NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,206
- 12,747
Nafungua code TCRA na jeshi la Polisi Tanzania lifanyieni Kazi haraka ili kukomesha tabia ya wizi/utapeli kupitia simu.
Asalam alaykum Jammiya, Bwana Yesu asifiwe watumishi wa mungu hakika Kristo ni Tumaini letu sote Mimi na mwenzangu Cute Wife ni wazima wa afya.
Ni hivi mitandao ya simu Tanzania, Ina vibarua wanaopita mitaani wanaojulikana Kama mawakala (freelancers) Hawa hulipwa kwa commission kulingana na idadi ya sim card (laini za simu) watakazo sajili kwa mwezi na malipo yao hulipwa mwezi Hadi mwezi.
Hii shughuli ni mtu yoyote mwenye kujua na kusoma anaweza kufanya kazi na ajira zao hazina mkataba Wala hakuna Barua kutoka serikali za mitaa Hawa freelancers huwa Wana simamiwa na kiongozi wao (team leader) lengo ni kusimamia vifaa kazi /vya kutendea kazi lakini malipo ya mshahara wao hulipwa na system ya mtandao husika.
Twende kwenye point Kama kichwa habari kinavyojieleza.
Kumekua na meseji za "ile pesa tuma kwenye namba hii" /waganga kutoka sumbawanga/mtu kupiga simu nakuanza kujifanya katuma pesa kwenye namba yako.
Kwa kweli ukifikiria sana unagundua kabisa kuwa matapeli Wana Uhuru mwingi sana na wanajiachia sana.
Sasa swali linakuja je Hawa matapeli wanasajili laini kw kutumia vitambulisho vya Nani???
Kwa hali halisi hawawezi kutumia vitambulisho vyao maana wanahofia kukamatwa endapo Yale majina yatafatiliwa.
Matapeli hununua laini kwa Hawa freelancers (mawakala) wanaopita mtaani kusajili laini /wanaweza kujifanya hawana kitambulisho lakini wanahitaji sana laini husika kwa kuwa wakala anataka hela hufanya juu chini na kumpa tapeli laini bila ya kujua kuwa aliyempa laini ni MTU wa namna gani.
Kinachofanywa na mawakala (freelancers) ili kupata laini, wanapokua wanamsajilia mtu mwenye kitambulisho halisi humsajilia Mara ya kwanza na kukamilisha laini Kisha anamdanganya mteja kuwa ile namba ya kwanza mtandao umegoma kwa hiyo atamuomba mteja Tena kuchagua namba nyingine ili amsajilie Tena.
Mteja atakapo chagua Tena nakusajiliwa anakuwa amesajiliwa sim card mbili bila yeye kujua hapo atapewa moja na nyingine wakala anaondoka nayo kwenda huko anapokutana na mtu ndiyo hao matapeli anaiuza Kisha tapeli anaendelea kufanya kazi yake.
Huu mchezo unachezwa sana na hawa freelancers (mawakala) vitambulisho za mama zetu/bibi zetu/ wajomba zetu wanasajiliwa Mara mbili mbili sana na Kisha majina yao yanakwenda kutumika huko kutapelia watu.
Tcra mkishirikiana na Jeshi la Polisi NALIA NGWENA kupitia jamii forum nimeona nifungue mbinu ovu inaayotumiwa na freelancers (mawakala) wanaozunguka huko mitaani.