Tetesi: Ushuhuda mali walizohifadhi wajerumani.

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,006
1,500
Wana wa jf heshima iwe kwenu.
Nimeamua kuuleta uzi huu kwenu ili kutufumbua macho kutoka ktk biashara hii ninayoiita mimi ni ya kufikirika ya MALI WALIZOFICHA WAJERUMANI.
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikiisikia habari hii pia biashara hii ambayo sina uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ipo na kuna mtu yeyote ambaye imekwisha mnufaisha zaidi ya baadhi ya ninaowafahamu biashara hii haikuwaacha salama.Angalizo biashara hii mimi binafsi siiamini pia siifahamu na siitamani ila ninapenda kusikia michango mbalimbali kutoka kwa wale walokwishakumbana na biashara hiyo na walikabiliana nayo vipi na walifaidika nini kutoka kwenye hiyo biashara.
Nawasilisha kwa mawazo ya kuelimisha.
 
pevu

Senior Member
Sep 2, 2016
110
225
Tatizo la hum,, Kuna watu,,,, bado Sana kuielewa jamii forum,,,, tutofautishe na sms za sm. ambazo anasoma mtu mmoja tu,,,, ila humu ni wengi Mkubwa,,
 
Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,827
2,000
Utapeli Utapeli Mtu Akikuletea Swagga Kama Hizo Kama Una Sime Ndani Fuata Mcharange Hata Kisogoni Wengi Walishalizwa Sana Mara Pasi Ya Kijerumani Mara Fukumark Pesa Ya Kijerumani Mara Sitomvu Ni Utapeli Tu
 
RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,375
2,000
Hahaha umenikumbusha jamaa mmoja alikuwa busy kuzifuatilia kwenye milima ya Kisarawe, masharti ni kwenda usiku na mganga maana wanadai wajerumani ni wachawi hatari. Kwa hiyo inabidi uwe na huyo mganga akupeleke. Sasa basi, sharti lingine mkizipata lazima mzigawane sawa. Hadi naondoka mitamboni sikuwahi kuona kama alibahatika kuzipata hizo ghawira au madini sijui zaidi ya stori za kuambiwa si unamuona ridhiwani kikwete mara sijui nani wote wanapiga hiyo michongo.
Binafsi siamini sana kwenye dili! Hahahaha
 
r2ga

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,231
2,000
Asante kwa ushuhuda,karibu tena juma lijalo. Wakaribishe na wenzako.
 
SHAMAC

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
1,345
2,000
Hivi kuna kitu mimi sikijui hapa TZ....?? Naona watu mna comment tu huku mie hata cjamuelewa mwanzisha thread...!!
 
YABUUU

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,523
2,000
kutafta lupia ya mjeruman kumewaacha weng maskin jaman achen 2, mara unaambiwa ipo kule unaenda unaambiwa fanya hivi, mara nenda kwa mganga, mara cjui nenda kenya mwisho wa ck unatumia tuhela twako twote unabak na pmb tuu. 2tafte hela wadau
 
Madame B

Verified Member
Apr 9, 2012
28,457
2,000
Wana wa jf heshima iwe kwenu.
Nimeamua kuuleta uzi huu kwenu ili kutufumbua macho kutoka ktk biashara hii ninayoiita mimi ni ya kufikirika ya MALI WALIZOFICHA WAJERUMANI.
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikiisikia habari hii pia biashara hii ambayo sina uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ipo na kuna mtu yeyote ambaye imekwisha mnufaisha zaidi ya baadhi ya ninaowafahamu biashara hii haikuwaacha salama.Angalizo biashara hii mimi binafsi siiamini pia siifahamu na siitamani ila ninapenda kusikia michango mbalimbali kutoka kwa wale walokwishakumbana na biashara hiyo na walikabiliana nayo vipi na walifaidika nini kutoka kwenye hiyo biashara.
Nawasilisha kwa mawazo ya kuelimisha.

Nenda Habari na hoja tafuta uzi wa "Hazina ya Mjerumani"
Humo kila kitu kiko wazi.
Ni uzi mrefu, mtamu na una shuhuda mbalimbali mpaka maeneo yametajwa kwenye hizo hazina.
Ila angalizo: Kuna matapeli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom