Ng'wamapalala;
Hebu tujadiliane labda tutawasaidia CHADEMA kumaliza kwa usalama mgogoro wao dhidi ya ZZK kwa sababu km ambavyo mimi naamini,basi vivyohivyo najua na wewe unaamini kuwa pasipo upinzani imara sasa kwa Tanzania yetu hii basi kama ulivyosema tutakuwa tunailirejesha Taifa nyuma ktk ukuaji maendeleo na ustawi wake kiuchumi,kisiasa (kidemokrasia) na kijamii.
Twende kwenye hoja yako,na mtazamo huu ufuatao;
Bado naamini kwamba chama kama taasisi bado kipo kwenye right track katika kuushughulikia mgogoro huu pamoja na kwamba zipo kasoro za hapa na pale katika mchakato mzima. Na hii asitudanganye mtu awaye yeyote kwa sababu hizi kasoro zipo kwenye kila chama cha kisiasa hata ndani ya CCM ni tatizo tu!!
Mkuu
Kitaturu ,
Ni kweli kabisa ukuaji na ukomavu wa chama cha siasa unabainishwa na uwezo wa kupambana na changamoto zilizoko mbele yake.
Sielewi una maana gani unaposema chama kiko kwenye right track katika kupambana na changamoto hii na hizi tunazoziona ni kasoro ndogo ndogo?
Mkuu wangu, hivi unadhani chimbuko la mgogoro huu ni nini?. Ninatumaini ukinieleza chimbuko ndiyo tutafahamu pia njia za kuweza kuuponya kwa sababu tusije tutawa tunatoa vidonge vya kupunguza maumivu badala ya dawa ya dawa ya kuponya. Kumpa mgonjwa vidonge vya kupunguza maumivu huko siyo kumponya bali ni kuyasogeza matatizo na ugonjwa mbele.
Kuhusu Tundu Lissu vs Zito Kabwe kumwagiana siri hadharani (Tundu za Kabwe) na Kabwe naye kumjibu Tundu kwa kumwanika Mwenyekiti wake kwa kama hichohicho yeye anachotuhumiwa nacho. Naomba hapa niwe upande wa Lissu na chama chake na kwa hiyo kwa mwenyekiti wao ambaye kiukweli ndiye taswira ya chama kizima kwa sababu moja;Tundu Lissu alikuwa pale kukitetea chama chake dhidi ya kesi liyofunguliwa na mwanachama mmoja Zito Kabwe,
Ni kweli kabisa kazi yake ni kukitetea chama lakini kumbuka kuwa unapompa solicitor kesi yako akutetee kwenye vyombo vya sheria lazima vile vile umweleze kila kitu ili aweze kujenga ushahidi mzuri kisheria. Kosa hapa siyo la Mh.Tundu Lissu bali la uongozi anaoutetea kwa kutompa Mh. Lissu maelezo yote yanayohusiana na kesi. Hawakumweleza 'madudu' waliyoyafanya huko nyuma wakati wakiwa na Mh. Zitto kwenye harakati za kukijenga chama ili Mh. Tundu Lissu aweze kujenga hoja mbadala za kisheria huku akiruka viunzi kama kutoyasema hayo aliyoyasema kwa faida ya mstakabali wa chama.
Mkuu wangu, kwa hiyo unataka kusema "Naibu Katibu Mkuu" hakuwa pia taswira nzima ya chama? Naibu Katibu Mkuu ni kiongozi mkuu ndani ya chama ambacho ni makini.
katika hili kosa la Lissu ni moja tu kwamba kama hayo ni kweli na waliona mwanachama na kiongozi mwenzao amekiuka taratibu na kanuni za chama,basi hayo ya kuhongwa magari na Mkono wangeyaingiza kama sehemu ya tuhuma/mashtaka.
Kama nilivyokueleza, hili siyo kosa la Mh. Lissu bali ni kosa la uongozi anaoutetea (wewe unasema ni chama) wa kutomweleza ukweli na kikubwa kabisa wasingeweza kuweka hizi shutuma ndani ya mashitaka kwa vile walifahamu kabisa kufanya hivyo ni kufunga mlango wa wao pia kujikuta wana mashitaka au hoja nzito za kujibu kwa wananchama wao.
Kwa kifupi tu, huu mgogoro bado haujawekwa wazi ili 'wapita njia' kama mimi na wewe tuweze kuuchambua vizuri. Kauli kama hizi zinaonyesha kuwa kuna mambo mengi sana wanatuficha sisi 'wapita njia' na sielewi sijui kwa faida yao au ya chama. Time will tell!
