Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep Quite!, Don't Ridicule Them!.

Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep Quite!, Don't Ridicule Them!.

CC ya CDM inaiumiza sana CCM ndo maana wanakomaa lakini mwisho wa yote wameshindwa na sasa chama kinaendelea na safari kama kawaida

Huyu mbunge wa mahakama si alisema anaenda kulecture ama alisubiri kuona atalipaje madeni ya waume zake CCM?


Waache maccm waendelee kukomaa na Zito wao, na CDM kiendelee na safari kama kawaida, na iendelee kuipokonya CCM kata katika chaguzi ndogo za udiwani zitakazofanyika februari 9, kama ilivyokuwa inafanya katika chaguzi ndogo zilizopita.

BTW: kampeni zitaanza wiki ijayo januari 16.
 
uwa mara nyingi sana nazielewa mada zako, na uwa una michango mizuri na mawazo mazuri, japo tunajua upande wako, ila kwa ili la leo na hasa kwa aya ya mwisho sikutegemea kama utaandika hiko kitu. ni vyema kuitengeneza heshima yako ikue, au ibaki palepale, kuliko kuifanya heshima yako ishuke.
 
Hongera Sana Zitto, nakupongeza hata sijui ameshinda nini? pingamizi limekubaliwa? harafu baada ya hapo? Hivi mwenye nyumba akikupa notes kabla ya muda kuisha ukakimbilia mahakamani, kweli mahakama ikakuruhusu uendelee kukaa kwenye nyumba hiyo utakuwa na amani kabisa rohoni mwako na utakaribisha wageni na ndugu zako kwenye hiyo nyumba na kujidai kabisa kwamba wewe ni zaidi ya mwenye nyumba? kwa kweli zitakuwa hazikutoshi!! Ni kweli KAZI yako haijakamilika ya kuisambaratisha CHADEMA kama ulivyotumwa lakini sina uhakika kama utaweza. KOMAA
Mwache ajinasibu na kujilisha upepo lakini nafsi inamsuta,atangangania tu mwisho ataachia.
 
Wanabodi,

Kwanza nampongeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kwa ushindi wa kishindo mahakamani leo kwenye kesi dhidi ya Chadema!.

Tangu day one niliwaeleza humu kuwa maamuzi ya CC ya Chadema, ni maamuzi ya kipuuzi kabisa sijapata kuona!, niliuliza hiyo CC ilipata wapi mandate ya kumvua ZZK madaraka yake wakati haina uwezo huo?!. Kesi ya msingi nayo pia atashinda!, Chadema italazimishwa kumrejeshea vyeo vyake vyote, kisha ufuate utaratibu rasmi kumvua vyeo hivyo na hatimaye kumvua rasmi uanachama wake!.

Ushauri wangu wa bure kwa Zitto, nakuomba sana, be calm, keep quite, don't boast, don't ridicule Chadema!. Pia usiendelee kutoa siri nyingine zozote za viongozi wako zaidi ya zile ulizokwisha toa!.

Sijapenda jinsi ulivyo toa siri za M/Kiti wako alivyopokea mihela ya Rostam na Mkono!. Sijapenda 'ulivyonunua' lile gari la Mkono bila kueleza popote umelinunuaje na kwa nini ulinunue kwake!, na pia sijapenda jinsi 'unavyolikodisha' lile gari jingine, huku ukiendelea 'kulilipia bila matatizo' bla kueleza lolote!.

Nakushauri baada ya kushinda kesi hii ya pingamizi, pia utashinda ile kesi ya msingi, ila Baraza Kuu, litakuvua rasmi vyeo vyako vyote na litakuvua uanachama wako, ambapo nafahamu utarudi tena mahakamani kuweka pingamizi mpaka 2015!.

Kwa vile umeishajua mustakabali wako Chadema na kiukweli hatimaye utaondoka, sisi baadhi ya tunaokukubali, tunakuomba na kukusihi, usiendelee kuibomoa Chadema!. Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.

Narudia tena, hongera sana Zitto Zuberi Kabwe!.

Congratulations!.

Pasco.


Pamoja na kwamba umetukimbia vijana wa madrasa kwenye MINAKASHA YETU,ILA KWA KUWA MIMI NI TEAM ZITTO KATIKA KUTOKOMEZA UDINI,UKANDA NA UKABILA BASI NAKUUNGA MKONO KWENYE HOJA YAKO HII,,

LEKATUTIGUTEEE..ZITTO GOGO LA UDIII,,TATIZO WAZEE WA SACOSS HII NA MTEI WAMEZOEA VYA KUNYONGAA,,SAFARI HII WAMESHIKISHWA ADABU,,PU,MBA.VU ZAO
 
Wewe PASCO ni m.p.u.m.b.a.v.u sana.Thibitisha kwamba chadema ni chama cha udini,ukabila na ukanda.Nyie ndio mnachochea wale wapuuzi wachache wanaojifanya waislamu kukichukia Chadema na kuanzisha vurugu zisizo na msingi.Wapeni kiburi tu siku wakikinukisha ndo mtatia akili wewe na mijimagamba wenzako.Hako kazito ni kajinga tu kapenda sifa na limbukeni hakajui alitendalo.
 
