Simulizi: Mji tulivu ulionipa ugonjwa wa milele

Msaidizi Mkuu

Senior Member
Aug 19, 2020
195
153
Sehemu Ya Kwanza (1)

Maisha wakati mwingine si jitihada pekee zinazoweza kukutoa sehemu moja kwenda nyingine, kuna wakati bahati inahusika katika maisha.

Si kwa wote lakini mimi nilibahatika kuwa mtoto kutoka familia ya kimasikini ambaye baadaye nilienda kusoma na kisha kupata kazi nzuri ambayo ilinitoa katika umasikini na kunitupa katika daraja la kati na baadaye nikawa tajiri.

Nikayabadili maisha ya kizazi changu na kuwaweka katika mirija ya kujiendesha wenyewe. Hadi ninafikisha miaka thelathini tayari nilikuwa nimeyaweka maisha yangu sawa, nikiwa nimesaidia ndugu zangu kwa kiwango cha uwezo wangu pamoja na marafiki pia.

Baada ya kutimiza ndoto hizi ndipo kwa mara ya kwanza nikafikiria juu ya utulivu wa hali ya juu niliokuwa nauhitaji na niliwahi kuuota tangu nikiwa nasoma, nilijiahidi kuwa nitakapomaliza kuinyanyua familia yangu sasa nitaangalia vyema maisha yangu.

Niliwahi kuwa na marafiki wa kike lakini sikuwahi kunyanyua kinywa changu na kuwatamkia kuwa nina nia ya kuingia nao katika ndoa.
Nilikuwa nina deni, sikutaka nijiongezee majukumu mengi yatakayosababisha nishindwe kutimiza vile nilivyopanga kutimiza.

Katika mkesha wa mwaka mpya nilimpigia mama yangu simu na kumweleza bayana kuwa ndoto mojawapo katika mwaka unaoanza ni kuyabadili maisha yangu kwa kujihifadhi katika mji tulivu. Akaniuliza iwapo nataka kuhama Tanzania, nikacheka na kumweleza kuwa sina wazo la kuhama Tanzania bali nahitaji kuingia katika mji tulivu.

“Unataka kuoa?” mama aliniuliza. Nikacheka bila kumjibu chochote, naye akacheka kisha akanitakia kila la heri. Nikampongeza kwa kuelewa maana yangu upesi sana!

Mwaka ulianza vyema na shughuli zikiendelea kama kawaida huku lile wazo likiwa kapuni kusubiri utekelezaji wake. Naomba niweke wazi kuwa nilikuwa aina fulani ya mwanadamu ambaye napenda sana kufanya jambo kadri ya wakati, maana niliwahi kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na kujikuta nikiharibu ama kutoyafanya kwa ufanisi mambo mengine.

Hivyo sikuwahi kupanga siku ya kuusaka mji ule tulivu!! Siku hii ikiwa ni miezi miwili baada ya mwaka kuanza pale ofisini kwetu palikuwa na nafasi za kazi zilikuwa zimetangazwa na watu wengi sana walikuwa wameomba nafasi. Katika ile hatua ya awali ya usahili walifika wasahiliwa mia moja na hamsini.
Nafasi zilikuwa tano tu zilizokuwa wazi.

Katika ngazi ya mwisho kabisa nd’o ambayo mimi na wakurugenzi wenzangu tulikuwa tunahusishwa lakini hatua za awali walisimamia wenzetu waliokuwa na vyeo vya chini. Baada ya hatua za awali hii siku ndiyo ilikuwa ile ya kupata mbivu na mbichi. Wasahiliwa ishirini wa mwisho.

Katika usahili nilikuwa natazamwa sana, hakika sikuwa mtu wa mchezo, ukifanya vibaya usitarajie kuwa nitakubeba kisa tu u msichana ama umeonyesha huruma ya aina yoyote.

Sikuwa mtu wa aina hiyo kabisa, na kilichokuwa kinanifanya niwe hivi ni njia ambazo nilikuwa nimepitia, hakuna njia ya panya yoyote niliyopitia katika safari yangu ya kimasomo hadi kutafuta kazi.

Na pia nilikuwa nina hofu na Mungu! Kitendo cha kumpitisha mtu asiyekuwa na vigezo na kumwacha mwenye vigezo kungeisononesha nafsi yangu sana. Katika usahili nilikuwa naogopwa sana. Hata siku hiyo nilikuwa yuleyule, maswali yangu yalikuwa si magumu lakini yenye mitego. Maswali yangu yakiwa na nia moja tu, kuupima uelewa halisi wa msailiwa.

Walipita wasahiliwa wote katika hatua ya kwanza, niliwanukuu majina yao. Baada ya hatua zote za usahili kumalizika hatimaye tuliwaeleza kuwa baada ya majuma mawili tutawapigia simu katika nambari walizotuachia.

Tukawaaga wakaondoka!!
Masuala ya usahili yakaishia hapo…..
Nikaendelea na shughuli nyingine hadi majira ya saa tatu usiku ndipo niliifunga ofisi yangu na kutoka nje kuelekea katika gari langu.
Nilifungua mlango na kuiwasha gari nikaiacha ikiunguruma kwa muda huku nikiwa nimewasha kiyoyozi ili kuleta hewa safi, mara nikasikia hatua zikijongea nilipokuwa. Nikatambua huyo atakuwa aidha mlinzi ama kijana mwingine tu amekuja kuniomba shilingi mia tano.
Nikaandaa hiyo pesa ili tusizungumze sana.

Sikuwa napendelea sana kusikiliza maelezo yao kwa sababu huwa wanadanganya wana njaa kisha ukiwape pesa wanaenda kujidunga madawa ya kulevya.

“Samahani kaka…” nikaisikia sauti ya kike. Nikageuka upesi kumkabili anayeniita, sikuitarajia kabisa sauti ya kike muda ule. Sikuwa na mazoea na watoto wa kike kabisa. Mazoea ya kikazi yalitosha kabisa! “Nikusaidie nini?” nilimuuliza bila kuijibu salamu yake.

“Naitwa Nyambura…. Naitwa Nyambura Kone…” alijitambulisha jina lake. “Samahani sidhani kama nakufahamu..” nilimjibu huku nikijiandaa kuingia garini ili niondoke. Akajieleza kuwa siku hiyo alishiriki usahili katika kampuni ninayofanyia kazi.
Aliposema vile jina likanikaa sawa kichwani.

Anataka kutoa rushwa!! Nilijiwazia huku nikimsikiliza aendelee kuzungumza na hapo nikamwomba ajieleze kwa haraka kidogo, kichwani tayari nikiwa nimepanga shambulizi kubwa na kumpa ili nimuaibishe ikiwa atanishawishi kunipa rushwa ya aina yoyote, tena bora angezungumzia pesa ila akithubutu kunieleza rushwa ya ngono hata vibao nitamchapa hadharani.

Akajikohoza kisha akazungumza. “Naitwa Nyambura..” nikamzuia kwa mkono na kumsihi aendelee kwani jina lake tayari alilitaja awali. Na huku niliona ni kupoteza muda anakoelekea. Yule binti aliyejitambulisha kwa jina la Nyambura Kone akajieleza.

“Mimi ni mtoto wa tatu katika familia yangu… nimetoka Musoma vijijini kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya usahili huu, usahili ambao naamini kuwa kwa leo hakika sijafanya vizuri, lakini hiyo sio tafsiri ya jinsi nilivyo, ninauguliwa mama yangu na sijui hata kama nitamkuta akiwa hai, sijala tangu nilipokula jana mchana, zaidi ya yale maji mliyotupatia sijala chochote….. nimekuja kwa miguu katika usahili na nitarejea kwa miguu kama unavyoniona…. Nakusihi sana na sijui kwanini nimekusudia kuonana na wewe lakini nakuomba utakapofanya maamuzi basi nipe nafasi ya upendeleo.

Sipo kama nilivyojaribu kujieleza katika usahili…. Nina matatizo makubwa sana yananikabili… ni matatizo yangu na si ya kampuni yenu lakini nakuomba kwa maelezo yangu haya mafupi unisaidie uwezavyo. Mama yangu anakufa, lakini wadogo zangu wanahitaji kula, achana na kusoma maana imeshindikana tayari… mimi ni kila kitu kwao.” Aliweka kituo yule binti.

Akabaki kunitazama
Maneno yake hayakunishawishi sana, kwa sababu ninaamini katika ushawishi wa katikati ya chumba cha usahili na si vinginevyo.
Nikaitoa pochi yangu na kutoa noti tatu za shilingi elfu tano nikampatia kama nauli na nikamweleza kuwa nimesikia ombi lake.
Nilimweleza ilimradi tu kuyamaliza yale mazungumzo, aondoke na mimi niondoke.
“Namba ya simu si yangu ni ya huyo aliyenipokea, ikiwa nitapata nafasi ya kupigiwa simu utamwambia anifikishie ujumbe.”

Akamaliza kunisihi huku akishindwa walau kutoa shukrani kwa kiasi cha pesa nilichompatia.
Hakika jambo lile liliniudhi sana, nikahisi huyu ni changudoa aliyebobea na kwangu mimi alitaka pesa nyingi ili niununue mwili wake, sasa sijaununua na nimempatia kiasi kidogo cha pesa.

Pesa zangu ziliniuma sana!
Niliondoka pale lakini sikwenda nyumbani moja kwa moja, sikuwa nimeoa niliishi peke yangu. Hivyo ilinilazimu kupita hotelini kupata chakula.
Kitendo cha kuondoka eneo lile nikamsahau na kumpuuzia yule dada aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Nyambura!
Nilipomaliza kupata chakula, wakati nalipia bili ndo nikamkumbuka tena Nyambura na kujisemea kuwa laiti kama nisingempatia ile pesa basi ndo ningeitumia kulipa ile bili ya chakula.

Niliondoka pale, sasa nilikuwa naelekea nyumbani.
Tofauti na siku zote, nilishangazwa na ile foleni katika barabara ya Morogoro kutokea Kariakoo nilipopitia, nilitazama saa yangu na ilikuwa saa nne usiku. Foleni ilikuwa kubwa kiasi kwamba gari zilikuwa hazitembei kabisa.
Taratibu taratibu hadi gari ikafikia kile chanzo cha foleni, kuna ajali ilikuwa imetokea.

Nilipotambua kuwa ni ajali nikapandisha vioo vya gari langu, kwani mazingira kama hayo kwa jiji la Dar es salaam huwa vibaka nao wanaingia kazini.
Lakini nilibaki kutazama nione hiyo ajali kupitia kioo kwenye kioo.
Hapo sasa gari zilikuwa hazitembei kabisa, nikashusha vioo na kujaribu kuwauliza madereva waliokuwa wameshuka.
Wakanieleza kuwa njia imefungwa kwa mbele, raia wamegomea gari zisiondoke kwa sababu katika hii foleni ipo gari iliyogonga!

Niliishiawa nguvu nikaamua kushuka na mimi garini.
Nilidadisi na kuelekezwa majeruhi alipokuwa.
Nilifika na kujikuta natazamana na mwanamke aliyejivika mavazi mafupi sana yaliyouacha mwili wake wazi, vijana wa pembeni wakawa wanamteta wakisema kuwa ni changudoa alikuwa kazini. Mwil wake ulikuwa umetokwa na fahamu na hakuonekana kujeruhiwa sana…..

Maneno yale yakapenya na kunifikia, nami nikakiri kuwa huenda kweli ni changudoa.
“Unasema changudoa… unamaanisha changudoa ana haki ya kugongwa na gari akiwa upande wake sahihi…. Sharia ya wapi uliyoisoma wewe inayoruhusu mtu kugongwa na gari kwa sababu tu ya shughuli zake…. Sikiliza kaka usipokuwa na uhakika na kitu ni heri ukakaa kimya! Angekuwa dada yako ungesema sawa afe kwa sababu ni changudoa!!!” ilisikika sauti kali ya kike ikijibu mapigo kwa jazba.
Nikaguswa na maneno yake, kwa sababu nami na elimu yangu nilikuwa nimekiri kuuwa ni sawa tu agongwe kwa sababu ni changudoa.

Nikageuka kutazama ni nani anayetokwa na maneno yale makali.
Nyambura!! Mungu wangu, nilishtuka sana.
Sijui ni kwanini nilishtuka vile, lakini kuna kitu kama hofu kiliniingia.
Nikachelewa kubandua macho yangu kwake, mwishowe nikajikuta natazamana naye.

NAKUSIHI!!
Usimuhukumu mtu yeyote kwa sababu ya muonekano wake, kwa sababu ya kipato chake, kwa sababu ya kabila ama imani yake kidini.
FIKIRI KABLA HUJATENDA!!
Ndugu msomaji, nilikusihi usimuhukumu mtu kwa sababu ya kile unachofikiri wewe juu yake.
Na sasa Nakusihi tena JIPIME MARA mbili zaidi kabla hujapata wasaa wa kumpima mwenzako.

Baada ya yule dada kutonitambua sikupoteza wakati zaidi eneo lile, nilihisi kuwa na yeye ni walewale.
Nikazikumbuka pesa zangu, na hapa nikakiri kuwa yule binti alikuwa ananitaka kimapenzi hakuwa na lolote la ziada, sasa Mungu kawapa pigo.

Nikajiondokea nikaingia kwenye gari na hapo foleni ilikuwa inaanza kusogea. Bila shaka huko mbele palikuwa pamesuluhishwa tayari.
Nilifika nyumbani kwangu nikiwa nimechoka sana nikajitupa kitandani, kwanza nikapitiwa na usingizi nikaja kuamka baadaye sana nikaoga na kulala tena.
Asubuhi nilikuwa nimemsahau yule dada na vimbwanga vyake.
_____
BAADA YA JUMA MOJA, majina yalikuwa yametoka tayari. Sikukumbuka wala sikujali juu ya yule dada ambaye alihitaji nimsaidie aweze kuchomoza na kwa jinsi nilivyompa alama chache katika ule usahili basi ilikuwa lazima tu aanguke.
Kweli hakuwemo!

Nilikuwa ofisini kwangu nikapokea simu kutoka kwa Hadija ambaye ni katibu muhtasi wangu, nikaipokea upesi na kumsikiliza huku nikimsihi kuwa nitapenda zaidi kama atazungumza kwa muda mfupi. Alinieleza kuwa yupo mtu anahitaji kuonana na mimi na amesihi sana kuwa ni muhimu.

Nikamruhusu aingie.
Zikapita sekunde kadhaa kabla mlango wangu haujasukumwa.
Alisimama mbele yangu yuleyule binti, Nyambura!
“Shkamoo..” alinisalimia.
Nilisita kuitikia kwa sababu nilitambua wazi kuwa umri wake haukuwa wa kuniambia mimi shkamoo.
Alisalimia tu kwa sababu ya nidhamu ya uoga.

“Habari yako…” nikamsabahi.
“Jina langu halipo katika orodha,” alisema kisha akaendelea, “Ni kwa sababu haukuweza kunisaidia…..” akajaribu kuzungumza lakini akakosa cha kusema. Akabaki kutupatupa mikono hewani.
“Kuna jingine labda naweza kukusaidia…” nilimuuliza huku nikipambana kuizuia hasira yangu isichukue nafasi kubwa.
Maana niloiona yule binti ananichukulia mimi dhaifu kama wanaume wengine….

Akazungumza huku akiwa amesimama, akanieleza kuwa mama yake alikuwa amepoteza maisha tayari. Akanisihi kama ninao msaada wowote ili aweze kufika Musoma basi nimsaidie.
“Ujue ile siku ya kwanza nilipokusaidia sio kwamba nilikuwa boya sana, naomba uondoke na kamwe usirudi hapa….” Nilimkaripia huku nikisimama.
Akanikazia macho yake kisha akazungumza.

“Unaweza kunipiga kama utahitaji… mwili huu umezoea suluba tayari.” Alinijibu kiujasiri.
Kisha akaendelea kuzungumza, alisema mengi sana ambayo labda yangemgusa mwanaume wa kawaida, lakini mimi yalionekana kama maigizo tu na hakuna alichokuwa anamaanisha.
Hakika sikumsaidia kitu chochote.
“Naitwa Nyambura! Asante sana kaka kwa moyo wako….” Alimaliza kisha akaondoka.
Alipoondoka nikatazama fungu la pesa lililosheheni katika meza yangu pale ofisini, pesa ambayo niliipata kwa kazi isiyokuwa ya kutoa jasho.

Kwani ningempa hata laki ningepungukiwa nini! Nilijiuliza.
Nikanyanyua simu ya ofisini, nikampigia Hadija na kumuuliza kama yule binti anaonekana pale amwite.
Akanambia kuwa amepita kasi huku akiwa analia sana.
“Kwani umemfanyaje?” aliniuliza.
Moyo ukaniuma, nikakata simu na kujikuta najuta.
Hivi ninakuwaje mimi! Sasa najuta nini? Si ni ukweli ni malaya yule na ananiongopea tu hapa au!!

Nilijifariji lakini bado moyo wangu ulikuwa hauna amani.
Ilikuwa kawaida yangu nikiwa naikosa amani ya nafsi basi huwa nampigia mama yangu mzazi na ananishauri ama kunitia moyo.
Hata siku hii nilimpigia pia.
Nikamweleza juu ya hali ile, ilimsikitisha pia lakini mwisho alisema kuwa mjini pana mengi.

Huenda hata huyo ananiongopea tu!
Akanisihi niwe na amani.
Kweli amani ikatawala.
Nikaachana na Nyambura.
_____
Baada ya miezi miwili kupita afisa habari wa kampuni alipoteza maisha kwa kile kilichosemekana alikula ama kulishwa chakula chenye sumu, hivyo baada ya muda fulani nafasi ya kazi ikatangazwa.
Na kitendo cha kuwa na afisa habari mmoja kilisababisha wakurugenzi na bodi nzima wapendekeze kupatikana kwa maafisa habari wawili yaani mtu na msaidizi wake.

Nafasi za kazi zikatangazwa magazetini. Kama kawaida wasahiliwa kutoka kila kona wakafika na bahasha zao za kaki siku ya usahili.
Kwa sababu afisa habari alihitajika upesi sana usaili huu ulifanyika siku mfululizo.
Hatimaye yakabaki majina sita ya mwisho.
Hawa walipangiwa siku yao, wanawake watatu na wanaume watatu.

Ikafika siku yao ya usahili wa ziada kama ulivyo utaratibu wa kampuni.
Wasahiliwa wakaingia mmoja baada ya mwingine.
Hatimaye wakalifikia jina la Neema Wilson.
Akaingia binti ambaye kimavazi alipangilia kama ilivyostahili, nikatazama katika karatasi zangu, binti yule alikuwa vizuri katika lugha tatu… kifaransa, Kiswahili na kiingereza.

Nikaamua kuwa mchokozi nikachagua kuzungumza naye kifaransa katika usahili wake.
Kwa sababu wenzangu walikuwa hawajui lugha hii wakaniachia mimi mwenyewe.
Nikanyanyua uso wangu ili nimtupie swali la kwanza.
Mungu wangu! Nilikuwa natazamana ana kwa ana na Nyambura, yule binti kutoka Musoma ambaye aliwahi kufanya usahili katika kampuni yetu.

Swali nililopanga kuuliza likayeyuka nikajikuta natokwa na swali ambalo sikutarajia.
“Wewe ni Neema ama Nyambura….” Nilimuuliza. Akanitazama kwa sekunde chache akiwa hana mashaka hata kidogo akanieleza kuwa yeye ni Neema.
Nikajaribu kujiweka sawa nikauliza maswali ya msingi kwa kifaransa, akanijibu vyema.

Nikamruhusu atoke.
Lakini nikimweleza kwa kifaransa kuwa aningoje nje!
Akatii!
Baada ya usahili nikaonana naye na kumuuliza kwa mara ya pili jina lake ni nani.
“Naitwa Nyambura!” alinijibu bila wasiwasi.
“Na kwa nini umejitambulisha kama Neema.” Nilimuuliza kitafiti.
“Neema ni jina langu pia. Unaweza kunitambua kwa yote ukihitaji….” Alinijibu kisha akaniaga na kuondoka.
Lakini kabla hajafika mbali aligeuka.

“Hauamini kama mimi ni Nyambura…. Ulinipa elfu kumi na tano mara ya mwisho na sasa sijakuomba hata kunisaidia ili nipate nafasi katika kampuni yako…” alinieleza kisha akaondoka zake, akianiacha nisijue kuna kitu gani kinaendelea.
Upesi nkatika ofisi yangu nikapekua nyaraka kadhaa za wasahiliwa wa wakati ule wa Nyambura. Nikakutana na nyaraka zinazoelezea wasifu wa Nyambura… nikabahatika kuona viambatanishi.

Cheti chake cha kidato cha nne kiliandikwa jina NYAMBURA na cha kidato cha sita pia.
Nikaviweka kando na kutazama hivi vya sasa.
Jina lilikuwa NEEMA…..
Ni kitu gani anaficha huyu binti? Nilijiuliza huku nikizidi kushangaa ile kasi ya kuingia katika akili yangu ilivyokuwa inaongezeka.
NAKUSIHI!
Sio kila ukionacho kinang’ara basi ni dhahabu hiyo, kuna ming’aro mingine inatengenezwa ing’ae kuliko dhahabu. Ilimradi tu kukuchanganya wewe unayetaka dhahabu halisi……
*******************

WAKATI mwingine katika maisha sio kila kitu ukionacho ukubali kuwaza kukimiliki.
Kile kitendo cha kuiruhusu akili yako kuwaza juu ya kumiliki kitu fulani, unajiwekea deni katika akili yako na hapo akili inaanza kukulazimisha ulilipe.
Na uombe sana deni hilo lisiwe mahusiano ya kimapenzi
KWA jinsi Nyambura alivyojieleza katika usahili basi lingekuwa jambo la ajabu kumnyima nafasi ya uafisa habari katika kampuni yetu.
Niliunga mkono nafasi ile akabidhiwe binti yule.

Katibu muhtasi akapiga simu, Nyambura akaanza kazi rasmi.
Uchapaji kazi wa Nyambura ulinifanya nijisikie hatia sana nilipoyakumbuka maneno yake siku alipokuwa ananisihi sana nimsaidie apate kazi kwa sababu anao ndugu wanamtegemea kwa dhati sana.
Nakumbuka kuwa nilimpuuza na kumwona kuwa na yeye ni walewale.
Wasichana wa kileo
Kwa sababu yeye alikuwa ni afisa habari wa kampuni na mimi nikiwa katika bodi ya wakurugenzi, hatukuweza kuonana mara kwa mara kwa sababu kama ni habari angeweza kuzikuta kwa katibu muhtasi wetu!
Habari ikiwa nyeti sana ndo angeweza kuonana na mkurugenzi moja kwa moja.
Waswahili wanasema kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.

Sifa za Nyambura zilisambaa upesi sana, alikuwa ni mfanyakazi makini sana anayeijali ofisi yake na asiyekuwa na mazoea kama ya wafanyakazi wengine ya kuanza kutegea kazi pindi wanapoizoea ofisi. Nyambura hakuwa hivyo!
Haikushangaza pale alipopewa zawadi na kampuni kutokana na utendaji kazi wake.
Kuajiriwa kwa Nyambura kukaifanya kampuni yetu ya kusambaa kwa kasi sana mkoa kwa mkoa.

Nyambura hakuchoka wala kuonyesha dalili ya kuchoka, alizidi kuchapa kazi.
Nyambura alikuwa zaidi ya afisa habari!
Miezi mitatu baadaye Nyambura alikuwa amejenga ushawishi hadi kampuni yetu ikafungua tawi kubwa jijini Arusha. Ni katika ufunguzi huu wa tawi nilichaguliwa kwenda kukata utepe nikiwa kama mkurugenzi mtendaji.
Na hapa nikatakiwa kuongozana na afisa habari wa kampuni!
Nyambura!!

Ndugu msikilizaji, licha ya kwamba nilikuwa nina pesa za kutosha lakini sikuwa mpenzi wa kusafiri kwa njia ya ndege. Safari kama hizo nilikuwa natumia gari yangu binafsi, aidha ninaendesha mwenyewe ama namchukua dereva wa kuniendesha.
Safari hii pia niliamua tusafiri kwa kutumia gari langu.

Niliketi na Nyambura kwa dakika kadhaa kuzungumzia kitu ambacho tunapaswa kwenda kufanya kule, hasahasa wakati wa kuzungumza na watu wa Arusha juu ya kampuni yetu iliyokuwa inahusika na mambo ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi.

Ni hapa ndipo nilipokiri kuwa Nyambura alikuwa anajua jinsi ya kuzipanga karata na kumfunga mpinzani wake, alizungumza hadi nikatamani hiyo siku yeye ndo asungumze na wakazi wa Arusha mimi niwe kando.
Yule binti alikuwa na akili halafu na kipaji cha ziada…

Alikuwa anajiamini na hatoi neno lisilokuwa na maana mdomoni mwake.
Safari ya Arusha ikaiva!
Tukaondoka na dereva, mimi na Nyambura tukaketi nyuma tukiendelea kupanga mikakati ya hapa na pale.
Mikakati ilipomalizika tukaanza kupeana stori za hapa na pale kuhusu maisha.
Kisha utani kidogo, nikakumbuka kumwomba msamaha kwa kumcheleweshea kazi alipokuja katika usaili siku ya kwanza.

