tunaokopesha kibiashara huwa tuna.mikakati ya kuokoa hela zetu zisifie kwa manyang'au...
mimi mpaka sasa nina laki 8 iko nje kwa watu lakini inaniletea riba karibu 100,000 kila wiki.
wachache sana wameshindwa kuleta pesa na ndio nimewakamatia vitu vyao kama Tv, majiko ya gesi n.k.
kukopesha ni fursa ya kukupa hela usiifanye kisamaria.
Twanga watu riba sio unatoa hela kif.ala!
achukue laki alete 120,000 baada ya wiki 2.
Hii Tv mpaa leo iko kwangu na sina presha. Elfu 50,000 sijaiona hadi leo na mwenyewe kakusha tu. Kila Juma3 anatakiwa alete 10,000 kama riba, wiki ya 3 kakausha.
sundar 17" led Tv
huyu hapa alichukua mkopo wa Tsh 20,000 akaweka bondi jiko la gesi.
Akaahidi kuleta na riba ya Tsh 2,000 jioni yake.
nilimuwahi nikachukua elfu 10 akabakiza elfu 10.
Hii ni wiki ya 5 sijaona hata mia yake na jiko liko kwangu na wala sina presha.
Mikopo kwangu ni biashara Tosha.
nazibeba shida za watu nazigeuza faida.