Pili,Zito Kabwe kwa upande wake naye tayari alikuwa na mashtaka/tuhuma alizopaswa kujitetea kwazo mbele ya vyombo halali vya utetezi vya chama chake na kwa maana hiyo basi Zito alikuwa kwenye position nzuri ya kutoa defence kwa kuibua haya kama sehemu ya utetezi wake,badala yake yuko mahakamani kwa kuukuza mgogoro wa yeye na chama chake na si Mbowe tena kama ambavyo wengi tunadhani!!.
Mkuu wangu, ninadhani unaelewa kuwa kujibu mashitaka ni tofauti na kuweka mashitaka.
Kwanza lazima uelewe kuwa kuna mambo mawili hapa.
1) Mashitaka ambayo yanapelekea;
2) Kuvuliwa uongozi ndani ya chama.
Mh. Zitto alijibu mashitaka yaliyoletwa kwake ndani ya siku 14 kama kanuni zinavyomtaka lakini vile vile akawa yuko kwenye mchakato wa kukata rufaa kwenye Baraza Kuu la chama kwa kuvuliwa uongozi kwa sababu hakukuwa na kigezo au hakupewa huo waraka uliomshutumu ambao ulikuwa ni kigezo cha kumvua uongozi ndani ya chama.
Katika majibu yake kwenye mashitaka alimalizia kwa kusema hivi,
a)
Nakanusha kila tuhuma mojamoja na kwa ujumla wake dhidi yangu. Mashtaka yote dhidi yangu sio kweli na sijavunja Katiba au Kanuni za Chama.
b) Naiomba Kamati Kuu ijiridhishe kwa kiasi kinachostahili kuhusu mashtaka yote niliyoshtakiwa nayo kwa kuangalia ushahidi wote uliotolewa au utakaotolewa dhidi yangu.
c) Utetezi wangu umetolewa bila kupewa nakala ya Waraka unaosemekana nimeuandaa ilhali kukiwa na maelezo kwamba kuna waraka ‘feki' na waraka ‘original' ambao umetumika na Kamati Kuu kufikia maamuzi yake.
d) Ndugu Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwa maneno yao wenyewe wametamka kwamba hawakunishirikisa na sikushiriki kwenye uandaaji wa waraka ambao ndio msingi wa mashtaka haya. Kamati Kuu inao ushahidi huo.
Wako katika ujenzi wa Chama,
.............................. ......................
Mh. Zitto Zuberi Kabwe (MB).
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ka-yote-sio-ya-kweli-na-sijavunja-katiba.html
Kwa maana hii, hata waraka ambao ulikuwa unamtuhumu hakuweza kupewa ili kujenga utetezi katika maono ya haki ya mtuhumiwa.
Na kwa mtazamo wangu (na kama nitakuwa kinyume nirejeshe),ni kwamba aliwahi mno kwenda mahakamani badala ya kupambana kwanza kwa kutumia vikao vyao halali ndani ya chama na kama ingeshindikana na yeye kujiridhisha kuwa ameshindwa kusikilizwa,akaeleweka na hivyo kuadhibiwa kwa kuonewa,basi mahakama ndiyo ingekuwa mahali mwafaka kwake....and not at that early stage!!
Nilieleza kule juu kuwa tatizo la msingi linalotukabili sisi 'wapita njia' ni kutokuelewa undani wa mgogoro huu kitu ambacho wengi kinatufanya kuanza kununua spinning kutoka pande zote za mgogoro huu.
Nikiangalia kwa undani kutokana na maelezo ya Mh. Zitto ninagundua kuwa kulikuwa na jitihada za makusudi ambazo zilifanywa na upande wa pili ili upande wingine ujikute unavunja taratibu na kanuni katika procedure za kichama kwa kufahamu au bila kufahamu kuwa kufanya hivyo pia ni kukiuka katiba ya nchi ambayo ndiyo msingi mkuu wa uwepo wa Katiba za vyama vya siasa na kutokana na hivyo, hapa ndipo mahakama inapoingia kwenye mgogoro huu.
Naomba ujiulize, kwa nini Mh. Zitto ameshinda pingamizi lake mahakamani ambalo mawakili wa upande wa uongozi walilipinga kama kweli procedures zilikuwa zimefuatwa na uongozi wa chama, lakini vile vile, kumbuka kuna kesi ya msingi ambayo inaanza kusikilizwa Feb 13 ya kukitaka chama kimpatie mwenendo wa shauri lililofikia mpaka yeye kuvuliwa uongozi kama taratibu na kanuni za chama zinavyotaka. Hii inaonyesha kuwa uongozi haukutaka hata kumpatia mwenendo wa shauri mpaka akaamua kwenda mahakamani ili mahakama iushinikize ufanye hivyo.
Binafsi,sina tatizo na Zito namkubali kwa kiwango cha juu kabisa kuwa ni mwanasiasa mahiri na katika siasa za upinzani za Tanzania,ni miongoni wanasiasa vijana aliyeleta hamasa kwa vijana wengi kupenda siasa na kujiunga na siasa.