Nyambura akacheka kidogo! Kisha akanitazama na kuzungumza huku akiwa anatabasamu.
“Mama yangu alikufa… na wadogo zangu wawili wakamfuata nyuma. Lakini mimi nipo hai na ananiona ninavyopambana huko alipo…” alizungumza huku lile tabasamu likitoweka katika uso wake.
Sikutaka tuendelee kuzungumza sana juu ya jambo lile, kwa sababu niliona waziwazi kuwa nilikuwa upande wa hatia kwa sababu alinieleza awali na bado sikutaka kumtetea ili aweze kuipata ajira.
Nikabadili mada!
______
SHUGHULI za kikazi Arusha zilienda vyema kabisa huku Nyambura akizidi kunidhihirishia kuwa yeye ni moto wa kuotea mbali.
Siku ya mwisho ya kuwa Arusha nilimwalika Nyambura chakula cha usiku katika hoteli niliyokuwa nimefikia.
Tukakubaliana muda wa kukutana.
Nilifika majira ya saa mbili, yeye akafika nusu saa baadaye….

Nilimuona kuanzia mbali alivyokuwa anatembea kimadaha, vazi lake la usiku lilikuwa limeukamata mwili wake na kuufanya urembo wake kuonekana bayana. Hata kabla hajanifikia niliweza kutambua kuwa manukato yake yalikuwa yanatoa harufu mwanana sana.
Nikajiskia fadhaa sana kwa sababu nilikuwa nimevaa kawaida sana.
Wakati Nyambura alikuwa amejipanga vyema.

Alifika na kunisalimia katika namna ya kunikumbatia.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nikajikuta natamani mwanamke aendelee kunikumbatia kwa muda mrefu zaidi!
Nyambura akaketi tukaagiza chakula na vinywaji huku tukivunja kanuni ya chakula, tulikuwa tunazungumza tena mazungumzo yalikuwa mengi kuliko mwendo wa kula chakula.

Usingeweza kumdhania hata kidogo kuwa huyu Nyambura ndo yule afisa habari machachari wa kampuni yetu.
Kila sekunde zilivyozidi kusogea mbele nami nikajikuta nazidi kutamani kuendelea kuwa pamoja na Nyambura.
Nikapiga moyo konde na kumsihi twende chumbani kwangu ili tunywe pombe kwa tani yetu!
Awali alijaribu kupinga lakini nikasihi sana hadi akanikubalia ombi langu.
Tukaingia chumbani, tulikunywa sana.
Nyambura akawa wa kwanza kulewa, lakini alikuwa anajitambua.

Pombe zikamualika shetani katikati yetu, zaidi kwangu mimi akanisukuma kumuhimiza Nyambura tuvunje amri ya sita.
Nyambura akanikatalia huku akilia kilevilevi, nikasikia kama anasema kuwa kamwe hajawahi kufanya kitendo hicho.
Nikadhani zile ni pombe tu zinamsukuma kusema vile. Nami mashetani yalikuwa yamenipanda na sikuweza kujizuia.
La! Haula! yalikuwa maajabu makubwa sana kupata kuyashuhudia!!
Nyambura alikuwa yu salama bado, alikuwa na usichana wake!!
Alipambana sana na siku ile sikuweza kumfanya jambo lolote lile.

Pombe zilipotutoka kichwani nikajikuta namtamkia Nyambura kuwa ninampenda sana.
Hakuzungusha maneno sana badala yake alinijibu.
“Sina wazazi lakini nina baadhi ya ndugu, kama unanipenda kanitolee mahari unioe!!” alijibu huku amenikazia macho.
Jibu lile la Nyambura likanifanya nizidi kumtazama kwa jicho la tatu kama msichana wa tofauti sana.
Na hapo rasmi nikajikuta naingia katika matamanio ya kumuoa hasimu wangu wa zamani, Nyambura!!
Haikuwa safari nyepesi hata kidogo.
Na sikujua safari ile kama ingenifikisha pale iliponifikisha!!!!
********************
Kujaribu kumsahau mtu unayempenda ni jambo gumu sana, ni sawa kabisa na kujaribu kumkumbuka mtu ambaye hata hujawahi kumuona.
Tazama jinsi ambavyo haiwezekani!!
ILIANZA kama masihara, mara nikajikuta nazama katika uhitaji wa kuwa karibu kabisa na Nyambura.

Walisema penzi ni kikohozi!
Ilikuwa hivi hata kwangu, wafanyakazi wakaanza kutubadilisha majina hatua kwa hatua hatimaye nikafungua kinywa na kuwaeleza kuwa ni kweli tupo katika mahusiano na tunataka kuyabadili yawe ndoa mapema sana.
Wengi walitupongeza na kututakia heri!
Kasoro rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa yu katika ndoa tayari, yeye aliniuliza ninamfahamu Nyambura kiasi gani.
Sikutaka kujishughulisha na swali lake nikamweleza kuwa tunafahamiana sana!
Akatabasamu kisha akanipongeza, nilijua wazi kuwa hakuwa akimaanisha.

Siku mbili baadaye alinifuata ofisini, aliniomba nimsikilize kwa dakika chache, akanielezea mashaka yake juu ya uhusiano wa ghafla sana kati yangu na Nyambura. Akanisihi sana nijipime upya tena kama ni kweli nahitaji kuwa na yule binti kama mke wangu.
“Sikiliza Joshua, sikatai kuwa Nyambura ni mchapakazi na kila mtu anampenda, kuhusu hilo sina swali kabisa lakini je ana utayari wa kuwa mke kaka… au ndo furaha uliyopata Arusha imekusukuma huko?” aliniuliza yule rafiki yangu na mkurugenzi mwenzangu pia kwa pale ofisini.

Niliyasikiliza vizuri sana maneno yake. Kuna namna alimchambua Nyambura kwa ajinsi alivyomuona yeye, sikuipenda ile hali na nikawa namjibu tu ilimradi aondoke zake.
Mapenzi, yasikie tu mapenzi na uombe lisiwe penzi la kwanza… penzi la kwanza maishani huwa lina kila aina ya ubora. Kuaminiana kwa hali ya juu, hapa hujajua maana ya kutendwa!
Nilimwalika Nyambura chakula cha jioni katika hoteli moja ya kifahari, huko nikamweleza jinsi gani Revokatus yule mkurugenzi mwenzangu anavyosema kuhusu yeye.
Nilitarajia kuwa Nyambura atakasirika lakini haikuwa hivyo, alinijibu kikarimu sana.

“Yule ni mwanandoa mzoefu tayari, unapaswa kumsikiliza na usimkasirikie, hawezi kuwa na chuki yoyote juu yetu…. Ni vyema kumsikiliza halafu kwa vitendo sisi tutamwonyesha kuwa alivyowaza juu yetu si sawa…”
Majibu ya Nyambura yalizidi kunifanya nimpuuzie Revo na badala yake nikapiga hatua mbele siku ile nikamtamkie tena Nyambura kuwa ninataka kumuoa na ninahitaji kwenda rasmi kumtolea mahari, akanielekeza kwa ndugu zake waliopo Musoma.
Kwa sababu mimi nilikuwa mkurugenzi, jambo la ruhusa kwangu lilikuwa dogo sana.
Nisingeweza kukosa.

Nikazungumza na Revo aweze kunisindikiza akanieleza kuwa mkewe anaumwa hivyo hataweza kwenda, nikapata marafiki wawili wa kwenda nao pamoja na mjomba wangu ambaye nilimtumia kama mshenga!!!
Baada ya siku nne mambo yalikuwa tayari, tukafanya safari.
Tulipokelewa vizuri sana na ndugu zake Nyambura, nilistaajabu kabisa jinsi mkoa wa Mara unavyozungumzwa jijini Dar es salaam ni tofauti kabisa na uhalisia tuliokutana nao.

Walitufanyia ukarimu sana, na sisi tukajishusha mno ili tupate Baraka na kuachiwa mke.
Ile siku ya tatu wilayani Musoma mkoani Mara, tukapokea simu kutoka jijini Dar es salaam.
Revo, yule rafiki na mkurugenzi mwenzangu alikuwa hoi hospitali baada ya kula chakula kilichosadikika kuwa kimewekewa sumu.
Tuliendelea kuwajulia hali mara kwa mara jijini Dar es salaam hadi tulipopewa taarifa kuwa hali yake inaendelea vizuri, hapo nasi tukapata ahueni.
Masuala ya Musoma yakamalizika hatimaye tukarejea jijini Dar es salaam.
Ile nafika tu nikakutana na barua ofisini, Revo alikuwa amenuia kuuza hisa zake na kuachana na kampuni ile tuliyoianzisha wote kwa jasho sana!!

Hii ilinishtua sana, maelezo yake hayakuwa yamenyooka sana, nilipatwa na ukakasi sana kuweza kuelewa chanzo cha haya….
Nikampigia simu, akapokea na kunisisitiza kuwa anahitaji kupumzika na mkewe waweze kulea watoto wao mapacha.
Sababu ambayo sikuipima katika ujazo wa kusema yawezekana ikawa ni sababu kuu.
Kama kawaida nikamtafuta Nyambura faragha na kuzungumza naye.
Akanijibu kwa hekima kabisa kuwa ni heri nikazinunua hisa za Revo ili niweze kuwa na umiliki mkubwa zaidi wa ile kampuni inayotanuka.

“Wewe zinunue lakini ili kuboresha urafiki wenu mweleze kuwa wakati wowote akihitaji kurejea katika kampuni basi anakaribishwa!”
Nikayapokea vyema manenoya kinywa cha mwanamke, nikayafanyia kazi.
Mwezi mmoja baadaye nikazinunua zile hisa na kisha nikatangaza tarehe rasmi ya kufunga ndoa na Nyambura!!
Nilipanga iwe ndoa ya kanisani.

Revo akasahaulika nami nikawa mmiliki mkubwa zaidi wa kampuni ile, hapo nhikiwa na asilimia 90 ya umiliki.
Nilikuwa na sauti kubwa zaidi katika vikao vya kampuni.
Katika kikao kimoja nikampandisha cheo Nyambura kutoka kuwa msemaji mkuu wa kampuni hadi kuwa msimamizi wa ofisi zote za kampuni yetu zilizoko mikoani!!
Sikuwa najua ninachofanya kinaweza kuwa na madhara yoyote, nilichotazama ni kwamba nafsi yangu inafurahi huku ya Nyambura ikifurahi zaidi.
Baada ya maamuzi hayo, nikampigia mama simu na kumfahamisha kuwa ule mji tulivu nilioapa kuwa ninahitaji kuupata basi nimebakiza hatua chake kabla ya kuingia.

Mama akanitakia heri!
Lakini hakusahau kutoa maonyo yale ya mzazi kwenda kwa mtoto.
“Uwe makini baba eeh! Sisi wanawake hatutabiriki kabisa….” Yalikuwa maneno ya mama…..
JIFUNZE!
Usipende kuamini sana kupita kiasi, kwa sababu huko kuamini kwako nsdo chanzo cha maumivuyako.
Sisemi kwamba usiamini la! Nasema usiamini sana kupitiliza…

ITAENDELEA..
 
Attachments

  • IMG_20200826_020319.jpg
    IMG_20200826_020319.jpg
    12.3 KB · Views: 17
Sio unaleta epsode mbili halafu unalala mbele, hatujakutuma, umeamua kushusha we shusha
 
ITAENDELEA..View attachment 1548234
Simulizi : Mji Tulivu Ulionipa Ugonjwa Wa Milele
Sehemu Ya Pili (2)

MASHAKA yakiingia katika ndoa yoyote ile iliyokuwa imara hapo awali… huu ni mwanzo wa ndoa kugeuka kuwa kama bomu lililotegeshwa na lisijulikane ni lini litalipuka!
HATIMAYE ikawa kama nilivyopambana kwa udina uvumba iwe. Nyambura akawa mke wangu halali kabisa aliyetambulika kwa kila mtu.

Tuliendelea kufanya kazi katika kampuni yangu….lakinihatukudumu sana, Nyambura akanieleza kuwa anajiona utendaji kazi wake unashuka kwa kasi kubwa sana, akaniweka chini na kunishauri kuwa kama sitajali basi yeye ashughulike na biashara nyingine na mimi niendelee kuwa mkurugenzi wa ile kampuni.

Wazo la Nyambura halikuwa baya, niliridhika kabisa na maelezo yake na nikampa uwanja wa kuamua ni kitu gani tunaweza kufanya.

Nilimpa nafasi ya kutulia na kuandika mchanganuo wa chochote chenye manufaa ambacho anadhani ni sahihi kufanya.
Wakati akiwa katika kuunda wazo lake la biashara, mama yangu alipatwa na maradhi yaliyochangiwa na utu uzima, sasa alikuwa analalamika kuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Taarifa za ugonjwa wa mama nilimshirikisha Nyambura pia, huku nikiacha kuzipa uzito mkubwa sana.
Usiku tukiwa mezani kwa ajili ya kuupitia mchanganuo wa Nyambura, badala atoe makaratasi aliyoyatumia kuandika mchanganuo ule, Nyambura alizungumza maneno machache tu.

“Nitaenda kumuuguza mama kwanza!”
Sikutarajia hata kidogo kauli ile kutoka kwa Nyambura, nilistaajabu.
Nikacheka nikijua anatania lakini alikuwa anamaanisha kile alichokuwa anakisema.
Hakutaka biashara wala kitu kingine kile alisema kuwa suala la afya ya mama lianze kwanza!

Ndugu msikilizaji kama mapenzi huwa yanaongezeka uzito na yanaweza kupimika, basi Nyambura alikuwa ameongeza kilo tano za mahaba yangu kwake.
Nikaukumbuka usemi usemao kuwa ukimpata mwanamke ambaye anaweza kuwa mama kwako, mama kwa watoto wako na mama kwa familia yako basi mkamate kwa mikono miwili kamwe usimwache aende zake.

Nami nikakiri kuwa Nyambura alikuwa na sifa hizi, alinipenda mimi na familia yangu!!
Siku mbili baadaye alifunga safari kuelekea kijijini alipokuwa akiishi mama yangu!
Nikabaki mjini peke yangu.
______
Sifa za Nyambura kutoka kwa mama zilinifanya nizidi kuvimba kichwa na kila mara nikitabasamu na kujisifu kuwa nilichagua mke ambaye wengi hawana!
Kwanza nilimkuta akiwa ni msichana bado, pili ana akili sana na ni msikivu!
Hakika nilikuwa na kila sababu za kujisikia kuwa mimi ni wa pekee zaidi.
Siku moja asubuhi niliamka kama kawaida, si unajua tena mazoea hujenga tabia. Ilikuwa kawaida ya mke wangu kuniandalia nguo za kuvaa, yaani ni yeye aliamua leo navaa hiki na kesho kile.

Alikuwa ananyoosha nguo zangtu vyema na kuniwekea juu kabisa ya nguo nyingine ama wakati mwingine alikuwa akiziweka katika kochi, nikitoka kuoga nazivaa.
Siku hii hakuwepo basi kila kitu nikalazimika kufanya mimi mwenyewe.
Nilipatwa na uvivu na kutamani hata kuvaa nguo ambazo si za kunyoosha ila ofisini nilikuwa nimekabiliwa na ugeni wa heshima sana nisingeweza.

Upesi nikaitafuta pasi ilipo, na baada ya kuiwasha nikaliendea kabati la nguo, nikaanza kutafuta nguo, nilivuruga hovyo!
Badala ya kupata nguo nikakutanana kitu kigeni kabisa katika macho yangu ambacho sikutarajia kukutana nacho.

Nilikutana an akaratasi jeupe sana huku likiwa limeandikwa jina langu kwa kalamu nyekundu.
Hapakuwa na maelezo yoyote zaidi ya jina langu kamili. Nilitumia dakika tano nzima kuitazama karatasi ile ambayo haikuwa pale bahati mbaya bali ilikuwa imehifadhiowa.

Sasa ni karatasi ya nini? Nilijiuliza…..
Na kwanini nimeandikwa jina langu kwa kalamu nyekundu.
Nilitamani kumpigia simu mke wangu Nyambura ili nimuulize nini maana ya karatasi ile lakini nikahofia kuwa kinaweza kuzuka kizaaazaa wakati akiwa na mama kule kisha nikaonekana kama mtu nisiyejua kutafakari mambo kwa kina.
Nikalimezea lile jambo sikumgusia Nyambura kabisa.

Nikanyoosha nguo niliyoichagua nikavaa na kwenda kazini, kinyonge kabisa huku akili yangu ikiwa inahangaika kujiuliza ni nini kinaendelea.
Au ameniendea kwa mganga? Nilijiuliza punde tu baada ya kuingia ofisini. Wazo hilo lililonipitia ghafla kichwani lilinifanya nijisikie vibaya sana kwa sababu katu maishani sijawahi kufanya mambo ya kishirikina japokuwa siwezi kuapa kuwa kamwe sitashiriki.

Wakati nafikiria juu ya jambo lile mara ghafla moyo wangu ukapiga kwa nguvu sana nikajikuta nimesimama, mwili wangu ukikumbwa na joto kali licha ya uwepo wa kiyoyozi.
Nilikuwa nimekumbuka kuwa nimeona kitu kingine cha ziada katika lile karatasi ambacho sio cha kawaida kabisa.

Katika yale majina yaliyoandikwa pale lilikuwa limeambatanishwa pia jina langu la utotoni!!
Jina ambalo niliacha kulitumia miaka mingi sana huko nyuma, jina ambalo lilisahaulika kabisa.
Fantom!!
Jina hili mke wangu alilitoa wapi, na aliliandika kwa kalamu nyekundu ili iweje.
Niliumia sana kichwa, nikawaza na kuwazua.

Mwisho wa siku nikanyanyua simu na kumpigia katibu muhtasi.
“Waambie sitaweza kushiriki mkutano leo, nitafutie muwakilishi tafadhali!” nilimweleza na sikungoja majibu, nikakata simu na kujilaza katika meza yangu ya ofisi, nikishindwa kabisa kupata maana ya ile karatasi katika kabati yangu!
“Au sio Nyambura aliyeiweka mle ndani…” nilijiuliza, lakini nikalipuuza wazo lile, mle ndani tuliishi wawili tu. Sasa iweje lile karatasi liingie biola kuingizwa?
Na kama sikuliingiza mimi basi ni Nyambura!
Sasa kwa nini?

Niliomba kimoyomoyo jambo lile liwe katika namna zozote zile lakini isiwe mambo ya kishirikina, sikutaka hata kidogo kuamini kuwa yawezekana Nyambura amenipika na kunifanya anavyotaka.
Siku hii sikuweza kulala nyumbani, sikuwa na amani kabisa nikaamua kulala nyumba ya kulala wageni, Nyambura aliponipigia simu niliongea naye na kumweleza kuwa nilikuwa nyumbani.

Nilipokata simu nafsi ilinisuta, kwa mara ya kwanza nilikuwa nimemdanganya mke wangu!
Sikuupata usingizi siku hii, hadi majira ya saa nane usiku bado nilikuwa macho tu.
Hakika lile karatasi lilikuwa limenichanganya sana na sikujua nitaanza vipi kumueleza mke wangu ilimradi tu tusigombane.

Nililala nikiwa nasumbuliwa na kisa kimoja…. Asubuhi mambo yakapamba moto!
*****************
ASUBUHI majira ya saa nne nilikabidhi chumba kisha nikaongoza njia kuelekea nyumbani, nia ikiwa kubadili nguo kisha nielekee ofisini.
Nilianza kupuuzia juu ya karatasi lile lililoandikwa kwa wino mwekundu majina yangu matatu, moja kati ya jina hilo nikiwa nimeacha kulitumia kiwa miaka mingi sana.

Nilipanga kuwa nitakapotoka kazini nitaenda nyumbani kwa Revo rafiki yangu kumgusia juu ya jambo lililotokea nyumbani kwangu, lakini nilipanga kuyapanga maneno ili asije akapata pa kusemea eti alinieleza kuwa nisiwe na papara katika kuoa na sikutaka kabisa arejee lile swali aliloniuliza ikiwa ninamjua vizuri Nyambura.

Nilifika nyumbani na kuingiza funguo mlangoni.
Ajabu! Mlango ulikuwa wazi tayari.
Ina maana nilisahau kuufunga au? Nilijiuliza huku nikiingia ndani kwa tahadhari kubwa kabisa.
Nilianza kusikia dalili ya uwepo wa kiumbe hai pale ndani. Upesi nikawahi kuchukua chupa tupu ya soda pale sebuleni tayari kwa kukabiliana na yeyote atakayethubutu kunikabili.

Nilienda hadi nikakifikia chumba, sasa nikasikia sauti ya kike ikiwa katika kilio cha kwikwi.
Nyambura mke wangu yuko safarini, huyu ni nani ndani ya nyumba yangu!
Nikaufungua mlango upesi huku nikitanguliza ile chupa mbele.
Lahaula! Alikuwa ni Nyambura, akanitazama kwa jicho kali jekundu lililoiva haswa kwa hasira.

Nilijikuta ile chupa inanitoka huku ikipasuka vipande.
“Ulikuwa na nani huko ulipolala?” aliniuliza huku akisimama. Mikono yake ilikuwa inatetemeka sana, alikuwa amevaa nguo ya kulalia pekee.
Michirizi ya machozi ilijionyesha dhahiri katika mashavu yake.

Alikuwa ananisogelea, mimi nilikuwa katika pumbazo nisijue nini cha kujibu.
Sikutarajia kabisa shambulizi lile la ghafla kiasi kile.
“Joshua ulilala na nani, hadi kufikia hatua unaniongopea kuwa upo nyumbani kumbe unalala kwa hawara zako, Joshua ni nini hiki unanifanyia eeh! Ni nini Joshu….” Alilalama huku akibubujikwa na machozi. Akashindwa kumalizia akanitazama kidoleni….

“Na pete ya ndoa ukaona uivue kabisa, ukamwambia kuwa hauna mke….wanaume sijui mnataka nini katika maisha ya wanawake. Au Mungu alifanya makosa kutuumba? Au kwa sababu tulitoka katika mbavu zenu” Alizungumza huku akinitazama kidole changu ambacho kilitakiwa kuwa na pete.

Aisee! Nilijisikia aibu sana, si kweli kwamba nilikuwa nimeivua pete kwa sababu za kumsaliti mke wangu lakini niliivua ili kuisafisha na nikasahau kuivaa tena.
Sasa ile bahati mbaya imegeuka kuwa kesi inayohitaji majibu. Ningeyatoa wapi majibu!!

Mdomo ulikuwa mzito sana kana kwamba umedungwa sindano ya ganzi.
“Umekuja lini?.” Nilijitutumua nikamuuliza huku nikiwa sijiamini. Lilikuwa swali la kizembe sana
“Ulitaka nikueleze siku ambayo ninakuja ili uvae pete na kuja kunipokea uwanja wa ndege na maneno matamu kuwa unanipenda sana eeh!” alisema kwa uchungu Nyambura, nikajaribu kumshika ili nimsihi, akajitoa katika mikono yangu na palepale akaninasa kofi kali usoni.

Niliumia lakini kwa hali aliyokuwanayo Nyambura sikuwa na chochote cha kumfanya. Nilikuwa upande wa mashtaka na yeye akiwa ni mshtaki.
Alizungumza mengi sana mwanamke yule kiasi kwamba nikajikuta nikikosa walau doti ya ujasiri kuweza kumshutumu juu ya kile kikaratasi chenye jina langu katika wino mwekundu.

_____
KESI ile iliisha lakini Nyambura akiwa mnyonge kabisa. Lakini hakuwa na budi kukubaliana na utetezi wangu, maisha yakaendelea.
Ili kuyajenga tena upya mazoea ya kusahau kile kilichotokea nililazimika kumpa mke wangu likizo fupi kidogo ili aende nyumbani kwao kusalimia ndugu zake.

Licha ya kwamba alipoondoka nilimweleza kuwa natamani abaki lakini kwa uhakika nilitamani sana aondoke, sikuwa nikiishi kwa amani kabisa huku Nyambura akiwa ameninunia.
Kuondoka kwa Nyambura kukairejesha amani yangu lakini kukinifanya niwe mtu ninayeishi kwa tahadhari sana ili nisije kufanya makosa katika hatua ninazopita kisha nikamkwaza mke wangu kwa kitu ambacho si kweli kabisa.
Napenda kukiri mbele yenu tena kuwa nilimpenda Nyambura kwa dhati kiasi kwamba sikuwa napatwa na msisimko wowote ule nikianza kumfikiria msichana mwingine.

Labda hili ndo kosa kubwa zaidi ambalo niliwahi kufanya katika maisha yangu, kupenda kwa dhati!!
Sijui kama maamuzi haya yalinifanya kuwa mjinga, ama zezeta!

Itaendelea...
 
Sehemu ya nne

MKE wangu bila kujua kuwa mumewe nilipitia njia za mkato katika kusababisha ile mimba ipatikane alinisihi sana twende kumpa zawadi yule daktari ambaye alituwezesha hadi nikapona na kuweza kumjaza mimba.

Nafsi ilinisuta sana siku tuliyofunga safari hadi kwa daktari kwa ajili ya kumpatia zawadi ambayo haikuwa stahiki yake.
Lakini ningeanza vipi kukataa mbele ya mke wangu?
Kama ningekataa kwenda basi nilitakiwa pia kuwa tayari kumweleza kuwa ile mimba chanzo ni nguvu za giza.

Sikuwa tayari!!
Kwa daktari napo zikanitoka pesa taslimu shilingi laki tano kama asante kwa daktari, akatupongeza huku akimsihi Nyambura ajitahidi kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili aweze kuimarisha afya yake na ya mtoto ambaye hajazaliwa bado.

Kwa sababu aliyetusaidia ni daktari yule basi tukaamua pia kliniki kufanyia kwake.
Pesa zikaendelea kukatika tu!
Roho iliniuma sana kuiona ile nusu milioni ikiteketea kwa mtu asiyehusika nayo hata kidogo.

Ujauzito ulipofikisha miezi mitatu, mama yangu akahamia rasmi nyumbani kwangu kwa ajili ya kufanya uangalizi wa karibu kabisa kwa mkamwana wake. Jambo hili lilinifurahisha sana, mama yangu alikuwa mtu wa kujali siku zote.

Kabla sijaoa aliwahi kuniambia kuwa hata nikikukataza kuoa kabila fulani lakini ukaamua kuoa kwa sababu zako mwenyewe nitampenda kwa dhati mkeo!!
Sasa yalikuwa yanatimia.

Siku tatu za mama kukaa pale nyumbani, aliniita siku moja na kunieleza kuwa alipoingia tu pale ndani na kutazamana na Nyambura amesisimka vibaya mno, vinyweleo vimemsimama na amekosa raha kabisa. Kauli ya mama ilinishtua sana, nikajisemea kuwa utu uzima dawa labda mama ametazamana na kile kiumbe ambacho kimepatikana kwa sababu ya nguvu za giza.

Lakini sikuwa tayari kukiri kuwa kuna tatizo mahali, nikaendelea kupigana hii vita dhidi ya wanaonitazama na dhidi ya nafsi yangu mwenyewe!
Nilimwondoa mama hofu kabisa na kumweleza kuwa aondoe mashaka hakuna kitu kibaya kinachoendelea pale.

“Joshua wewe ni mwananngu wa kumzaa kabisa wala sijapewa na mtu kumlea…. Nimekwambia nilichohisi. Sasa usije ukayabeba na kuyapelekwa kwa mkeo akaanza kunichukia. Wewe ni mtu mzima sawa baba!” alinieleza mama huku akinishika shika bega langu kirafiki kabisa.

Nilijisikia hatia sana, nikaamini kuwa chanzo cha mama kusisimka ni kitendo cha mimi kwenda kwa mganga na kufanikiwa kupata uwezo wa kumpa mimba mke wangu.
Nisingeweza kumwambia mama, zaidi nilikuwa naombea tu isijekuwa kituko mtoto atakapozaliwa… niliombea iwe heri tupu.
Lakini nilijionya kuwa si kila uombalo hutimia kama lilivyo!
Mama aliendelea kuwa karibu kabisa na Nyambura, akimpa ushauri wa hapa na pale na wakati mwingine kumpikia pale anapopatwa na hamu ya kula.

“Nyambura, ulinidekeza sana ulipokuja kule kijijini wakati naumwa… sasa ni zamu yako. Yaani nidekee kuliko anavyodeka mtoto wa mwisho, wewe ndo mkamwana wangu wa pekee….” Niliwahi kumsikia mama akimwambia Nyambura, nilifurahi sana kuona mama anaelewana vizuri kabisa na mke wangu.
Miezi sita ikakatika, mama akanijia tena kwa mara nyingine safari hii ilikuwa ni ndoto.

Akanisimulia ile ndoto ilikuwa inatisha lakini niliamua kuipokea kama ndoto, alinieleza kuwa aliona katika ndoto mke wangu anazaa lakini nilipotaka kumchukua mtoto akamkatalia na kumpa mwanaume mwingine. Ukazuka ugomvi na mwisho wa siku yule mtoto akaanguka chini na kupasuka kichwa akavuja damu hadi akafa mimi nikakamatwa na kupelekwa polisi kwa kesi ya kushiriki katika mauaji…

Kwa mara nyingine nilijichekesha na kumwondoa mama hofu. Nilimwambia anaota ndoto hizo kwa sababu anawaza sana juu ya mapokeo ya mjukuu wa kwanza.
“Usijisikie vibaya mwanangu, mimi nakueleza kwa sababu tu nakupenda na sitaki siku moja nikwambie eti niliwahi kuota, ni bora niiseme tu hii ndoto ijiondokee zake” aliniambia mama yangu kwa upendo mkubwa.

Kisha akaelekea chumbani kwa Nyambura kumjulia hali.
Hofu ikaanza kunikaribia hasahasa kulingana na haya maneno ya mama na njia nilizotumia kumpata mtoto yule mtarajiwa. Lakini nilijipa moyo kuwa ndoto itabaki kuwa ndoto tu haiwezi kuwa na madhara yoyote.

Nikaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutengeneza kipato kikubwa kwa ajili ya familia yangu.
Hatimaye ikatimia miezi tisa, mke wangu akajifungua salama kabisa mtoto wa kike!!
Mtoto alikuwa mwenye afya tele, nisiwe mwongo mtoto alimfanana sana mama yake.
Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwetu, hasahasa mama ambaye alimnyanyua juu mjukuu wake kwa mara ya kwanza. Akamuombea dua kabla ya kumkabidhi kwa mama yake.

Tukamuita mtoto Agness, jina la hayati mama yake Nyambura.
Juma moja likapita nikaona nisifanye mzaha kusubiri kupigiwa simu na mganga, nikaamua kwenda mwenyewe kwa sababu mizimu ilihitaji kitu kutoka kwangu baada ya kunifanikishia kupata mtoto.
Nilimkuta mganga akiwa anatabasamu, kabla sijasema lolote akanipa hongera kwa kupata mtoto wa kike.

Nilishangaa amejuaje juaje? Lakini sikumuuliza akanikaribisha ndani nikaketi na kumweleza nia yangu.
Akanieleza kuwa mizimu inapokea zawadi na kuzungumza na marafiki siku ya ijumaa usiku pekee, hivyo natakiwa kufika pale siku ya ijumaa nisikie mizimu inasema nini.
Siku ile ilikuwa ni jumatano, nikamuachia mganga posho kidogo na kuahidi kuwa nitafika hiyo ijumaa.

“Hata jina mlilomchagulia ni jema sana…. Agness naamini mizimu italipokea vizuri!” alinieleza wakati ananiaga….. nilishtuka sana kuwa mganga huyu amekuwa mwepesi sana kugundua kila kinachoendelea katika maisha yangu.
Je? Haitakuwa hatari sana kwangu pindi wakiamua kumdhuru mtoto wangu!! Nilijiuliza kwa mashaka huku nikiondoka.
______
Niliona siku kama haziendi kabisa, nilitamani kumalizana na mizimu kabisa ili niwe huru na mambo yangu hasahasa kumlea mtoto wangu na ndoa kwa ujumla.
Ikawa usiku ikawa mchana ikawa usiku tena kukakucha, ijumaa ikafika.

Niliwahi sana ofisini na kufanya shughuli zangu zote za muhimu, nikawagawia watu majuukumu. Na mwisho wa siku nikaondoka majira ya saa kumi, nikawasili nyumbani majira ya saa kumi na moja. Nikamwona mama na Nyambura wakifanya mazoezi ya kutembea, nikautazama ule upendo wa mama yangu kwa Nyambura nikamshukuru Mungu kwa kunipa mama yule.

Nikaingia ndani na kubadili nguo kisha nikaaga kuwa naenda kuonana na wadau fulani kuna jambo kubwa tunataka kulifanya hivyo tunaenda kujadiliana. Kibindoni nikiwa nimebena pesa taslimu shilingi milioni tatu.

Niliamini mizimu itaomba pesa.
Nyambura alinisihi sana nisiende anatamani niwe pembeni yake, lakini haikuwezekana nisingeweza kuacha wakati ndo siku pekee ya kuzungumza na mizimu.

Nilimbembeleza hadi nikaondoka, nikambusu Agness shavuni na kuondoka.
Moja kwa moja hadi kwa mganga!
Mganga alinipokea vyema, akaniambia niliache gari nyumbani kwake na sisi twende kwa miguu akasema si mbali sana, na hata kama ni mbali hatuwezio kwenda kuipigia mizimu kelele kwa kuitembelea tukiwa na gari.

Hapo ilikuwa ni saa tano usiku safari ilipoanza.
Tulitembea kwa mwendo wa saa zima hadi kulifikia eneo la tukio, lilikuwa ni shamba kubwa ambalo lilikuwa halina mazao yoyote, tukajongea hadi pale, mganga yule akaanza kupiga manyanga yake huku akizungumza lugha nisiyoijua.

Mwisho zikaanza kusikika ngurumo na mwanga mkali kutoka katika mti mmoja katika lile shamba. Nilikuwa natetemeka sana, hapo kabla sikuwahi kukutana na mizimu……
Sasa leo naja kuzungumza nayo!
“Mizimu imeshuka tayari… sasa nakuacha uzungumze nayo.

Hili halinihusu mimi….” Mganga aliniaga huku akitaka kuondoka, nikamzuia.
“Sasa lugha nitaielewaje…” nilihoji kwa mashaka
“Ni Kiswahili, kuwa makini katika kujibu tafadhali usije kuiudhi mizimu… ukiwaudhi umeniua na kujiua wewe mwenyewe na ukoo wako.” Alinionya.
Nikabaki kungoja, ule mwanga ukaanza kufifia kiasi kisha kikatoka kibabu kizee kikiwa na mkongojo.

“Kijana wangu Joshua.. karibu katika ulimwengu wetu…” alizungumza kikongwe yule.
“Nimeagizwa kama mwakilishi, nimeambiwa kuwa tayari umepata kile tulichokuahidi… na sasa ni zamu yetu kukuona wewe ukitimiza ahadi yako.”

Nikatikisa kichwa kukubali, kikongwe yule akaendelea.
“Sogea… sogea hapa…” aliniamrisha. Nikasogea hadi alipokuwa, akanionyesha bahasha fulani nyekundu, akaniambia niiokote.

Bahasha ile haikuwepo hapo kabla!
“Wazee wameandika kila kitu. Utasoma na kama kuna maswali utamuuliza aliyekuleta hapa kisha akatuita nasi tukashuka.” Alimaliza kisha mwanga ule ukang’ara ukinimulika machoni, ngurumo zikasikika na ulipotoweka ule mwanga yule kikongwe hakuwepo.

Nilitishika sana kwa sababu yale yalikuwa mauzauza taslimu.
Nikiwa nimeganda pale na bahasha yangu alifika yule mganga akanishika mkono tukaondoka… moja kwa moja hadi nyumbani kwake.

Alinionya nisiseme lolote kuhusu kilichotokea hadi tutakapofika nyumbani, hivyo njia nzima kila mmoja alikuwa kimya.
Hatimaye tukafika!
Tukaifungua bahasha na kuisoma vyema nini matakwa ya mizimu.

Nilirudia kuisoma mara mbilimbili hakuna kilichobadilika, walichohitaji ndo kile nilichokuwa nakiona pale katika maandishi yale machache.
Niliishiwa nguvu, tumbo likaanza kuunguruma na kichwa kuniuma sana.
Nikampa yule mganga asome upya na kunielewesha.

Na yeye akaona vile nilivyoona mimi!
Kichwa kikazidi kuuma, sikuamini hata kidogo kuwa niliposema kuwa nitatoa zawadi yoyote ingewezekana kuwa hii waliyoomba.
Nilitamani nyakati zinisaidie kwa kurudi nyuma ama kunifanya niwe ndotoni ili niamke na kuachana na maono haya.
Lakini hapakuwa na ndoto!

Maandishi yalikuwa yameandikwa kwa kalamu nyekundu iliyokolea.
Halikuwa ombi bali amri!

Itaendelea..
Sehemu ya tano

NILIRUDIA tena kuisoma karatasi ile iliyoandikwa kwa wino mwekundu, na mganga naye akarudia kuisoma.
Nilichanganyikiwa sana….

Mganga akanisihi niende nyumbani nikafikirie kwa kina kisha tutaonana siku inayofuata kwa sababu nilipewa siku saba za kufanya utekelezaji basi zinatosha sana kwa ajili ya kutuliza akili kufikiria kwa kina na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Nilimweleza kuwa siwezi hata kuendesha gari nahisi nikiendesha nitapata ajali, akaniambia kama inafaa basi nilale nyumbani kwake.
Nikamweleza haitawezekana kwani mke wangu hawezi kulala bila mimi kurejea nyumbani.

Akafikiri kwa muda kisha akanifanyia msaada mmoja, akaniendesha hadi nyumbani kisha yeye akarejea nyumbani kwake kwa kutumia usafiri wa pikipiki.
Kweli nilimkuta Nyambura hajalala alikuwa sebuleni anatazama runinga.

Aliponiona akanifuata na kunikumbatia huku akinipa pole kwa uchovu.
“Mbona unatetemeka hivi?” aliniuliza.
“Kichwa kinaniuma sana ghafla… sijui malaria hii?” nilitoa jibu la uongo.

Nyambura akanishika kiuno akanikongoja hadi chumbani, akanivua shati na viatu, kisha suruali yangu na mwisho akanipeleka hadi bafuni tukaoga pamoja, huku akinipa pole kedekede na kunifariji.
Mke wangu alikuwa ananipenda sana jamani!

Alinifariji sana hadi nikasahau kuwa nina balaa linanikabili, masharti kutoka kwa wazee wa mizimu.
Tulilala akiwa amenikumbatia, alipopitiwa na usingizi nikajitoa katika mikono yake na kuanza kutafakari upya juu ya maombi ya wazee.

Maombi ambayo sikuwahi kufikiria hata kidogo kuwa mizimu ingeweza kuomba.
Nilijisahau kabisa na kuwa muoga wa kutoa kafara ama zawadi yoyote inayohusisha damu, mizimu ikanikubalia nami nikajitapa kuwa siwezi kushindwa kutoa zawadi nyingine watakayohitaji.
Nilijua watahitaji pesa!
Haikuwa!

“Kampuni yangu iwe yao, na pesa zilizopo benki ni mali yao na nisiziguse kuanzia dakika hiyo niliyopokea barua…” nilikumbuka baadhi ya maneno katika ile barua.

Milioni mia moja na sabini!!
Nilikikumbuka kiwango cha mwisho cha pesa nilichokiacha katika akaunti ya kampuni, halafu ilikuwa kiherehere changu tu, kuhamishia pesa kutoka katika akaunti yangu binafsi kwenda kwenye akaunti ya kampuni.

Sasa pesa zote zile ni mali ya mizimu, na si pesa tu bali kampuni yote kiujumla. Na kati ya hizo pesa katika kampuni, milioni mia moja nilikuwa nimekopa benki kwa kuweka dhamana hati ya nyumba yangu niliyokuwa nimejenga.

Pagumu hapo!
Nilipagawa nikaketi kitako, nikaminyaminya kichwa changu huenda nikapatwa na fikra mpya lakini hakuna nilichoambulia. Ukweli ulibaki uleule kuwa nilikuwa katika mtihani mmoja mzito sana na nilikuwanazo siku saba tu za kufanya utekelezaji.

Nikajaribu kukumbuka labda kuna sehemu ambayo inahusu kipingamizi katika barua ile lakini haikuwepo, hivyo lile halikuwa ombi bali amri.
Kutambua kuwa ile ni amri kulinifanya nikanyong’onyea zaidi….. Mizimu ilikuwa imenikamata pabaya mno.
Sikuwa na njia mbadala ya kufanya jambo lolote.

Nilipitiwa na usingizi baadaye hata sikumbuki ilikuwa saa ngapi.
Asubuhi majanga yakaendelea.
Mama Agy alikuwa anaumwa mgongo. Alipiga mayowe kadri maumivu yalivyokuwa yanazidi.

Mama akatoka mbio kuja kumtazama, huku akinihimiza kumpeleka hospitali.
Nilimbeba mama Agy hadi katika gari, mama akambeba Agy mwanangu, nikaendesha kuelekea hospitali. Tayari nilikuwa nimempigia simu daktari yule yule aliyemsimamia Nyambura hadi alipojifungua.

Wauguzi walimpokea Nyambura na kumkimbiza katika wodi ya wazazi, huko alifanyiwa vipimo na kilichofua hapo ni pesa moja baada ya nyingine.
Hadi siku inaisha na Nyambura kupata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani nilikuwa nimetumia kiasi cha shilingi laki mbili kasoro senti chache.

Akiba iliyobaki ilikuwa shilingi laki moja na nusu pekee.
Hii ndo pesa iliyokuwa mfukoni, kumbuka kuwa mizimu ilitopa tamko kuwa sitakiwi kutoa walau senti tano katika akaunti ya kampuni yangu.
Nilianza kutetemeka, hasahasa nilipokumbuka kuwa sitaruhusiwa na mizimu kutoa walau senti tano katika akaunti yangu.

Na pia sikutakiwa kusimamisha shughuli za ofisi.
Jioni majira ya saa kumi na mbili baada ya kumrejesha Nyambura nyumbani, simu yangu iliita na ilikuwa ni namba binafsi ya katibu muhtasi wangu.
Alinieleza mambo kadhaa juu ya siku nzima ya ofisini, kwa sababu ilikuwa ni siku ya jumamosi ofisi yetu ilikuwa inafungwa saa saba mchana.

Akanieleza kuwa siku ya jumatatu kuna pesa tunatakiwa kuingiza kwenye akaunti ya kituo kimoja cha runinga kwa ajili ya kulipia tangazo ambalo huwa linarushwa katika kituo chao.
“Ni shilingi ngapi?” nilimuuliza.
“Ni laki saba wametupunguzia awali walisema milioni moja.” Alinijibu.
Nilisikia kama lugha za kichina zinaniingia masikioni na nisielewe zina maana gani hata.

Laki saba? Naitoa wapi mimi…. nilijiuliza
Ni kweli ilikuwa ni pesa ndogo sana katika milioni mia moja sabini zilizokuwa katika akaunti.
Lakini siruhusiwi kuzitoa ama la nizitoe na kukutwa na mabalaa makubwa.
Mfukoni nilikuwa na shilingi laki moja na nusu.

Nikamweleza katibu muhtasi kuwa nimemuelewa, tukaagana akakata simu.
Wazo la kukopa likanijia kichwani mwangu.
Nikamfikiria Revo, kweli akanikopesha shilingi laki tano.
Lakini haikufaa kitu, matatizo yalikuwa mengi sana, nikajikuta hadi jumatatu inafika nikiwa na shilingi laki nne tu.

Nilijitahidi kutoa matumizi yaleyale ya siku zote nyumbani kwangu kwa sababu sikutaka mtu yeyote agundue kuwa kuna utofauti.
Nilikuwa naugulia ndani kwa ndani.
Mtoto nilikuwa nampenda na aliniletea heshima lakini kwa hali ilivyokuwa nikajikuta taratibu natamani nyakati zirudi nyuma ningoje muujiza wa Mungu tu niweze kupata mtoto.

Lakini shida ni kwamba nyakati haziwezi kurudi nyuma kamwe. Tayari nilikuwa nimejiingiza katika janga la mizimu, njia ambayo hata haikuhitaji kiwango chochote cha elimu kutambua kuwa haikuwa njia sahihi.
_____
UBAYA wa mawazo ni kwamba unaweza kuwaficha wengine lakini sio kuuficha mwili wako uliokubeba, ukiwaza sana mwili nao unanyauka.
Naam! Nikaanza kupungua, zilikuwa ni siku chache tu lakini nilionekana dhahiri kuwa sikuwa sawa hata kidogo.

Nikiwa bado natafakari ni kitu gani nitafanya, Nyambura mke wangu ananipa rungu jingine katika utosi wangu.
Ananipa nambari za mtu nimuwekee kiasi cha shilingi milioni nne, amchukulie mzigo katika biashara waliyokuwa wanafanya ili aendelee kumzungushia asijekusahaulika katika biashara hiyo aliyokuwa anafanya..

Akanieleza kuwa anatamani angeenda benki kujichukulia pesa katika akaunti yake lakini hajioni kama yupo sawa.
“Usijali mke wangu, wewe haujawa wa kutembea bado… nitakufanyia usijali.” Nilimjibu huku moyo wangu ukipiga kwa nguvu sana kana kwamba nilikuwa nimekamatwa ugoni.

Hiki nini Mungu wangu!! Nilijiuliza baada ya kujifungia chumbani, kama laki saba ya matangazo ilikuwa mbinde kuipata, vipi kuhusu hii milioni nne?
Machozi yakaanza kunitoka, jasho nalo halikubaki nyuma.

Nilikuwa mwenye hofu!
Siku zikasogea na hatimaye zilibaki siku mbili sawa na masaa arobaini na nane kabla sijakutana na wazee na kuwakabidhi kampuni yao pamoja pesa zote katika akaunti.
Ahadi yangu ilikuwa inanihukumu mchana kweupe!
Nilichanganyikiwa sana, nikaiona dunia inanionea, nilitamani kumshirikisha mtu lakini ingesaidia nini na mizimu imesema hilo sio ombi bali ni lazima.

Mara kwa mara mama alinieleza kuwa kuna jambo nawaza na linanipelekesha puta sana akanisihi nimweleze lakini sikuwa na ujasiri huo nikaishia kumpiga danadana tu!
Hatimaye siku ya tukio ikawadia!!
NAKUSIHI
Kamwe usitoe ahadi wakati ukiwa na hasira pia usitoe ahadi wakati umechoka na ninakukumbuka kuwa usifanye maamuzi wakati una furaha kubwa.

Kwa asilimia tisini ahadi hizo utazijutia! Hata kama hautajuta mbele ya watu….
Moyoni utakuwa shuhuda!
***************
Kila mtu hufanya makosa katika Maisha, lakini haimaanishi kuwa lazima yamgharimu maisha yake yote.
Wakati mwingine watu wema hufanya uchaguzi usio sahihi (mbaya) hii haimaanishi kuwa ni watu wabaya, ila inamaanisha kuwa ni Binadamu.

Kubali kukosea na ujifunze kukosolewa! "
KABLA ya kwenda kwa mganga nilimpigia simu na kumueleza kuwa kama inawezekana aiombe mizimu inivumilie kwa siku walau nne mbele kwa sababu bado mwanasheria wangu alikuwa anaandaa nyaraka maalumu kwa ajili ya kuuza hisa zangu kwenda kwa mtu mwingine.

Nilimueleza kwa kirefu sana huku nikiwa natetemeka, akaniambia kuwa atanipigia baada ya muda.
Ikawa hivyo, akanipigia baada ya robo saa kupita akanieleza kuwa ili aende kuzungumza na mizimu hawezi kwenda mikono mitupu. Akanitajia mahitaji ya kwenda kuonana na mizimu.

Akanitajia mbuzi mweusi, mafuta ya nazi lita moja, nazi saba na makorokoro mengine mengi.
“Ambavyo ni sawa na shilingi ngapi?” niliuliza kinyonge huku kichwa kikiwa kinaniuma sana, kwa wakati ule kitu chochote kiitwacho pesa kilikuwa kinaniumiza sana kichwa!

Kila ikitajwa pesa nakum,buka masharti ya mizimu iliyonipa mtoto juu ya kampuni yangu.
“Laki moja na elfu ishirini.” Alinijibu kwa sauti kavu kabisa.
Nikakata simu huku kijasho chembamba kikinitoka.
Nikafikiria ni wapi tena pa kukopa.

Nikatafuta majina katika simu yangu na hatimaye nikampigia bwana mmoja kutoka katika mojawapo ya makampuni niliyowahi kufanyanayo kazi. Ni bwana ambaye tulikuwa tunaheshimiana sana, hata kama hatanipatia pesa ninayohitaji lakini anaweza kunipa walau nusu yake.

Nikamweleza shida yangu ya pesa, nikataja kiasi kuwa nina haja na shilingi laki tano.
Akaniahidi kuwa atanitumia ndani ya saa moja, akatimiza ahadi yake!!
Nikatuma kiasi alichohitaji mganga ili aniombee kwa mizimu niongezewe siku, kiasi kilichobaki nikafanya matumizi ya nyumbani.

Jioni kabisa mganga akanieleza kuwa mizimu imenielewa na imenipa hizo siku tano nilizoomba zaidi ya hapo hapatakuwa na muda wa ziada.
Nilishukuru sana, nikamtumia elfu hamsini kama shukrani.
Akanieleza kuwa haikuwa shughuli nyepesi hata kidogo kuishusha mizimu ili imsikilize.
Walau amani yangu ilirejea japokuwa haikuwa amani ambayo ingedumu kwa siku nyingi.

