Usioe kama hauna kipato cha kueleweka

Usioe kama hauna kipato cha kueleweka

Amin ili uwe mwanaume kamili ni lazima ukabili majukumu na siyo kukwepa, mwanaume unahitaji uwe na mtoto/watoto na hao watoto wanastahili upendo wa pande mbili wako na wa mama yake ni lazima nioe mwakani Mungu akipenda

Mambo ya kuhofia kuhudumia huo ni ubinafsi , kuogopa changamoto maana yake unataka uolewe wewe
Kila la kheri mkuu, usiache kumtanguliza Mungu
 
Unawapotosha vijana. Binafsi yangu, kipindi naoa ndo kwanza nina miaka miwili nimemaliza chuo alafu sikuwa na kazi yoyote ya kuniingizia kipato.

Mke wangu amekuwa chachu ya mafanikio yangu hadi hapa nilipo. Ninachokiamini, maisha hayana kanuni, kila mtu na riziki yake.
Hongera sana mkuu, mpende sana mke wako
 
Habari zenu wakuu,

Kuoa ni zaidi ya upendo, kuoa ni majukumu na sio kuitana Babe au Mahabuba.

Kama hujajipata tafadhali nakuomba usiikimbilie Ndoa, maana utaumia na kuichukia hiyo Ndoa kilasiku kwenye maisha yako. Maisha ya ndoa yanahitaji pesa za kilasiku na hilo jukumu ni la kwako wewe Mwanaume na sio mwengine, kwahyo hakikisha kuwa unakipato cha kueleweka ili kuepusha matatizo mbeleni.

Kila mtu ana ndoto za kuwa na ukwasi kwenye maisha yake, unapooa wakati hujajipanga huenda ukashindwa kufikia hizo ndoto kwa kiasi kikubwa.

Nimeona baadhi ya vijana wenzangu wakioa lakini mwisho wa siku wanazitesa familia zao kwa Njaa, maana kilasiku wanalia shida kusaidiwa hela kulisha familia zao.

NB. KUOA NI MAJUKUMU, JIPANGE KABLA YA KUYATIMIZA HAYO MAJUKUMU.
Maisha hayana formula ujue, kuna waliooana majobless wanaungaunga maisha na baada ya ndoa mambo yakawanyookea mbaya na kuna waliooana wote mambo safi lakini ghafla mambo yakawageukia na kuwarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi Mkuu, ila kujipanga ni lazima.

UNAWEZAJE KUOA UKIWA HAUNA HATA KITANDA AU MSOSI WAKO MWENYEWE UNAKUPIGA CHENGA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Unawapotosha vijana. Binafsi yangu, kipindi naoa ndo kwanza nina miaka miwili nimemaliza chuo alafu sikuwa na kazi yoyote ya kuniingizia kipato.

Mke wangu amekuwa chachu ya mafanikio yangu hadi hapa nilipo. Ninachokiamini, maisha hayana kanuni, kila mtu na riziki yake.
This is another paradox!!! Fafanua vizuri ulikuwa unamtunzaje?
 
Acha kupotosha vijana watapata stress bure..
Ulioaje huku hauna kitu maana yake kuna watu walikuwa wanakusupport sasa usishawishi wenzako wauvagae mkenge.
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Hata Mungu mwenyewe alimpatia Adam msaidizi(Mwanamke) baada ya kumpa kila kitu.

Nawashauri vijana wajitafute kwanza wajipate ndio watafute wake.
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Sio kumfurahisha Mke ni kujifurahisha wewe mwenyewe Mkuu.

Mke atakusaidia kwenye mambo mengi ukiachana na kukupa familia.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Mke angekuwa anafurahisha Bill gates asingeachana na mke wake
 
Aisee! Sio rahisi kipato kupotea kama mnavyosema wakuu.

NIAMBIE NI WATU WANGAPI UNAWAJUA AMBAO KIPATO KIMEWAISHIA KIASI HAWAWEZI KUTOA HUDUMA KWA FAMILIA ZAO..?

Unachokisema ni IMAGINATIONS tu Mkuu, maisha hayapo hivyo.
Watu kipato kinashuka hadi wanazikimbia familia zao unafanya mchezo mkuu? Kipato hakina guarantee, unaweza kuwa nacho na siku moja ukabaki huna hata mia mbovu.
 
Unawapotosha vijana. Binafsi yangu, kipindi naoa ndo kwanza nina miaka miwili nimemaliza chuo alafu sikuwa na kazi yoyote ya kuniingizia kipato.

Mke wangu amekuwa chachu ya mafanikio yangu hadi hapa nilipo. Ninachokiamini, maisha hayana kanuni, kila mtu na riziki yake.
Hongera mkuu, kusema ulikuwa huna kazi kabisa sio kweli umetuongopea

Wanawake wa hivyo ni ngumu mno kuwapata 1/100
 
Habari zenu wakuu,

Kuoa ni zaidi ya upendo, kuoa ni majukumu na sio kuitana Babe au Mahabuba.

Kama hujajipata tafadhali nakuomba usiikimbilie Ndoa, maana utaumia na kuichukia hiyo Ndoa kilasiku kwenye maisha yako. Maisha ya ndoa yanahitaji pesa za kilasiku na hilo jukumu ni la kwako wewe Mwanaume na sio mwengine, kwahyo hakikisha kuwa unakipato cha kueleweka ili kuepusha matatizo mbeleni.

Kila mtu ana ndoto za kuwa na ukwasi kwenye maisha yake, unapooa wakati hujajipanga huenda ukashindwa kufikia hizo ndoto kwa kiasi kikubwa.

Nimeona baadhi ya vijana wenzangu wakioa lakini mwisho wa siku wanazitesa familia zao kwa Njaa, maana kilasiku wanalia shida kusaidiwa hela kulisha familia zao.

NB. KUOA NI MAJUKUMU, JIPANGE KABLA YA KUYATIMIZA HAYO MAJUKUMU.
kuoa sio fedha,ni maelewa o baina ya mume na mke,pesa sio muhimu hivyo
 
Back
Top Bottom