Kinachonipa shida kwa Zito ni kitu kimoja kuwa kuwa ktk siasa ni pamoja na kuwa mjanja na mwerevu sana kwani elimu kubwa sana kwa maana ya vyeti na uwezo pekee wa kujenga hoja havitoshi ktk kufanya siasa za kishindani zilizojaa majungu na fitina za kiafrika. Ndiyo sababu hasa ya mgogoro huu,Zito kutokutambua hili. Laiti kama angetambua hili mapema na akautumia ujanja na werevu,akayaainisha madhaifu ya uongozi anaoudhania yeye kuwa hautoshi na unakiangamiza chama pasipo kuleta damage ya chama huku akiungwa mkono ndani kwa ndani,hauna elimu kama yake kupambana na anaowaita wahafadhina ndani ya chama chake angeweza ku -survive sana na pengine ingetokea siku moja mbeleni akapata anachokitafuta!!
Yes. Ninakukubalia sana na wewe kwa hili kuwa na yeye Mh. Zitto anaudhaifu sana ambao ukiangalia unasababishwa na UJANA.. Vijana mara nyingi hawana subira kwa sababu wana hii kitu inaitwa KUJIAMINI SANA au unaweza kusema, HAWAOGOPI risks zitokanazo na maamuzi yao kwa sababu huwa wanadhani wanaweza kupambana nazo, kwa lugha nyingine, vijana wengi hili neno SWOT analysis kwao ni uchafu na hawataki kulidadavua.
Kwa hoja yako hili tunarudi tena kule kule niliposema uongozi wa CHADEMA umeshindwa kuushughurikia ipasavyo huu mgogoro kwa kuruhusu jaziba kuwa ndiyo kipimo cha uongozi bora. Kama chama kingekuwa serious, basi kingefahamu kuwa kwa vile msingi wake wa ukuaji ni vijana, basi kungekuwa na umuhimu wa kwanza katika kuweka mechanism ya kuwajenga kimfumo hawa vijana ili wasije kuathiri mwenendo mzima wa ukuaji wa chama.
Na haya yote yanaposhindikana (kwa maana ya yeye Zito kushindwa kurekebisha mambo ndani ya chama chake anachoona hakipo sawa,hayaendi vizuri kwa kufuata taratibu sahihi),basi the best aption kwa wanasiasa walio komaa na wenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii huwa wanatoka,wanajitenga na kundi hilo kwa kufuata njia sahihi na za wazi zinazolinda heshima yao!!
Hapa ndipo ninapopingana na watu wengine!.
Baraza kuu la chama ndani ya CHADEMA ndiyo kipimo kikuu cha chama. Ndiyo chama chenyewe. Hawa ndiyo waamuzi wa mstakabali wa chama. Ndiyo nguzo kuu ya chama.
Tatizo analoliona Mh. Zitto siyo chama ambacho muhimili wake mkuu ni Baraza kuu. Ndiyo maana anapenda mambo yake yapelekwe kwenye Baraza Kuu kama taratibu na kanuni zinavyotaka ili akahukumiwe huko, lakini kwa kuangalia kwa nje, inaonekana kuwa baadhi ya viongozi wakuu hawakutaka kufanya hivyo na hasa ukirejea kesi yake ya msingi itakayoanza kusikilizwa Feb 13. Tatizo analoliona Mh. Zitto ni baadhi ya viongozi wakuu na sababu zake kila pande haitaki kuzieleza kwa undani kutokana na maslahi yao.
Sasa mkuu wangu ulitaka aondoke bila wenye chama kumwambia kuwa yeye ndiyo amepotoka kwa sababu anakokwenda siko ambako chama kinakwenda kwa sababu yeye hajaona kama amepotoka.
JE, KWA HALI HII KUPARUANA WATAFIKA NA KUBAKI STRONG AS BEFORE?
Kwa maoni yangu YES
Mwanasiasa mmoja wa Uingereza, Harold Wilson alishawahi kusema, 'a week is a long time in politics'.
Kwa sasa siwezi kufahamu kama CHADEMA itakuwa weak au strong kwa sababu mgogoro bado hata haujakaribia kuisha. Kitu ninachokifahamu tu kwa sasa ni kwamba, ile nguvu yake ya kisiasa iliyokuwa inaongezeka kwa kasi imepungua kutokana na tafrani inayokikumba chama.
Imani ya chama katika mioyo ya jamii ndiyo msingi mkuu wa ushindi katika vyama vya siasa, na pale chama kinapoanza kupoteza imani katika mioyo ya jamii basi hilo huwa ni mwanzo wa anguko kisiasa.
Siamini kama huu mtifuano ndani ya CHADEMA ndiyo unajenga imani ndani ya jamii na kwa maana hiyo, nguvu zake zimepungua kw kiasi fulani.