Usimkopeshe hela mtu

Hii imenitokea na sasa imenip mtizamo mpya...mara nyingi nimekuwa mwepesi wa kusaidia na rafiki akinicheki kwa shida yake sijiulizi sana.

Hizi hela ndogo za kuwa nisaidie 50k, 30k hapo nitarejesha baada ya siku 2...nimezitoa na nyingi hazirejeshwi na wahusika. Anakausha kana kwamba hajui chochote vile.

Hawa watu wasio waaminifu wanafanya kuwasaidia watu wahitaji iwe ngumu...
Mm kuna rafik yangu alinikopa 5,000/=mpaka leo anitafuti tena.
 
Mimi nimepoteza ndugu watatu. Mmoja Ni mtoto wa mjomba, kanikopa kwa shida zake mwaka wa tatu huu. Juzi nikikuambia asinijue na nisimjue na namba zake nikazifutilia mbali. Wengine wawili Ni watoto wa baba yangu, nao vivyo hivyo hata tulikutana popote kila mtu na hamsini zake. Ni Bora kua na marafiki WACHACHE kuliko utitiri wa ndugu mbwa.
 
Kwakweli Binafsi nimedhukumiwa laki sita na jamaa yangu mmoja, tena yeye niilmpa kadi ya benk kabisa akachukue aliomba laki tano badae napata message kachukua laki sita tangu 2015 daah!

Ila na mimi nadaiwa na jamaa zangu wawili mmoja ananidai laki mmoja mwingine 60,000/= mmoja kanipigia sana jana sijapokea maana sina hela namwambiaje sasa ila nitalipa tu.
 
Rafiki yangu nilimkopesha pesa mwaka jana, siku zimeenda kafilisika kibiashara na sioni dalili ya. Kupata hiyo pesa yangu, roho yaniuma sana
Pole sana mkuu. Kaka yangu mmoja alinieleza "siku ukimkopesha rafiki yako, ni mwanzo wa urafiki kufa" Sikumuelewa mpaka siku yaliponikuta ya kunikuta. Unamkopesha mtu na hana hata aibu ya kusema alipe deni. 🤬
 
Back
Top Bottom