Usikope fedha wala kuomba fedha ili ukatoe sadaka.

Usikope fedha wala kuomba fedha ili ukatoe sadaka.

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,955
Habari wanajukwaa!
Napenda kuwaambia waumini wenzangu kuwa Mungu ni mwema na wala hataki tufadhaike mioyoni mwetu.
Usiache kwenda kwenye nyumba ya ibada kisa huna fedha ya sadaka.
Wengine kwakuwa wamekuwa maarufu kanisani kwao, na wengine kwa kuona aibu basi hufikia hata kukopa fedha ili naye aonekane akipeleka mkono kapuni.
Wengine huweka mkono tupu ili tu waonekane kuwa wameweka mkono kapuni.
Wengine huomba fedha kwa marafiki au ndugu au wazazi ili tu waweke mkono kapuni.
Kwakufanya hivi unamkasirisha Mungu aliyekuumba, maana anaona kuwa ni kama hofu yako iko kwa mwanadamu mwenzako na si yeye Muumba.
Watoto wadogo ndio wanaopaswa kupewa sadaka na wazazi ili wajifunze kumtolea Mungu ktk kweli.
Sadaka ni kutoa kile ulichokifanyia kazi na si alichokifanyià kazi mwenzako. (1Fal 21:24).
Good night
 
Hahahah kumbe kuna watu wanakopa sadaka??aiseee,.
Sijui kwanini binadamu tunapenda sana kufurahisha kadamnasi kuliko Mungu atupae hivyo vyote...
 
Nimeombwa sadaka jpili iliyopita!!
 
Kutoka 23:15, Wala hapataonekana mtu mbele zangu atakayekuja na mikono mitupu.
Hii sentensi inazungumzia future
Hii sentence lazima tujue aliambiwa nani, na je, impact yake imeanza kuonekana au bado?
Taratibu za ibada wakati huo wa sheria na sasa ni sawa?
Zamani sadaka ilikuwa ina uhusiano na kufuta dhambi za mtu, je, sasa hivi sadaka kama mahindi, fedha, unga n.k vinaweza kufuta dhambi?

Bible hiyo hiyo inasema usiende mikono mitupu nyumbani mwa Bwana sijui inakuwaje hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo agano la kale halina nguvu kwasasa? Ni zilipendwa au?
Kutoka 23:15, Wala hapataonekana mtu mbele zangu atakayekuja na mikono mitupu.
Hii sentensi inazungumzia future
Hii sentence lazima tujue aliambiwa nani, na je, impact yake imeanza kuonekana au bado?
Taratibu za ibada wakati huo wa sheria na sasa ni sawa?
Zamani sadaka ilikuwa ina uhusiano na kufuta dhambi za mtu, je, sasa hivi sadaka kama mahindi, fedha, unga n.k vinaweza kufuta dhambi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, lina nguvu ila lazima tujue katika biblia neno fulani alilengwa nani na kwa wakati gani.
Kuna maneno moja kwa moja alilengwa Myahudi kwa asili
Kuna maneno alilengwa Myahudi kwa imani, kama mimi na wewe wote tuliomwamini Yesu.
Na kuna maneno yalilenga kwa wote.
Kuna neno lilitolewa na tayari lishatimia na halitatukia tena. Kuna neno continues, linaendelea kila Leo na kuna neno linasubiri utimilifu wake
Kwahiyo agano la kale halina nguvu kwasasa? Ni zilipendwa au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutoka 34:20

Mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa kunitolea kondoo. Kama hutamkomboa utamvunja shingo. Watoto wenu wote wa kiume ambao ni wazaliwa wa kwanza mtawakomboa. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom