Ushauri wangu juu ya kurejesha namba ya simu iliyopotea au kuibwa

Jul 14, 2021
25
26
Kumekuwa na utaratibu wa kwenda polisi pindi mteja wa mtandao wa simu anapo potelewa ama kuibiwa simu yake ili kurejesha namba yake.

Watanzania hawapendi usumbufu pia tuna haiba ya woga, kwa hiyo lipokuja suala la kwenda polisi kwa sababu kupotelewa na laini ya simu linakuwa changamoto kubwa sana.

Kutokana na hali hii watanzania wapoteza vitu vingi sana ambavyo vina umuhimu mkubwa kwao moja kupotezana na ndugu zao maana wanapopoteza laini zao awaendi polisi kupata loose ripoti ili walejeshewe namba zao za awali bali usajili mpya.

Pia kwenye laini ambazo wamepoteza huwa kunakuwa na pesa japo inawezakana si nyingi kwa mmoja mmoja ila zikikusanywa huwa nyingi, pesa hizi zote unufaika makampuni ya simu.

Nashauri kwenye ofisi zote za makampuni ya simu kuwe na kitengo kidogo cha Polisi ili kuwarahisishia wateja kwenda hadi polisi kupata hizi lose report
 
Back
Top Bottom