USHUHUDA: Dunia, uchawi umeniacha hoi. Mungu nikumbuke

USHUHUDA: Dunia, uchawi umeniacha hoi. Mungu nikumbuke

We acha tu,siwezi elezea yote hapa,lkn nipo katika wakati mgumu sana,na nipo ugenini.lilianza moja,sasa hivi kila kukicha yanaongezeka, nipo ndani toka ijumaa sijaenda hata kufungua sehem yangu ya biashara,jana wamekuja polisi na community kunitafuta ofisini kwangu,kwamba nilinunua laptop na play station.vitu ambavyo sivijui,yani ni mitihani mtindo mmoja
Tuwasiliane pm kiongozi tuna mitihani kila mtu kwa namna yake lakini upo nchi ya watu na hayo matatizo ni hatari
 
kuna njia moja tu inaweza kukuponya maisha yako yote, na utarudi hapa kutoa ushuhuda kama utafuata masharti yake. Unaweza kuwa umeshajaribu sana njia nyingi na pengine hii pia ila bila kufuata masharti vizuri. na kwasababu umekamatika, hauna jinsi ila kutafuta kina namna ili upone na maisha yako yarudi kama awali. Maadamu u mzima, unaweza kuongea, unaweza hata kuandika jf, BADO LIPO TUMAINI, unayo nafasi ya kupona kabisa na ukawa ushuhuda mwingine kwa watu.

sikiliza. Njia hii, ni njia ya wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Mungu ameweka njia hiyo tu kwamba wanadamu wooote wenye dhambi, wenye matatizo wapitie hiyo wakaitue mizigo yao yote, wakatue magonjwa yao yote, na yeye atakubebea, wewe utabaki kuwa huru.

unachotakika (masharti), Umkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kuamini moyoni kwamba Mungu alimfufua katika wafu, kwamba alikufa na kufufuka kwa kufanyika kafara la ukombozi wa maisha yako. Yesu Kristo ni Mwokozi, mponyaji na ndiye njia kweli na uzima.

sijui dini yako, sijui ulikopitiapitia. ila nikuambiacho, ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako na kuamua awe Mwokozi wa maisha yako, utaokoka roho, mwili na nafsi, na mali zako zote, na kazi, na watoto, na familia n.i. ila, lazima ujitoe maisha yote. You must surrender toka ndani ya moyo wako, Imani yako kwa Mungu through Yesu Kristo iwe kipaumbele cha kwanza na vingine vyote ni secondary. mwanadamu hawezi kumwona Mungu hadi asalende maisha yake yote, fikra zake, kila kitu akijenge kwenye misingi ya Imani ndani ya Yesu Kristo, hapo ndipo Mungu hufanya makao maishani mwetu, atakupigania kwa watesi wako, atawafukuza wachawi, mashetani n.k, na anao uwezo kurudisha miaka yako yoote iliyoliwa na matatizo. MUNGU ANAWEZA.

pia, anza kusoma Neno la Mungu, Biblia. nikiri kwamba, sio kwamba nabagua dini au la, ila kwa ushuhuda wa maisha yangu, hicho tu ndicho kitabu kilichobadilisha maisha yangu.

Mimi nilishapitia maisha kama hayo ya kwako, lakini amini usiamini, it takes no longer than a day Mungu kubadilisha maisha yako kama akiamua, na mazingira gani yatamfanya aamue? pale utakaposalenda maisha yako kwake ili awe Mungu wako, na ukijua kwamba hapa duniani tunaishi tu ila bila Mungu shetani anaweza kufanya lolote dhidi yetu. hatuna nguvu za kumshinda shetani bila Mungu. shukuru Mungu bado mzima.

ulifanya kosa sana kutoamini kama wachawi wapo. mimi hata watoto wangu huwa nawafundisha kwamba wachawi wapo, hivyo maisha yao wawe wanamtumaini Mungu ndiye atakayewalinda na wachawi. nasema hivyo kwasababu nilishawahi kulogwa na kufanywa fukara wa kutupa. huwa naamini kwamba kati ya watu waliowahi kupitia maisha magumu duniani wakiwa na elimu ya Masters, ni mimi na mke wangu. tulifika kipindi kila tunachofanya hakifanikiwi, kila mlango umefungwa, wale tuliowasaidia wanatucheka kwamba tumekwisha wakati sisi ndio tuliwasaidia kufika walipo, kila mtu alitukimbia, tukabaki sisi na Mungu. tulichoamua ni kuanza kumtafuta Mungu na kumuomba Mungu kwa bidii. tulitfuta uso wa Mungu, ikafika majira ambayo Mungu aliamua kushuka kututetea, IMEKUWA HISTORIA. kila kitu kilikuwa kinakuja dabodabo. siongei kishabiki, ni hakika, mafanikio yalianza kutufuata tu ni kama milango imefunguka.

