Ushauri wa bure kwa Waislam

Ushauri wa bure kwa Waislam

Status
Not open for further replies.
KHIDMAT DWAAT LISIAMIYAT CENTRE REGISTERED TRUSTEES
P. O. BOX 16106, MOB. 0713-290272, 0784-403020.

1. Uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi utaleta madahara makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile Wakristo hawagawanyiki katika suala la kuipinga, lakini sisi Waislamu tunagawanyika katika suala hilo. Kwa taarifa yako napenda nikuhakikishie kuwa Waislamu wa Madhehebu ya AnsarSunna HAWAIKUBALI Mahakama hiyo kwa vile wanaelewa kuwa itakuwa chini ya BAKWATA.

2. Pia wanaelewa kuwa miongoni mwa mamlaka ya Kadhi ni kutangaza mwezi wa Ramadhani kufunga na kufungua na wao wanaye Amir wao ambaye hutangaza mwezi kwa kufuata mwezi unaoandama Saudia (Saud Arabia). Kwa maana hiyo katika nchi yenye Kadhi kutokea mtu mwingine nje ya Kadhi kutangaza mwezi ni kosa la jinai.

3. Kitu ambacho kitaleta madhara makubwa kuliko mafanikio ingawa AnsarSunna ni kundi dogo lakini wanaburuza kundi kubwa sana la Waislamu, kuliko Taasisi yoyote ya Kiislamu hapa Tanzania kwa vile ushawishi wao ni mkubwa sana katika jamii ya Kiislamu.

4. ANSAR SUNNA ndio wanaoendesha Shuura ya Maimam, GAZETI LA AN-NUUR, AL-HUDA, NASAHA na RADIO IMANI. Pia wana ushawishi mkubwa TIMES FM. Je, BAKWATA wana uwezo wa kupambana na vyombo hivyo?

5. Je, Serikali inaweza kukabidhi Mahakama ya Kadhi kwa wanaharakati wa Kiislamu? Nina hakika haiwezi kufanya jambo hilo na kama haitofanya hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kupata hasara zifuatazo:
(a) Wakristo wote wanaweza kujitoa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga katika chama cha CHADEMA ambacho hakina Mahakama ya Kadhi katika Ilani yake.
(b) Waislamu wote walioko chini ya Shuura ya Maimamu ambayo ni Mpinzani Mkuu wa BAKWATA wataendelea kuipinga Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuikumbatia BAKWATA na huku wakiendelea kuiunga mkono CUF, hivyo CCM itajikuta imebakia na Waislamu wanaoiunga mkono BAKWATA tu. Suala la wanaharakati kuipinga Mahakama ya Kadhi ni jambo rahisi sana kwa vile Mahakama ya Kadhi sio madai yao ya msingi.

6. Waislamu (wanaharakati) dai lao la msingi ni MGAWANYO SAWA WA MADARAKA. Hivyo Serikali inapounda Wizara, wao hutizama Baraza la Mawaziri, WAISLAMU NI WANGAPI NA WAKRISTO NI WANGAPI NDIO MAANA WANAIUNGA MKONO CUF, KWA VILE CUF IMEELEWA TATIZO LAO NA WAO WAKAJA NA KAULIMBIU YA HAKI SAWA KWA WOTE, yaani kwa Wakristo na Waislamu, wala Ilani ya Uchaguzi ya CUF haisemi lolote kuhusu Mahakama ya Kadhi WALA HAITOSEMA!!

7. Pia Waislamu wanaharakati wanaelewa kuwa Mahakama ya Kadhi haina manufaa yoyote kwa Waislamu, kwa vile Zanzibar ipo na WAISLAMU WA ZANZIBAR HAWANA MAENDELEO YOYOTE KUWAPITA WALE WA BARA, NA UISLAMU SI NDOA NA MIRATHI TU WALA MUNGU HASEMI "SOMETHING IS BETTER THAN NOTHING." Huu ni msemo wa Wazungu.

8. Mwenyezi Mungu anasema: INGIENI KATIKA UISLAMU WOTE NA MSIFE BALI MMEKUWA WAISLAMU KAMILI (Surat Baqarah ya 2 aya ya 208). Kwa hiyo mimi nikiwa kama Mwislamu nashauri kuwa Mahakama hiyo ISIWEPO kwani haitakuwa na manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na italeta mgawanyiko miongoni mwa wanachama wako, chukulia mfano Zanzibar, Mufti na Kadhi wanavyopingwa na wanauamsho ambao wanaongozwa na Sheikh Farid hali wanauamsho ndio Shura ya Maimam na Shuura ya Maimam ndiyo Uamsho.

KWANINI MASHEIKH WA BAKWATA WANAITAKA?
9. Wanaelewa wanachokifanya, wao wanajua fika kuwa Serikali itakapoanzisha Mahakama ya Kadhi watakuwa wamepata AJIRA, kwa hiyo wao wanapigania maslahi yao tu, hawawezi kuangalia madhara yatakayokikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huku wakijua kuwa ushawishi wao ni mdogo katika Jamii ya Kiislamu na hawana hata Miundumbinu ya kuwashawishi Waislamu wote waweze kumkubali Mufti, na hali ya Mufti ameshaweka wazi milango kwa Taasisi zote za Kiislamu na Waislamu waje washirikiane naye.

10. Masheikhe hawa wanaelewa kuwa hakuna Hakimu anayehukumu makosa mawili tu, yaani NDOA na MIRATHI, ukiletewa mzinifu huruhusiwi kumhukumu, ukiletewa mwizi huruhusiwi, nk. lakini wanang'ang'ania hivyo hivyo kwa ajili ya mishahara tu na hiyo ni hatari.

11. Hujaribu kutoa hata mifano ya Serikali ya Uingereza kwamba mwaka 1920 iliweka Mahakama hizo, ukweli ni kwamba Serikali ya Uingereza haikuweka Mahakama za Kadhi tu bali za Maakida na Maliwali, lakini pia sababu ya kuziweka Mahakama hizo siyo kwa ajili ya kuutunza Uislamu au uliwali bali ilikuwa ni mbinu ya kuwatuliza Viongozi hao ili waweze kuwatawala bila vurugu kwani mkoloni aligundua kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii kwa hiyo ile ilikuwa ni mbinu ya kiutawala ili Masheikhe, Maliwali na Maakida wajione kuwa na wao ni sehemu ya Serikali ya Muingereza, kumbe ni watawaliwa, hivyo bado hoja hiyo haina msingi wowote wala haina maana kwamba Serikali ya Mkoloni ilikuwa nzuri kwa Waislamu kuliko hii ya CCM, na huku tukiambiwa kuwa Waislamu ndiyo walioanzisha harakati za kudai Uhuru, kama walikuwa wazuri kwa nini tuliwaondoa.

12. CCM inayo mambo mengi ya kujivunia kwa Waislamu kama vile kuwapatia Chuo Kikuu, na hilo ni jambo muhimu na la msingi kwa maendeleo ya Uislamu na Waislamu, kwa hiyo JAMBO HILO LA MAHAKAMA YA KADHI mnapaswa kuliangalia kwa umakini ijapokuwa limo ndani ya Ilani yenu. Lakini si kila jambo lililomo ndani ya Ilani litekelezwe, mengine yanaweza kushindikana kwa matatizo mbalimbali na hili ni tatizo kubwa KWANI LINAWEZA KUZAA MGOGORO WA KIDINI!!

WAKRISTO WANA HAKI YA KUPINGA MAHAKAMA YA KADHI
13. Sehemu kama Zanzibar ni rahisi kuweka Mahakama ya Kadhi kwa vile Waislamu kule ni asilimia 99.99 hali kama hiyo Wakristo kule ni kama hawapo wamemezwa kwa uchache wao. Lakini BARA NI PAGUMU kwa vile HUENDA WAKRISTO NI WENGI KULIKO WAISLAMU. KWA VILE WAISLAMU KWA UHAKIKA HUPATIKANA MIKOA ISIYOZIDI SITA AMBAYO NI DAR ES SALAAM, LINDI, TANGA, MTWARA, KIGOMA NA TABORA, pia katika mikoa hiyo siyo Wilaya zote, kwa mfano Mkoa wa Kigoma ni Ujiji na Kigoma Mjini tu.

14. Pamoja na hayo Masheikhe wa BAKWATA wanaoshikilia suala la kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi bado hawajafahamu nini tatizo la Wakristo, hata hawakubali kuwepo kwa Mahakama hiyo, siyo kweli kabisa kwamba Wakristo hudhani Mahakama hizo zitawahukumu wao, la hasha na Masheikhe hutumia muda mwingi kuwaelimisha juu ya hilo, wakati hilo sio tatizo lao, na ni udhaifu wa kutokujua madai au matatizo ya mpinzani wako, ni nini tatizo la Wakristo ni hili:
(a) Mkumbuke kwamba mwaka 1993 hapa Tanzania kulikuwa na mgogoro wa bucha za nguruwe, mgogoro huo ulizaa harakati kubwa za Waislamu ambazo makao yake makuu yalikuwa msikiti wa Mtoro na kiongozi mkuu alikuwa marehemu Kasim bin Juma. Waislamu walipinga kuwepo Ubalozi wa Vatican hapa Tanzania na bado wanaendelea na msimamo huo hadi leo, wakati ubalozi huo hauendeshwi kwa Fedha za walipa kodi wa Tanzania bali ni Vatican yenyewe. JE, ITAKUWAJE LEO WAKRISTO WAKUBALI ZIWEPO MAHAKAMA AMBAZO ZITATOA AJIRA KWA WAISLAMU, KUANZIA MTAA, KATA, TARAFA, WILAYA, MKOA HADI TAIFA, TENA KWA FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA WAKIWAMO NA WAO WAKRISTO? Hilo ndilo tatizo lao na hapo ndipo BAKWATA wanatakiwa wapatolee maelezo.
(b) Kwamba, mabilioni ya Watanzania yatakayowalipa Masheikhe kila mwezi nao wao watanufaikaje? Huo ndio mgogoro uliotengenezwa na Ilani yenu na ambao unaweza kuwagharimu katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 ENDAPO WAKRISTO WAKIIGA MFANO WA WAISLAMU WA MSIKITI WA MTORO walipoamua kukusanya Kadi za CCM mwaka 1993 ingawa jaribio hilo lilizimwa na Viongozi wa CCM.

HOJA ZA SHEIKH BASALEH
15. Sheikh Ali Basaleh ndiye ambaye amelielewa tatizo la Maaskofu ingawa ametoa mfano mzuri wa kuwatuliza katika kipeperushi chake cha Wito cha tarehe18/08/2006. Ijumaa kuwa kama mtu ana watoto wawili mmoja anakula sana na mwingine hali sana, Je, baba atamzuia yule anayekula sana ili alingane na yule asiyekula sana? Mfano wake ni mzuri lakini haufanani na tatizo lililopo kwani fedha za baba hazichangiwi na watoto wake, bali baba huzitafuta yeye mwenyewe kwa nguvu zake, LAKINI FEDHA ZA BABA SERIKALI ZINATOKANA NA KODI YA WAISLAMU NA WAKRISTO, HIVYO SERIKALI HAIPASWI KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA DINI MOJA LAZIMA ITALETA MGOGORO NA NDIYO MAANA SISI WAISLAMU TUMEKUWA TUKIDAI HAKI SAWA!

16. Katibu Mkuu ni matumaini yangu kuwa hekima itatumika katika kulitatua tatizo hilo kwani ni rahisi kuziba ufa kuliko gharama za kujenga ukuta mwisho nakutakia kazi njema pamoja na afya njema.

WABILAH TAUFIQ,
ASANTE.
USTADH A. S. MKAMBAKU,
KATIBU MKUU.
 
Umeongea vizuri sana, na hapa ndiyo root causes ya tatizo lenyewe. Kwamba mahakama ya kadhi ni kwaajili ya waislamu tu. Kwamba wakiristu haiwahusu kabisa.

Sasa kama ni hivyo kwanini basi wakiristu na watu wengine wasiohusika na mahakama ya kadhi wagharamikie kuiendesha hiyo mahakama ambayo haiwahusu kabisa.

Mimi sina tatizo kama katiba itatambua uwepo wa mahakama ya kadhi. Lakini uendeshwaji wake na gharama zake uwe ni juu ya waislamu wenyewe.

Mpaka leo tunasikia malalamiko kutoka kwa waislamu wengi kwamba serikali iliwaundia BAKWATA. Kwanini tena leo mnataka serikali hiyo hiyo uwaundie MAHAKAMA YA KADHI?!

Hapa ndio kunapoleta mashaka makubwa

kod tunalipa wote
 
Mimi ni Mkristo tena mwenye msimamo mkali. Mimi napenda mahakama ya kadhi iwepo na IENDESHWE kwa gharama za michango ya waislamu PEKE YAO kwa faida zifuatazo.

1. Ukatili na udhalilishaji wa binadamu utakuwa wazi kwa waislamu ambao hawajui sheria za mahakama hyo nikiwa na uhakika ni wengi.

2. Kutokana na namba 1 hapo juu, wanawake na watoto wataonewa na watu wa dini yao,na kwa dunia ya sasa hivi hakuna atakayekubali kuishi maisha ya kunyanyaswa kisa dini inayotembea na upanga kunyemelea mtu ili wamkate mikono angali anajua maisha ni mamoja hapa duniani,na zaidi akija kubatizwa atapokelewa na atajua Kweli na Kweli itamwokoa. Wana wa kike wenu wakikutana na wana wetu wa kiume wataolewa,na wetu wakiona hali ndio hyo kwenu,hawataolewa na nyie. Na maisha yataendelea,au vp.

3. Madhehebu makuu ya waislamu hapa Tz,wanapingana kuhusu kuwepo kwa mahakama hyo. (Rejea post zilizopita). Wale waislamu walio wachache na matajiri wanaipinga,wale walio wengi na hohehahe wanaililia. Mtafaruku huu ni mtamu sana kwa Wakristu. Kuwakumbusha tu,"vita vya panzi......"

