Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

hata akitumia miezi sita ya kumchora lowasa poa tu.maana yy hachori ili kumfurahisha mtu,anachora kufikisha ujumbe.
na nadhani ujumbe ume upata vilivyo

Arap sang yupo thehague anasota kwa mama bensouda
 
Kwahiyo mwigulu kukamatwa anatoa rushwa siyo habari,kabaka kukutwa na form 20000 za kupigia kura siyo habari,nape kuhojiwa na pccb kwa rushwa siyo habari,ndugai kumpiga mtu na kumjeruhi siyo habari,wasira kumpiga mtu siyo habari?wacheni kutufanya watu wote kuwa ni mazuzu kama nyinyi mlivyo mazuzu

Kwa hiyo wewe kwenye upande wa taswira kwa njia ya picha unamtegemea masoud tu?
 
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo

Kama magazeti yote vichwa vya habari ni Lowassa unataka wachira katuni wamchore nani,????
 
We jamaa vipi?

Kwa kuwa umeendika kuwa na wewe ni msanii then the only thing you can do ni kukomaa na hayo ambayo Kipanya hajihusishi nayo,kwani umekatazwa au lazima umsome yeye tu?

Kila mtu ana hadhira yake kama wewe yanakuchefua,fanya kupotezea tu maanake tayari una mbadala ambaye ni Said Michael.

Hata kama amelipwa ndo msimu wenyewe huu mkuu na wewe si msanii bhana,tafuta wa kukulipa siyo kulialia humu.
 
Na hili ndo tatizo la wafuasi wa Chadema ambao sasa nchi nzima saivi imeshuhudia mlivo misukule wa ajabu.
Kipanya ni mwandishi huru anayetoa habari zake kupitia katuni. Kuna haki zinalindwa na katiba ikiwemo uhuru wa kutoa habari, uhuru wa mawazo na kujieleza, Kipanya amesimama kwenye misingi hii bila kuvunja sheria yeyote ile, labda ninachokiona ni kuwa amewakamata kisawa sawa wafuasi wa Chadema na Lowassa kiasi ambacho mnashindwa mumzuie kivipi.
Kama mlishindwa kumuhonga ili achore katuni zinazowasifia kwa kula matapishi yenu basi kaeni mtulie sindano iwaingie vizuri.

Hongera sana Kipanya, Kusema kweli unaitendea haki tasnia hii ambayo kazi kubwa si tu kuhabarisha bali kuelimisha.

Namshauri Jakaya kabla hajamaliza muda wake atoe Nishani kwa wanamichezo,wanahabari na wasanii na katika hao Masoud Kipanya awepo.

Kipanya ni hazina katika taifa hili kwa upande wa tasnia ya habari na katuni.
 
wahariri huchagua ipi ya kuitoa ipi ya kuiacha
anchora zaidi ya moja kwa siku
 
Ha haa, hii kidogo inivunje mbavu, teh teeeh!
Mkuu usicheke, ni kawaida mwanadamu ana vipindi anavyopitia katika maisha. Kawaida ya sanaa hususan ya michoro humtambulisha mchoraji wake haiba na tabia yake.

Aidha kuwajibu waliosema mhariri huchagua mojawapo kati michoro mingi huyo hana anachojua kwani INGEKUA WAHARIRI WANAFANYA HIVYO HEADLINES ZA MAGAZETI ZISINGEKUWA NA MAKOSA. Hiyo imebaki nadharia na sifa ya jina MHARIRI. Hawana sifa hiyo tena wala ueajibikaji, ndio sababu unaweza kukuta miguu ya habari badala ya kichwa cha habari. Aidha kilichoandikwa hakifanani... bahati mbaya Tanzania tumeishiwa waandishi habari tumebaki na waandika habari.

Hakuna ubunifu wala weledi, na hili linatokana wanunuzi wenyewe wa magazeti...

TETESI ZINAUZA KULIKO HABARI HALISI!!!
UPUUZI UNANUNULIWA KULIKO ELIMU...

HII IKO TANZANIA TU!!!
 
Na hili ndo tatizo la wafuasi wa Chadema ambao sasa nchi nzima saivi imeshuhudia mlivo misukule wa ajabu.
Kipanya ni mwandishi huru anayetoa habari zake kupitia katuni. Kuna haki zinalindwa na katiba ikiwemo uhuru wa kutoa habari, uhuru wa mawazo na kujieleza, Kipanya amesimama kwenye misingi hii bila kuvunja sheria yeyote ile, labda ninachokiona ni kuwa amewakamata kisawa sawa wafuasi wa Chadema na Lowassa kiasi ambacho mnashindwa mumzuie kivipi.
Kama mlishindwa kumuhonga ili achore katuni zinazowasifia kwa kula matapishi yenu basi kaeni mtulie sindano iwaingie vizuri.

Hongera sana Kipanya, Kusema kweli unaitendea haki tasnia hii ambayo kazi kubwa si tu kuhabarisha bali kuelimisha.

Namshauri Jakaya kabla hajamaliza muda wake atoe Nishani kwa wanamichezo,wanahabari na wasanii na katika hao Masoud Kipanya awepo.

Kipanya ni hazina katika taifa hili kwa upande wa tasnia ya habari na katuni.

Tatizo sijui upo idara gani ya kazi kwahiyo kukulaumu nitakuwa nakuonea bure
 
Lowassa na Ukawa ndio wanaouza magazeti bila kusahau kitengo waliandaa bilioni 18 maalum kupambana ili kuidhoofisha ukawa kwa hiyo usishangae Masoud Kipanya anaweza kuwa ni mmoja wa waliopitiwa na mgao kama wale wahariri wa Raia Mwema!
huyu kapoteza mwelekeo bora Michael anapiga kote kote, au mapangara, huyu anaangukia upande mmoja.
 
Hajaanza nae leo;toka akiwa ccm kwenye mchakato Wa kumpata magufuli alikua anamchora na anaendelea nae akiwa chadema,team lowassa acheni kudeka,mmezoea kubebwa na magazeti ndio mkipata changamoto kidogo tu kwa waandishi waliokataa kuhongwa kama masudi na jenerali ulimwengu mnatoa povu
 
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo

Mfukutuzi hivi kwanini nyie hamkubali watu wawe na mawazo tofauti na nyie? Hebu kuweni kidogo na muache utoto. Masoud kama mtazania yeyote anahaki yakutoa mawazo yake. Kama hupendi cartoon zake ACHA KUSOMA magazeti yenye cartoon hizo. Hii ndio demokrasia kwenye ile 'de' ya chadema. Acheni kutufanya tuamini mnachoamini nyinyi.
 
Back
Top Bottom