ni kweli ukilala usiku umegeuza chupi ndani nje wachawi wanakuogopa?
 
Ile methali isemayo " panapofuka moshi moto..... isipuuzwe Utaungua
 
Mchawi mmoja tulipishana kauli sehem flani, akanipa vitisho kibao, baada ya hapo wenyeji wakaanza kunifuata kila mmoja kwa muda wake kunishauri nimfuate nikamwombe msamaha atanifanyia kitu mbaya wanamjua simtu mzuri. Nikawaambia kamwambieni akkawaambie na mababu zake wote waje hawana uwezo wa kunifanya lolote. Haya matakataka ya kichawi, nguvu za kiza, mizimu sjuwi na nini ni ushenzi mtupu!
 
Aiseeh!
 
Back
Top Bottom