Ndugu V.P

Zitto still believes in the Mission of the Party, but he doesnot believe in The Personal Interests of the small bunch of Conmen.

The solution is not to quit, Zitto is not a quitter, he is a fighter, and he will fight until truth triumph over falsehood, He will fight until justice takes its rightful position in the party.

So worry not V.P , its unwise to let your meatstore under the leadership of hyenas. These Conmen will destroy the party, The party needs the likes of Zitto to fight and come to its rescue.

These Conmen are hopeless sinners, liars, selfish. And to let the party which millions of tanzanians had hopes and aspirations in it is a betrayal.

THATS WHY I SAY BROTHER ZITTO IS RIGHT, TO FIGHT FOR HIS RIGHTS AND THE TRUE PRINCIPLES OF THE PARTY, NOT THE PERSONAL PRINCIPLES OF MBOWE AND SMALL BUNCH OF STIFF NECKED FOOLS LIKE LEMA AND THE ARROGANT LISSU

Atakiwi sasa bro c bora asepe zake
 
Atakiwi sasa bro c bora asepe zake

hatakiwi na nani?- Lema, Lissu, Mbowe na genge la wahuni wachache?, kama ni hao basi wala haimsumbui kichwa, they can go to hell , Zitto ni mwanachama halali wa Chadema kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama.

Mbona wanakataa kumpa mwenendo wa Shauri lake ili limsaidie kujenga hoja za utetezi katika baraza kuu?

Pamoja na Zitto kuappeal baraza kuu " Under protest" kwa kuwa amenyimwa mwenendo wa shauri lake kwenye CC, Mbona basi bado wanaogopa kupeleka Rufani yake kwenye baraza kuu?.

Dawa ya Shamba lenye kuvamiwa na Nyani siyo kususa, Ukisusa Nyani wanachekelea, dawa ni kupambana mpaka kieleweke.

Uonevu wameufanya sana kwa Wanachama wengine, kina Kafulila , Machali, Shonza, Chacha Wangwe. SASA ENOUGH IS ENOUGH
 
Tukubaliane tu kuwa CHADEMA kama chama wameshindwa kujionesha kama ni taasisi inayoweza kushughurika na changamoto ambazo huwa haziepukiki pale chama kinapokua kwa kasi kutokana na chama kilichoko madarakani kushindwa kusimamia misingi ya chini kabisa katika ukuaji wa taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kuna watu mnanishangaza sana na hoja zetu za kutumia jicho moja katika mgogoro huu ambao umefika hapa kwa sababu ya uongozi kuruhusu jaziba ziwe ndiyo kipimo cha uongozi bora ndani ya chama.

Hebu nisaidie, unachanganua vipi kama hizi ni siri zinazokiathiri chama na zingine hazikiathiri chama wakati zinatolewa na viongozi wa hicho chama kuhusu viongozi wa hicho chama.

Mh. Tundu Lissu alipotoa siri za Zitto ili kutaka kuharalisha hoja yake kuwa Mh. Zitto ni tapeli wa kisiasa hukuweza kumkanya kwa sababu kwa mawazo yako kuchafuka Mh. Zitto kisiasa siyo kuchafuka kwa CHADEMA!, lakini Mh. Zitto alipotoa angalizo kumwambia Mh. Tundu Lissu kama anachokisema kwake kinampendezesha, basi lazima afahamu kuna mengi amuulize Mh. Mbowe ili yampendezeshe zaidi. Maneno ya Mh. Zitto ambayo yanafanana na yale aliyoyatoa Mh. Lissu ndiyo pekee unayaona yanakibomoa chama!.


By the way, hii dhana ya kufananisha chama kama taasisi na ndoa ya mtu inaingiaje kwenye uhai na utendaji wa chama?

Ng'wamapalala;

Hebu tujadiliane labda tutawasaidia CHADEMA kumaliza kwa usalama mgogoro wao dhidi ya ZZK kwa sababu km ambavyo mimi naamini,basi vivyohivyo najua na wewe unaamini kuwa pasipo upinzani imara sasa kwa Tanzania yetu hii basi kama ulivyosema tutakuwa tunailirejesha Taifa nyuma ktk ukuaji maendeleo na ustawi wake kiuchumi,kisiasa (kidemokrasia) na kijamii. Na binafsi sitaki na sipendi kuona CCM chama kikongwe kabisa sasa barani Africa na hapa kwetu Tanzania kikiachwa kutawala bila kuwepo kwa upinzani makini na wa ukweli.Maana yake ni lazima tufikiri na kujiuliza kwamba; Iwapo bado tuna vyama vya upinzani (japo chini ya migogoro ya ovyoovyo na lukuki) chini ya hawa CHADEMA,CUF,NCCR,TLP na vingine lakini bado Chama tawala CCM pamoja na serikali kinayiongoza vinafanya madudu ya kutisha,hivi itakuwaje iwapo kutakuwa na weak opposition au kusiwepo kabisa??......

Twende kwenye hoja yako,na mtazamo huu ufuatao;
  1. Bado naamini kwamba chama kama taasisi bado kipo kwenye right track katika kuushughulikia mgogoro huu pamoja na kwamba zipo kasoro za hapa na pale katika mchakato mzima. Na hii asitudanganye mtu awaye yeyote kwa sababu hizi kasoro zipo kwenye kila chama cha kisiasa hata ndani ya CCM ni tatizo tu!!
  2. Kuhusu Tundu Lissu vs Zito Kabwe kumwagiana siri hadharani (Tundu za Kabwe) na Kabwe naye kumjibu Tundu kwa kumwanika Mwenyekiti wake kwa kama hichohicho yeye anachotuhumiwa nacho. Naomba hapa niwe upande wa Lissu na chama chake na kwa hiyo kwa mwenyekiti wao ambaye kiukweli ndiye taswira ya chama kizima kwa sababu moja;Tundu Lissu alikuwa pale kukitetea chama chake dhidi ya kesi liyofunguliwa na mwanachama mmoja Zito Kabwe,katika hili kosa la Lissu ni moja tu kwamba kama hayo ni kweli na waliona mwanachama na kiongozi mwenzao amekiuka taratibu na kanuni za chama,basi hayo ya kuhongwa magari na Mkono wangeyaingiza kama sehemu ya tuhuma/mashtaka.Pili,Zito Kabwe kwa upande wake naye tayari alikuwa na mashtaka/tuhuma alizopaswa kujitetea kwazo mbele ya vyombo halali vya utetezi vya chama chake na kwa maana hiyo basi Zito alikuwa kwenye position nzuri ya kutoa defence kwa kuibua haya kama sehemu ya utetezi wake,badala yake yuko mahakamani kwa kuukuza mgogoro wa yeye na chama chake na si Mbowe tena kama ambavyo wengi tunadhani!!.Na kwa mtazamo wangu (na kama nitakuwa kinyume nirejeshe),ni kwamba aliwahi mno kwenda mahakamani badala ya kupambana kwanza kwa kutumia vikao vyao halali ndani ya chama na kama ingeshindikana na yeye kujiridhisha kuwa ameshindwa kusikilizwa,akaeleweka na hivyo kuadhibiwa kwa kuonewa,basi mahakama ndiyo ingekuwa mahali mwafaka kwake....and not at that early stage!!
  3. Binafsi,sina tatizo na Zito namkubali kwa kiwango cha juu kabisa kuwa ni mwanasiasa mahiri na katika siasa za upinzani za Tanzania,ni miongoni wanasiasa vijana aliyeleta hamasa kwa vijana wengi kupenda siasa na kujiunga na siasa.Hakuna anayebisha kuwa kina David Kafulila,Machali,Silinde,Mdee(Halima),Sugu na wengine kibao wapo pale kwa kuvutiwa na huyu jamaa na wakaona kuwa kumbe vijana WE CAN na si hivyo tu hata sisi huku nje ya mifumo rasmi ya kisiasa tuna ujasiri sasa wa hata kuhoji mambo ambayo zamani ilikuwa ngumu. Na hapa hatuwezi kamwe kuwaacha kaka zake kama Mwenyekiti wake (Mbowe) na wazee wake ndani ya chama chake ambao ndiyo waliompokea na kumlea kwa jina la chama chake na sasa anatukanana nao.
  4. Kinachonipa shida kwa Zito ni kitu kimoja kuwa kuwa ktk siasa ni pamoja na kuwa mjanja na mwerevu sana kwani elimu kubwa sana kwa maana ya vyeti na uwezo pekee wa kujenga hoja havitoshi ktk kufanya siasa za kishindani zilizojaa majungu na fitina za kiafrika. Ndiyo sababu hasa ya mgogoro huu,Zito kutokutambua hili. Laiti kama angetambua hili mapema na akautumia ujanja na werevu,akayaainisha madhaifu ya uongozi anaoudhania yeye kuwa hautoshi na unakiangamiza chama pasipo kuleta damage ya chama huku akiungwa mkono ndani kwa ndani,hauna elimu kama yake kupambana na anaowaita wahafadhina ndani ya chama chake angeweza ku -survive sana na pengine ingetokea siku moja mbeleni akapata anachokitafuta!!
  5. Na haya yote yanaposhindikana (kwa maana ya yeye Zito kushindwa kurekebisha mambo ndani ya chama chake anachoona hakipo sawa,hayaendi vizuri kwa kufuata taratibu sahihi),basi the best aption kwa wanasiasa walio komaa na wenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii huwa wanatoka,wanajitenga na kundi hilo kwa kufuata njia sahihi na za wazi zinazolinda heshima yao!!

JE, KWA HALI HII KUPARUANA WATAFIKA NA KUBAKI STRONG AS BEFORE?


