Ushuhuda: Mapenzi Yanahitaji Muda Wa Pamoja Zaidi, Si Pesa Tu

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Jana baada ya kusoma sms ya M-Pesa imethibishwa umepokea… kama shukrani.
Nilipokea simu ya mteja wangu akiwa na furaha kweli. Furaha yake ni baada ya kusikia maneno aliyokua anasubiri kuyasikia kutoka kwa mpenzi wake. Lakini kabla ya hapo hebu nikushirikishe kisa chake ili nawe upate kujifunza.

Yeye ni mfanyakazi wa TRA, upande wa kazini yupo vizuri na ofisini wanamuheshimu. Ni shabiki mzuri wa mpira, ukikaa naye anaweza kukuambia kuhusu fainali zote za UEFA na nani amechukua. Pia ni mtanashati, muda wote ni msafi. Pia mfuatiliaji mzuri wa mambo ya kisiasa duniani.

Lakini kwenye kumridhisha mpenzi wake ndo kulimnyima usingizi na kumuumiza kichwa.

Mwaka 2022 mwezi wa 6 mwanzoni ndo alinitafuta, akitaka kujua anafeli wapi kwenye mahusiano yake, mana amekua hamuelewi mpenzi wake hata kidogo, mahitaji ya ndani anamtimizia na kumnunulia zawadi lakini bado haoni mwanamke akijitoa, akimpetipeti au kumchombeza kama zamani. Jambo lilimfanya ahisi anachunwa tu na kutumiwa kwa hela zake.

Kwa kuwa alimpenda na hakutaka kumpoteza, alianza kumfuatilia maana alihisi kuna jamaa huko nje anamchapia jambo lililomuumiza zaidi. Lakini akagundua hachapiwi ila kuna mwanaume anamawasiliano naye mara kwa mara. Naye akawa anajitahidi kumshawishi mpenzi wake kwa zawadi na pesa lakini bado mambo hayakubadilika, maumivu na mawazo yaliongezeka badala ya kupungua.
Aliniambia hakutaka wafikie hatua ya kuchapiwa au kuanza kumfatilia huyo mwanaume, hivyo anahitaji msaada wa haraka kumuepusha na maumivu ya kusalitiwa mana yeye hajawahi kumsaliti mwanamke wake.

Tatizo lake kubwa aliamini kama kila sehemu isemwavyo kwamba ukiwa na pesa unaweza mshwawishi mwanamke akakupenda sana, au ukimpa zawadi mbili tatu atakukubali zaidi. Lakini alipofanya uchunguzi aliona kuna watu walifanya kama yeye anavyofikiri na wana pesa lakini bado waliishia kuchapiwa, hivyo anahitaji mbinu mpya.

Taratibu akaanza kujifunza kuwa mwanamke naye ni mtu mwenye mahitaji mengine zaidi ya pesa yake, anahitaji zaidi muda wenu pamoja kama wapenzi ili kutunza mahusiano. Hapa alikiri amekua bize na kazi kiasi cha kuondoka asubuhi na kurudi jioni, na mara chache wakifanya basi anafanya viwili kisha analala kwa uchovu.

Nikamuuliza “kwa mwezi wa tano umemtoa out mara ngapi huyo mpenzi wako?”
Akanijibu mara moja ila mara nyingine tulikua tunaenda kanisani pamoja.
Nikamwambia, kwenda kanisani pamoja haina maana ya kuwa pamoja, maana huwezi pata muda wa kumsikiliza kiundani au kumkiss kwa mahaba kanisani wala hamuwezi kufanya mambo ya kikubwa huko.

Ilimchukua mwezi kuelewa hili kwa kuwa ye aliamini anatakiwa akatafute pesa muda wote akirudi ampe mwanamke ya matumizi kisha akaendelee kutafuta, ampe zawadi, bila kujali yeye mwanamke anahitaji nini ukiachana na pesa. Mapenzi walikua wanafanya na mpenzi wake lakini kwa sababu tu wameishi kwa mwaka mmoja, kwa mazoea.

Baada ya kuelewa hilo akaanza kujifunza jinsi ya kumuelewa mwanamke wake anahitaji nini. Akajifunza kuwa mwanamke ni mtu wa muda huo, haijalishi jana ulimfanyia nini leo atayasahau hayo na kuzua jipya hivyo amuelewe wala asimkasirikie na kuanza kumkumbusha kuwa nilikununulia zawadi hivyo inabidi unipende.