Angalizo kwa waislamu ni kuwa warejee katiba ya nchi hii kuwa haina dini. Pili,wakristo hutatua mambo yao haswa ndoa huko huko makanisani mwao. Mbona hawajawahi kuomba kutambuliwa na katiba? Kwa nini? Ili nini na iweje? Michango yao makanisani na harambee inawatosha kufanya yao. Leo mnajisemea ndio wengi hapa Tz,changeni huko misikitini na endesheni harambee pia kwa mambo yenu. Ina maana nyie ni masikini sana kushindwa kufanya hayo angali mna wake wanne,michepuko na watoto wa nje ya ndoa? Kwa nn mnatafuta mbinu ya kuwaua hao watoto wa nje ya ndoa? Kwa nn mnanyemelea kodi za watanzania kuhalalisha unyanyasaji? Najua mashehe wengi ambao ni wazaliwa nje ya ndoa,wanazungumziaje hili suala?

Ukimwambia mtu mwenye akili timamu madai haya possibly atawaza waislamu hapa Tz wameendela mno,wamejenga vyuo vya kila namna,mashule makubwa, miradi nyeti, hospitals nk. na sasa wanataka kujenga research facilities kote nchini na wameona wakuze imani yao kwa hii mahakama.
Nina imani hakuna muislamu anayeweza kujibu kwa hoja zaidi ya kuniita kafiri. Na mimi kafiri nimesemaaa...KODI YANGU SIKUPI NG'O. Kanisemee
 
Hujanikwanza mkuu.
Umesema vema kwamba mambo yakiislam tuwaachie waislam wenyewe, hayatuhusu, sasa kwakuwa hayatuhusu watanzania wote, kwanini liwekwe kwenye katiba? Kwani mukianzisha hata leo tatizo nini, nani kawazuia, kunasababu gani za msingi zakuwekwa kwenye katiba?
Walioweka Suala la Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba ni Serikali ya CCM ndio wa

kulaumiwa Sio wa kulaumiwa Waislam. Waislam wameomba kuwa na Mahakama yao ya kadhi na hiyo Mahakama ya kadhi kazi yake ni mambo ya

ndoa, talaka na mambo ya mirathi. Waislam wanacho kitabu chao Quran amabacho hakibadilishwi na mtu yoyote tangu alipo kiacha

Mtume Muhammad S.A.W. sasa ni wajibu kukifuata kitabu chao wao wafuasi wa Dini ya Kiislam Serikali haiwahusu sasa Serikali ndio imeamuwa

kuweka Suala la Mahakama ya kadhi ndani ya katiba yao ambayo kila baada ya miaka Katiba inarekekbishwa wakati Kitabu cha Waislam

Quran ndani yake kuna Sheria za Mwenyeezi Mungu hazibadilishwi kamwe. Tuwaachie Waislam na Mahakama yao ya Kadhi.

Mambo ya Ngoswe Muachie Ngoswe Mwenyewe.
 
Waisilamu nchini wamekuwa wakiilamu serikali kwamba imewaundia chombo ambacho ni BAKWATA, na kwamba hawakitaki kwa kuwa hakijaundwa na waisilamu. Waisilamu hao hao wanaitaka serikali iwaanzishie chombo kinachoitwa Mahakama ya Kadhi. Sasa hapa naona kuna ujinga fulani. Unalalamika serikali kuwaingilia kwa kuanzisha BAKWATA, halafu unalalamika kwa nini serikali haiwaingilii kwa kuwaanzishia Kadhi. Waisilamu wawe wazi basi, wanapenda kuingiliwa au kutoingiliwa na serikali?

My take:
Kwa kuwa waisilamu wameshalalamika sana kwa suala la 'kuundiwa BAKWATA', naishauri serikali isijiingize kabisa kujaribu kuwasaidia tena, kwani watakuja kuilaumu tena na tena serikali kwa kuwaingilia. Waisilamu wajipange, waanzishe Mahakama ya Kadhi, waiendeshe wenyewe, wahukumiane wenyewe na hata hukumu zikiwa mbaya, walaumiane wenyewe
Mkuu sipendi kabisa kujadili mambo ya dini lakini inanilazimu kukujibu kutokana na wewe mwenyewe kutoelewa ama kutazama upande mmoja tu.

Ebu niwaulizeni, Ikiwa serikali itaamua kutumia sheria za secularism kwa wote, Je mtakubali sheria hiyo hiyo inamruhusu mwanamke wa kudai taraka mahakamani - Wwakatoliki wataikubali? maana itakuwa sheria kwa wote na tunalazimika kuifuata pasipo kujali imani za dini. Sasa hawa jamaa zetu wanaomba utaratibu wao ambao hautambuliwi na serikali, japo ktk ibada zao za kesi za madai ni lazima zipitie mahakama ya kadh,i kuna kosa gani kwa serikali hii kutambua maamuzi ya mahakama hiyo kama inavyotambua maamuzi ya kikanisa juu ya ndoa na migogoro ya unyumba baina ya waumini wake.

