MZIMU
JF-Expert Member
- Apr 29, 2011
- 4,058
- 1,377
Nimekubali matusi yote sheikh.....Ila ungejibu hoja,ni surat gani kwenye quran inayohalalisha mahakama ya kadhi? au wapi mwamedi kaizungumzia mahakama ya kadhi iundwe na serikali?.... Jifunzeni uislamu wadogo zangu.
Dogo,nipe surat kwenye quran inayozungungumzia mahakama ya kadhi usizugezuge....kama haujui sema wanazuoni tukufundishe.
Matumbo hata tukikupa Sura na Aya, utaelewa au utaendelea kutusumbua. Mahakama za Kadhi ni kwa Mujibu wa Qur-an. Hapa nakuwekea baadhi ya Sura na Aya kama ifuatavyo.
......... Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu." (Qur-aan, 4:58)
...Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda wanaohukumu kwa haki. (Qur-aan, 49:9)
...Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na ucha Mungu... (Qur-aan, 5:8)
Matumbo hili ni somo refu watu wana Degree za Islamic Sharia. Hapa nakuweka sawa kidogo tu.