Usioe kama hauna kipato cha kueleweka

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Habari zenu wakuu,

Kuoa ni zaidi ya upendo, kuoa ni majukumu na sio kuitana Babe au Mahabuba.

Kama hujajipata tafadhali nakuomba usiikimbilie Ndoa, maana utaumia na kuichukia hiyo Ndoa kilasiku kwenye maisha yako. Maisha ya ndoa yanahitaji pesa za kilasiku na hilo jukumu ni la kwako wewe Mwanaume na sio mwengine, kwahyo hakikisha kuwa unakipato cha kueleweka ili kuepusha matatizo mbeleni.

Kila mtu ana ndoto za kuwa na ukwasi kwenye maisha yake, unapooa wakati hujajipanga huenda ukashindwa kufikia hizo ndoto kwa kiasi kikubwa.

Nimeona baadhi ya vijana wenzangu wakioa lakini mwisho wa siku wanazitesa familia zao kwa Njaa, maana kilasiku wanalia shida kusaidiwa hela kulisha familia zao.

NB. KUOA NI MAJUKUMU, JIPANGE KABLA YA KUYATIMIZA HAYO MAJUKUMU.
 
kama wengine tusingeamua kuowa na tusingeowa kabisaa.....system ilipania kutunyoosha na kutukomoa kabisa
 
Bado nitachagua ndoa, muoe vijana mnaogopaje changamoto za ndoa na bado mnajiona ni wanaume timilifu,mwanaume ana sifa moja kuu ya kupambana na changamoto zinazomkabili katika maisha vijana mnaogopa ndoa najiuliza uanaume wenu ni wa faida gani
 
😂😂😂Wa kupigia puchuu
Viganja vimewakakamaa,akikushika mkono unajua kabisa huyu mpiga puchu🤣
 
Bado nitachagua ndoa, muoe vijana mnaogopaje changamoto za ndoa na bado mnajiona ni wanaume timilifu,mwanaume ana sifa moja kuu ya kupambana na changamoto zinazomkabili katika maisha vijana mnaogopa ndoa najiuliza uanaume wenu ni wa faida gani
Upo sahihi Mkuu, ila kujipanga ni lazima.

UNAWEZAJE KUOA UKIWA HAUNA HATA KITANDA AU MSOSI WAKO MWENYEWE UNAKUPIGA CHENGA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Jamani hizi mada za ndoa zimekua nyingi sana na zote zinawakatisha tamaa vijana.Hebu tuwaache vijana waoe hakuna jambo linalo kosa changamoto.Jamani ndoa zinachangamoto nyingi na tofauti tofauti lakini isitufanye tuogope ndoa sasa familia bora zitajengwa na kina nani km sio sisi.Njooni na mada hata za huyu shemeji yenu ataniua kwa mapishi au mahaba
 
Sawa Mkuu, ila Kinga ni bora zaidi.

TUNAWAAMBIA UKWELI ILI WASILALAME MBELENI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Upo sahihi Mkuu, ila kujipanga ni lazima.

UNAWEZAJE KUOA UKIWA HAUNA HATA KITANDA AU MSOSI WAKO MWENYEWE UNAKUPIGA CHENGA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Kuiipanga hiyo ni kanuni lazima uwe nacho cha kuweza kuweka mambo ya familia yaende

Ila sasa mambo ya kuogopa ndoa mtu hodari ni yule anaepambana na changamoto na kuzipatia majibu kuogopa kuzikabili ni uoga usio wa kujenga,
 
Back
Top Bottom