Wanabodi,
Kwanza nampongeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kwa ushindi wa kishindo mahakamani leo kwenye kesi dhidi ya Chadema!.
Tangu day one niliwaeleza humu kuwa maamuzi ya CC ya Chadema, ni maamuzi ya kipuuzi kabisa sijapata kuona!, niliuliza hiyo CC ilipata wapi mandate ya kumvua ZZK madaraka yake wakati haina uwezo huo?!. Kesi ya msingi nayo pia atashinda!, Chadema italazimishwa kumrejeshea vyeo vyake vyote, kisha ufuate utaratibu rasmi kumvua vyeo hivyo na hatimaye kumvua rasmi uanachama wake!.
Ushauri wangu wa bure kwa Zitto, nakuomba sana, be calm, keep quite, don't boast, don't ridicule Chadema!. Pia usiendelee kutoa siri nyingine zozote za viongozi wako zaidi ya zile ulizokwisha toa!.
Sijapenda jinsi ulivyo toa siri za M/Kiti wako alivyopokea mihela ya Rostam na Mkono!. Sijapenda 'ulivyonunua' lile gari la Mkono bila kueleza popote umelinunuaje na kwa nini ulinunue kwake!, na pia sijapenda jinsi 'unavyolikodisha' lile gari jingine, huku ukiendelea 'kulilipia bila matatizo' bla kueleza lolote!.
Mkuu, kwanza nashangaa kwa nini unatumia neno "Sijependa", Kwani wewe ni Zitto? Au unataka kutuambia kwamba wewe ndo mshauri mkuu wa Zitto afanye nini wakati gani? Pia unataka kutuambia kwamba dili zote anazopiga Zitto na wewe huwa unashiriki lakini hizi na mkono hakukushirikisha? Lastly, kwa hayo ambayo hujapenda tena ya Kifisadi kabisa na yanaelezea kwa namna zote Unafiki, uongo, ulaghai, Usaliti na Ulimbukeni wa zitto siyo tu kwa chama alichomo (kwa amri ya mahakama) na kwa wanachama wake bali pia kwa watanzania wote (Anadanganya hataki posho kumbe anapiga dili kubwa kubwa yeye na Mbowe - They are all the same) bado unamgrade Zitto kama mwanasiasa anaefaa mbele ya jamii pana ya watanzania?
Nakushauri baada ya kushinda kesi hii ya pingamizi, pia utashinda ile kesi ya msingi, ila Baraza Kuu, litakuvua rasmi vyeo vyako vyote na litakuvua uanachama wako, ambapo nafahamu utarudi tena mahakamani kuweka pingamizi mpaka 2015!.
Logics zako kama marehemu vile, wewe huyuhuyu unasema asiibomoe CHADEMA, lakini pia unasema lazima baraza kuu litamfukuza na kumvua kila kitu, pia unasema ataweka pingamizi hadi 2015 why na kwa manufaa ya nani? This is too narrow. Mnataka kumuua huyu kijana.
Kwa vile umeishajua mustakabali wako Chadema na kiukweli hatimaye utaondoka, sisi baadhi ya tunaokukubali, tunakuomba na kukusihi, usiendelee kuibomoa Chadema!. Chadema ina wenyewe ambao udini kwao sio tatizo, ukabila kwao sio tatizo wala ukanda kwao sio tatizo!, pigania haki yako, ili uondoke Chadema kwa heshima bila kunyea kambi!.
Unaweza kuthibitisha udini, ukabila, ukanda n.k wa CHADEMA? I would be happy utufahamishe au unionyeshe mahala popote, forms au kitu chochote kinachoonyesha kwamba ukitaka kujiunga CHADEMA lazima ujaze form na uwe approved unatoka ukanda,dini na kabila gani? This is also extreme pathetic for you to denounce them publicly like you did in this awkward post.
NB: Kukaa kimya kama ulivyomshauri Zitto wakati mwingine ni jibu. Wewe hukutakiwa kuandika haya. Yamekuacha uchi kuhusu weledi na nia yako kwa taifa hili na watanzania maskini.
NArudia tena, hongera sana Zitto Zuberi Kabwe!.
Congratulations!.
Pasco