Usimkopeshe hela mtu

kpng12

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
299
500
Naandika haya nikiwa na machungu sana,
Siku hizi uaminifu umepotea sana tena ni adimu kama cent 5 hasa kwenye suala la pesa.

Mwaka jana nilikopesha sana watu na asilimia kubwa ni hawa "marafiki na workmates" siyo kwamba ninafedha hapana, hapa nilipo hata uwanja tu sina.

Mtu anakuja anakueleza matatizo yake na unamwambia kwakweli saizi sina kitu, anakubembeleza weeeee mwisho unamwonea huruma unaamua kuingia kwenye account na kumpa kiasi kadhaa.

Muda wa kurejesha ukifika sasa maelezo yanaanza kuwa mengi mara ooh subiri kidogo matikiti yapo shamba wiki ijayo naenda kuvuna, baada ya wiki ukimpigia simu hapokei na ikipokelewa anapokea mkewe tena anakuambia mwenye simu hayupo

Wengine sasa... Brother naomba nivumilie kidogo mwisho wa mwezi nitarekebisha then anaingia mitini. Juzi jamaa kanipigia simu (saizi yupo chuoni) ameenda kujiendeleza na ni mwajiriwa serikalini, aliniomba nimtumie hela kwani amekwama sana nikamjibu sina then nikakata simu yake, huyo jamaa mwaka 2017 nilimkopesha laki kwa makubaliano atarudisha mwisho wa mwezi lakini akatokomea kusiko julikana na mimi niliamua tu kusamehe.

Leo nimeamka nikapiga hesaba kama watu wote wangenirudishia hela yangu ningekuwa na kiasi fulani cha pesa nikabaki nahuzunika tu nakujiona kumbe mimi mjinga sana

Saizi sitaki kabisa mchezo na pesa yangu, hela yangu watapata ndugu wa damu moja na wazazi FULL STOP.
 

Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
463
1,000
Kuna mtu ana milioni 4.5 yangu aliniahidi kati ya mwezi atalipa siku zimepita naona kimya, mishahara imetoka napo naona kimya sasa leo iwe mbwai alipe pesa yangu ama urafiki ufe.

Mtu awapo na shida anakuwa anatia huruma kweli pindi ukimkopesha tu akatatua matatizo yake usumbufu unaanza, watu wa kariba hii sio wa kuwasaidia kabisa.

Nimejifunza.
 

Tempus Fugit

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
430
1,000
Hii imenitokea na sasa imenip mtizamo mpya...mara nyingi nimekuwa mwepesi wa kusaidia na rafiki akinicheki kwa shida yake sijiulizi sana.

Hizi hela ndogo za kuwa nisaidie 50k, 30k hapo nitarejesha baada ya siku 2...nimezitoa na nyingi hazirejeshwi na wahusika. Anakausha kana kwamba hajui chochote vile.

Hawa watu wasio waaminifu wanafanya kuwasaidia watu wahitaji iwe ngumu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom