Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Mfukutuzi

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
239
175
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo
 

Attachments

  • 11694128_1624801841101091_4028444249333882041_n.jpg
    11694128_1624801841101091_4028444249333882041_n.jpg
    19.3 KB · Views: 17,200
  • 11754592_710416232398427_7222184485457784930_o.jpg
    11754592_710416232398427_7222184485457784930_o.jpg
    51.7 KB · Views: 8,617
Kweli Masud Kipanya anatumiwa na CCM kuiattack CDM. Wasira anashinda Bunda kwa UTYSON, Celina Kombani mpaka Kanisani anahubiriwa, Kabaka na Nyangwine wamebaka kura Musoma, Kipanya haoni. Be fair Masoud
 
Msanii hutakiwi kuonesha feelings zako upande gani, otherwise akaandikie Uhuru na Mzalendo ndo tutamwelewa! Zaidi ya hapo ni kujikosha tu, anafikiri kwamba kumponda Lowassa ndo atapata cha kupeleka kinywani. Asome na alama za nyakati na aangalie na Mtu anyemchafua bila sababu.
 
Huo ni wivu usio wa kimaendeleo sababu kakugusa unahaha kumpa ushauri leo
wasanii wako wengi na hao wote wamekua wakiandaa katuni zenye taswira tofauti kwa nyakati tofauti kulingana na jambo linaloonekana kuwa muhimu kwa wakati huo,

Suala la harakati za kisiasa hasa wakati huu ni suala linaloonekana kugusa karibu vyombo vyote vya habari na hivyo kuwafanya wasanii na wana habari kujikita katika jambo hili zito ili kuwapa habari na kukosoa pale inapobidi kutumia taaluma yao ukizingatia kuwa wakati huu ambapo vyama vinawatafuta wagombea wa nafasi mbali mbali katika ngazi tofauti hivyo ni haki yake Kiapanya kuandaa katuni zinazoendana na mambo hayo japo anaweza kuandaa zingine pia lkn kumbuka hawezi kidhi haja ya kila mmoja

Kwa hiyo mleta mada ulipaswa kuleta mada ya tatizo la umeme kwa namna unavyoliona na siyo kumponda kipanya kwa wivu wako usio na kichwa wala mkia
 
Back
Top Bottom