Kwanini ni muhimu kulinda simu yako ukipeleka kwa fundi kwa ajili ya matengenezo

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Habari za hivi majuzi za mwanafunzi ambaye picha zake za faragha zilifichuliwa baada ya kutuma iPhone yake kwa ajili ya matengenezo ni ukumbusho kwa watumiaji kufunga data zao, wataalam wanasema.

Apple ilisuluhisha kesi na mwanamke mwenye umri wa miaka 21 baada ya kutuma iPhone yake kwenye kituo cha matengenezo mnamo 2016, na kugundua kuwa wafanyakazi walikuwa wamepakia picha na video chafu binafsi kwenye akaunti yake ya Facebook kutoka kwa simu wakati wa mchakato wa matengenezo. Inasemekana kuwa kampuni hiyo ilimlipa mwanamke huyo mamilioni ya dola ili kusuluhisha kesi hiyo. Ni hatari ambayo watu wengi wanaingia wakati wa kutengeneza simu zao.

"Unapokabidhi simu yako kwa matengenezo, sio kifaa tu bali unapeleka hifadhi yako yote ya data zako binafsi," mtaalam wa faragha Pankaj Srivastava, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa kampuni ya ushauri ya usimamizi ya PracticalSpeak, alisema katika mahojiano ya barua pepe.

Je, kuna hatari gani unapopeleka simu kwenye matengenezo?

Maeneo mengi ambapo ungepeleka simu yako kwa matengenezo yatakuwa ya uaminifu, kwa hivyo uwezekano kwamba taarifa zako binafsi kusomwa na kutumiwa vibaya ni mdogo sana, Attila Tomaschek, mtafiti katika tovuti ya ProPrivacy alisema katika mahojiano ya barua pepe.

Mimi hufanya nakala rudufu (backup) ya data zangu na kisha kufuta kila kitu kwenye vifaa vyangu kabla ya kutafuta huduma ya matengenezo. Kwa kufanya hivyo, unaondoa kichocheo kwa mtu yeyote kuchungulia, hata kwa bahati mbaya.

"Lakini, bado kuna uwezekano mdogo kwamba unapopeleka simu yako mahali ambapo fundi hatokua mwaminifu na kuchunguza data za simu yako au hata kuiba, kwa hivyo inafaa kuwa waangalifu wakati wowote unapopeleka simu yako kwa matengenezo," Tomaschek aliongeza.

Kulinda Data zako

Ili kuhakikisha kuwa unakabidhi simu yako sehemu ya matengenezo inayotambulika kwanza fanya utafiti, Tomaschek anapendekeza. Angalia ukaguzi wa kampuni mtandaoni, na uangalie tovuti ya kampuni ili uone kama inaonekana kuwa ya kitaalamu.

Kama umeamua kwenda kufanya matengenezo, utahitaji kuchukua hatua zinazofaa ili kulinda simu yako.

"Jambo la chini kabisa unalopaswa kufanya kabla ya kukabidhi simu yako kwa fundi ni kutoka kwenye akaunti na programu zako zote kwenye simu yako ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu ambaye hajaidhinishwa anayeweza kufikia data yoyote kwenye programu zako," Tomaschek alisema.

Pia unaweza kutumia programu inayofunga baadhi ya faili kama vile picha na ujumbe kwenye simu yako ili zisiweze kufikiwa bila ‘password’ yako, aliongeza. Hakikisha umeondoa laini yako, pamoja na kihifadhi data chochote kama vile kadi ya microSD ambayo unaweza kuwa nayo kwenye simu yako. Na mwisho, kabla ya kukabidhi simu yako kwa fundi, utahitaji kuhakikisha kuwa umeunda nakala rudufu (backup) kamili ya simu yako.

"Kwa njia hiyo, unaweza tu kukamilisha urejeshaji wa mipangilio iliyotoka nayo kiwandani na kufuta kabisa data kwenye simu yako kabla ya kuiwasilisha kwa ajili ya mategenezo ili kuhakikisha hakuna data nyeti binafsi ambayo fundi ataweza kuipata," Tomasheck alisema.

Apple na Android hurahisisha kuhifadhi nakala na kuzirejesha kwenye kifaa chako, ili uweze kurejesha simu yako katika hali yake ya awali dakika chache baada ya kurejesha simu yako kutoka kwenye matengenezo.

Ingawa hakuna sababu kwa mtu yeyote katika sehemu ya matengezo kuchukua data zako binafsi, mara nyingi kuna mahitaji ya kweli ya kufungua ili kurekebisha kifaa, Srivastava alisema. Kwa sababu hii, sehemu nyingi za matengenezo watakutaka utie sahihi kanusho (disclaimer) ambalo pia hukutaka uondoe data zako binafsi kabla ya kuikabidhi kwa matengenezo.

"Kila mara mimi hufanya nakala ya data zangu na kisha kufuta data kwenye vifaa vyangu kabla ya matengezo," aliongeza. "Kwa kufanya hivyo, unaondoa kichocheo kwa mtu yeyote kuchungulia, hata kwa bahati mbaya."
 
  • Thanks
Reactions: LA7

simu mbovu utawezaje Fanya hayo mambo
 
Back
Top Bottom