Kutambua kuwa mizimu imenielewa basi hata tabasamu bandia usoni niliweza kulipachika.
Baada ya kuhemea vitu kwa ajili ya nyumbani, nikarejea katika makazi yangu, nilimkuta mama amelala kwenye mkeka sebuleni, sikutaka kumsumbua nikanyemelea hadi chumbani niweze kumshtua kidogo mke wangu na tuweze kutaniana kidogo.

Kwani ni siku nyingi nilikuwa sijamtania kwa sababu ya ule msongo mkubwa wa mawazo
Nilinyemelea hadi mlangoni, nikamsikia mke wangu anazungumza na simu.
Nilitulia pale mlangoni nikisubiri amalize kuzungumza, mazungumzo yake hayakunishangaza sana kwa sababu alikuwa anazungumzia masuala ya paspoti huku pia akijadili kuhusu nauli na mtu ambaye alikuwa anazungumza naye. Nikatambua kuwa alikuwa anazungumza na wafanyabiashara wenzake, sema kuna jambo jipya nililisikia, aliuliza kuwa akisafiri na mtoto mchanga haitakuwa na madhara?
Sijui upande wa pili ulijibu nini…

Mazungumzo haya yakanikumbusha kuhusu pesa ambazo Nyambura alikuwa ameniomba nimtumie mtu wanayefanyanaye biashara na nilikuwa sijafanya hivyo bado!
Mwili ukaingiwa uvivu!

“Sasa Nyambura anataka aanze kusafiri na Agy mapema hivi…” niliwaza, kisha nikatulia alipomaliza kuongea nikagonga mlango….
Akaitikia nikafungua na kuingia.
Macho yangu na ya Nyambura yakagongana… nikasisimka vibaya mno.
Msisimko huu ukanikumbusha ule msisimko ambao mama yangu mzazi alinieleza kuwa aliwahi kuupata siku ya kwanza kutazamana na Nyambura wakati akiwa mjamzito.

Kuna nini? Nilijiuliza…..
Lakini mara zote hizi nilikuwa najitupia lawama mimi mwenyewe kuwa huenda kisa cha yote haya ni yule mtoto wa mizimu. Nilimkumbatia na kumbusu kisha nikambusu na mtoto, nikampatia Nyambura zawadi niliyomnunulia mjini. Akashukuru kwa kunibusu.

Baadaye kidogo nikamsikia mama anaimba nikatambua kuwa ameamka tayari nikamuaga Nyambura kuwa naenda kumsalimia mama.
Mama aliponiona nikiwa nimevaa fulana aliniita kwa ukaribu zaidi, akanisihi niketi, hapo hata salamu yangu hajajibu.

“Una nini Joshu mwanangu, zungumza na mimi… mimi ndiye mama yako. Wala hauna mama mwingine…..una tatizo gani” alinihoji, nikiwa bado sijapata neno la kusema akaendelea.
“Huu sio mwili wako baba, umekonda sana Joshua. Unawaza nini.. hebu niambie mwanangu. Ni mimi niliyekubeba miezi tisa tumboni mwangu, nikawa mkweli kwako hata wakati ninakulea sasa umekuwa mtu mzima hebu nawe kuwa mwaminifu kwangu. Una nini?” alinihoji zaidi

“Mama ni biashara tu haziendi vizuri lakini eti kusema kuna kitu nakuficha. Walaa!” niliongopa huku nafsi yangu ikiingia katika mfadhaiko mkubwa sana.
Kumdanganya mama!!
Lakini ningefanya nini unadhani….
Mama akanitazama kwa huruma, kisha akaniambia kuna kitu anataka kunipatia.

Akainuka na kujikongoja hadi jikoni, akarejea akiwa na kibakuli. Akanipatia.
Nikafunua na kukutana na mlenda pori.
Zawadi hii ya mama ikawa imenikumbusha mbali sana. Enzi ambazo nilikuwa naishi maisha magumu kupita kawaida pamoja na familia yangu.

“Nilijitahidi sana niwe nachuma mboga hiyo ili mle muishi, nilikuwa muaminifu sana kwenu! Ni Mungu tu ndiye shahidi ikiwa nyie mtakataa kushuhudia hilo, siku ambapo mboga ilikosekana niliwalaza miguuni mwangu nikawaambia ukweli kuwa siku hiyo tunalala njaa mvumilie.
Nilikuwa mkweli sana Joshu! Mkweli kwa sababu mimi ni mama yenu niliyewazaa….. kula huo mlenda Joshu na kama ukiendelea kuwa mkaidi kwangu, mi nitamuachia Mungu! Haupo sawa mwanangu.”

Alimaliza mama akaniacha pale, nilijaribu kunywa ule mlenda lakini haukupita kooni.
Mama alikuwa amenisema na kuugusa sana moyo wangu.
Lakini nitaanzaje mimi kumweleza mama kuwa nilienda kwa waganga na sasa nadaiwa??
Mgogoro wa nafsi ukanichukua, ukanikabaa koo na kuanza kunipiga makonde mazitiomazito mfululizo!
Niliteseka sana!
___
Siku iliyofuata nilienda kwa mwanasheria wa kampuni yangu na nikamueleza nia yangu ya dhati ya kuuza asilimia 90 ya hisa zangu.
Alishangaa sana ni taarifa ambayo hakutarajia kuisikia kutoka katika kinywa changu, yaani kwa jinsi nilivyopambana hadi kuifikisha kampuni katika kilele kile cha mafanikio eti ghafla ninauza hisa zote.
“Joshua unataka kuhama nchi nini?” aliniuliza, nikabaki kujichekesha tu.

“Halafu umepungua balaa… una matatizo yoyote rafiki yangu”
“Tatizo langu ndo hilo moja tu, ninahitaji kuuza hisa za kampuni yangu hivyo nahitaji uniandalie uthibitisho wa kisheria juu ya jambo hili.” Nilimjibu bwana yule, akabaki kuniangalia hata asinimalize.

Nikaondoka nikiwa nimemsisitiza kuwa jambo hilo lisizidi siku mbili.
Akakubali….
____
Niliporejea nyumbani majira ya saa mbili usiku, nilimkuta mama sebuleni. Haikuwa kawaida yake kuwa macho hadi muda huo.
“Nilikuwa nakusubiri Joshua..” aliniambia punde tu baada ya kukanyaga pale sebuleni.

“Joshua mwanangu, sina amani katika nafsi yangu na ninadhani nikiendelea kuishi hapa nitaugua na kukuletea shida wakati mkeo ana mtoto mnalea sitaki niwe mzigo.” Alisita akanitazama, kauli yake ikanifanya nisogee na kuketi jirani naye na kumuuliza kulikoni.

“Joshua mwanangu mimi ni mama yako halali, nimekulea hadi ukajitambua, nakujua kuliko wewe unavyodhani unajijua… kuna tatizo unalo linakukabili na hutaki kunishirikisha mimi mama yako, nimekosa amani kabisa na kuona kuwa sina stahiki tena katika maisha ya mwanangu. Naomba unipatie nauli Joshua mimi asubuhi nitarudi kijijini….” Mama alizungumza huku sauti yake ikikwama kwama katika mirindimo iliyoashiria kuwa yupo katika hatua za mwisho kabisa kuelekea kuangua kilio.

Mungu wangu! Yaani mama alie mbele yangu na sababu nikiwa mimi!? Nilihamanika vibaya mno.
Nilijisikia vibaya sana kwa kauli ile ya mama yangu, nikajiona jinsi gani simtendei mama yangu mzazi haki.

Kusema nimpe nauli aondoke nadhani hii ingemuongezea mawazo labda angeondoka pale na wazo kuwa mimi na mke wangu tulikuwa tumemchoka tayari. Kitu ambacho si kweli kabisa.
Nikasema sasa liwalo na liwe, nikamshika mama mkono na kumwita nje.

Akanifuata akiwa mnyonge kabisa.
“Ni kweli mama nina tatizo. Tena ni tatizo kubwa sana mama, na ninakueleza wewe kama madhara yatatokea ujue nimefanya kwa ajili yako mama, sikutakiwa kukueleza.” Nikasita na kutazama anga, niliposhusha kichwa nikazungumza bila kumtazama mama usoni.

“Mama unaamini katika ushirikina?” nikamtupia swali la ghafla.
“Najua upo ila siamini kama ni njia sahihi.” Alinijibu.
“Umewahi kushiriki?”
“Mdogo wako alipokuwa bado mdogo alishikwa na magonjwa ya ajabu ajabu baba yako akashauri tukampeleka katika hizo tiba za asili, sijui kama nazo ni ushirikina.”

Aliponijibu vile na mimi nikamsimulia kwa ufupi juu ya sakata langu la kukosa mtoto katika njia za kawaida na hatimaye kukimbilia njia za kishirikina.
Mama hakushtuka aliendelea kuniskiliza, nikamweleza hadi nikafikia mafaniko ya kupata mtoto sanjari na ahadi yangu kwa mizimu.

Sasa ahadi inanisulubu.
Mama alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akanikumbatia kwa nguvu.
“Asante sana mwanangu kwa kunijali.”
“Naomba unipatie nauli, kesho nirudi kijijini nikazungumze na wazee wa kwetu waiambie mizimu yetu ikazungumze na hiyo mizimu ikiwezekana wabadili malipo hayo wanayotaka.

Hiyo mizimu iliyokupa mtoto ni mizimu ya wapi?” mama aliniuliza. Sikuwahi kusikia majina ya mizimu ile, labda kutokana na hofu yangu, ama kukosa umakini.
“Mama hauoni kama mizimu itachukia?” nilimuuliza. Sasa nikiwa mdogo kabisa mwenye aibu kubwa.

“Ni heri kujaribu kuliko kubaki kimya, hiyo waliyokupa ni adhabu na sio zawadi wanayotaka, wewe utamlea viipi mtoto bila kuwa na kazi?? Nitawasihi sana, kama ni mizimu inayofahamiana kila kitu kitakuwa sawa mwananangu.”
Alinijaza nguvu mama, nikashangaa nilikuwa wapi kumweleza juu ya hayo siku zote.

Nikampatia nauli ya kutosha.
Asubuhi akamuaga mama Agy na kuondoka.
Mimi nikaingia katika pilikapilika za hapa na pale, jioni nikapiga simu niwasiliane na mama…. Kwa sababu niliamini amefika tayari.

Simu yake haikuita kabisa!
Nikajaribu tena na tena…..
Hali ilikuwa ileile, mwisho nilipigiwa mimi simu na nambari mpya.
Nikapokea nikidhani ni mama…
“Joshua, ni nini umemsababishia mama yako hiki? Sina la kukusaidia safari hii sasa!” ilikuwa ni sauti tulivu ya yule mganga wa jadi.

Akamaliza na kukata simu
Kusikia mganga yule akitaja jina la mama yangu, nikaishiwa nguvu!

ITAENDELEA
 
Sehemu Ya Sita

Baada ya kupokea simu ile na kugundua kuwa mpigaji alikuwa ni yule mganga wa jadi na alikuwa ananieleza kuwa kuna jambo baya ambalo limemtokea mama kwa sababu yangu, nikajua wazi kuwa yawezekana kile kitendo cha kumshirikisha mama juu ya mambo yanayonikabili ndo chanzo cha wazi kabisa cha yeye kukumbwa na balaa lolote lililomkumba.

Lakini niliomba sana hilo balaa lisijekuwa eti ni kifo kwa mama yangu.
Nilimsihi sana yule mganga anieleze nini kimemsibu mama yangu, akanieleza kuwa mizimu imemchukua na itakuwa tayari kumrejesha ikiwa tu nitatimiza ahadi yangu, lakini vinginevyo nitakuwa nimemtoa mama yangu kafara.

Akanilaumu kuwa nimeikasilisha sana mizimu kwa kumshirikisha mama yangu juu ya jambo linaloendelea.
Damu ilichemka sana kusikia hivyo, nikaituliza akili yangu na kujiuliza ni kipi nitafanya.

Mama ndo mtu pekee ambaye alikuwa akinifariji hasahasa nikiwa nimezidiwa na mawazo kama hivyo, sasa naambiwa kuwa amechukuliwa na mizimu.
Licha ya kujaribu sana kuituliza akili bado nilikuwa katika mchecheto.

Nilichukua simu yangu na kumpigia mwanasheria wangu kumsihi anifanyie hima sana juu ya zile nyaraka za kuhakikisha kuwa hisa zimeuzwa.
“Joshua!” mwanasheria aliniita baada ya kuwa nimezungumza naye na kumsihi. Nikamuitikia, akanieleza kuwa kama ninaweza nionane naye usiku huohuo kuna maswali anahitaji kuniuliza ili aweze kukamilisha vizuri zile nyaraka bila dosari yoyote.