Kwa maoni yangu YES watafika and they will remain even more stronger than before lakini kwa gharama kubwa sana ikiwemo kumpoteza huyu jamaa ZZK na pengine baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono. Na ofcoz hili si la ajabu kwa sana kwani siku zote tiba ya ugonjwa wowote inaumiza na kuchefua na pengine kukosa hamu ya kula na kutapika juu lakini mara upatapo afya unasahau hayo yote!!...Kwa nini naamini hivi? Ni kwa sababu moja tu nayo ni;
  • Zito Kabwe ameshatengwa,yuko peke yake nje ya mfumo mpana wa taasisi anayoitumikia na hao wenzake anaoamini ni wabaya,wabovu na wahafidhina......wanapambana naye kwa jina la taasisi (chama) na kiukweli atamshindwa tu (na hili ZZK naamni hata yeye ameshaliona) hata kama kweli kina Mbowe na wenzake wana madhaifu hayo yanayoimbwa. Kwa hiyo CHADEMA kama taasisi itasimama na hawa sasa wanaobaki na chama chao,kwa kuwa wamedhamiria kumfukuza na hii ni iwapo tu watau-manage vizuri mchakato wa kumtoa (na kuna uelekeo na ishara kuwa wameweza)

Haya ni maoni yangu na mtazamo wangu tu,tuendelee kujadili.........................
 
Sina shaka kabisa na msimamo wala maamuzi ya cdm juu ya Zitto na ninaunga mkono hilo kwa 100% kumuondoa ndani ya CDM. Shaka niliyonayo ni moja tu, kwamba taratibu na katiba ya kumchukulia hatua zzk huenda zilikuwapo na ndio zinazotugharimu CDM leo na katika kesi hii, lakini pia nna imani hatimae tutashinda. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu....

Toka awali nimekuwa na imani kubwa sana kwa mwenyekiti na katibu wake, na tukio hili linaidhihirisha imani yangu kwao zaidi kwani yale niloyajengea imani sqasa yanathibitika, vivyo hivyo toka awali nilikua na shak sana juu ya mwenendo thabiti wa zzk na leo hili pia linathibitsha kwangu kuwa zzk si mkweli na hapaswi kuungwa mkono asilani.

Mh. Mbowe, ni mtu ambaye kweli amejitoa kihali na mali kumpigania Mtz ambapo inasikitisha kuwa leo wapo ndani yetu wanaombeza..... of course ni kwawaida kwani mara zote unapoishi duniani lazima wawepo wanaokupenda na wanaokuchukia kinyume cha hapo basi lazima una tatizo. Big up Mh. Mbowe, Big up Mh. Slaa, Big up CC CDM na wengine wote wenye mapenzi mema na wanaotaka ukombozi wa kweli CDM

Kwa tahmini yangu ya haraka haraka juu ya utendaji wa viongozi wangu, ni Mkiti na Katibu amabo utendaji wao unazidi wenyeviti na makatibu wote east and central Africa. Chini yao chadema imepata mafanikio makubwa na kuongeza mizizi yake mpaka kwenye grass root level. Hili linajidhihirisha katika namna mbalimbali, 1. idadi ya wabunge toka 5 - zaidi ya 45 hivi sasa, kuongezeka kwa utawala wa CDM mpaka kiwango cha vitongoji, mabadiliko ya haraka na kazi kama vile CDM kuongoza halmashauri ndogo Arumeru muda mfupi tu toka uchaguzi mkuu lakini pia kwa mtidno uleule kuchukua Jimbo la Arumeru magharibi kwa kishindo kikubwa na kutoa upinzani mkali igunga pamoja na hujuma kubwa zilizofanyika huko, lakini moja kati ya mafanikio ya uongozi huu ni hamasa/ari kubwa nadani ya wananchi hivi sasa Tanzania ya kujua na kudai haki zao, jambo ambalo Mkiti wakati wote amekuwa akiliosema kama moja ya vitu ambavyo anavisimamia kuvijenga, ili hata kama CDM itachukua madaraka isiswaburuze wananchi bali iwajibike kwao. Yapo mengi ya kurejea kama mafanikio ya uongozi huu, wana JF wema hebu sasa tupate muda wa kuyaorodhesha yote ili malumbano haya yasiendelee kwa watu kuzomeana tu ila pia yatoe somo na watu wauone ukweli, nina imani kuwa ukweli huongea vizuri zaidi kuliko matusi au kuzomeana?????, nilichogundua hapa ni kwamba watu hawasomi hata magazeti kujua dhana fulani fulani, ni muhimu sana sasa tuusome waraka ule wa akina zitto wa kutaka mabadiliko ya uongozi na kuu critic kwa hoja bila hivyo tutapoteza muda na kutoka bila elimu wala kupanuana mawazo.

