Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Ushauri wa bure kwa Masoud Kipanya

Inawezekana pia we ni mshabiki wa YANGA....KP yupo fair acha kuaribu reputation za watu
 
Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Mkuu mimi matukio yote mawili yalinikuta eneo la tukio hasa lile la Olasiti walipotushambulia kwa bomu la kurushwa kwa mkono na risasi zilizotoka katika bastola na bunduki SMG na tulioumizwa na matukio hayo tupo wengi halafu zingatia mimi ni mwanachama wa kawaida tu cina cheo chochote Chadema ,sasa tukisema tuanze wote kudai kulipwa kwa yaliotokea nnadhani haitakuwa sahihi.Sote tunataka mabadiliko na dhana ile ile ya kuumia/kuumizwa /kuuwawa kwa baadhi ya wafuasi wa chama hichi ndio gharama za mabadiliko na hili la Lowasa kujiunga na upinzani Dkt Slaa akubaliane na mabadiliko hayo kwa sababu ukweli umejulikana na tunataka kusonga mbele sio kurudi nyuma.

Maneno yako ni ya kichochezi sana ,hayaachi umoja katika chama na yanatupeleka katika ubinafsi
 
Anapwaya sana siku hizi hata posts zake kule fb zina walakini sana, ngoma imelia sana sasa inataka kupasuka.
 
Kipanya kamchora sana Mkapa gazeti la Majira, kipindi anagombea urais pamoja Salmin komando kule Zanzibar, mpaka gazeti likapigwa marufuku kufika Zanzibar, acheni kulia lia na Lowasssa.
 
Mtoa mada kweli hujui kazi ya sanaa,kazi ya sanaa ni situational. Mbona magazeti yote ni lowassa,Hilo hulisemi??
 
Tatizo team Lowassa mnataka kuandikwa kwa mazuri tu hasa ya kipropaganda.

Ila unapokuja ukweli mnakua kama mbogo.!
 
the one who tells you about others will tell others about you
 
Wewe unakerwa Lowassa kuchorwa?? Wewe ni Lowassa??? Pilipili usiyoila inakuwashia nini?? Watu wengine bhana, eti anaumia kabisa akichorwa Lowassa. Hivi Lowassa alipokatwa na CCM wewe uliumia eeh!??? Na bado atachorwa sana mwaka huu. Subiri Watanzania wamkate tarehe 25 October ndio utaona atakavyochorwa na Masoud wa Kipanya.
 
Narudia tena! Masoud Kipanya ana akili Kuliko CHADEMA. Anachofanya tu ni kuzungumza uhalisia, baas! Hapeperushwi na upepo kama wanavyofanywa wale wanaojiita Makamanda
 
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo
CHADEMAkwa ulalamika?
Khaaa!!!!

Hata mkipata urais kwa bahati mbaya mtalalamika!!!
 
Masoud kipanya unafanya kazi nzuri sana. Jamani mnataka atoe uongo? Huo ndio ukweli sasa tatizo liko wapi? Yani mnataka akae kimya kwa manufaa ya nani hasa? Huu upuuzi mnaouleta nyie NYUMBU haukubaliki.
 
Kama mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa kazi za wasanii wetu leo naomba kusema hili linalonikera, toka Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Lowassa ahame CCM na kujiunga na CHADEMA msanii mwenzangu, msanii wa katuni Bw. Masoud Kipanya amekuwa akimshambulia wiki ya pili sasa katika namna tofauti tofauti, kila siku ni Lowassa Lowassa Lowassa, ninachojiuliza ni kweli hakuna habari nyingine?

Kama msanii hakuna jingine la kuelimisha jamii? Yaani huoni hata la TANESCO tu kuwa na mgao usioeleweka? Huoni hata la vigogo wa CCM wanaokamatwa na rushwa na baadae wanaachiwa kiurahisi na kuendelea na michakato yao kama kawaida au hata wanaowapiga wenzao majukwaani bila hata kuchukuliwa hatua zozote za kisheria? au je alivyokuwa CCM mbona hukumchora kwa kasi kubwa namna hiyo au kwa sasa kabadilika nini? Utasema msanii anaaangalia hadhira yake lakini je ni hadhira gani inayotaka kusikia ama kuona yale yale?

Kwa wanaojua sanaa watakubaliana na mimi kuwa hii ni "failure" kwa msanii, hapa kuna mawili, yawezekana anatumika na chama fulani ama la alifikria kumwandika kitambo ila alikuwa anamwogopa akiwa ndani ya mfumo wa chama dola, lakini yote kwa yote hili ni tatizo kubwa. Msanii unaporuhusu mihemuko (personal feelings) kwenye kazi au ukakubali kutumika na kundi la watu lazima utaharibu tu. Kama mzalendo na mpenda mafanikio ya wasanii wetu namshauri sana Bw. Kipanya, alienda vizuri sana hivyo asiruhusu kujiharibia kwa wapenzi na mashabiki wake kwa pesa za muda kama wanavyotumika wasanii wengine na baadae wanatelekezwa na kupoteza mwelekeo.

Ningeweka katuni na michoro hiyo hapa lakini naona kama nitajaza mipicha tu humu na kupoteza maana ila waswahili wanasema "kama wimbo umetungiwa wewe ni rahisi sana kuuelewa", naamini ujumbe umefika kwa muhusika na waandishi na wasanii wengine wa namna hii, unakuwa kama waandishi wa gazeti la Raia Mwema kila kukicha wao front page ni "udaku" wa Dk. Slaa kuhama Chadema, kipo cha kujifunza, jifunze kwa wenzio akini Said Michael ambao sasa wanavuka boda katuni zao sasa ni vibwagizo vikubwa katika vyombo vikubwa vya habari kama DW Kiswahili.

Unajishushia heshima bure kijana, fanya sanaa.
attachment.php

Katuni ya leo
Huna hoja zaidi ya kutuonesha wewe ni cdm, KP hajaanza kumchora lowasa leo ni toka kwenye mchakato wa kugombea urais kwa jirani zenu ccm alikuwa anachorwa mbona hukuja kulia hapa.

Tulieni watu wafanye kazi zao.
 
Makomeo wa nini ? ... hana Impact .. kila mtu anajua kuwa atakuwa Rais wa Kuendeshwa kama Gari bovu ...
 
Mwambie U DC asahau Kikwete kamaliza muda wake, apunguze mihemko yake

Nadhani na yeye ni miongoni mwa wale ambao hawakufikishwa kileleni
 
Back
Top Bottom