wachawi wapo, ni maajenti wa shetani, na wengine huwa wanakuwa watu wako wa karibu mno. ishi ukijua kuwa kama kuna Mungu basi na shetani na maajenti wake wapo, na hizo ndio falme zinazoshindana/adui siku zote. ukiamua kuwa upande wa Mungu jua kabisa kuwa upande wa shetani ni adui zako, na ukiamua kuwa upande wa shetani jua upande wa Mungu sio watu wako. ukiamua kuwa wa shetani utapata vya shetani ila kuna siku atakuteketeza na kukufedhehesha, utalipia ulivyokula, ila ukiwa kwa Mungu gharama pekee utakayolipa ni kujitoa kwa Mungu na kufuata sheria zake tu na gharama zingine zote Mungu ameshalipa kwa Damu ya Yesu Kristo.

Mungu akusaidie.
Ubarikiwe sana mm pia nimepata kitu kikubwa sana hapa.Naomba mtoa mada apitie hapa kwa umakini ni commitment na Mungu atamsaidia🙏
 
Hii dunia ionen tu iv iv mpaka nikajiita mbeba lawama ilkua hiv.. katka familia mm kama mtoto w kiume kuzalia katikat nlbahatika kupata Kaz katika umr mdogo Sana Kaz ilnlpa pa kubwa Sana na kwakua skua na majukum nliona pesa yangu ndio iwe nguzo kwa ndugu zangu wengne na tumezaliwa pande mbil Yan kwetu na was mama mwngne nlipo jchanganya n kuanza kusaidia na wale wengne s ndio wakaanza kuleta maneno anajkuta yeye ndio anapesa yeye ndio anakaz kaanza kumjengea na mzee wake nyumba asee walmwengu sjui waliniloga na nn toka 2019 nljkuta siwez kuingia ofcn naliogopa get la ofcn nlkaa nje ya ofs bila kuingia kazn mpka 2021 mwez wa 7 Kaz ikaisha ma hr washanikalsha Sana em nenda kwenu hii sio akil yako Sasa hata nikienda kwetu naenda kuanzia wap sielew nkawa nakunywa pombe hatar kesi zisozo na kichwa wala miguu zikainuka juu yangu uko ofcn mpka wengne wakawa wananiita Tapel.

Hakuna mtu aliejtokeza kusaidia Kat ya ndugu zangu saiv nasota mwenyew hata Kaz ya kuendesha school bas nakosa nshaomba Sana Kaz lakn milango ya Kaz iko blocked kabsa nmekwama mtoto wa kiume ile hulka ya watu walikua wakifurah uwepo wangu imepotea kabsa saiv naishia kujikalia ndan atakae nkumbuka ndio ananitumia 10000 ukimwomba wik inayofata anakwambia unamatumiz mabaya ya pesa kwel?

uchawi upo sanaaa na funzo nililolpata ukiwana pesa usisaidie maskin n watu wabaya Sana nahawafurahishw na maendeleo yako hata kidogo ndio Mana watu wengne hua awakanyag kijijin kwao pale wanapoanza kuinuka kimaisha.. pole Sana ndugu hil n letu sote Nshazunguka kwa waganga wachungaj mashekhe Sasa nmenyoosha mikono nasubr nione maisha yananpeleka wap Mana hii Hal n ya hatar Sana
Hili ata usimlaumu mtu ulishindwakujitibu au kuomba msaada Kwa watu pole sana kukaa ndani hakutabadili chochote jitibu ombasaada Kwa mama au Mzee yoyote anayejua maswala ya kiganga
 
kuna njia moja tu inaweza kukuponya maisha yako yote, na utarudi hapa kutoa ushuhuda kama utafuata masharti yake. Unaweza kuwa umeshajaribu sana njia nyingi na pengine hii pia ila bila kufuata masharti vizuri. na kwasababu umekamatika, hauna jinsi ila kutafuta kina namna ili upone na maisha yako yarudi kama awali. Maadamu u mzima, unaweza kuongea, unaweza hata kuandika jf, BADO LIPO TUMAINI, unayo nafasi ya kupona kabisa na ukawa ushuhuda mwingine kwa watu.

sikiliza. Njia hii, ni njia ya wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Mungu ameweka njia hiyo tu kwamba wanadamu wooote wenye dhambi, wenye matatizo wapitie hiyo wakaitue mizigo yao yote, wakatue magonjwa yao yote, na yeye atakubebea, wewe utabaki kuwa huru.

unachotakika (masharti), Umkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kuamini moyoni kwamba Mungu alimfufua katika wafu, kwamba alikufa na kufufuka kwa kufanyika kafara la ukombozi wa maisha yako. Yesu Kristo ni Mwokozi, mponyaji na ndiye njia kweli na uzima.

