Ninaposema Waislam ni wote siseme kundi fulani au wewe ulitaka niseme Waislam wa namna gani? Hebu nifundishe basi?unapotaja "waislam" uwe una specify, waislam wa dhehebu lipi? vilevile hakuna aliyewazuia waislam kuanzisha mahakama ya kadhi, hata serikali imewaruhusu ila imetaka watumie garama zao kwasababu hii ni mahakama ya kidini ambayo ni part of ibada kwenu ninyi, hivyo hamuwezi kuweka kipengele cha ibada kwenye katiba ya umma (katiba inayojumuisha waisilamu na pia wapagani na wakristo makafiri wasioamini uislam). kodi za wakristo na wapagani hazitakiwi kutumika kuendesha ibada yenu ya mahakama ya kadhi, huo utakuwa upendeleo kwa dini yenu. kwanini suala ambalo ni la imani ya mtu liwekwe kwenye katiba ya umma inayojumuisha waislam na watu wengine?how special are you among the many other Tanzanians? ninyi ni nani haswa hata katiba iwapendelee peke yenu, mbona mambo ya kikristo hayajaingizwa mle kwenye katiba, na je, mnataka tuamini kuwa uwezo wenu kifedha au kuendesha dini yenu ni mdogo hamuwezi kitu hadi kutegemea kodi zinazojumuisha wauza nguruwe na pombe ili muendeshe ibada yenu ya mahakama ya kadhi?(mmetuamia kuwa kadhi haikwepeki kwasababu ni haki ya kuabudu kwenu na kuendesha mahakama hiyo ni mojawapo ya ibada ya kiislam.).
mbona kuna waislam wenzenu wanapinga hili suala, ninyi mnaong'angania ni waislam special sana ehee, halafu UISLAM NI NDOA MIRATHI NA TALAKA TU? ukitaka kupractice uislam hapa tz utakuwa umetimilizwa kwa ndoa mirathi na talaka peke yake? masuala mengine yaliyoandikwa kwenye vitabu vyenu mtayaacha? akizini mtamwacha akahukumiwe na kafiri, akiiba aende kuhukumiwa na kafiri etc, halafu, hivi mahakimu na majaji wote Tanzania ni wakristo ehee?
hizo jumuiya kama zitakuwa hazitambuliwi kisheria zitakuwa hazina maana.huwezi kuunda jumuiya inayo towa taraka kwa waislam pindi wakiachana kisha ukienda mahakamani unaambiwa taraka hiyo batili.
mahakama ya kadhi haiwahusu nyinyi wakristo,tunahusika sisi waislam.
Sheria ya mirathi kwa waislamu mtoto wa asie zaliwa ndani ya ndoa haruhusiwi kurisi mali ya marehem.je mahakama za serikali inalitambuwa hilo?
Wakristo kwanini mnapinga mahakama ya kadhi wakati haiwahusu?tukisema mna husda nyinyi wakristo mtabisha?
Naomba nijifunze kutoka kwako mkuu.Walioweka Suala la Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba ni Serikali ya CCM ndio wa
kulaumiwa Sio wa kulaumiwa Waislam. Waislam wameomba kuwa na Mahakama yao ya kadhi na hiyo Mahakama ya kadhi kazi yake ni mambo ya
ndoa, talaka na mambo ya mirathi. Waislam wanacho kitabu chao Quran amabacho hakibadilishwi na mtu yoyote tangu alipo kiacha
Mtume Muhammad S.A.W. sasa ni wajibu kukifuata kitabu chao wao wafuasi wa Dini ya Kiislam Serikali haiwahusu sasa Serikali ndio imeamuwa
kuweka Suala la Mahakama ya kadhi ndani ya katiba yao ambayo kila baada ya miaka Katiba inarekekbishwa wakati Kitabu cha Waislam
Quran ndani yake kuna Sheria za Mwenyeezi Mungu hazibadilishwi kamwe. Tuwaachie Waislam na Mahakama yao ya Kadhi.
Mambo ya Ngoswe Muachie Ngoswe Mwenyewe.
Dhehebu kubwa hapo Tanzania la Waislam ni lipi? Ninakuuliza wewe? ukisha nijibu hapo ndio hao wanaotaka Mahakama ya Kadhi.Naomba nijifunze kutoka kwako mkuu.