Tuna aina mbili ya sheria, secular na pia mila na tamaduni zinakubaliwa (cultural law) ambazo zinatokana na jamii yetu hivyo nyie mnaona taabu gani kuwaachia waislaam wafanye maamuzi yao na yatambuliwe na sio swala la wao kwamba wanaomba fedha za walipa kodi kuendesha mahakama zao bali mahaka hizi zitambuliwe kisheria ili isije sheria za secular zitumike ktk ndoa za Kiislaam.
 
Naona mnajiuliza na kujijibu wenyewe. Waisalamu wa JF wameamua kwa dis, maana hamana jipa, manaongelea mambo msio yajua badala ya Kuyauliza. Be prepared! Kizazi hiki cha Waislamu sio kile cha Mwalimu Nyerere alie wasaliti na Kuwaua hata Waasisi wa Muungano. Hakuna katiba Mpya Bila Mahakama ya Kadhi. Kama mmechoka kuishi na sisi kwa amani poa tu. Mkimwaga Mboga sis tuta Mwaga ugali.
hakuna cha kudiss wala nini! Ni wazi kuwa mmekosa cha kujibu kwa kuwa hoja mlizopewa zinajitosheleza na kujieleza, najua hali anayokuwa nayo mtu pale anapoujua ukweli ila kwa kiburi chake hataki kukubali huo ukweli, atabaki kung'aka na kuleta mikwara mbuzi! Akili yako ya kigaidi inakupa busara kwamba mtu akimwaga mboga wewe umwage ugali! ila kwa mwenye kufata imani yenye hekima ya kiungu, ukimwaga mboga yeye atakula ugali mkavu ambao utamfanya aishi hadi kesho akitazamia kudra za mwenyezi Mungu.
 
mahakama ya kadhi haiwahusu wakristo na tunachotaka waislam itambuliwe kwenye katiba kama zinavyotambuliwa mahakama zingine kama za ardhi,biashara,kazi nk pia kama taasisi na swala la kugharamia gharama ni jambo jingine na ni jukumu letu tutaju sisi pa kuzipata. lakini mbona nyinyi wakristo munapewa pesa kupitia mkataba wa MOU uliosainiwa na lowasa mwaka 1992 ?? sisi hatujapewa mkataba huo mpaka leo?
Umuhimu wa kutambuliwa kwa mahakama ya kadhi ni nyingi ila nitataja moja kwa kuwa leo kdhi kashateuliwa na muft kupiti bakwata laki hatambuliki
endapo kwa mfano imetokea kadhi ametoa hukumu kati ya JUMA na HASSAN kwamba mali hii ni ya JUMA kwa mujibu wa mafundisho.lakini HASSAN hataki kukabidhi utatumia njia gani kumlazimisha HASSAN kutoa mali kumpa JUMA wakati kadhi hatambuliki kisheria??
na mambo hayo yanatokea leo kesi nyingi zinazohusu kadhi zimepelekwa bakwata na hukumu inatoka lakini inakuwa tabu kutekelezeka
 
Ukiupenda chukua usipoupemda sepa.

Nawashsuri waislam kwakuwa mahakama ya kadhi ni ibada waunde jumuiya ndogondogo za waislam ambazo watafanya ibada zao huko na watashitakiana ndoa zao huko na watapeana talaka huko. Ndoa zitasuluhishwa na Waislam wenyewe. Hii itakuwa rahisi kwakuwa waislam wote ktk jumuiya zao watakuwa wanafahamiana. Hii waendeshe kama idara fulani ndani ya jamii zao na hili ni jambo dogo sana ambalo halina sababu za msingi kuliweka kwenye katiba. Ni kama vile wakrisito walivyounda jumuiya zao wala hawakuomba ziandikwe kwenye katiba kwasababu walijua ni ibada yao sio jambo lakitaifa na hivyo halihitaji kuandikwa kwenye katiba.

Kuhusu mirathi tunazo mahakama za serikali iliyochaguliwa na wananchi wote ambazo zinafanya vizuri na zinautaratibu mzuri wakusimamia mirathi hivyo mirathi ya waislam itashughulikiwa huko. Sioni hoja wala sababu yamsingi waislam kutaka mahakama yao special kwa ajili yamirathi wakati tayari kunamahakama inasimamia mirathi hivyo hakuna ulazima wakuandika kwenye katiba.

Karibuni tujadili kwa hoja, matusi njoo PM tutukanane mpaka nikukomeshe.

Kwani Msikitini huwa wanaenda kufanya nini? Kwanini wawe na sehemu mbili tofauti za ibada?

1. Who appoints Chief Kadhi and Kadhis?
2. What are the qualification for appointment to the office of a Kadhi (including a Chief Kadhi)?
3. Since the Kadhis are not trained lawyers who understand the Evidence Act and the Civil Procedure Act, how and/or what will they use to administer their Courts?
4. Muslims are mainly of two sects in Tanzania - the Sunni and Shia. Majority of the Muslims in Tanzania are Sunni Muslims but there is a significant population of Shia Muslims too and consideration ought to be given to the appointment of Kadhis of the Shia Sect to cater the interest of the Shia Muslims. Will they have two difference Courts? For Sunni and Shia?
5. How will Muslim Women be protected since: Muslim law regards women as less than men in matters of both marriage and divorce, as well as devolution of property: Holy Quran Surah 2:228-232, and Surah 65:1-7 (only a man may divorce his
wife even if he is required to provide for her); a man may beat his wife, even if lightly, the evidence of two women, is equal to evidence of one man (Surah 2:282). The application of such beliefs of faith are contrary to the Constitution.

Islamic "Kadhi" courts is illegal and discriminatory. The Kadhi court system will elevates Islam over the country's other religions, and should be deemed unconstitutional because it does not coincide with Tanzania's secular mandate and should not be included in the nation's new constitution.

MY CONCERNS
(a) There is no valid basis whatsoever for the inclusion of the Kadhis' Courts in the Constitution;

(b) If Muslims alone get preferential treatment for setting religious Courts, then other communities and faiths would come forward to have separate courts

(c) Provision such as Kadhis' Courts is normally covered under the general law. It should not be part of the main body of the Constitution,

(d) Due to different school of interpretation of the Holy Koran and Hadith which figh will the Kadhis' Courts follow? Will there be Kadhis' Court as per separate jurisdiction of Shias and Sunis? What would be the views of Ismaili or Bohra Communities on the issue?

(e) Even in Pakistan, no universal Islamic courts could be established due to confusion and conflicts between the figh Jaferia of Shias and the figh of Sunis

(f) Several sects of Muslims community do not follow Kadhis' Courts but have their own jurisprudence.

(g) The awards of the Kadhis' Courts are based on the sole discretion of the Kadhi. What view do the Muslim Women have on this system? Do the majority of the Muslim Women concerned get a fair trial in Kadhis' Courts? Are they convinced that their welfare and fundamental rights are protected at the hearings?

MY RECOMMENDATIONS
(1) All people should be given options to go to independent or higher courts. The High Court and Court of Appeal should be above religious courts, if such courts are part of the Constitutional provision either directly or indirectly;
(2) There should be an open door policy to change the laws which cannot be challenged,
(3) Courts should be authorized to employ scholars who would enlighten judges on the interpretation of religious doctrines;
(4) The draft recommends setting up Village Councils to deal with minor problems in rural areas, which can take care of local religious sentiments to protect national unity and religious harmony. Expand the role of Village Councils to deal with social disputes;

CC: Eiyer FaizaFoxy Lisa Valentine Mkuu wa chuo Gavana Buchanan MziziMkavu
 
Ishmael ...a special committee formed to advice the BMK on the matter will definitely benefit from your professional advice. Well said mkuu!
 
Last edited by a moderator:
IN THE MATTER OF THE KADHIS' COURT, OTHER COURTS
AND

IN THE MATTER OF CONSTITUTIONAL REVIEW
AND

IN THE MATTER OF ENFORCEMENT OF FUNDAMENTAL RIGHTS
AND FREEDOMS OF THE INDIVIDUAL UNDER SECTIONS OF THE CONSTITUTION OF TANZANIA

The Grounds of the Summons and Supporting Affidavits:

A. Tanzania is a multi-religious and multi-cultural state and the Constitution defends this position;
B. The separation of the state and religion must be respected and promoted but allowing Kadhi Courts in Tanzania's Constitution will contradicts this cardinal principle;
C. There is no valid basis whatsoever for the inclusion of the Kadhis' Courts in the Constitution;
D. The entire process of the Constitutional Review has been skewed, biased against Christians and other Tanzanians and bereft of any iota of Constitutionalism;

1. Who appoints Chief Kadhi and Kadhis?
2. What are the qualification for appointment to the office of a Kadhi (including a Chief Kadhi)?
3. Since the Kadhis are not trained lawyers who understand the Evidence Act and the Civil Procedure Act, how and/or what will they use to administer their Courts?
4. Muslims are mainly of two sects in Tanzania - the Sunni and Shia. Majority of the Muslims in Tanzania are Sunni Muslims but there is a significant population of Shia Muslims too and consideration ought to be given to the appointment of Kadhis of the Shia Sect to cater the interest of the Shia Muslims. Will they have two different Courts? For Sunni and Shia?
5. How will Muslim Women be protected since: Muslim law regards women as less than men in matters of both marriage and divorce, as well as devolution of property: Holy Quran Surah 2:228-232, and Surah 65:1-7 (only a man may divorce his wife even if he is required to provide for her); a man may beat his wife, even if lightly, the evidence of two women, is equal to evidence of one man (Surah 2:282). The application of such beliefs of faith are contrary to the Constitution.

Islamic "Kadhi" courtsis illegal and discriminatory. The Kadhi court system will elevates Islam over the country's other religions, and should be deemed unconstitutional because it does not coincide with Tanzania's secular mandate and should not be included in the nation's new constitution.

MY CONCERNS
(a) There is no valid basis whatsoever for the inclusion of the Kadhis' Courts in the Constitution;
(b) If Muslims alone get preferential treatment for setting religious Courts, then other communities and faiths would come forward to have separate courts
(c) Provision such as Kadhis' Courts is normally covered under the general law. It should not be part of the main body of the Constitution,
(d) Due to different school of interpretation of the Holy Koran and Hadith which figh will the Kadhis' Courts follow? Will there be Kadhis' Court as per separate jurisdiction of Shias and Sunis? What would be the views of Ismaili or Bohra Communities on the issue?
(e) Even in Pakistan, no universal Islamic courts could be established due to confusion and conflicts between the figh Jaferia of Shias and the figh of Sunis
(f) Several sects of Muslims community do not follow Kadhis' Courts but have their own jurisprudence.
(g) The awards of the Kadhis' Courts are based on the sole discretion of the Kadhi. What view do the Muslim Women have on this system? Do the majority of the Muslim Women concerned get a fair trial in Kadhis' Courts? Are they convinced that their welfare and fundamental rights are protected at the hearings?

MY RECOMMENDATIONS
(1) All people should be given options to go to independent or higher courts. The High Court and Court of Appeal should be above religious courts, if such courts are part of the Constitutional provision either directly or indirectly;
(2) There should be an open door policy to change the laws which cannot be challenged,
(3) Courts should be authorized to employ scholars who would enlighten judges on the interpretation of religious doctrines;
(4) The draft recommends setting up Village Councils to deal with minor problems in rural areas, which can take care of local religious sentiments to protect national unity and religious harmony. Expand the role of Village Councils to deal with social disputes;

Respectfully submitted,

August 24, 2014

CC: Eiyer FaizaFoxy Lisa Valentine Mkuu wa chuo Gavana Buchanan MziziMkavu
 
Well narrated Ishmael .

While appellate jurisdiction is mainly used to correct the errors that may be committed by trial Courts. Now in Kadhi Courts, what jurisdiction will they use in the event the Plaintiff or Defendant wants to appeal?
 
Last edited by a moderator:
Una jua thinking capacity yako very low umefika mwisho pole sana kwa kuzaliwa masikini
Toa sababu za msingi acha matusi. Tupo kujigunza na kuelimishana. Hakuna Surat yoyote kwenye Quran imeagiza mahakama ya kadhi iwekwe kwenye katiba. Kama ipo iweke hapa.
 
Walioweka Suala la Mahakama ya kadhi ndani ya Katiba ni Serikali ya CCM ndio wa

kulaumiwa Sio wa kulaumiwa Waislam. Waislam wameomba kuwa na Mahakama yao ya kadhi na hiyo Mahakama ya kadhi kazi yake ni mambo ya

ndoa, talaka na mambo ya mirathi. Waislam wanacho kitabu chao Quran amabacho hakibadilishwi na mtu yoyote tangu alipo kiacha

Mtume Muhammad S.A.W. sasa ni wajibu kukifuata kitabu chao wao wafuasi wa Dini ya Kiislam Serikali haiwahusu sasa Serikali ndio imeamuwa

kuweka Suala la Mahakama ya kadhi ndani ya katiba yao ambayo kila baada ya miaka Katiba inarekekbishwa wakati Kitabu cha Waislam

Quran ndani yake kuna Sheria za Mwenyeezi Mungu hazibadilishwi kamwe. Tuwaachie Waislam na Mahakama yao ya Kadhi.