sijui dini yako, sijui ulikopitiapitia. ila nikuambiacho, ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako na kuamua awe Mwokozi wa maisha yako, utaokoka roho, mwili na nafsi, na mali zako zote, na kazi, na watoto, na familia n.i. ila, lazima ujitoe maisha yote. You must surrender toka ndani ya moyo wako, Imani yako kwa Mungu through Yesu Kristo iwe kipaumbele cha kwanza na vingine vyote ni secondary. mwanadamu hawezi kumwona Mungu hadi asalende maisha yake yote, fikra zake, kila kitu akijenge kwenye misingi ya Imani ndani ya Yesu Kristo, hapo ndipo Mungu hufanya makao maishani mwetu, atakupigania kwa watesi wako, atawafukuza wachawi, mashetani n.k, na anao uwezo kurudisha miaka yako yoote iliyoliwa na matatizo. MUNGU ANAWEZA.

pia, anza kusoma Neno la Mungu, Biblia. nikiri kwamba, sio kwamba nabagua dini au la, ila kwa ushuhuda wa maisha yangu, hicho tu ndicho kitabu kilichobadilisha maisha yangu.

Mimi nilishapitia maisha kama hayo ya kwako, lakini amini usiamini, it takes no longer than a day Mungu kubadilisha maisha yako kama akiamua, na mazingira gani yatamfanya aamue? pale utakaposalenda maisha yako kwake ili awe Mungu wako, na ukijua kwamba hapa duniani tunaishi tu ila bila Mungu shetani anaweza kufanya lolote dhidi yetu. hatuna nguvu za kumshinda shetani bila Mungu. shukuru Mungu bado mzima.

ulifanya kosa sana kutoamini kama wachawi wapo. mimi hata watoto wangu huwa nawafundisha kwamba wachawi wapo, hivyo maisha yao wawe wanamtumaini Mungu ndiye atakayewalinda na wachawi. nasema hivyo kwasababu nilishawahi kulogwa na kufanywa fukara wa kutupa. huwa naamini kwamba kati ya watu waliowahi kupitia maisha magumu duniani wakiwa na elimu ya Masters, ni mimi na mke wangu. tulifika kipindi kila tunachofanya hakifanikiwi, kila mlango umefungwa, wale tuliowasaidia wanatucheka kwamba tumekwisha wakati sisi ndio tuliwasaidia kufika walipo, kila mtu alitukimbia, tukabaki sisi na Mungu. tulichoamua ni kuanza kumtafuta Mungu na kumuomba Mungu kwa bidii. tulitfuta uso wa Mungu, ikafika majira ambayo Mungu aliamua kushuka kututetea, IMEKUWA HISTORIA. kila kitu kilikuwa kinakuja dabodabo. siongei kishabiki, ni hakika, mafanikio yalianza kutufuata tu ni kama milango imefunguka.

wachawi wapo, ni maajenti wa shetani, na wengine huwa wanakuwa watu wako wa karibu mno. ishi ukijua kuwa kama kuna Mungu basi na shetani na maajenti wake wapo, na hizo ndio falme zinazoshindana/adui siku zote. ukiamua kuwa upande wa Mungu jua kabisa kuwa upande wa shetani ni adui zako, na ukiamua kuwa upande wa shetani jua upande wa Mungu sio watu wako. ukiamua kuwa wa shetani utapata vya shetani ila kuna siku atakuteketeza na kukufedhehesha, utalipia ulivyokula, ila ukiwa kwa Mungu gharama pekee utakayolipa ni kujitoa kwa Mungu na kufuata sheria zake tu na gharama zingine zote Mungu ameshalipa kwa Damu ya Yesu Kristo.

Mungu akusaidie.
Amen
 
Ll check it up on Google later in the day ,sema the level of pain na body aches hainipi muda wa kupumua , eventually nkiovercome hili ,aliyeniseti ataanza kuhesabu siku zake Dunia hii , whatever goes around eventually comes around
Fafanua kidogo ili uliloandika apa boss nasi tupone
 
Hata youtube kaelezea vitu vingi vya msingi sana

Hata akisikiliza somo la spiritual intelligence by apostle Joshua Selman, you tube, he will never remain the same
Wanga kazi wanayo ni KOINONIA kwenda mbele😂😂
 
Wew tatizo ni mshamba na una kitu kinaitwa conservativeness ya jamii yako tushapiga parefu tembea jua familia yako unaleta showoff za kishamba hao wakina bakhresa wangerudi kwao kuwekeza mbona wako bongo

We ushapiga parefu una Maisha yako shobo za nn na kwenu watu wa karibu wabaya sana usiambiwe.

Mi tangu nipate matatizo kipindi fulani nilipokuwa chuo maana nilirudi home kufika nikawa sioni yaani macho nikapata upenyo kuja chuo tena nilikuja kwa ishu postpone nilikuja dar nikakaa siku tatu nikapona ghafla machale yakanicheza kule kuna tatizo sina asili sina ukabila nikaona kule hakunipendi japo ni kwetu sijarudi tena mpaka nilienda naishia lodge nakutana na mzee juu kwa juu nampa pesa nalisha familia kila nwezi mm nilishagundua michezo michafu sirudi labda maiti yangu ndo itarudi mbele kwa mbele

Watu ni wajinga sana wanachukia mafanikio ni mzee nilimchana nikamwambia hapo kwako sitafika ndugu zako wanga shenzi kabisa nilipofaulu tu anatangaza kila mtu anajua michongo nilishtua sikutaka zawadi wala kufanyiwa graduation wala sherehe tangu naanza nursery hizo zawadi watu wanaweka mauchawi yoa humu ndo maana hawaendelei ujinga tu
Nina regrets Ila sijui nisemeje mkuu ,ndo Dunia kunipa mafunzo
 
Nafuu Inarudi ,Kuna jamaa nlipelekwa kwake , Ila I won't divulge details za yy ni nani ,Ila siyo mshirikina au mganga , imekuwa siku mbili as of today maumivu yamereduce by a large extent , nangoja siku zipite nione how things will go
Ukipona tupe ushuuda apa
 
Story imetungwa kwa ubunifu hafifu sana! Sijui kama malengo yako yatatimia.

Hata katika story ukaongeza ...usisaidie maskin...! Ndo nikajua we sio mzima. Umechoka mwili na roho. Kwa taarifa yako kila mwenye hela anajua raha ya kusaidia.

Anajua namna gani anajiona ana thaman dunian. We uko kundi la kupewa huwezi jua hili. Unaamini furaha ni kuwa na pesa unasahau je ukishakuwa na pesa furaha inakuwa nini! Pesa ni tool ya kupata furaha sio furaha yenyewe!.

So, siwez kukupa ushauri wowote mana ni riwaya. Ila tambua tu maisha huweza kukuweka kona yoyote bila kuhusisha kurogwa wala kutenda wema wala ubaya.

Wema na ubaya ni mwanga na giza. Kuchagua ni hiari yako.

Tatizo la binadam ni kuamini hali nzuri inatuhusu lakin hali mbaya ni kwa wengine. Ndo maana mpumbavu akipata huwadharau anaowazidi.

Mianya iliyofunguka kwa nguvu za asili huweza kufunga pia kwa nguvu za asili. Ulichopata leo akakosa yule huweza kupewa mwingine ukakosa wewe.

Jifunze kupitia walau siasa za nchi yetu na jinsi awamu zinakuwa. Ulaji unavokuwa!

Kama una elimu dunia kidogo, jarib kuitumia kabla hujafikiria vya kufikirika!
Hii nimeipenda
 
Itakuwa huwajui watu yaani mtu anamsaidia ten alafu hiyohiyo inatumika kukulogea
 
Kusaidia Maskini sio tatizo tena ni BARAKA.

Tatizo hukuwa na uhusiano mzuri na Mungu muumbaji wako.

Mungu angekulinda wewe na mali zako na zingeongezeka zaidi na zaidi.

Mkabidhi Yesu Kristo maisha yako yasonge mbele mpaka ushangae.
 
Nafuu Inarudi ,Kuna jamaa nlipelekwa kwake , Ila I won't divulge details za yy ni nani ,Ila siyo mshirikina au mganga , imekuwa siku mbili as of today maumivu yamereduce by a large extent , nangoja siku zipite nione how things will go
Wengine tusaudie iyo connection ya mtoa tiba twaweza saidika pia mkuu
 
MITIHANI IPO DUNIANI,NAPITIA WAKATI MGUMU SANA MAISHANI.TOKA J MOSI NIPO NDANI SITOKI,PESA NASAIDIWA NA NDUGU TOKA TANZANIA,NA NNA FAMILIA YA MKE NA WATOTO WATATU,NIPO MBALI NJE YA TANZANIA, MAISHA YAMENIBADILIKIA GHAFLA ,YANI NDANI YA SIKU 3 MAISHA YAMEKUWA JUU CHINI,HAPA NIPO NDANI NA NNA R5 TU,SAWA NA 700 YA TANZANIA.
WATOTO WAMEENDA SHULE,WAKIRUDI SIJUI INAKUWAJE.
Pole sana kama hauumwi jitahidi sana kutoka nenda hata nyumba ya ibada inaweza kukupa kdogo amani na nafuu katika nafsi.
 
Ll check it up on Google later in the day ,sema the level of pain na body aches hainipi muda wa kupumua , eventually nkiovercome hili ,aliyeniseti ataanza kuhesabu siku zake Dunia hii , whatever goes around eventually comes around
Mungu wetu mwema akuponye urudi katika afya yako uendelee kusaidia taifa letu.
 
Back
Top Bottom