Tunafahamu kwamba hakuna maelewano mazuri kati baina Tanaka mbili zaislam hapa tz yaani Suni na Shia, sasa Je tutahitaji mahakama ya kadhi ya washia na mahakama ya kadhi ya wasuni?
Vipi tutahitaji magereza za waislam?
Samahani naomba nisikukwaze lengo nikujifunza mkuu.
Kama haiwahusu Wakristu, kwa nini mnataka uendeshaji wake ugharamiwe na serikali ambayo ina kila aina ya wananchi wenye kuamini dini na wasio amini?Wakristo kwanini mnapinga mahakama ya kadhi wakati haiwahusu?tukisema mna husda nyinyi wakristo mtabisha?
Wewe ndugu Idimi Msikilize Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere anavyosema .Kama haiwahusu Wakristu, kwa nini mnataka uendeshaji wake ugharamiwe na serikali ambayo ina kila aina ya wananchi wenye kuamini dini na wasio amini?
Kabla yakuja Waarabu Waafrika wote walizaliwa nje ya ndoa. Kanusha kama umesoma.
Kitu ambacho mimi sielewi ni kwanini hawa makafiri huwa wanaoongelea hii kitu?
Kwani inawahusu nini? Je wameambiwa ipo siku watashtakiwa humu?
Watuache bwana..wakiona nawao dini yao inahitaji mahakama basi waombe nawala sio kujifanya ni wasemaji wa dini nyingine....kila kukicha wakianzisha mada ni hii hii tu...Badilikeni bwana mnakera!
Kama haiwahusu Wakristu, kwa nini mnataka uendeshaji wake ugharamiwe na serikali ambayo ina kila aina ya wananchi wenye kuamini dini na wasio amini?
Muulize huyo Idimi kaleta Topic ya Ukristo ndani ya Thread ya Mahakam ya kadhi imehusu nini hapo? Kwani suala la Mahakam ya Kadhi Wakristo linawahus kitu gani? Kwani Serikali ya Tanzania inafuata Dini gani?Napenda kujua jambo moja, "wosia" wa marehemu unatambulika vipi katika suala hili la mirathi? Je mtu hana kauli juu ya kugawa mali zake kwa mtu yeyote amtakaye? Wakati wa kufanya zinaa hamuoni kama wakosaji ni wazazi na si mtoto anayezalwa? Kosa la motto ni lipi hata asipate sehemu katika mali za wazazi waliomleta duniani? Haki ya Mungu iko wapi hapa?
Napenda kujua jambo moja, "wosia" wa marehemu unatambulika vipi katika suala hili la mirathi? Je mtu hana kauli juu ya kugawa mali zake kwa mtu yeyote amtakaye? Wakati wa kufanya zinaa hamuoni kama wakosaji ni wazazi na si mtoto anayezalwa? Kosa la motto ni lipi hata asipate sehemu katika mali za wazazi waliomleta duniani? Haki ya Mungu iko wapi hapa?
Nikiwa kama muislamu naunga mkono mahakama ya kadhi iwepo kwa mujibu wa sheria. Lakini suala la kuiendesha kwa kodi ya jumla ndio siungi mkono, naona itapelekea kuendeshwa na pesa chafu za wauza pombe na nguruwe.
Mimi mawazo yangu ni kuunda kitengo maalumu ndani ya TRA ambacho kazi yake itakuwa kukusanya kodi ya kuendeshea mahakama ya kadhi tu. Kitengo hiki kiwe na kitu kama fomu hivi ambayo walipa kodi wakiislamu wenye TIN wata declare kwa hiyari yao kuongezewa percent ndogo kwenye kodi wanazolipa kuendeshea mahakama ya kadhi. Naamini waislamu ni walipa kodi wazuri na wanaipenda dini yao, hawawezi kupinga utaratibu kama huu.
kweli mdau kapotosha, lakini hilo la kusema eti uislamu umependelea mwanamke? hapo hapana, nchi za kiislamu zipo kibao Saudi, Iran, Iraq, Afghanistan, pakistani, somalia, northern nigeria etc, tunaona jinsi wanawake wanavyopendelewa huko ambako serikali inafuata FULL SHARIA not just KADHI COURTS!