USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

Cd4 kushuka inasababishwa na vitu vingi baadhi ni kupata milo duni,kufanya ngono zembe,kuwa na msongo wa mawazo(stress)na kutotumia dawa za Arv
Kwa upande wangu kuanzia mwaka jana nilianza kuishi mwenyewe hivyo nikawa nakosa mlo kamili uliojitosheleza ukijumlisha na kutotumia Arv ni lazima Cd zishuke mkuu ila nashukuru sasa zimepanda kwa kiasi kikubwa mno na ninazingatia mlo kamili hata iweje bora nikose vyote lakini sio kukosa milo mitatu yenye nguvu
Mungu akupe afya njema zaidi aisee
 
Kuna friend alizaliwa na virusi vya ukimwi tunezika 2015 akiwa na miaka 25. Na alikuwa akipata lishe nzuri, matibabu ya daraja la juu kwa sababu family yao pesa ipo. Alikosea wapi au muda wowote mtu anaondoka akiwa na hali hiyo? Samahani lakini kwa swali hili.
 
Ukisafiri ama ukiketi nyumbani popote ulipojistiri jua kifo kipo pembeni,mara ngapi umesikia mtu kaenda kulala halafu anapitiliza ndio kwa heri ya kuonana,kila mtu mtu atakufa kwa staili yake unaweza ukawa mzima tu ukaanguka kisha ndio kwa heri,vyovyote vile kila nafsi itaonja mauti mkuu
 
unasema upo mzima wa afya inamaana umepona au mimi ndo sijaelewa kabisa!
 
Kuishi na HIV ni tatizo kwa wasio na taarifa sahihi tu.

Utashangaa mtu akijua jirani yake anaishi na VVU anamuonea huruma ili hali ndani kwake kuna Mtu ana kisukari, na anateseka mbaya....sasa nani wa kuhurumiwa hapo?
 
Ha ha ha kwa pamoja tuseme HIV positive is normal
 
Back
Top Bottom