Kuhusu ZZK kwa kweli nimekuwa mfuasi wake bali wa mashaka (Urafiki wa mashaka) nimempenda kwa hoja zake mbali mbali japo mara zote nimekuwa nikikatishwa tamaa na namna ambavyo amekuwa akikosa udhati wa kuonyesha nia halisi ya kushughulikia yale anayodai kuyasimamia, nilimpenda sana kipindi alipotolewa nje ya bunge na kufanya Operesheni sangara, labdas hili ndilo pekee lililonikosha zaidi juu yake. Vinginevyo anaonekana zaidi katika mazingira yenye mashaka mashaka na kwa haraka haraka namuona Zitto Akiwasiliana sana na Mkurugenzi TISS 2010 katika kipindi kigumu CDM ikichakachuliwa juu ya matokeo ya urais/ubunge wakati ambapo Dr Slaa akilalamikia matokeo ya urais; Namuona zzk akitweet haraka sana kwa urahisi wakati wa matokeo kule Igunga akikiri CDM kushindwa eti kwa sababu chama hakijajengeka vijijini (Hata kwa matokeo yale yaliyochakachuliwa usemi wa zzk hauna ukweli na hasa ukizingatia ndio kwa mara ya kwanza CDM ilisimamisha mgombea), namuona zzk akifanya bidii kuahakikisha Pinda, Dewji, Mkono n.k akipambana kukihujumu CDM na wagombea wake ili CCM na maswahiba wake wapite bila kupingwa, namuona zzk akigoma kutoka nje ya Bunge rais alipokwenda kulihutubia eti kwa vile amemjengea barabara nk (Hapa uanaona ubinafsi wa dhahiri wa mbunge ambae leo nataka zugukia sehemu zote tanzania ati Mzalendo), namuona zzk ikulu akigonga glasi na rais kumpongeza kwa baraza jipya la mawaziri wakati M/kiti wake yupo Arusha akilaani kitendo cha katiba kuvunjwa kwa kuchguliwa baadhi ya mawaziri, Mh Mwinyi kushika wizara ambazo si za muungano, namuona zzk akiwa mabli na viongozi wenake nyakati zote - Akijitenga, Namuona zzk akiwa mbele kwenye ajenda ya kutaka uongozi wa juu kwa udi na uvumba bila staha- Urais, uenyekiti, uongozi wa upinzani bungeni (taamaa ya madaraka; namuona zzk akienda Anticlockwise wakati wenzake wakienda clockwise nk. Nabaki mwenye mashaka makubwa juu ya uzalendo na ukweli wake na sasa namuona ni msalitit anaepaswa kufukuzwa chama tu.

Ukweli hapa kulingana na mtazamo wangu ni kuwa zzk kwa kutofautina na uongozi wote amepoteza sifa na hawezi kubaki cdm, this does not need rocket sayansi kulitambua, ni wazi kuwa atatapata wana cdm wanaomuunga mkono lakini wale ambao hwapo uongozini kumbe itakuwa ngumu kwake kuongoza cdm, haiwezekani wewe peke zako ukaongoza chama katika mazingira ambayo cdm imefikia, hilo linawezekana UDP, TLP, UDP etc etc.

Ukweli ni kwamba M/kiti na katibu CDM wamekuwa mwiba kwa CCM kwani wamevaaa sura ya serikali mbadala inyojihidhirisha ndani ya uongozi thabiti wa kutohongeka na kujitolea kwa hali na mali, lakini pia muamko na ari kubwa ya watanzania juu ya CDM uliotokana na uongozi wao. Wote tutakiri jinsi ambavyo watanzania wamekuwa mbele kuichangia cdm hata kwa mpesa mpaka hujuma ya kukata kodi ya mabilioni toka CDM m-pesa ilipotungwa. Mh. Mbowe hakuzivaa combat kwa bahati mbaya au kifasheni zaidi kama ambavyo inaonekana sasa bali vazi lile liliendana fika na mwandani wake, ukweli, nia, thirika na utendaji wake. Niliwahi safiri na dada mmoja ambae aliwahi fanya kazi na mbowe, akanithibitishia hilo, kwamba Mbowe ni mtu ambae akishaamua kufanya kitu akaanza basi ni mpaka akimalize/akikamilishe, akanimabia kwamba wakati akijenga Bilicanas alikesha usiku na mchana site aliondoka asubuhi tu tena kwa muda mfupi kwenda kwa Bfast kubadili nguo na kurudi site kwa mkesha mwingiine, alipokuta mkewe anadunduliza ili ajenge nyumba yao kisiri, aliingilia kati plan hiyo kuanza na kujenga nyumba nadni ya mwezi mmoja nk, hii ilinikumbusha muda wote hata kabla chadema haijafika hapa Mbowe akizunguka kwa kampeni zake za urais akitumia Helikopta kuhutubia vijijini pamoja na kukijenga chama akiibua hamasa ya mabadiliko.
Hakika sura yake na Dr. Slaa katika siasa za tz inatisha ccm ndio maana wanatafuta mamluki ili kile kilichotokea NCCR kijirudie....Tulianza na mungu tutamaliza na mungu.

