Ushauri wangu Kuhusu Machinga Jijini Mwanza

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Wamachinga ni wafanyabiashara wadogo wadogo wanaotafuta riziki zao kama wafanyabiashara wengine.

Wana familia, watoto, wajukuu ndugu n.k. Wamachinga wanashiriki pia katika kukuza uchumi wa nchi na hivyo wasipuuzwe. Katika siku za karibuni kumetolewa tangazo kuwa Wamachinga wanaopanga bidhaa pembeni mwa barabara, mbele ya milango ya wafanyabiashara wakubwa watafutiwe sehemu nzuri ya kuwaweka ili waendelee na biashara zao.

Mimi binafsi naunga kauli hii kwa asilimia mia moja. Sasa nije kwa ushauri wangu kuhusu wamachinga wa Jijini Mwanza. Naishauri Serikali Kuu, Halmashauri ya Jiji la Mwanza KUHAMISHA Shule ya Sekondari ya Pamba ili eneo litafutwe ili Shule hii ijengwe mahali pengine ili eneo la Pamba Sekondari pajengwe maghorofa ya kufanyia biashara kwa ajili ya wamachinga. Nashauri Shule ya Sekondari ya Pamba ihamishwe na pajengwe pale eneo la Nane Nane.

Serikali inaweza kutenga eneo la ekari kumi kwa ajili ya ujenzi huu. Kwa ushauri huu tutakuwa tumetibu suala la wamachinga. Wamachinga hawataki kutoka mjini.

Huu ni ushauri wangu na wanaweza kulifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom