Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep Quite!, Don't Ridicule Them!.

Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But,,,!, Be Calm!, Keep Quite!, Don't Ridicule Them!.

Wanabodi,

Kwanza nampongeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kwa ushindi wa kishindo mahakamani leo kwenye kesi dhidi ya Chadema!.

Tangu day one niliwaeleza humu kuwa maamuzi ya CC ya Chadema, ni maamuzi ya kipuuzi kabisa sijapata kuona!, niliuliza hiyo CC ilipata wapi mandate ya kumvua ZZK madaraka yake wakati haina uwezo huo?!. Kesi ya msingi nayo pia atashinda!, Chadema italazimishwa kumrejeshea vyeo vyake vyote, kisha ufuate utaratibu rasmi kumvua vyeo hivyo na hatimaye kumvua rasmi uanachama wake!.

Ushauri wangu wa bure kwa Zitto, nakuomba sana, be calm, keep quite, don't boast, don't ridicule Chadema!. Pia usiendelee kutoa siri nyingine zozote za viongozi wako zaidi ya zile ulizokwisha toa!.

Sijapenda jinsi ulivyo toa siri za M/Kiti wako alivyopokea mihela ya Rostam na Mkono!. Sijapenda 'ulivyonunua' lile gari la Mkono bila kueleza popote umelinunuaje na kwa nini ulinunue kwake!, na pia sijapenda jinsi 'unavyolikodisha' lile gari jingine, huku ukiendelea 'kulilipia bila matatizo' bla kueleza lolote!.

Nakushauri baada ya kushinda kesi hii ya pingamizi, pia utashinda ile kesi ya msingi, ila Baraza Kuu, litakuvua rasmi vyeo vyako vyote na litakuvua uanachama wako, ambapo nafahamu utarudi tena mahakamani kuweka pingamizi mpaka 2015!.

Kwa vile umeishajua mustakabali wako Chadema na kiukweli hatimaye utaondoka, sisi baadhi ya tunaokukubali, tunakuomba na kukusihi, usiendelee kuibomoa Chadema!. Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.

Narudia tena, hongera sana Zitto Zuberi Kabwe!.

Congratulations!.

Pasco.

Can u elaborate vizuri kuhusu huo ukanda + udini???
 
Pasco

Kwa nini hupendi ukweli kuhusu ufisadi katika vyama vya upinzani unapojidhihiri?

Unatetea usiri na mazingaombwe kwamba tuna upinzani safi wakati upinzani wenyewe uko ICU mguu mmoja kaburini?
 
Last edited by a moderator:
hakuna kitu kiliniumiza kama Lema kupokwa ubunge na mahakama ya Arusha. leo hii nimeumia kwa maumivu yale yale juu ya mbegu ya upandikizi na usaliti kupata haki mbele ya mahakama dhidi ya chama changu Chadema. hakika Zitto hatashinda. Kama kweli kabisa anafanya haya huku akijuwa anatumiwa na CCM kukivuruga chama. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu Zitto hatoshinda.

Muda utasema.
 
Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.

Congratulations!.

Pasco

Pasco, nilikuwa nakuheshimu sana bro, ila tabia ya kupandikiza hayo uliyoandika! Je tunajenga Taifa la aina gani
 
Attachments

  • 1389114996765.jpg
    1389114996765.jpg
    35.5 KB · Views: 145
Tusisahau, umeme juu,Gasi juu na subirini impact yake viwandani,Mashambani n.k ili tujifunze kusimama na kushabikia ya msingi.Huyo Zitto anakwenda kunywa mvinyo wake baada ya ushindi na Msando alafu waandamanaji watakutana na giza majumbani mwao baada ya luku kukata ghafla kutokana na kuweka umeme wa kuungaunga!

Watanzania haya yanafaa kuwa madogo na yale yanayogusa maisha yetu yawe makubwa! Gesi 65,000/= , Umeme unit 8 ni 10,000/= , maji hakuna wiki sasa alafu habari kama hizi ndio zinageuka BIG ISSUE!