Wana JF, mkakati wa zzk, kitila na Mwigamba haupaswi kuungwa mkono kwa namna yeyote sio tu na CDM au wanachama wake bali wanamageuzi wote Tz. Ni kweli katka chama au jamii kwa ujumla hakukosekani makundi lakini makundi hayo yasiwe ya mafungate au kimtandao bali ya hoja na yenye afya kwa chama kwa maana watu watafungama na hoja sio mtu fulani. Hili ndilo linalowasumbua ccm hata leo, ndio maana wanashindwa kuwajibishana, kujivua magamba nk. Raisi Kikwete alipokutana na makatibu wa Wilaya/Mikoa dodoma aliongea kama analia tu hana meno kwa ajili ya mtandao ndani ya ccm akaishia kuwalalamimikia kwamba mtindo wao wa kuchukua posho za simu kila mwezi wa laki mbili kila mwezi utakiua chama, haya ndio matokeo ya Mitandao. Katika mtindo wa mitandao watu hawatahoji CDM imesema nini bali nani kasema ndani ya cdm, kiwe cha ujinga au busara ili mradi kasema zzk sawaaaaa!!!! akasema mbowe holaaaaaaa!!!!!!!! Slaa mjinga!!!!!!!!!!!!!, tusifike hukoooo hakuna maslahi ya taifa hili.

Mh. Mbowe & Slaa, zzk na waheshimiwa wote wenye nia nzuri, ukiona unapingana na wengi ndani ya CDM its time to quit, ndio taratibu za siasa!!!! Mwl. Nyerere aliwahi kumshangaa Mh. Kawawa kwamba anadai hwezi toka ccm!!! yeye akaweka bayana kabisa kuwa ccm sio babake wala mama kwamba huwezi mbadili na kwamba kwamba ccm haitatekeleza kile anachoamini ataondoka....!!! Lyatonga Mrema laifanya hivyo mara kadhaa na wakati wote wafuasi wake walimfuata. Mh zzk ni wazi kwangu wewe unapingana na wenzako na kwa hali hii nakushauri utoke na wafuasi wako watakufuata tuu...... Vinginevyo hisia za watu kwamba --------- na ccm zitaongezeka kwani itakuwa kama vile kukimbia kazi ambayo umeshalipwa kumbe uanang'ang'ania ili kuikamilisha...... Tazama Damu za watu zimeshamwagika kuipigania CDM na ukombozi wa taifa hili sehemu nyingi, kkwa mzalendo halisi angekubali kupoteza maslahi yake ili chama hiki kifike mahali kutoa heshima ya damu iliyomwagika, na mungu afurahie hilo, usikatize mapango wa mungu laana itakufuata kwani damu ya wanyonge hawa bado inalia juu ya taifa hili

Aluta Continua CDM

Mungu ibariki CDM... Mungu ibariki TZ

Tulianza na mungu.... Tutamaliza na Mungu, Amen.

Bro Zitto,

Kwanza nikupe pole kwa hizi changamoto unazokabiliana nazo ndani ya chama.

Dhamira yangu ni kukupa ushauri mfupi lakini ninaamini utakusaidia kama utauzingatia, ninaamini utanielewa kwa kuwa nimewahi kuwa na mazungumzo nawe juu ya maswala mbalimbali na nilikuona kwamba ni kijana mwenye upeo mzuri wa mambo na bado ninaamini una uwezo mkubwa wa kupima mambo.

Ninachotaka kukushauri ni kwamba ktk hili sakata la wazi kati yako na viongozi wa Chadema, hapa kama mtu mzima lazima utambue kwamba hamuwezi tena mukaaminiana na kufanya kazi kwa pamoja, kama imefikia hatua ya kuamini kwamba wenzako wamejaribu njama za kukudhuru na wanachama wanaamini kwamba wewe ni msaliti, it is rather immateurish kulazimisha kuwa ktk nafasi yako kwa kutumia mahakama. End of the day 'personal relationship na confidence' na viongozi wenzako ni muhimu kuliko amri za mahakama.

Kung'ang'ania uongozi ndani ya Chadema kunawapa wachambuzi wa mambo sababu ya kuamini haupo hapo kwa ajili ya chama bali kwa ajili yako binafsi. Kimsingi haiwezekani ukijenge chama ktk mahusiano mabaya na viongozi wenzako.

Nakushauri uwe na matured approach kama ile ya Mheshimiwa Kagasheki.

Sina nia ya ku comment on who is right and who is wrong between you and the rest of leadership, the take home message ni kwamba you will not be in a position to lead kama viongozi wa ngazi ya juu are against you, whether differences zao with you ziko legitimate ama sio does not really matter.

Unaposema you will be the last person to quit the party hiyo statement ina udhaifu mkubwa sana, inaashiria upo hapo kwa sababu maalumu. Afadhali ungesema utakuwepo Chadema for as long as u believe in the mission of the party, as long as you believe in leadership etc.

Na hao CCM wanavyokutetea ndio wamezidi kuharibu na kukuharibia reputation yako na ku solidify hisia kwamba wewe ni kibaraka wao ndio maana hawataki kusikia unatoka Chadema. Bora wangekaa kimya, kimsingi hawana hata basic skills za ku manage perception.

I am personally disappointed na hii immaturity iliyooneshwa na Chadema leadership ktk mgogoro huu wa ndani. Kwa kweli bado Chadema is not ready to lead this country, utoto umekuwa mwingi.
 
naona mmejifunga vibwebwe kulitumbukiza taifa hili la tanzania kwenye machafuko kwa nguvu zenu zote.....kwa nini akili zenu zinawatuma kutumia propaganda za kishenzi/wildness yaana za kuchochea machafuko kwa nija ya kidini, ukabila, ukanda na propaganda za kishenzi kama hizo hali ninyi waandishi ndiyo hasa mnatakiwa kuubiri amani, umoja, mshikamano, kuvumiliana kusaidiana baina ya waafrika wazaliwa na waamiaji wa tanzania? Kwa nini..!

Nakumbuka ulishawahi kuonywa huko nyuma juu ya propaganda zako hizi za kishenzi, ulisikia na ukaacha. Sijaelewa ni nini kimekusibu. Kwa ulichoandika hapa...natangaza kupatika arap sang wa bongo mwingine akimfuata the big show. Kwa kuwakumbusha tu...arap sang ni mtangazaji na mwandishi wa habari wa kenya ambaye ameshitakiwa huko icc-the hague kwa kutumia matangazo yake ya redio kuchochea maauaji ya wakenya baada ya uchaguzi mkuu nchini humo

kwa nguvu zangu zote popote nitakapo pata nafasi nitapinga utumiaji wa propaganda za kishenzi za udini, ukabila, n.k zinazoelekea kuleta machafuko nchi.

Ndugu wananchi, waafrika, watanzania wenzangu...tuwapige vita wale wote wanaoeneza udini, ukabila, na mengine kama hayo ili kuleta machafuko nchi kwa kisingizio chochote kile. Kwa hili tuanze na pasco wa jf na mwenzake the big show.

Nina imani tutaishinda vita hii maana tunaweza bila hata kuwewezeshwa na ndugu zetu wa mataifa ya nje.


udini,ukanda na ukabila ndan ya chadema sisi sio waanzilishaji,umeanzwa kusemwa tokea enzi za marehemu chacha wangwe,sisi hatuchochei,sisi tunakemea,

kama wewe unaumia kwa hilo,pole sana hatuna jins ya kukusaidia,ila hatutaacha kusema kuhusu hili,,

hadi pale tutapobaini mmeacha huu udini,ukanda na ukabila wenu,,full stop..!!
 
Hata kama mahakama itagangana abaki CDM , atabaaki ka gharasha ajue hivyo !!

Hii nchi inahitaji wanasiasa nguli wenye mawazo huria kama wa Kenya,baada ya mgombea binafsi kuruhusiwa zitafanyika coalition nyie na mavyama yenu yaliyooza mtajiju sisi tutachagua watu wenye maono sio wale too local au too old au saccos
 
Bro Zitto,

Kwanza nikupe pole kwa hizi changamoto unazokabiliana nazo ndani ya chama.

Dhamira yangu ni kukupa ushauri mfupi lakini ninaamini utakusaidia kama utauzingatia, ninaamini utanielewa kwa kuwa nimewahi kuwa na mazungumzo nawe juu ya maswala mbalimbali na nilikuona kwamba ni kijana mwenye upeo mzuri wa mambo na bado ninaamini una uwezo mkubwa wa kupima mambo.

Ninachotaka kukushauri ni kwamba ktk hili sakata la wazi kati yako na viongozi wa Chadema, hapa kama mtu mzima lazima utambue kwamba hamuwezi tena mukaaminiana na kufanya kazi kwa pamoja, kama imefikia hatua ya kuamini kwamba wenzako wamejaribu njama za kukudhuru na wanachama wanaamini kwamba wewe ni msaliti, it is rather immateurish kulazimisha kuwa ktk nafasi yako kwa kutumia mahakama. End of the day 'personal relationship na confidence' na viongozi wenzako ni muhimu kuliko amri za mahakama.

Kung'ang'ania uongozi ndani ya Chadema kunawapa wachambuzi wa mambo sababu ya kuamini haupo hapo kwa ajili ya chama bali kwa ajili yako binafsi. Kimsingi haiwezekani ukijenge chama ktk mahusiano mabaya na viongozi wenzako.

Nakushauri uwe na matured approach kama ile ya Mheshimiwa Kagasheki.

Sina nia ya ku comment on who is right and who is wrong between you and the rest of leadership, the take home message ni kwamba you will not be in a position to lead kama viongozi wa ngazi ya juu are against you, whether differences zao with you ziko legitimate ama sio does not really matter.

Unaposema you will be the last person to quit the party hiyo statement ina udhaifu mkubwa sana, inaashiria upo hapo kwa sababu maalumu. Afadhali ungesema utakuwepo Chadema for as long as u believe in the mission of the party, as long as you believe in leadership etc.

Na hao CCM wanavyokutetea ndio wamezidi kuharibu na kukuharibia reputation yako na ku solidify hisia kwamba wewe ni kibaraka wao ndio maana hawataki kusikia unatoka Chadema. Bora wangekaa kimya, kimsingi hawana hata basic skills za ku manage perception.

I am personally disappointed na hii immaturity iliyooneshwa na Chadema leadership ktk mgogoro huu wa ndani. Kwa kweli bado Chadema is not ready to lead this country, utoto umekuwa mwingi.

unatumia sababu zipi kusema kuna kung'angania madaraka chadema? mbowe ni mwenyekiti hii 2014 anafikisha miaka 9 ya uenyekiti na uchaguzi unafanyika haijulikani kama atafikisha 10, kikwete lazima afikishe 10 wa ccm, mwenyekiti wa cuf anazaidi ya miaka 20 ya uenyekiti. sasa sijui unamaana gani au unamtindio wa ubongo wa kuhongwa kama makahaba wa buguruni na kufanya kila akuagizacho bwana wako?
 
Bro Zitto,

Kwanza nikupe pole kwa hizi changamoto unazokabiliana nazo ndani ya chama.

Dhamira yangu ni kukupa ushauri mfupi lakini ninaamini utakusaidia kama utauzingatia, ninaamini utanielewa kwa kuwa nimewahi kuwa na mazungumzo nawe juu ya maswala mbalimbali na nilikuona kwamba ni kijana mwenye upeo mzuri wa mambo na bado ninaamini una uwezo mkubwa wa kupima mambo.

Ninachotaka kukushauri ni kwamba ktk hili sakata la wazi kati yako na viongozi wa Chadema, hapa kama mtu mzima lazima utambue kwamba hamuwezi tena mukaaminiana na kufanya kazi kwa pamoja, kama imefikia hatua ya kuamini kwamba wenzako wamejaribu njama za kukudhuru na wanachama wanaamini kwamba wewe ni msaliti, it is rather immateurish kulazimisha kuwa ktk nafasi yako kwa kutumia mahakama. End of the day 'personal relationship na confidence' na viongozi wenzako ni muhimu kuliko amri za mahakama.

Kung'ang'ania uongozi ndani ya Chadema kunawapa wachambuzi wa mambo sababu ya kuamini haupo hapo kwa ajili ya chama bali kwa ajili yako binafsi. Kimsingi haiwezekani ukijenge chama ktk mahusiano mabaya na viongozi wenzako.

Nakushauri uwe na matured approach kama ile ya Mheshimiwa Kagasheki.

Sina nia ya ku comment on who is right and who is wrong between you and the rest of leadership, the take home message ni kwamba you will not be in a position to lead kama viongozi wa ngazi ya juu are against you, whether differences zao with you ziko legitimate ama sio does not really matter.

Unaposema you will be the last person to quit the party hiyo statement ina udhaifu mkubwa sana, inaashiria upo hapo kwa sababu maalumu. Afadhali ungesema utakuwepo Chadema for as long as u believe in the mission of the party, as long as you believe in leadership etc.

Na hao CCM wanavyokutetea ndio wamezidi kuharibu na kukuharibia reputation yako na ku solidify hisia kwamba wewe ni kibaraka wao ndio maana hawataki kusikia unatoka Chadema. Bora wangekaa kimya, kimsingi hawana hata basic skills za ku manage perception.

I am personally disappointed na hii immaturity iliyooneshwa na Chadema leadership ktk mgogoro huu wa ndani. Kwa kweli bado Chadema is not ready to lead this country, utoto umekuwa mwingi.


Ulionesha kama unamshauri vizuri Zitto lkn kwenye kumalizia ukaharisha uharooooo

sasa wewe unaona ni bora kuongozwa na waoamrisha jeshi kuua raia eti WAPIGE TU TUMECHOKA.

Hao wanahamishia kodi yetu nje ya nchi

Hao wanamaliza Tembo wetu na kuuza Twiga wazimawazima

wanaosafiri kila nchi kutafuta neti na kondom

wanamaliza raia Nyamongo haku wazungu wanatuachia mahandaki

wanaoongoza duniani kwa kuuza UNGA

Wanatibiwa ulaya huku raia wakifa kwa magonjwa yanayotibika

wanaua kizazi cha watanzania kwa kuwanyima elimu bora huku watoto wao wakisoma kwenye shule za mamilioni ya fedha

Wanaopandisha umeme usiku na mchana na kuuzia wananchi maji machafu kwa bei juu

KWAKWELI KUENDELEA KUITETEA CCM YENYE MADUDU YOOOTE HAYO NI UJUHA WA HALI YA JUU SANA.

C C M NI MAJANGA
C C M NI UCHAFU

NO CCM NOOOOO.
 
Yule jamaa amekuja kunidisappoint pale alipoanza kuropoka kwa kutaja tuhuma za madhambi ya viongozi wenzake.

Amekuwa silent kwa miaka yote hiyo, leo hii ndio anaona sifa kusema baada ya usaliti wake kugundulika.

Hata kama ni ukweli umekuja at wrong timing, dawa ni aende tu.
 
Back
Top Bottom