Laiti kama angekuwa ananiitia mambo mengine hata nisingeweza kwenda, lakini kwa sababu ilikuwa ni juu ya nyaraka zile muhimu niliamua kwenda.
Tukakutana katika mgahawa mmoja tulivu sana usiokuwa na kelele na vurugu za hapa na pale.

Yule mwanasheria ambaye kiumri alikuwa ananizidi alinitazama kwa muda bila kuuliza chochote, kisha akaniuliza kuhusu ndoa yangu kama imetulia na ni salama.
Nikamjibu kuwa kila kitu kipo sahihi kabisa.
“Joshua mdogo wangu, nahitaji tuzungumze kirafiki tafadhali usinijibu kana kwamba mimi ni adui yako.” Alinisihi kwa upole.

“Ndugu, niulize maswali juu ya mkataba na sio vinginevyo..” nilimfokea kidogo. Akatabasamu kisha akapiga funda moja la bia aliyokuwa amenunua kabla sijafika.
“Mkeo ana biashara gani anazofanya na Revo?” aliniuliza swali ambalo sikujua lilikuwa na mantiki ipi.

Sikumjibu na nilizidi kupagawa kwa sababu huyu bwana nilimwona akinipotezea muda wangu angali mimi nina tatizo kubwa sana.
Nilikuwa nahema juu juu huku hasira nazo zikichukua nafasi katika nafsi yangu, kitendo cha yule bwana kuzungumza juu ya mke wangu kikanifanya nikumbuke kuwa alikuwa ameniomba shilingi milioni nne na hadi wakati huo nilikuwa sijampatia na sikuwa na dalili hizo,

“Joshua… sina maana mbaya kukuuliza hivyo. Naomba tu unijibu.” Alinisihi.
Nilijitahidi hasira zangu zisije zikavuka mpaka na kumvunjia heshima yake.
Nikamjibu kuwa hakuna biashara yoyote kati ya mke wangu na Revo.
“Na unadhani kwa nini Revo aliuza hisa zake ghafla baada ya wewe kumtolea mahari Nyambura?”

Hili swali likanilainisha kidogo, ni swali ambalo kama jibu lake lingepatikana basi lilimaanisha kuwa kuna mahusiano kati ya Revo kuuza hisa zake na mahusiano yangu na Nyambura.
“We umewaona wapi Revo na Nyambura?” nikauliza, sasa nikirejea juu ya lile swali la kwanza Nyambura ana biashara gani anafanya na Revo.

Mwanasheria akanitajia mazingira ambayo amewahi kuwaona Nyambura na Revo akauelezea uhusiano baina yao tangu niliposafiri na unavyoendelea hadi wakati huu ambao nina matatizo.
“Unavyosema juzi umewaona, unamaanisha juzi kabla hajajifungua mtoto ama akiwa na mtoto?” nilimuuliza kwa namna fulani ya kumsuta uongo nikijifanya namuamini sana Nyambura wangu.

“Juzi katika maana halisi ya juzi, na hakuwa na mtoto, si mara moja wala mara mbili.. nadhani ni mara tatu. Wanakutana katika baa fulani iliyojificha mtaani kwetu… ni baa ambayo huwa napenda kujificha hapo nakunywa bia kwa amani kuliko kwingine ambapo nitasumbuliwa na marafiki wapenda ofa.” Alinijibu kwa utulivu sana huku akijiamini mno.

Sasa sikuwa na hasira tena bali wingi wa maswali pasi na majibu.
“Kwa hiyo kaka unadhani wanafanya biashara gani?” nilijikuta natokwa na swali la kipuuzi.
Akatabasamu kisha akapiga funda moja la kinywaji chake.

Hakunijibu!!
“Huwa wanakuwa watatu wakati mwingine wanne, sidhani kama ni biashara ndogo. Ila we si ulinambia mkeo anafanya biashara?? Labda ndo hiyo?”
“Hapana, hawezi kufanya biashara na Revo halafu asinishirikishe, anaujua urafiki wetu vyema, na Revo hawezi kuacha kunishirikisha juu ya hilo.” Nilipinga.

“Unaonyesha unapenda sana kuamini kwa asilimia mia eeh!” alihoji kwa kebehi kiasi fulani. Nikagundua alichomaanisha.
“Siwezi kujua anyway, ila nimeona tu nikushirikishe kama mdogo wangu, uzuri ni kwamba ukimwambia mkeo kisha akanichukia atakuwa anamchukia mtu ambaye hamjui na hata Revo akijua nimekwambia akachukia haitafaa chochote maana sisi wanasheria tunachukiwa sana na tunapendwa vilevile, mimi ni mwanasheria wako!” alimaliza akapiga funda moja la mwisho na kutaka kunyanyuka. Nikamsihi asiondoke.
Nilikuwa nahitaji sana kusikia zaidi kutoka kwake.

Yaani kwa ufupi nilikuwa hoi kimawazo, huku nawaza juu ya mizimu na upande wa pili nikiwaza kuwa eti yawezekana mke wangu ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu wa karibu kiasi kile??
“Kaka tafadhali naomba uniambie basi unahisi kuna nini ukiniacha hivi kaka nitagongwa na gari mimi,

nimechanganyikiwa kaka yaani kuna mambo yananiendea kombo kiasi kwamba ninajiona nina kitu kama jini la mitihani nimetupiwa…” nilimsihi
“Kwani unahisi mkeo anaweza kujihusisha kimapenzi na Revo ama alikuwa akijihusisha naye hapo kabla hujamuoa ama?” alinihoji,

wakati huohuo akampungia muhudumu mkono na kuongeza kinywaji kingine.
Nikafarijika kuwa ataendelea kubaki zaidi.
“Kaka, sina walau hata hisia potofu kidogo tu dhidi ya mke wangu, nimekuwa naye kiuaminifu sana na ninaamini ananipenda.” Nilimjibu nikiwa namaanisha.

“Aisee! Umesema kuwa huwa anasafiri mara kwa mara kwa shughuli zake za kibiashara, je? Umewahi kufuatilia walau tiketi za mabasi na ndege ambazo anatumia?”
Lile lilikuwa swali zito sana na nikajiona ni mzembe sana kutofuatilia nyendo za mke wangu eti kisa tu naamini kuwa ananipenda.

“Haya basi nambie na wewe ni kwanini unauza hisa za kampuni, tena unauza zote tisini, unayemuuzia simjui unanilazimisha tu kuandaa makubaliano. Joshua ni nani anayekulazimisha kuuza hisa zako najua hauuzi kwa hiari yako mwenyewe… ni mkeo ama?” alipouliza vile akanikazia macho yake nikakosa ujasiri wa kuendelea kumtazama.

Nafsi ilikuwa inanisuta.
Nilikosa cha kujibu. Nilitamani kumweleza ukweli lakini kwa yaliyomtokea mama yangu. Nilihofia kuyakuza zaidi nikimsimulia na mwanasheria.
“Kesho makubaliano yatakuwa tayari, kumbuka kama unanidanganya mimi unajidanganya mwenyewe.

Mimi ni mwanasheria mteja wangu akiniongopea balaa huja kwake si kwangu…”
Alimalizia maneno yale kisha akainuka na kuondoka zake hata bia yake hakuimalizia.

Maneno ya mwanasheria wangu yalikuwa yameniletea ugonjwa mpya uitwao mashaka, nilikosa kujiamini… nikimtazama mke wangu machoni namwona asiyekuwa na hatia lakini busara za mwanasheria nazo zilikuwa na makali yake katika upande wa kuishtua akili yangu.

Usiku huu niliporejea nyumbani nikawa namuwaza mke wangu, namuwaza rafiki yangu Revo, namuwaza mwanasheria na maneno yake lakini zito zaidi nikimuwaza mama yangu mikononi mwa ile mizimu inayotaka kuimiliki kampuni yangu na kila kitu kilichomo.
Niliyafumba macho yangu, nikaanza kulijengea picha wazo la kwanza.

Nyambura na Revo!
Nikafikiria jinsi ambavyo huwa tunacheza bafuni huku tukiyaacha maji yamwagike pasi na jambo la msingi. Ananigusa huku nami namgusa kule.
Nikajitoa pale bafuni kisha nikamuweka Revo.

Yaani Revo naye anamgeuza nyuma Wambura na kumuuliza hii alama hapa mgongoni ulikuwaje?
Nilijiuliza huku nikipambana kuidhibiti ghadhabu yangu.

Lakini si ana mke kabisa Revo! Halafu mkewe mrembo haswa kuliko hata huyu Nyambura, sasa kama wana mahusiano kweli… kampendea nini?
Nilizidi kuumia kichwa nikiyakosa majibu kabisa.

Nikiwa ningali katika mawazo mazito kabisa, Nyambura mke wangu akanitikisa nakuniambia kuwa kuna mambo kadhaa anahitaji kuzungumza na mimi.

Nilimweleza kama inawezekana tuzungumze asubuhi akakataa akasema ni lazima iwe usiku uleule!
Nikakubali japokuwa niliamini kuwa sikuwa tayari kumsikiliza kwa umakini.

Akaanza kwa kunikumbusha juu ya zile pesa alizoomba nimsaidie kuweka kwenye nambari aliyonipatia, nikazuga kushtuka na kumtaka radhi kuwa nilisahau.

“Sawa achana na hilo, nahitaji kuzungumza juu ya mama.” Akasema kisha akasita.
Ile kutaja jina mama, moyo wangu ukalipuka vibaya sana. Nikaingiwa na ganzi na ubaridi ukitambaa katika mwili wangu.
“Nilizungumza na mama kabla hajaondoka!” akaweka mkato tena, kisha akaendelea, “Kwanini umemfukuza mama?” akanirushia swali la ghafla.

“Nani? Mimi?” nikatokwa na swali la kizembe. Nyambura hakusema kitu akaniacha nibabaike.
“Mimi nimemfukuza mama? Nani kakwambia? Ni mama kakwambia mi nimemfukluza?” nikabaki kujiuliza na kujipa majibu katika namna ya kutaharuki.
“Baba Agness…” akaniita kwa utulivu, akaendelea baada ya mimi kuitika,

“Ulinieleza kuhusu historia yako, na mama pia alinieleza juu ya hilo. Leo hii umekuwa mtu mzima unamficha mama mambo yako, mimi je? Si ndio utaniua kabisa kwa kunificha siri zako?” aliuliza katika namna ya kulalamika.
Nilikuwa nimekamatika!
“Tazama! Unadhani sikuoni unavyokonda kila siku, unadhani sioni kuwa hauna raha wala amani? Nayaona yote haya….

Lakini mimi ni uchafu tu mbele yako, hata nikiuliza najua hautanijibu, kama mama yako mzazi umemkatalia katakata je mimi mpita njia!” aliendelea kulaumu, sasa alikuwa amejinyanyua na kuegemea mkono wake akinitazama vizuri.
“Ni nini chanzo cha kuapa kanisani kuwa sasa mimi ni ubavu wako rasmi, nakuaje ubavu wako! Nakuaje kiungo katika mwili wako ikiwa siyajui maumivu yako? Sijui hisia zako… sijui unachopitia!!” alishindwa kuendelea sasa machozi yakaanza kumtiririka.

Looh! Nilichanganyikiwa kupita awali, nikaanza kumbembeleza lakini Nyambura katukatu hakutaka kunisikia.
“Joshua! Nalala sebuleni, naomba usinifuate huko, na kesho usiku nitalala kitandani ikiwa tu aidha mama amerejea hapa! Au utanipa nafasi mimi kama mke wako kujua nini unapitia… la sivyo! La sivyo Joshua …..” akaiacha hewa sentensi yake akaondoka zake.

Kama ni mpambano wa masumbwi, nilikuwa nimepigwa ngumi mfululizo nazipangua halafu nikajisahau nikatoa mikono na nikaingizwa pigo moja mahususi liitwalo ‘uppercut’, huu ni mtindo wa ngumi ambapo mpinzani wako anaikunja ngumi yake na kisha anairusha kwa kutokea chini inatua katika kidevu chako.

Pigo hili linaweza kuvunja taya ya mlengwa!
Nami nilivunjwa vibaya, nikabaki kama tahira kitandani.
Moyo wa kike ukanivaa, nikaanza kulia kana kwamba nimefiwa!
Ama! Yalikuwa yamenifika Joshua mimi.

JIFUNZE!
KATIKA mahusiano ya kimapenzi, hususani ndoa. Mahusiano mengi huanza katika namna sahihi kabisa ya tatu jumlisha tatu jibu ni sita, lakini kuna nyakati katika ndoa mahesabu hayo hubadilika, mmoja ataiona ile sita ni tisa na mwingine ataiona sita ni sita. Na kila mmoja akiamini kuwa yupo sahihi!
Ni hapa FUKUTO huanzia!

ITAENDELEA...
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom