Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Mkuu mimi matukio yote mawili yalinikuta eneo la tukio hasa lile la Olasiti walipotushambulia kwa bomu la kurushwa kwa mkono na risasi zilizotoka katika bastola na bunduki SMG na tulioumizwa na matukio hayo tupo wengi halafu zingatia mimi ni mwanachama wa kawaida tu cina cheo chochote Chadema ,sasa tukisema tuanze wote kudai kulipwa kwa yaliotokea nnadhani haitakuwa sahihi.Sote tunataka mabadiliko na dhana ile ile ya kuumia/kuumizwa /kuuwawa kwa baadhi ya wafuasi wa chama hichi ndio gharama za mabadiliko na hili la Lowasa kujiunga na upinzani Dkt Slaa akubaliane na mabadiliko hayo kwa sababu ukweli umejulikana na tunataka kusonga mbele sio kurudi nyuma.

Maneno yako ni ya kichochezi sana ,hayaachi umoja katika chama na yanatupeleka katika ubinafsi

Umenena mkuu.. Watatuelewa tu mda unavyoenda.
 
Mfukutuzi

attachment.php

vp na hizi katuni za King Kinya?
Ujumbe haujakupata tu
Lowassa na Mbowe wanaendelea na Vikao wakitudanganya Dr naye yupo nanyi CHADEMA
Masoud ni bingwa katika siasa naomba tuachie wenyewe tushereheke naye
 
Haka kajamaa nakajua vzr kanastyle za ki congo! hapo kakishatoa kanapiga sim kwa vigogo fulani ..." umesoma leo nimemchana jamaa...." then kanapewa mpunga!

Hata mimi nahisi hivyo
 
Kununua Gazeti la Raia mwema siku hizi ni kuharibu pesa. Siku hizi gazeti hilo haliandiki mambo ya msingi kama zamani. Linaelekea kupoteza mvuto kwa watu wengi.
 
Kununua Gazeti la Raia mwema siku hizi ni kuharibu pesa. Siku hizi gazeti hilo haliandiki mambo ya msingi kama zamani. Linaelekea kupoteza mvuto kwa watu wengi.

Umeona eeh, siku hizi magazeti ya udaku yameongezeka, pesa ni hatari sana
 
Ila nashukuru naona somo limemuingia vilivyo, kuanzia juzi naona kajirekebisha kidogo
 
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo

Mti wenye matunda siku zote ndo unaopgwa mawe
 
Lowasa ndo hot news kwa sasa wewe unataka achore tumbili ndo ufurahi...?? Kila jambo na wakati wake acha ushabiki mbuzi...
 
Mimi Naona Wewe Ndiyo Unahitaji Ushauri Wa Kina Kwa Kuwa Na Uelewa Mdogo Kuhusu Katuni Za Masoud Kipanya.
 
magufuli alikuwa anashambulia serikali almost kila siku.., na wewe ulietoa post ukaona sawa.., sasa week hii tu kuandika habari ya lowasa roho imekuuma tena katka katuni ulizotuma unaona moja hiyo ni kama anamponda magufuli kuwa anaomba aandikwe coz lowasa ana make headlines kwenye magazeti yote yeye anasahaulika.., hivi kila mtu atafanya kama unavyotaka wewe?? basi tafuta dunia yako uishi..., yaani mzee wetu MA SA BU LI aliona mbali.., kuna watu hamtumii ubongo muda wode kufikiri
 
Huyo jamaa nimemshusha thamani

Halafu Bahati Mbaya Sana Huyo Unayemshusha Thamani Humfikii KIAKILI, PESA, UMAARUFU Na UBUNIFU. Hebu Tuonyeshe Yaliyo Ndani Yako Ili Nasi TUKUPANDISHE Thamani. Sijaona Genius Cartoonist Tanzania Kama Masoud Kipanya. Uwezo Wa KUFIKIRI Wa Masoud Kipanya Ni Sawa Na Wanachama Wa CHADEMA 1200. Big Up Mno Kipanya Na Nakukubali KULIKOTUKUKA!
 
Hapana bhana KP yup right,why mnalaumu?anachokichora ndo kipo hot kwa sasa na kina ukweli,tumuache afanye kaz,hawez fanya kaz zake kwa kutufurahisha tuuuu,kuna siku atatukera,now katuni unaona zinakera

Hata huyu mleta mada ameleta katuni moja ya Magufuli halafu anasema kipanya anamchora EL tuuu.

Haeleweki
 
Masoud n i level ingine sio rahisi mtu wa akili ndogo amwelewe. Pamoja na kunichukulia demu wangu miaka 10 iliyopita namkubali sana kama kichwa cha sanaa. He Is a genius in that. Acha wivu.

Alivyokuchukulia NDITO Wako Hakukuchora Ulivyokuwa Unalia Na Msura Wako Huo Mbaya Utadhani Sokwe Anatoa Haja Kubwa?
 
Mbona kimekuuma sana?kwani lowasa ni nani wako?unavyolalamika mmmh......?
 
Back
Top Bottom