Ushauri wa bure kwa diaspora wenzangu na wale wanaokwenda kutafuta maisha nje ya Tanzania

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu wakuu,

Ama baada ya salam napenda nijikite kwenye mada ili nisiwachoshe wasomaji. Ndugu zangu unapokuwa nje ya nchi kwa lengo fulani la kutafuta maisha, ili ufanikiwe unatakiwa ufanye haya ninayoyataja hapa chini, lkn pia kama kuna mengine ambayo sikuyaandika hapa ktk list yang basi wengine mnaweza pia kujazia.

(1) Jambo la kwanza kama uliingia ktk nchi ya watu kihalali basi fata utaratibu wa kuendelea kuwa ktk hiyo nchi kihalali ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kutokea mbeleni

(2) Kama upo ktk hiyo nchi husika kikazi au kibiashara basi fata utaratibu unaoeleweka ili uweze kufanya kazi/ baishara yako kwa amani bila kubughuziwa na mamlaka ya nchi

(3) Kama ww ni mfanyakazi inabidi utafute sehem ambayo unajua ina watu wengi lkn haina huduma ya kutosha ya biashara unayofanya (bila kuangalia umaarufu wa mji)

(4) Jiepushe na maisha ya anasa.. i mean focus kwa kile kilichokupeleka ili usije ukateleza na kuangukia pua

(5) Tafuta marafiki au ndugu ambao wanaendana na mawazo yako.. i mean wale wanaoweza kukushauri kuhusu maendeleo ya kazi/ biashara yako na pia maisha yako (hapa simaanishi udharau wengine)

(6) Wekeza nyumban kwa kufungua miradi mbali mbali, jenga nyumba, nunua viwanja au mashamba, pia uwe na mawazo ya kurudi nyumban siku 1 hasa pale utapoona mambo yako ugenini yanaanza kuyumba

(7) Uwe na utaratibu wa kurudi nyumban mara kwa mara, hii itakusaidia kujua ni kipi unachohitajika kuwekeza nyumban kwa faida na maendeleo yako ya baadae. Ndugu zangu hayo ni baadhi ya mambo ambayo nimeamua kuwashauri kama rafiki yenu, ndugu yenu, mdogo wenu au mkubwa wenu. Kwahiyo mtu ana hiyari ya kuufuata au kuuacha ushauri huu.

Kwa upande wang namshukuru Mungu nimeweza kujisimamia ktk mambo fulan, kwa kufuata hayo niliyoandika hapo juu japo. Naweka na picha ya baadhi ya vichache nilivyojaaliwa kama faida ya kile kilichonitoa nchini kwangu kuja ugenini.

Hayo na maduka tofauti, niliyofungua sehemu tofauti kwa lengo la kufanikisha baadhi ya mambo yang yaliyonileta huku

IMG-20210407-WA0011.jpg

IMG-20210407-WA0014.jpg

IMG-20210407-WA0015.jpg

IMG-20210407-WA0017.jpg

IMG-20210407-WA0018.jpg
 
SOUTH HIYO.

SASA MKUU NIKUULIZE MASWALI:

1.ULIINGIA SOUTH NA MTAJI WA SH.NGAPI?

2. ULITUMIA KIBALI GANI KUPATA LESENI YA BIASHARA HADI KUWA NA MADUKA MAWILI/MATATU?

3.ULIINGIA SOUTH MWAKA GANI NA WASTANI UNAPATA PROFIT YA SH.NGAPI KWA MWAKA?

4. UNAKABILIANA VIPI NA WIVU KUTOKA KWA WENYE NCHI YAO?
 
1) Sikuingia na mtaji wowote, nilikuja tu kutafuta maisha na mtaji nikaupata huku huku. 2) maduka ya aina hii huwa hayahitaji vibali. 3) Niliingia zaidi ya miaka 10 iliyopita, nilianza kwanz ku focus nyumban na baadae nikaamua kufungua biashara zangu huku. 4) Wivu upo kila sehem kikubwa ni kujifunza jinsi ya kuishi na watu waliokuzunguka hasa wenyeji.
 
Mkuu hiyo biashara ulianza na mtaji wa kiasi gani ? Naomba unijibu Kama hutajali mkuu.
 
Back
Top Bottom