Acha watukaange hadi tutie akili na ikibidi sembe kilo moja iwe laki na maharage hivyo hivyo!!!!!!!!!!:doh::doh::doh::doh::doh:

Mkuu wewe una busara sana, hii nchi ngumu sana, watetea wanyonge ndo huwa wanaundiwa zengwe! Daaa noma sana, natamani kuhama nchi!
 
Nakukubali sana zitto, nakubali harakati zako, najua unamapungufu ya kibinadamu lakini Wewe si mdhambi kuliko wote, haki ya mtu haipotei bure ,,komaa kaka

Sijapenda jinsi ulivyo toa siri za M/Kiti wako alivyopokea mihela ya Rostam na Mkono!. Sijapenda 'ulivyonunua' lile gari la Mkono bila kueleza popote umelinunuaje na kwa nini ulinunue kwake!, na pia sijapenda jinsi 'unavyolikodisha' lile gari jingine, huku ukiendelea 'kulilipia bila matatizo' bla kueleza lolote!.

Nakushauri baada ya kushinda kesi hii ya pingamizi, pia utashinda ile kesi ya msingi, ila Baraza Kuu, litakuvua rasmi vyeo vyako vyote na litakuvua uanachama wako, ambapo nafahamu utarudi tena mahakamani kuweka pingamizi mpaka 2015!.

Kwa vile umeishajua mustakabali wako Chadema na kiukweli hatimaye utaondoka, sisi baadhi ya tunaokukubali, tunakuomba na kukusihi, usiendelee kuibomoa Chadema!. Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.

Narudia tena, hongera sana Zitto Zuberi Kabwe!.

Congratulations!.

Pasco.[/QUOTE]
 
Zitto kwa mwanachadema yeyote linamaana kubwa sana, hasa katika mapinduzi ya chama, hoja zake za msingi zinawafanya msimpe nafasi katika muyapangayo na kuyajadili dhidi yake,hata mngebisha vipi ila ni kweli kuwa mnamwogopa zitto kama mngekuwa makini mngemvua madaraka kwa kufuata taratibu, unafikiri ni kwanini Mbowe alikuwa hapatani na zitto? huo ni wasiwasi usio na maana. Bomoeni chama mjenge nyama
 
Pasco wewe hata kama sio mwanasheria lakini umesomeshwa sheria!

Angalau unatakiwa kujua kuwa ushindi wa pingamizi sio ushindi wa kesi ya msingi.Kusema kuwa kushinda pingamizi automatically leads kushinda kesi ya msingi ni upotoshaji wa kiwango cha ushabiki!

Pia kusema kuwa kamati kuu(CC) ilikuwa haina mamlaka ya kumsimamisha Zitto nyadhifa zake ni kuendeleza upotoshaji uleule wa kiwango cha ushabiki.Anayekusoma anaweza aelewe kuwa pingamizi lilikuwa kupinga kuvuliwa nyadhifa zake wakati ukijua halikuwa hivyo.

Inajulikana unafanya hivyo kwa nia gani lakini basi usipotoshe ndugu yangu.We shangilia huo unaouita "ushindi wa kishindo" huku ukiendelea kusema yale ya kweli,usipotoshe.

Pia umeendelea kufanya udini,ukanda na ukabila kwamba kwa chadema hayo sio tatizo.Huyo unayempa ushauri alikuwa naibu katibu mkuu wa chama.Hatoki dini hiyo,kabila hilo wala kanda hiyo.
Unayempa ushauri amekuwa mwanachama tangu akiwa na umri wa miaka 16.Leo anamiaka 37.Amekaa kwenye chama cha kidini,kikabila na kikanda kwa miaka 21 sasa.Hili linawezekanaje?Acha kupotosha mkuu.Jikite kwenye kutuonyesha furaha yako ya pingamizi tu kama hauna mengine ya kweli ya kuisindikiza furaha yako.
 
Last edited by a moderator:
Ni upuuzi na kutojitambua kuendeleza tuhuma za udini, ukabila na ukanda dhidi ya cdm. Ukweli cdm imo miyoni mwa watanzania wengi. Wengi wanachukizwa na usaliti. Tungependa kuona kiongozi yeyote mwenye dhama ya uongozi cdm hawi msaliti.

Natunavyokaribia 2015 viongozi wote wale kiapo, kiapo cha kuhakikisha hanaerudishi nyuma juhudi za kuwang'oa wezi na mafisadi anadabishwa vijmkali. Sitegemei dola kurudishwa mikinoni mwa ccm(el, membe, makamba....). Makontena meno ya tembo yapo bandarini na mmiliki hajulikani? wauza unga hawajulikani na vjana wanaangamia! No!
 
Sarafu ya nusu laki imeishachongwa. Yaani unga utanunua kwa sarafu mbili tuu. Maisha bora kwa kila mdanganyika.
 
Huwezi Kumbomoa kwa njia za uonevu kiongozi aliyejitolea kwa moyo wake wote kukijenga chama halafu hicho chama kikabaki salama.

Tokea mwanzo watu tuliona wazi hili ni Jungu tu anapikiwa Zitto ili "Wenye Chama chao" waendelee kukiongoza chama kama kampuni yao ya mfukoni.

Kumfukuza Uanachama wanaweza, Lakini hii itaonyesha kwa Umma kwamba hiki si chama cha watu makini, kimejaa wababaishaji, wenye choyo, chuki na Husda.

yap, surely, kweli, true
 
Pamoja na zitto kuizuia kamati kuu kumjadili, haiondoi ukweli kwamba anakuwa mbunge wa mahakama..wanachama wote wanatambua kuwa zitto yuko nyuma ya ccm kukichafua chama na viongozi wake..mfano tuhuma za uongo zidi ya M-Kiti... na kibaya zaidi kwake CC imeshawazui wanachama kushilikiana na zitto... atabaki kuugwa mkono na maccm..
 
Wanabodi,

Kwanza nampongeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kwa ushindi wa kishindo mahakamani leo kwenye kesi dhidi ya Chadema!.

Tangu day one niliwaeleza humu kuwa maamuzi ya CC ya Chadema, ni maamuzi ya kipuuzi kabisa sijapata kuona!, niliuliza hiyo CC ilipata wapi mandate ya kumvua ZZK madaraka yake wakati haina uwezo huo?!. Kesi ya msingi nayo pia atashinda!, Chadema italazimishwa kumrejeshea vyeo vyake vyote, kisha ufuate utaratibu rasmi kumvua vyeo hivyo na hatimaye kumvua rasmi uanachama wake!.

Ushauri wangu wa bure kwa Zitto, nakuomba sana, be calm, keep quite, don't boast, don't ridicule Chadema!. Pia usiendelee kutoa siri nyingine zozote za viongozi wako zaidi ya zile ulizokwisha toa!.

Sijapenda jinsi ulivyo toa siri za M/Kiti wako alivyopokea mihela ya Rostam na Mkono!. Sijapenda 'ulivyonunua' lile gari la Mkono bila kueleza popote umelinunuaje na kwa nini ulinunue kwake!, na pia sijapenda jinsi 'unavyolikodisha' lile gari jingine, huku ukiendelea 'kulilipia bila matatizo' bla kueleza lolote!.

Nakushauri baada ya kushinda kesi hii ya pingamizi, pia utashinda ile kesi ya msingi, ila Baraza Kuu, litakuvua rasmi vyeo vyako vyote na litakuvua uanachama wako, ambapo nafahamu utarudi tena mahakamani kuweka pingamizi mpaka 2015!.

Kwa vile umeishajua mustakabali wako Chadema na kiukweli hatimaye utaondoka, sisi baadhi ya tunaokukubali, tunakuomba na kukusihi, usiendelee kuibomoa Chadema!. Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.

Narudia tena, hongera sana Zitto Zuberi Kabwe!.

Congratulations!.

Pasco.
Natamani kuona siku moja watanzania wakinena kile wanachokiamini,wakifanya kile wanachokiamini na kushudia kile wanachokiamini toka mioyoni mwao na si kuendeleza unafiki na nidhamu ya woga.Ni vigumu sana masikini(wa kipato na Kichwani) kuwa mtu huru na kufanya/kusema yale anayoyaamini kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano
 
Back
Top Bottom