baharia 1
JF-Expert Member
- Sep 13, 2019
- 1,884
- 2,287
Kichwa cha Habari
Biashara ya Mikopo au Ujambazi
iPhone 13 Pro Inauzwa Spea Kioo, Housing, Camera) Baada ya Mkopeshaji Kuniletea Masimango!
Iko hivi: Nina iPhone 13 Pro (128GB) niliyoichukua kwa mkopo. Nilituliza pesa ya kwanza down payment ya kutosha kabisa siku ya kwanza na sikutumia hii simu hata siku moja ilikaa ndani.
Kutokana na mambo kuyumba, simu ilikaa miezi 4 bila kulipiwa marejesho. Nilipokuja kuiwasha hivi karibuni, nimekuta wameipiga lock ya Lost iPhone.
Nimefanya uungwana mkubwa sana kuwapigia simu kistaarabu ili nianze kulipa kidogo kidogo kuanzia sasa hivi mambo yangu yalipoanza kukaa sawa.
Lakini badala ya kufanya biashara wameleta dharau, maneno ya shombo na masimango Tumeingia kwenye ubishi mzito na malumbano ya hovyo kwenye simu
wananikazia maneno na kunisema eti mimi mwanaume suruali, eti nakopa kitu ambacho sina uwezo nacho mbona sikuwa nalipa kwa miezi minne?
Niliwawachia makavu yao hapo hapo kwenye simu! Nikawaambia acheni upumbavu, mimi ningekuwa na hiyo hela ya mkupuo si nisingekopa simu tangu mwanzo mkaniletea hayo maneno yenu ya dharau
Wanadai eti haiwezekani nianze kulipa sasa hivi kama ndio nimechukua mkopo wanataka nilipe malimbikizo ya miezi yote minne kwa pamoja ndio wafungue simu
Sasa kwa dharau hizi, maneno yenu ya shombo, na kubishana huku kote, naomba niwambie kitu kimoja wote tukose Nyie mkoswe hela yenu na mimi nikose simu tuone nani anaumia.
Simu naivunja na kuipiga mnada wa spea au fundi aje aingize mitambo yake aing'oe hii lock. Wao wasipate hata mia ya lile deni lao la nyuma, na mimi niharibu chombo. Tukose wote yaishe
Kumbuka HUU SIO MTEGO! Sio mtego wa polisi wala wa kampuni ya mkopo. Nina hasira na shida ya chombo changu na niko tayari kwa lolotehata simu ikifa kabisa na kuwa tofali la jumla ikiwa kwenye matengenezo, iwe ndio basi tena yaishe, haina shida
1. KWA MAFUNDI WA SOFTWARE MASHARTI NI MAWILI TU
Malipo ni BAADA YA KAZI TU Unapiga mitambo yako, simu inawaka na kusoma laini hapa mbele yangu, unachukua chako. Story za kitapeli za tuma hela ya credit, token au tool kwanza" mtasubiri sana. Ukianza hizo hadithi nakula kichwa (block) papo hapo
2. KWA MAFUNDI WA SPEA ORIGINAL (NAUZA PARTS ZINAZOHAMISHIKA
Kama mnaona software imekataa na wote tunataka kukomoana na hao waliokataa hela yangu, njoo uchukue vitu original hapa uende ukafufue simu za wateja wako
Kioo Original (Super Retina XDR Display) – Kiko safi 100%, hakina hata mchubuko.
Kasha la Nje (Housing) – Jipya kabisa.
Kamera za Nyuma na Mbele (Camera Modules) – Nzima na safi zote tatu.
Betri Original (Battery) – Haijatumika tangu simu ichukuliwe.
Spika, charging port, na riboni zote za ndani.
Hata hivyo, kama kuna mtu wa hiyo kampuni ya mkopo yupo humu jukwaani na ana akili timamu ya kutaka tulipane kistaarabu kidogo kidogo bila hayo masimango yenu ya kishamba, milango ya PM iko wazi kabla sijaipiga mnada wa vipande