Mwanamke inabidi umfanye afurahi kwa muda huo au umkanye kwa muda huo wala usipotezee kwamba ntafanya baadae au nilifanya kwahiyo sina haja ya kufanya tena.

Kisha akajifunza kumsoma mwanamke wake na ishara anazompa. Mfano, kama zamani alikua anamshika kila muda lakini sasa hataki hata wagusane, akajua ukaribu umepungua na amekua mgeni kwake. Pia alikua anamtafuta katikati ya siku kumjulia hali na sasa hakuna hayo mambo. Alielewa kuwa vyote ni ishara ya mwanamke ili ajue ukaribu umepungua hivyo inabidi afanye kitu wawe karibu tena. Kumbuka mwanaume ndio kiongozi hivyo inabidi mwanaume aurudishe ukaribu.

Akabadili na kupanga upya ratiba zake ili aanze kutenga muda kwa ajili ya mpenzi wake, na uzuri alikua na usafiri wake akaanza kutoka jioni/usiku na mpenzi wake angalau mara moja kwa wiki.

Mwanzoni alipata shida mana mpenzi wake alishazoea kubweteka. Aliumia kwa kuwa alihitaji uvumilivu mkubwa kuanza kubadilisha mazoea waliyokuwa nayo.
Mara ya kwanza mpenzi wake alianza kwa kejeli za kuumiza kama “naona umeachika uko uliko umeamua kurudi” na “tufanye haraka tuondoke bhana, nataka kuwahi kulala”. Lakini aliamua kuvipotezea mana alivichukulia ni vipimo tu kutoka kwa mpenzi wake hakuna haja ya kuhangaika navyo. Pia alitambua kuwa mwanamke wake hamuamini kwa muda huo, hivyo inabidi aanze kujenga imani taratibu tena. Hivyo aliendelea kumtoa angalau mara moja kwa wiki, kumsikiliza zaidi wakiwa nje na kutenga muda wa pamoja mara kwa mara, bila kusahau vijizawadi vyake.

Ilipofika mwezi wa nane mwishoni, 2022, alianza kuona tabia za mwanamke wake kubadilika, akaanza kuandaliwa chakula cha kubeba kila siku asubuhi. Kanisani wakienda mpenzi wake hakutaka kukaa mbali naye, naye alifurahia. Pia kadri muda ulivyozidi kwenda alianza kupokea sms za kazi njema kutoka kwa mpenzi wake na hofu ya kuchapiwa ikaisha.

Sikuongea naye tena hadi jana aliponitafuta kwa kuwa amesikia maneno aliyokua anayasubiri kwa hamu sana kutoka kwa mpenzi wake, akaniambia mazungumzo yao yalikua hivi, mpenzi wake alimuambia “baby, nataka tuwe wamoja tuache kufanya dhambi” akaniambia alicheka sana alafu akamuuliza “unamaanisha nini honey?”, mpenzi wake akamjibu kwa sauti ya unyenyekevu “huoni itakua vizuri tukatambulishane kwa wazazi mpenzi wetu, alafu tufunge ndoa, asa tutaishi ivi mpaka lini?”. Jamaa kwa kuwa naye anampenda mwanamke hakuona cha kupinga zaidi.

Natumaini utakua umejifunza, na nikutakie siku njema katika kulijenga taifa.
Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
Mwanaume unatakiwa ubalance pesa na mapenzi, ukiegemea kwenye suala la pesa tu lazima utachapiwa na pia ukiegemea sana upande wa mapenzi bila ya kuwa na pesa lazima utachapiwa tu.

So you must balance.
 
Something more than money is needed. Love is not about money and gifts.
 
Mwanaume unatakiwa ubalance pesa na mapenzi, ukiegemea kwenye suala la pesa tu lazima utachapiwa na pia ukiegemea sana upande wa mapenzi bila ya kuwa na pesa lazima utachapiwa tu.

So you must balance.
Egemea swala la pesa tu mwache kidude chake aamue yeye mwenyewe ampe nani.
 
fanya yote bado utagongewa tena kavu mbele/nyuma, na bodaboda , anapewa Gono na kuja kukuambukiza wewe

Tafuta Pesa, Usiridhishe kiumbe, Jiridhishe wewe

wahanga wa tamthilia za kikorea ni wengi sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom