Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,644
- 860,880
Ganda la risasi halina madhara tena... Mabaki ya bomu lililolipuka pia hayana madhara tena.. Kwakuwa hayawezi kulipuka tena... Sana sana haya huchukuliwa na kuhifadhiwa vizuri kama sehemu ya ushahidi
hata kwenye mambo yetu haya ya kienyeji, ukishakuta mnyama keshachinjwa.. Unaweza kumchukua na kwenda kula kama kawaida bila madhara yoyote... Ukishakuta nazi nimekwisha palikuwa hakuna kitu tena hapo.. Unaweza hata kuzikanyaga na kama hali ya usafi inaruhusu unaweza hata kula
Nguvu ya tunguli na madawa ya kichawi formula yao ni moja na risasi au bomu.. Risasi ikishakutoka kama imekosa target ikitua ndio kwaheri... Bomu likishalipuka.. Mabaki yake hayana uwezo wala nguvu tena ya kulipuka... Sawasawa na uchawi uliokwisha fanyiwa kazi
Cha kuogopa ninini?
cha kuogopa sana ni risasi ambayo bado haijatoka kwenye bunduki... Ni bomu ambalo halijalipuka.... Sawa tu na uchawi aliotegewa mtu halafu kwa bahati mbaya ikatokea ukakumbana nao.. Kuna uchawi ambao ni universal sawa tu na bomu la kutegwa... Litampata wa kwanza kulikanyaga... Halafu kuna lile la kuset kwa remote ni mpaka mlengwa afike....
Kuna ndugu zangu wa kukumea... Mnapita njiapanda mnakuta tayari madude yalishapasuliwa tangu usiku halafu nyie mnaaza kuyakemea na kuyakwepa...!!!! Jamani tangu lini marehemu akawa na uhai?