Mambo ya Ngoswe Muachie Ngoswe Mwenyewe.
unapotaja "waislam" uwe una specify, waislam wa dhehebu lipi? vilevile hakuna aliyewazuia waislam kuanzisha mahakama ya kadhi, hata serikali imewaruhusu ila imetaka watumie garama zao kwasababu hii ni mahakama ya kidini ambayo ni part of ibada kwenu ninyi, hivyo hamuwezi kuweka kipengele cha ibada kwenye katiba ya umma (katiba inayojumuisha waisilamu na pia wapagani na wakristo makafiri wasioamini uislam). kodi za wakristo na wapagani hazitakiwi kutumika kuendesha ibada yenu ya mahakama ya kadhi, huo utakuwa upendeleo kwa dini yenu. kwanini suala ambalo ni la imani ya mtu liwekwe kwenye katiba ya umma inayojumuisha waislam na watu wengine?how special are you among the many other Tanzanians? ninyi ni nani haswa hata katiba iwapendelee peke yenu, mbona mambo ya kikristo hayajaingizwa mle kwenye katiba, na je, mnataka tuamini kuwa uwezo wenu kifedha au kuendesha dini yenu ni mdogo hamuwezi kitu hadi kutegemea kodi zinazojumuisha wauza nguruwe na pombe ili muendeshe ibada yenu ya mahakama ya kadhi?(mmetuamia kuwa kadhi haikwepeki kwasababu ni haki ya kuabudu kwenu na kuendesha mahakama hiyo ni mojawapo ya ibada ya kiislam.).

mbona kuna waislam wenzenu wanapinga hili suala, ninyi mnaong'angania ni waislam special sana ehee, halafu UISLAM NI NDOA MIRATHI NA TALAKA TU? ukitaka kupractice uislam hapa tz utakuwa umetimilizwa kwa ndoa mirathi na talaka peke yake? masuala mengine yaliyoandikwa kwenye vitabu vyenu mtayaacha? akizini mtamwacha akahukumiwe na kafiri, akiiba aende kuhukumiwa na kafiri etc, halafu, hivi mahakimu na majaji wote Tanzania ni wakristo ehee?
 
mahakama ya kadhi haiwahusu wakristo na tunachotaka waislam itambuliwe kwenye katiba kama zinavyotambuliwa mahakama zingine kama za ardhi,biashara,kazi nk pia kama taasisi na swala la kugharamia gharama ni jambo jingine na ni jukumu letu tutaju sisi pa kuzipata. lakini mbona nyinyi wakristo munapewa pesa kupitia mkataba wa MOU uliosainiwa na lowasa mwaka 1992 ?? sisi hatujapewa mkataba huo mpaka leo?
Umuhimu wa kutambuliwa kwa mahakama ya kadhi ni nyingi ila nitataja moja kwa kuwa leo kdhi kashateuliwa na muft kupiti bakwata laki hatambuliki
endapo kwa mfano imetokea kadhi ametoa hukumu kati ya JUMA na HASSAN kwamba mali hii ni ya JUMA kwa mujibu wa mafundisho.lakini HASSAN hataki kukabidhi utatumia njia gani kumlazimisha HASSAN kutoa mali kumpa JUMA wakati kadhi hatambuliki kisheria??
na mambo hayo yanatokea leo kesi nyingi zinazohusu kadhi zimepelekwa bakwata na hukumu inatoka lakini inakuwa tabu kutekelezeka

Kwani kisutu wameshindwa kumaliza kesi ya Juma na Hassan?
Kwanini musidai magereza munataka mahakama bila magereza?
Polisi wenu waendesha mashtaka watakuwa Boko haramu, Alqeda au Alshabab?
 
mahakama ya kadhi haiwahusu wakristo na tunachotaka waislam itambuliwe kwenye katiba kama zinavyotambuliwa mahakama zingine kama za ardhi,biashara,kazi nk pia kama taasisi na swala la kugharamia gharama ni jambo jingine na ni jukumu letu tutaju sisi pa kuzipata. lakini mbona nyinyi wakristo munapewa pesa kupitia mkataba wa MOU uliosainiwa na lowasa mwaka 1992 ?? sisi hatujapewa mkataba huo mpaka leo?
Umuhimu wa kutambuliwa kwa mahakama ya kadhi ni nyingi ila nitataja moja kwa kuwa leo kdhi kashateuliwa na muft kupiti bakwata laki hatambuliki
endapo kwa mfano imetokea kadhi ametoa hukumu kati ya JUMA na HASSAN kwamba mali hii ni ya JUMA kwa mujibu wa mafundisho.lakini HASSAN hataki kukabidhi utatumia njia gani kumlazimisha HASSAN kutoa mali kumpa JUMA wakati kadhi hatambuliki kisheria??
na mambo hayo yanatokea leo kesi nyingi zinazohusu kadhi zimepelekwa bakwata na hukumu inatoka lakini inakuwa tabu kutekelezeka
unaposema waislam tunataka, unawakilisha waislam wa dhehebu lipi? kuna madhehebu mengine ya waislam wanapinga hilo suala.sasa wewe unawakilisha waislam wepi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom