Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Mpaka Mheshimiwa Sana analalamika kweli Masoud balance habari picha zako aseee, heh heh...


attachment.php
 
Yaonyesha, it's too hard to swallow! Sioni kama Masoud Kipanya anakosea, kama unavosema yeye ni msanii. Na kazi ya sanaa ni kuiuza sanaa yako kwa jamii. Muache afanye kazi yake.
 
Kazi kweli kweli! natamani na mimi ningekuwa mwandishi kipindi cha mavuno hiki dah!
 
nampongeza sana masoud anafanya kazi zake vizuri. Masudi wachore tu hasa mafisadi

MAFISADI???... mbona wamejaa CCM afu hawachori??? kuna kundi kubwa la ESCROW lipo huko mbona hajiusishi nalo katika mchakatako huu??? na vipi yule NAIBU SPIKA aliyempiga mgombea mwenza ubunge huko kwao,mbona hakumchora???.. hv yule aliyekutawa na kashfa ya RUSHWA yule alimchora??
 
Hivi magufuli ameridhia kuwakilishwa na hiyo Katuni..? Tehee tehe teheeee

By the way, Kipanya siku zote hufanya jambo sahihi ndani ya wakati sahihi. Umeshindwa kukijengea hoja kilio chako.
 
kawaida ya mwanadamu inategemea na kina nani wamemzunguuka, nani wanamshauri, nani wanamfadhili awapo na shida zake. kinyume na hivyo mwanadamu hufanya upinzani ili abembelezwe na kupatiwa chochote akidhi haja zake.

Lakini pia kila mmojawetu ana namna yake ya kutoa stress zinazomsumbua...
Mwacheni kp yuko kipindi kigumu wakati huu maana michoro yake siku hizi inaashiria hivyo. Ule uwezo na kiwango chake cha ubunifu vimeshuka. Tumpe muda ataacha kuchora picha za utupu na kurudi katika hali yake.
 
kawaida ya mwanadamu inategemea na kina nani wamemzunguuka, nani wanamshauri, nani wanamfadhili awapo na shida zake. kinyume na hivyo mwanadamu hufanya upinzani ili abembelezwe na kupatiwa chochote akidhi haja zake.

Lakini pia kila mmojawetu ana namna yake ya kutoa stress zinazomsumbua...
Mwacheni kp yuko kipindi kigumu wakati huu maana michoro yake siku hizi inaashiria hivyo. Ule uwezo na kiwango chake cha ubunifu vimeshuka. Tumpe muda ataacha kuchora picha za utupu na kurudi katika hali yake.

Ha haa, hii kidogo inivunje mbavu, teh teeeh!
 
Na hiyo je?

Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.
 
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo

Aisee hongera sana kwa kuliona hilo,ninachojua huyo kipanya ni ccm wa kupindukia kwa maana hiyo anatumika kwa manufaa ya ccm na huo ndio ukweli
 
Wkt nchi ipo gizani masoud alichachamaa sana na tanesco/ serikali wkt wote. Hivyo hata hii ni nyakati kama nyakati zingine

Kwahiyo mwigulu kukamatwa anatoa rushwa siyo habari,kabaka kukutwa na form 20000 za kupigia kura siyo habari,nape kuhojiwa na pccb kwa rushwa siyo habari,ndugai kumpiga mtu na kumjeruhi siyo habari,wasira kumpiga mtu siyo habari?wacheni kutufanya watu wote kuwa ni mazuzu kama nyinyi mlivyo mazuzu
 
Mwaka huu utawaona wanahabari njaa.. hiki ndyo kipindi chao cha mavuno.
 
Masoud KIPANYA ni mmoja kati ya wanataaluma ya sanaa ninaowakubali.
kabla haujamtuhumu ulipaswa kupitia news paper tofauti tofauti na ukaona ni ipi habari picha kwa kila gazeti?
lazima ujue kwamba ktk tasnia ya habari kuna ushindani wa kibiashara pia.
 
Last edited by a moderator:
Msanii hutakiwi kuonesha feelings zako upande gani, otherwise akaandikie Uhuru na Mzalendo ndo tutamwelewa! Zaidi ya hapo ni kujikosha tu, anafikiri kwamba kumponda Lowassa ndo atapata cha kupeleka kinywani. Asome na alama za nyakati na aangalie na Mtu anyemchafua bila sababu.

Nikweli kabisa njaa hawa jamaa inawapelekesha sana,tamaa zimewajaa mwandishi anataka anunue gari kipindi cha uchaguzi bila kujali kuwa karamu yake ikitumika vibaya ndio inaliangamiza taifa
 
Back
Top Bottom